KUACHISHA KAZI
Kuachisha kazi kwa ujumla maana yake ni kumalizika/kuvunjika kwa mkataba wa ajira kati ya muajiri na muajiriwa. Kwa maneno mengine ni kumalizika kwa mahusiano ya kiajira kati ya muajiri na muajiriwa.Kusitishwa kwa mahusiano hayo kunaweza kuanzishwa na upande wowote wa mkataba huo(muajiri au muajiriwa)
Katika kanuni za ajira na Mahusiano kazin(Kanuni za utendaji bora)za mwaka 2007,imeelezwa kuwa kuachishwa kazi ni pamoja na:
a. Kuachisha kazi chini ya sheria ya kimila ya Uingereza(Common Law)
b. Muajiri kusababisha ugumu wa muajiriwa kuendelea na ajira
c. Kushindwa kuongeza mkataba wa muda maalum kwa masharti yaleyale au yanayofana kama kulikuwa na matumaini ya kuongeza mkataba
d. Kushindwa kumruhusu mfanyakazi kurejea kazini baada ya likizo ya uzazi au ulezi
e. Kushindwa kumuajiri tena mfanyakazi pale ambapo muajiriamewaachisha kaziwafanyakazi kadhaa kwa sababu kama hiyo au zinazofanan na ametoa nafasi za ajira kwa baadhi ya wafanyakazi walioachishwa kazi tu
KUACHISHA KAZI KIHALALI
Katika sheria ya Kimila ya Uingereza(Common Law) kuachisha kazi kumeelezwa kuwa ni pamoja na
I. Kuachisha kazi kwa makubaliano-hapa ni pale ambapo muajiri na muajiriwa wamekubaliana kusitisha mahusiano yao ya kiajira Kwa mfano kama mkataba wa ajira ni wa mwaka mmoja na muda huo umekwisha hapo mkataba utakuwa umefikia kikomo
II. Ajira kukoma yenyewe-hapa ni pale ambapo mkataba wa ajira unakuwa umesitishwa katika mazingira kama kifo au kumalizika kwa shughuli ya muajiri
III. Kuachishwa kazi kunakofanywa na muajiri-muajiri pia anaweza kusitisha mkataba wa ajira lakin itampasa kwanza kuzingatia na kufuata taratibu za kisheria.
Katika Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini(Kanuni za Utendaji Bora)za mwakwa 2007 Kanuni ya 7(1)inasema ku”pale ambapo muajiri anafanya ajira kushindwa kuvumilika ambapo pia inaweza kusababisha muajiriwa ajiuzulu,kujiuzulu huko kutakuwa sawa na kuacha kazi kwa kulazimika”
Sheria ya ajira na mahusiano kazini na kanuni zake ,pia imeeleza kuwa ili kuachisha kazikuwe ni halali basi ni lazima kuwe na sababu halali na ya haki(valid and fair reason) na utaratibu wa haki(fair procedure)uwe umefuatwa.Muajiri anapaswa kuwa na sababu halali na awe amefuata utaratibu wa haki katika kumuachisha kazi muajiriwa.
Taratibu za kuachisha kazi zinatofautiana kulingana na sababu inayopelekea kuachisha kazi,lakini taratibu zote hizo ni lazima zimpe muajiriwa nafasi ya kusikilizwa kabla ya uamuzi wa kumuachisha kazi.Bila kujali uzito wa kosa lililofanywa na muajiriwa ,bila kujali kuwa muajiri wake ana ushahidi wa kutosha,ni lazima sheria kufuata taratibu za kumuachisha kazi kama ilivyoelezwa katika sheria ya Ajira na Mahusiano kazini na 6. Ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007.
Kushindwa kufuata taratibu hizo kutamaanisha muajiriwa ameachishwa kazi bila kupewa nafasi ya kujitetea(summary dismissal)Kutompa muajiriwa nafasi ya kujitetea au kujieleza ni kumnyima haki yake ya kisheria.Kwa mujibu wa sheria za kazi kuachisha kazi kwa namna hii ni sawa na kuachisha kazi kusivyo halali(unfair termination)
Endapo itathibitika kuwa kuachisha kazi kulikofanywa na muajiri si halali inaweza kuamuriwa kuwa muajiri atekeleze moja ya mambo yafuatayo kwa mfanyakazi/muajiriwa husika
1. Kumrudisha muajiriwa kazini(reinstatement)hapa muajiriwa atarudishwa kazini na itahesabika alikuwepo kazini kutokea siku alipoachishwa kazi na atashahili kulipwa stahiki zake alizostahili kulipwa kwa kipindi chote tangu kuachishwa kwake.Pale ambapo amri ya kumrudisha muajiriwa kazini imetolewa na muajiri amashindwa kutekeleza amri hiyo,atapaswa kumlipa mfanyakazi huyo fidia ya mishahara ya miezi isiyopungua kumi na mbili(12) na stahiki nyingine alizostahili kulipwa tangu kuachishwa kwake
2. Kumuajiri upya mfanyakazi kwa mashari mapya yatakayoamuliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi au Mahakama kuu kitengo cha kazi(Labour Court). Endapo mwajiri atashindwa kutekeleza amri hii,atalazamika kulipa fidia ya mishahara ya miezi isiyopungua kumi na mbili pamoja na stahiki nyingineambazo muajiriwa alistahili kulipwa tangu siku aliyoachishwa kazi isivyo halali.
3. Kumlipa mfanyakazi fidia ya mshahara wa miezi isiyopunguakumi na mbili.Pamoja na fidia hiyo,pia atalazimika kumlipa stahiki zake nyingine anazostahili kulipwa kwa mujibu wa sheria yoyote ile au makubaliano yoyote yaliyokuwepo kati ya muajiri na muajiriwa.