Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

KUACHISHA KAZI

Kuachisha kazi kwa ujumla maana yake ni kumalizika/kuvunjika kwa mkataba wa ajira kati ya muajiri na muajiriwa. Kwa maneno mengine ni kumalizika kwa mahusiano ya kiajira kati ya muajiri na muajiriwa.Kusitishwa kwa mahusiano hayo kunaweza kuanzishwa na upande wowote wa mkataba huo(muajiri au muajiriwa)

Katika kanuni za ajira na Mahusiano kazin(Kanuni za utendaji bora)za mwaka 2007,imeelezwa kuwa kuachishwa kazi ni pamoja na:

a. Kuachisha kazi chini ya sheria ya kimila ya Uingereza(Common Law)

b. Muajiri kusababisha ugumu wa muajiriwa kuendelea na ajira

c. Kushindwa kuongeza mkataba wa muda maalum kwa masharti yaleyale au yanayofana kama kulikuwa na matumaini ya kuongeza mkataba

d. Kushindwa kumruhusu mfanyakazi kurejea kazini baada ya likizo ya uzazi au ulezi

e. Kushindwa kumuajiri tena mfanyakazi pale ambapo muajiriamewaachisha kaziwafanyakazi kadhaa kwa sababu kama hiyo au zinazofanan na ametoa nafasi za ajira kwa baadhi ya wafanyakazi walioachishwa kazi tu

KUACHISHA KAZI KIHALALI

Katika sheria ya Kimila ya Uingereza(Common Law) kuachisha kazi kumeelezwa kuwa ni pamoja na

I. Kuachisha kazi kwa makubaliano-hapa ni pale ambapo muajiri na muajiriwa wamekubaliana kusitisha mahusiano yao ya kiajira Kwa mfano kama mkataba wa ajira ni wa mwaka mmoja na muda huo umekwisha hapo mkataba utakuwa umefikia kikomo

II. Ajira kukoma yenyewe-hapa ni pale ambapo mkataba wa ajira unakuwa umesitishwa katika mazingira kama kifo au kumalizika kwa shughuli ya muajiri

III. Kuachishwa kazi kunakofanywa na muajiri-muajiri pia anaweza kusitisha mkataba wa ajira lakin itampasa kwanza kuzingatia na kufuata taratibu za kisheria.

Katika Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini(Kanuni za Utendaji Bora)za mwakwa 2007 Kanuni ya 7(1)inasema ku”pale ambapo muajiri anafanya ajira kushindwa kuvumilika ambapo pia inaweza kusababisha muajiriwa ajiuzulu,kujiuzulu huko kutakuwa sawa na kuacha kazi kwa kulazimika”

Sheria ya ajira na mahusiano kazini na kanuni zake ,pia imeeleza kuwa ili kuachisha kazikuwe ni halali basi ni lazima kuwe na sababu halali na ya haki(valid and fair reason) na utaratibu wa haki(fair procedure)uwe umefuatwa.Muajiri anapaswa kuwa na sababu halali na awe amefuata utaratibu wa haki katika kumuachisha kazi muajiriwa.

Taratibu za kuachisha kazi zinatofautiana kulingana na sababu inayopelekea kuachisha kazi,lakini taratibu zote hizo ni lazima zimpe muajiriwa nafasi ya kusikilizwa kabla ya uamuzi wa kumuachisha kazi.Bila kujali uzito wa kosa lililofanywa na muajiriwa ,bila kujali kuwa muajiri wake ana ushahidi wa kutosha,ni lazima sheria kufuata taratibu za kumuachisha kazi kama ilivyoelezwa katika sheria ya Ajira na Mahusiano kazini na 6. Ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007.

Kushindwa kufuata taratibu hizo kutamaanisha muajiriwa ameachishwa kazi bila kupewa nafasi ya kujitetea(summary dismissal)Kutompa muajiriwa nafasi ya kujitetea au kujieleza ni kumnyima haki yake ya kisheria.Kwa mujibu wa sheria za kazi kuachisha kazi kwa namna hii ni sawa na kuachisha kazi kusivyo halali(unfair termination)

Endapo itathibitika kuwa kuachisha kazi kulikofanywa na muajiri si halali inaweza kuamuriwa kuwa muajiri atekeleze moja ya mambo yafuatayo kwa mfanyakazi/muajiriwa husika

1. Kumrudisha muajiriwa kazini(reinstatement)hapa muajiriwa atarudishwa kazini na itahesabika alikuwepo kazini kutokea siku alipoachishwa kazi na atashahili kulipwa stahiki zake alizostahili kulipwa kwa kipindi chote tangu kuachishwa kwake.Pale ambapo amri ya kumrudisha muajiriwa kazini imetolewa na muajiri amashindwa kutekeleza amri hiyo,atapaswa kumlipa mfanyakazi huyo fidia ya mishahara ya miezi isiyopungua kumi na mbili(12) na stahiki nyingine alizostahili kulipwa tangu kuachishwa kwake

2. Kumuajiri upya mfanyakazi kwa mashari mapya yatakayoamuliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi au Mahakama kuu kitengo cha kazi(Labour Court). Endapo mwajiri atashindwa kutekeleza amri hii,atalazamika kulipa fidia ya mishahara ya miezi isiyopungua kumi na mbili pamoja na stahiki nyingineambazo muajiriwa alistahili kulipwa tangu siku aliyoachishwa kazi isivyo halali.

3. Kumlipa mfanyakazi fidia ya mshahara wa miezi isiyopunguakumi na mbili.Pamoja na fidia hiyo,pia atalazimika kumlipa stahiki zake nyingine anazostahili kulipwa kwa mujibu wa sheria yoyote ile au makubaliano yoyote yaliyokuwepo kati ya muajiri na muajiriwa.
...nimeelewa vema kabisa mkuu.
 
3. Kumlipa mfanyakazi fidia ya mshahara wa miezi isiyopunguakumi na mbili.Pamoja na fidia hiyo,pia atalazimika kumlipa stahiki zake nyingine anazostahili kulipwa kwa mujibu wa sheria yoyote ile au makubaliano yoyote yaliyokuwepo kati ya muajiri na muajiriwa.

Kiongozi mkali kwanza.
Hapo kwenye hiyo "option" ya tatu. Ni muajiriwa wa muda gani inamhusu kwa maana ya time toka afukuzwe?

Je hata mimi wa mwez mmoja toka nifukuzwe kihuni inanihusu?

Natanguliza shukran mkuu
 
Nimemuuliza jamaa yangu mmoja aliyesomea Law kabisa kaniambia ujinga ukianza kufanywa hata kama ni siku mkuu sheria inakuwa applicable. Hata kama una masaa umefanyiwa haya mambo provided hawajafata sheria wewe ukifata sheria unapata haki zako mkuu.
 
Je mwajiri anaweza kukupangia kazi ambayo sio profession?Na kama uwezi kuhimudu na unamwandikia barua bado anakulazimisha ukaimu kazi ambayo uipendi toka moyoni na sio ya fani yako.Je katika hiki kikombe nikiepuke vipi?naomba msaada wa kisheria ndugu cc:deonova
 
UBARIKIWE KIONGOZI (Mkali Kwanza)
 
Kiongozi, Asante kwa darasa zuri. Mimi nina matatizo makubwa kazini.
1. Wameniundia zengwe kuwa nimewapa wanafunzi mtihani
2. Wakanizuia kbsa kuingia shule
3. Wamenizuia hata kumalizia kusahisha
4. Wameshamchukua mwl mwingine
ILA
Hawajanihoji na wala sijaaandika maelezo yeyote kuhusu tuhuma zangu
JE
Ni sawa kisheria.?

Mwisho
vp sheria inasemaje kuhusu kumsimamisha na kumfukuza kazini mwajiriwa km mimi. Nimefanya kazi kwa miaka tisa (9) sasa

Wewe ni mtumishi wa umma ama unafanya kazi shule za private mkuu?
 
Mkuu kuna kundi la wafanyakazi waliopandishwa vyeo mwaka 2016 kwa barua kutoka katibu mkuu lkn mwaka 2018 wamepewa barua ya kusitisha upandishaji wa vyeo uliofanyika mwaka 2016 na badala yake barua imewatambua kwamba wamepanda mwaka 2017 sababu ni kwamba kipindi hicho serikali ilisimamisha upandishwaji wa vyeo kutokana na zoezi la uhakiki! hapo maswali kadhaa yameibuka je wanaweza kupewa ushauri gani wa kisheria?je,waliostaafu kabla ya barua hizi mpya wanakuwa na nafasi gani?je,Katibu mkuu anayo mamlaka kufuta barua aliyo itoa yeye mwenyewe na kusogeza mbele wakati watumishi hao walianza kutumikia vyeo vyao vipya mara baada ya kutunukiwa?

Kikubwa hapa walifanya hivyo ili kuepuka kucreate madeni kwa watumishi, kumbuka Rais alishawaagizi watendaji wa chini (makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa halmashauri) kuepuka kucreate madeni mapya, hivyo kwa yale maagizo naona ndio walipokuja kutoa barua mpya zinazoonesha tarehe na mwezi uliyopewa barua na sio ile ya nyuma manake inge-create malimbikizo ambapo ni tofauti na maelekezo ya serikali, na kumbuka ktk kipindi hicho ndipo uhakiki ulikuwa unafanyika.

Lakini pia bado una haki ya ku-querry kwa Katibu Mkuu ktk wizara yako kwa ufafanuzi zaidi chief.
 
Je mwajiri anaweza kukupangia kazi ambayo sio profession?Na kama uwezi kuhimudu na unamwandikia barua bado anakulazimisha ukaimu kazi ambayo uipendi toka moyoni na sio ya fani yako.Je katika hiki kikombe nikiepuke vipi?naomba msaada wa kisheria ndugu cc:deonova

Kufanya kazi ambayo ni nje na ile Job Description yako, tena kwa kulazimishwa ama kwa kuwekewa sanction kwamba usipoifanya utapata adverse repercussions kutoka kwa mwajiri....kimsingi hii ndio tunaweza kui-term kama 'forced labour'

Tazama kifungu cha 6 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004; kinachokataza kazi za shuruti mahali pa kazi;

"For the purposes of this section, forced labour includes bonded labour or any work exacted from a person under the threat of a penalty and to which that person has not consented"

Na kimeeleza kabisa pale mwanzoni kuwa "Any person who procures, demands or imposes forced labour, commits an offence"

Hivyo katika case yako ni suala tu la kukusanya evidence na kuwasilisha either Ofisi ya Idara ya Kazi iliyo ktk mkoa ulipo wao kama Maafisa Kazi waliotajwa kwenye hiyo sheria watamfungulia mwajiri kesi, au pia unaweza kufungua mwenyewe case kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
 
Mkuu deonova ubarikiwe sana kwa msaada wako mkubwa unao utoa hapa

Mm nina tatizo kwenye ajira yangu imepita miaka miwili sasa toka nimejiunga na hii kampuni
Ninakatwa hela 10% ya mfuko wa hifadhi ya jamii PPF lakini sijaungwa ppf kwahiyo hizo hela haziendi ppf wala ppf hawanitambui

Je ikitokea nimeachishwa kazi au nineacha kazi ninaweza kulipwa hiyo pesa na mwajiri wangu?

Au ni hatua gani napaswa kuzichukua sasa hv maana maana kila nikimkumbushia mwajiri kuhusu hili anasema ana lishughulikia lakini hamna matokeo chanya...

Naomba msaada kwenyehili
 
Pole kwa hilo mkuu, je una kadi ya uanachama ya kwenye huo mfuko wa PPF?
 
Stahiki baada ya mkataba kuisha ama kukatishwa

1.Maana

¨Hizi ni stahiki azipatazo mwajiriwa kutokana na mkataba wake wa ajira kukatishwa na mwajiri. Stahiki hizi hulipwa na mwajiri.

¨Aidha, kipengele cha 44 cha Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004 inampa mwajiriwa haki ya kulipwa stahiki mbalimbali pindi mkataba wake wa kazi unapokatishwa.

2. Aina za Stahiki
  • Malipo ya kazi yote aliyoifanya mwajiriwa kabla ya mkataba wake wa kazi kukatishwa.
  • Malipo kwa likizo yake ya mwaka ambayo atakuwa hajaenda kabla ya mkataba kukatishwa.
  • Malipo kwa likizo za mwaka zilizolimbikizwa. Hii inamaanisha katika kipindi chote cha mkataba kama kuna likizo ambazo mwajiriwa alikuwa hajachukua, basi atastahili kulipwa sawa sawa na idadi ya siku hizo.
  • Malipo yatokanayo na kukatisha mkataba pasipo kutoa/kutanguliwa na notisi. (Notice pay due). Hii ina maana kuwa, badala ya mwajiri kutoa notisi ya kukatisha mkataba kwa mwajiriwa, basi mwajiri anaweza kuamua kumlipa mwajiriwa malipo kiasi ambacho ni sawa sawa na kile ambacho mwajiriwa angekuwa anapata katika kipindi hicho cha muda wa notisi.
  • Kiinua mgongo (severance pay), kama tu mwajiriwa ametimiza vigezo vya kulipwa kiinua mgongo. (S.42, ELRA, 2004)
  • Gharama za usafiri kutoka eneo la mwajiri. Hii ni endapo mwajiriwa wanaachana na mwajiri katika sehemu ya kazi eneo tofauti na alipoajiriwa awali. Kwa mfano Mr. John anaajiriwa na kampuni A ambayo iko Dodoma, halafu baada ya muda akahamishiwa ofisi za kampuni hiyo hiyo zilizopo Arusha, mkataba wake ukikatishwa basi mwajiri atalazimika kumlipa Mr.John gharama za usafiri na kujikimu safarini kurudi hadi eneo alikoanzia ajira yake hiyo Dodoma.
  • Hati ya kazi (Certificate of service). Hii ni hati anayopatiwa mwajiriwa anayeacha/anayeachishwa kazi kutambua mchango wa nguvukazi yake katika huduma/kazi ambayo amekuwa akiifanya katika muda wote wa ajira yake katika kampuni/taasisi husika. Hati ya kazi haitakiwi kueleza sababu za kuacha/kuachishwa kazi.
Baadhi ya stahiki hizi zinatolewa kulingana na vigezo mbalimbali kama;

Ø Sababu za kukatishwa mkataba (grounds of termination)

Ø Aina ya mkataba wa ajira (type of employment contract)

Ø Muda ambao mwajiriwa amehudumu katika huduma/ajira (the length of service to your employer)

3. Ufafanuzi wa Kiinua mgongo (severance pay)

Ufafanuzi wa kipengele cha kiinua mgongo kadiri ya Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004, kifungu cha 42 kinaeleza kama ifuatavyo;

  • Kama mkataba wa ajira umekatishwa na mwajiri kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu ama ukiukwaji wa miiko ya kazi, basi mwajiri halazimiki kulipa kiinua mgongo.
  • Kama mkataba wa ajira umekatishwa kutokana na mahitaji mapya ya uendeshaji wa ofisi/kazi (termination on grounds of capacity or operational requirements), ama kutokana na uanzishwaji wa teknolojia mpya inayohitaji watu wenye utaalamu zaidi, na mwajiri ametoa ajira mbadala kwa watakaoathirika na mabadiliko hayo, lakini wafanyakazi wakaikataa hiyo ajira mbadala basi mwajiri anaweza kukataa kulipa kiinua mgongo.
  • Ni lazima mwajiriwa awe amehudumia katika ajira hiyo kwa muda usiopungua miezi 12 mfululizo ndipo atakidhi kigezo cha kupata kiinua mgongo. Aidha, lazima ukatishwaji huo wa mkataba uwe umesababishwa na mwajiri (termination initiated by employer)
4. Ukokotoaji wa kiinua mgongo

Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004, kifungu cha 42 kimeendelea kueleza juu ya Ukokotoaji wa kiinua mgongo. Kiinua mgongo ni kiasi ambacho ni sawa sawa na kiwango cha mshahara wa siku saba (7) kwa kila mwaka mzima ambao mwajiriwa ametoa huduma pasipo kukatisha; lakini haivuki miaka kumi (10)

Hivyo; Kiinua mgongo = kiwango cha mshahara wa siku 7 zidisha kwa miaka ambayo mwajiriwa ametoa huduma kwa mwajiri katika muda usiozidi miaka 10.

Kima cha mshahara kwa mwezi x 7 x idadi ya miaka

26
(yaani kima cha chini cha mshahara wa sekta husika, kigawanye kwa 26 (yaani siku za kazi 26) kisha zidisha kwa siku 7 halafu zidisha tena kwa idadi ya miaka uliyokaa kazini (hapa weka miaka iliyokamilika tu....mfano umekaa kazini miaka miwili na miezi minne, hapa tunachukua miaka miwili tu iliyokamilika, hiyo miez kwa sababu haijatimia miezi 12 hatuichukui)

5. Gratuiti (gratuity)

Huu ni ukokotoaji wa kiinua mgongo kwa kadirio la asilimia, kadiri ya ongezeko la mshahara wa kila mwezi kulingana na makubaliano ya mwajiriwa na mwajiri.

¨Kwa mfano, mwajiri anayelipa gratuiti asilimia 5%, maana yake kila mshahara asilimia 5% inahesabika kwenye stahiki za mafao.

Ongezeko la gratuity kwa 5% kwa mwezi

April

Mei

Juni

Julai

Mshahara

140,000

150,000

200,000

300,000

Gratuity 5%

7,000

7,500

10,000

15,000

7,000 + 7,500 + 10,000 + 15,000 = 39,500

NB; Asilimia hiyo anatoa mwajiri tu. (haitatokana na makato kwa mwajiriwa)

Samahani kidogo hii chart ya kuonesha ukokotoaji wa kiinua mgongo kwa Gratuity haijaweza kuiarrange vizuri hapa lakini angalau mkisoma mnaweza kupata concept.

Mwajiriwa hatakuwa amekidhi kigezo cha kulipwa kiinua mgongo kama mkataba wa ajira utakatishwa akiwa hajakamilisha mwaka mmoja (miezi 12) tangu alipoajiriwa. Kwa wanaolipwa gratuiti ukokotoaji utafanyika kwa miezi yote ambayo mwajiriwa amefanya kazi.

NINAWASILISHA

Maazimio ya pamoja ya Shirika la Kazi Duniani (ILO)
  • Yanahusu zaidi kanuni za kisheria ambazo zinatoa miongozo na haki katika sehemu ya kazi
  • Kwa ufupi, miongozo na haki sehemu za haki zinahusiana na;
1. Ajira za watoto: No 138/1973; 182/1999
2. Kazi za lazima: No 29/1930;105/1951
3. Ubaguzi: No.111/1958; 100/1951
4. Uhuru wa kuungana na kuingia makubaliano ya hiari ya pamoja: No.87/1948; 98/1949

Haki za mtoto S.5
  • Inazuia ajira kwa mtoto yeyote mwenye umri chini ya miaka 14
  • Mtoto mwenye umri wa miaka 14 au zaidi anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi tu,
  • Inazuia kumfanyisha mtoto kazi nyakati za usiku.
  • Ajira zinazozuliwa hapa ni pamoja na aina mbaya za ajira za mtoto kama utumwa, usafirishaji wa watoto, uwekaji rehani kwa ajili ya deni na aina zote za ajira za shuruti, biashara ya ngono na utengenezaji filamu za ngono, kuajiri watoto kwa lazima kwa shughuli za kijeshi n.k
Tazama pia Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

Kazi za lazima S.6
Sheria inakataza kazi za lazima lakini inatoa nafasi kwa aina fulani za kazi za lazima kama;
  • Kazi yoyote inayotekelezwa chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taifa ya mwaka 1966, kwa kazi ambayo ni ya kijeshi.
  • Kazi yoyote ambayo ni sehemu ya wajibu wa kawaida wa kiraia kwa raia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Kazi yoyote inayotekelezwa kwa dharura au hali ya hatari.
  • Kazi yoyote inayotolewa kwa mtu yeyote ikiwa ni matokeo ya kutiwa hatiani na mamlaka ya sheria.
Kuzuia ubaguzi sehemu ya kazi

S.7 - (1) Kila mwajiri atatakiwa kuhakikisha kwamba anaendeleza fursa sawa katika ajira na kujitahidi kuondoa ubaguzi katika sera yoyote ya ajira mazoezi kwa vitendo

(2) Mwajiri atalazimika kusajili kwa Kamishna wa Kazi, mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi

(3)Kamishna wa Kazi anaweza kumtaka mwajiri:-
  • Kuunda mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi kama inavyoelekezwa katika kifungu kidogo cha (2); na
  • Kuusajili mpango huo kwa Kamishna
  • Kutokuunda mpango huo na kuusajili ni kosa kisheria

(4) Mwajiri yeyote asifanye ubaguzi wa dhahiri au usiokuwa wa dhahiri kwa mwajiriwa, katika sera au mazoea katika moja ya sababu zifuatazo:

a)Rangi
b)Utaifa
c)Kabila au sehemu anayotoka
d)Asili
e)Uasili wa Taifa
f)Asili ya kijamii
g)Maoni ya kisiasa au kidini
h)Mwanamke au Mwanaume
i)Jinsia
j)Ujauzito
k)Kuolewa ama kutoolewa au majukumu ya familia
l)ulemavu
m)VVU/UKIMWI
n)Umri; au
o)Maisha anayoishi

HAKI KUUNGANA WAAJIRIWA

S 9 - (1) Kila mfanyakazi ana haki ya;

a)Kuunda na kujiunga na chama cha wafanyakazi.
b)Kushiriki katika kazi halali za chama cha wafanyakazi.

S 9 - (3) Mtu yeyote haruhusiwi kufanya ubaguzi kwa mfanyakazi kwa sababu huyo:-
  • Ametekeleza au alitekeleza haki yoyote chini ya Sheria hii au Sheria nyingine inayosimamiwa na Waziri.
  • Ni mwanachama au alikuwa mwanachama wa chama cha Wafanyakazi; au
  • Ameshiriki au alishiriki katika kazi halali cha chama

S 9(4) Mtu yeyote haruhusiwi kufanya ubaguzi, kwa mfanyakazi wa chama cha wafanyakazi au shirikisho kwa kukiwakilisha au kushiriki katika kazi halali za chama.

S 9(5) Mtu yeyote anayekiuka masharti ya vifungu vidogo vya (3) na (4), anatenda kosa.

S 9(6) Kwa madhumuni ya kifungu hiki;

a)“mfanyakazi” inajumuisha mwombaji wa kazi;
b)“mfanyakazi wa ngazi ya juu ya uongozi” maana yake ni mfanyakazi ambaye, kulingana na nafasi ya mfanyakazi huyo-
  1. Anatengeneza sera kwa niaba ya mwajiri; na
  2. Anaruhusiwa kuingia mikataba ya hiari kwa niaba ya mwajiri.

HAKI YA KUUNGANA WAAJIRI

S. 10 - (1) Kila mwajiri atakuwa na haki-

a)Kuunda na kujiunga na chama cha waajiri;*
b)Kushiriki katika kazi halali za chama cha waajiri,

S .10 - (2) Mtu yeyote haruhusiwi kufanya ubaguzi kwa mwajiri kwa sababu mwajiri-
  • Ametekeleza au alitekeleza haki yoyote chini ya Sheria hii au Sheria inayosimamiwa na Waziri;
  • Ni mwanachama au alikuwa mwanachama wa chama cha waajiri; au
  • Ameshiriki au alishiriki katika kazi halali za chama cha waajiri.

VIWANGO VYA AJIRA

1. Mikataba ya Ajira

a). Aina za mikataba
  1. Mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa (mara nyingi huitwa mkataba wa kudumu)
  2. Mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa
  3. Mkataba wa kazi maalumu
Kazi maalumu - maana yake ni zile zinazotokea mara chache au za msimu ambazo sio endelevu. ( ELRA Misc. Amendment No 38 of 2015; S.4)

b). Taarifa ya maelezo ya maandishi S.15
15-(1) Mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi, maelezo ya mkataba kwa maandishi kama-

i. Jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi
ii. Mahali alipoajiriwa
iii. Kazi yake
iv. Tarehe ya kuanza
v. Muundo na muda wa mkataba
vi. Kituo cha kazi
vii. Masaa ya kazi
viii. Ujira, njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine au malipo ya vitu; na
ix. Kitu kingine kilichotajwa

(2) Kama taarifa zote zilizotajwa katika kifungu kidogo cha (1) zimeelezwa kwenye mkataba wa maandishi na mwajiri amempa mfanyakazi mkataba huo, mwajiri anaweza asitie maelezo yaliyoandikwa yaliyotajwa katika kifungu cha 14.

(3) Kama mfanyakazi haelewi maelezo yaliyoandikwa , mwajiri anatakiwa kuhakikisha kwa yanafafanuliwa kwa mfanyakazi katika hali ambayo mfanyakazi anaelewa.

(4) Pale ambapo suala lililotajwa katika kifungu kidogo cha (1) litabadilika, mwajiri atatakiwa kwa kuwasiliana na mfanyakazi, kurekebisha maelezo yaliyoandikwa ili kuendana na mabadiliko na kumtaarifu mfanyakazi mabadiliko hayo kwa maandishi.

(5) Mwajiri atatakiwa kutunza maelezo ya maandishi yaliyotajwa katika kifungu kidogo cha (1) kwa muda wa miaka mitano baada ya kusitishwa kwa ajira

(6) Ikiwa katika mwenendo wowote wa kisheria, mwajiri atashindwa kutoa mkataba wa maandishi au maelezo ya maandishi yaliyotolewa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1), jukumu la kuthibitisha au kukanusha sharti la ajira linalodaiwa na lililotajwa katika kifungu kidogo cha (1) litakuwa ni la mwajiri.

(7) Masharti ya kifungu hiki hayatatumika kwa mfanyakazi ambaye anafanya kazi chini ya siku sita kwa mwezi kwa mwajiri.

2. Masaa ya Kazi

a) Masaa ya kazi – Masaa 9 kwa siku; Masaa 45 kwa wiki; na Siku 6 katika wiki yoyote

b) Si zaidi ya saa 50 ya ziada katika mzunguko wa wiki nne

c) Mwajiriwa hatatakiwa kufanya kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku hata kama wamekubaliana hivyo (kifungu cha 19)

d) Kazi zitakazofanyika usiku kati ya saa 02:00 usiku na saa 12.00 asubuhi, Mwajiri atatakiwa kumlipa mfanyakazi angalau 5% ya mshahara wa mfanyakazi huyo kwa kila saa atakayofanya kazi usiku na kama saa anayofanya kazi ni ya ziada; 5% itakokotolewa katika kima cha saa za zaida za mfanyakazi. (Kifungu cha 20(4)).

NB:
Kazi za usiku haziruhusiwi kwa mwanamke mjamzito miezi miwili kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, au miezi miwili baada ya tarehe ya kuzaa . (Kifungu 20(2))

e) Mapumziko katika siku ya kazi
S.23 - (1): Mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi ambaye amefanya kazi mfululizo kwa zaidi ya saa 5 mapumziko ya angalau dakika 60. (Break given if the job can be left unattended)

(2) Mwajiri anaweza kumtaka mfanyakazi kufanya kazi wakati wa mapumziko ikiwa tu kama kazi haiwezi kufanywa na mfanyakazi mwingine.

(3) Mwajiri hatakiwi kuwajibika kumlipa mfanyakazi katika kipindi cha mapumziko isipokuwa kama mfanyakazi anatakiwa kufanya kazi au kuwepo kwa ajili ya kazi wakati wa mapumziko

3. Ujira
a) S.26 (2): Kima cha ujira kwa saa, siku au mwezi kitatakiwa kuamuliwa kwa kufuata orodha iliyotolewa katika Jedwali la Kwanza

b). Malipo ya fedha yatakuwa katika bahasha iliyofungwa kama malipo yanafanyika kwa fedha taslimu au kwa hundi (Kifungu 27 (1)(c)); au fedha iwekwe katika akaunti ya benki ambayo mfanyakazi ameichagia mwenyewe kwa maandishi.

c). Mwajiri hatakiwi kufanya makato yoyote kwenye ujira wa mfanyakazi isipokuwa tu yale ambayo yapo kwa mujibu wa Sheria ama mfanyakazi amekubali kukatwa kuhusiana na deni.

d). Malipo yafanyike katika muda wa kazi, mahali pa kazi katika siku waliyokubaliana.

4. Likizo ya mwaka

a). Anayestahili:
Mfanyakazi mwenye miezi chini ya sita kazini hatakuwa na haki ya kupata likizo yenye malipo chini ya masharti ya sehemu hii. ELRA, see Section 29 (1)

Mfanyakazi mwenye utumishi wa chini ya miezi sita na ambaye amefanya kazi zaidi ya mara moja katika mwaka, atakuwa na haki ya kupata likizo yenye malipo chini ya masharti ya Sehemu hii kama jumla ya kipindhi alichofanya kazi kwa mwajiri huyo kinazidi miezi sita kwa mwaka huo. S.29-(1) (b)

S.30-(1) (c) “Likizo yenye malipo” maana yake ni likizo yoyote inayolipwa chini ya Sehemu hii na inayokokotolewa kwa kuangalia mshahara wa kawaida wa mfanyakazi.

S.31-(1) Likizo ya Mwaka; Mwajiri atatakiwa kutoa kwa mfanyakazia angalau siku 28 mfululizo kuhusiana na kila mzunguko wa likizo, na likizo hiyo itajumuisha siku yoyote ya sikukuu ambayo inaweza kuangukia ndani ya kipindi cha likizo

Employment and Labour Laws (Miscellaneous Amendment 2015- amends sect 31 on LEAVE

(6) Kwa makubaliano na Mfanyakazi, Mwajiri anaweza kumruhusu Mwajiriwa kumfanyia kazi katika kipindi ambacho Mfanyakazi huyo alitakiwa kuwa likizo kwa sharti kwamba mwajiriwa huyo asifanye kazi mfululizo kwa miaka miwili. (yaani unamuuzia mwajiri wako likizo yako)

(7) Mwajiri atamlipa mfanyakazi mshahara wa mwezi mmoja badala ya likizo ya mwaka ambayo mfanyakazi alitakiwa kwenda ama alitakiwa na mwajiri kumfanyia kazi badala ya kwenda likizo hiyo.

5. Likizo ya Ugonjwa (Kifungu cha 32

• siku 63 za kwanza – mshahara mzima
• siku 63 zinazofuata – nusu mshahara

Jumla ya siku 126 ambazo mfanyakazi atakuwa na haki ya likizo ya ugonjwa katika kila mzunguko wa likizo (Mzunguko wa likizo katika Sehemu hii ni miezi 36)

ED zinahesabika kama sehemu ya likizo ya ugonjwa

Likizo itatolewa kwa mfanyakazi kuwasilisha kwa mwajiri cheti cha matibabu kilichotolewa na tabibu aliyesajiliwa au tabibu mwingine yeyote anayekubalika na mwajiri, ambacho kukubalika kwake hakutakiwi kukataliwa bila sababu za msingi.

6. Likizo ya uzazi

i). Taarifa (S.33(1)) Mfanyakazi mwanamke atoe notisi kwa mwajiri kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua na notisi hiyo italazimika kuambatana na cheti cha kitabibu.

ii). Mfanyakazi anaweza kuanza likizo ya uzazi muda wowote kutoka wiki nne kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, au tarehe ya mapema kama tabibu atathibitisha kwamba ni muhimu kwa afya ya mfanyakazi au ya mtoto wake ambaye hajazaliwa

iii). Mfanyakazi hatatakiwa kufanya kazi ndani ya wiki sita baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake, labda tabibu awe amethibitisha kuwa anaweza kufanya hivyo. (Section 33(3)

iv). Likizo ya uzazi itakuwa siku 84 au siku 100 kama mfanyakazi atajifungua watoto zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. (Section 33 (6)

v). Mfanyakazi mjamzito au anayenyonyesha hataruhusiwa kufanya kazi ambazo ni hatari kwa afya yake au kwa afya ya mtoto wake., mwajiri atalazimika kumpa kazi nyingine mbadala inayofaa ikiwa inawezekana, kwa masharti na mazingira ambayo si mabaya zaidi ya masharti na mazingira yake.

vi). Mfanyakazi atakuwa na haki ya masaa hadi mawili kwa siku ya kumnyonyesha mtoto wakati wa saa za kazi.

(G.N No.47 Employment and Labour Relations (General) Regulations, 201)
"Mfanyakazi mwanamke, kwa kipindi kisichopungua miezi sita mfululizo baada ya kuisha kwa likizo ya uzazi, atatakiwa kuondoka mahali pa kazi angalau kwa masaa mawili katika wakati anaoona unafaa, kwa ajili ya kunyonyesha mtoto"

7. Likizo ya Uzazi ya baba na aina nyingine za likizo

a). Angalau siku 3 za likizo ya uzazi ya baba yenye malipo kama:
  • Likizo itachukuliwa ndani ya siku 7 tangu kuzaliwa mtoto
  • Mfanyakazi ni baba wa mtoto. (Section 34 (1)(b) and 34(1)(b)).
b)Angalau siku 4 za likizo ya malipo kwa sababu zifuatazo
  • Ugonjwa au kifo cha mtoto wa mfanyakazi
  • Kifo cha mke wa mfanyakazi, wazazi, bibi na babu, mjukuu au kitukuu
Siku 3 zilizotajwa hapo juu ni jumla ya idadi ya siku ambazo mfanyakazi ana haki bila kujali watoto wangapi wa mfanyakazi wamezaliwa ndani ya mzunguko wa likizo

NAOMBA KUWASILISHA.
 
Ndio kadi ninayo lakini nilijiunga nikiwa kwa mwajiri wangu wa zamani ambae alikuwa anaiingizia michango ppf vyema
baada ya mwajiri wangu wa zamani kusitisha ajira yangu.

Ndipo nikaingia kwa huyu mwajiri wangu mpya nikampa na namba yangu ya uanachama ya ppf ili awe anaingiza michango yangu huko. Lakini hakufanya hvyo

Kwahiyo ppf hawamtambui huyu mwajiri wangu mpya
 
Ndio kadi ninayo lakini nilijiunga nikiwa kwa mwajiri wangu wa zamani ambae alikuwa anaiingizia michango ppf vyema
baada ya mwajiri wangu wa zamani kusitisha ajira yangu
Ndipo nikaingia kwa huyu mwajiri wangu mpya nikampa na namba yangu ya uanachama ya ppf ili awe anaingiza michango yangu huko
Lakini hakufanya hvyo
Kwahiyo ppf hawamtambui huyu mwajiri wangu mpya

Upo mkoa gani chief?
 
Back
Top Bottom