Mkataba wangu kwanza ni wakudumu hivyo haki zangu hazijafafabuliwa sawasawa kuna kipengele kimoja kimeandika kuwa (a)mshahara wa mwajiriwa kabla ya makato ya ppf,nssf na paye havijaandikwa ni shilingi ngapi hivyo hiyo ni moja ya utapeli
(b)Na vipengele vingine ni kuhusu saa za kazi hakuna maelezo meengi kama mikataba ya kawaida
Sent using Jamii Forums mobile app
Je kunahitajika hela yoyore pale mpaka kujua haki zako zote(suluhisho)?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu! Binafsi nimefaidika sana na hii elimu uliyojitolea. Ninaomba msaada, mimi ninafanya kazi katika sekta binafsi ambapo niliingia mkataba wa miaka miwili mara ya kwanza, na ulipoisha nikaongeza mkataba mwingine wa miaka mitatu japo na wenyewe umeisha sasa hivi nipo tu nafanya kazi ila hatujasaini mkataba mwingine sasa hivi no mwezi was nane tangu kumalizika kwa mkataba wa pili. Hii mikataba yote ambayo imeishaisha haikuwa na kipengele chochote kinachoonesha gratuity wala kiinua mgongo. Je endapo mwajiri wangu amehamua kusitisha ajira yangu, ninaweza kuclaim hicho "kiinua mgongo changu?" au naweza pia kuclaim gratuity yangu ambayo haikuoneshwa kwenye mkataba?
Ahsante
Nashukuru sanaNdio mkuu, endapo ajira yako itasitishwa na mwajiri utastahili kulipwa kiinua mgongo, na kwa sababu mkataba haukutaja kama ukokotoaji utafanyika kwa utaratibu wa asilimia (gratuity) basi default formula itakayotumika ni ya Mshahara wa Siku 7 kwa kila mwaka uliokamilika (kuanzia mwaka ulipoanza kazi).......(i.e Daily Salary x 7 x Years of Service)
ni sahihi kwenda likizo bila mshahara yaani nimeenda likizo 1febr2019, nikapewa hela yangu ya likizo niliporudi nikaulizia salary nikaambiwa hakuna ni ileile ya likizo niliyopewa je hii ni sahihi
shukrani mkuu hawa jamaa wamenipigaUnapokuwa Likizo yako ya mwaka mshahara wako unapokea kama kawaida as if ungekuwepo kazini (paid leave); sasa Kifungu cha 5(2) cha Waraka wa Mishahara ya Kisekta (Labour Institutions Wage Order) kinatamka hivi...............An employee shall in addition to annual paid leave, be entitled to leave travel assistance once in every two years of continuous service with the same employer.
Kwamba kila baada ya miaka 2 ukiwa na mwajiri wako huyo huyo, utakuwa unapewa "leave travel assistance" (hii inajumuisha nauli yako na mwenza na watoto wako plus gharama mnazoweza kukutana nazo njiani mfano kulazimika kulala njiani mpaka kufika nyumbani unakoenda likizo pamoja na gharama za nauli ya kurudi). Tunaposema kila baada ya miaka 2 means mwaka huu ukienda likizo na ukapewa hizo leave travel assistance basi mwaka ujao hupewi, mwaka unaofuata unapewa, unaofuata hupewi.
NB: Hapa mshahara wako uko pale pale hata kama upo likizo.(annual leave)
Hii inaapply kwa watumishi wote wa Serikali na Private.
Na mm nasisitiza mwenye kanuni na sheria ya ajira na mahusiano kazin naomba azitumeMwenye kanuni za kudumu kwa kiswahili atutumie humu
Naomba kujua ikiwa mtu umeajiriwa kwa mkataba wa makubaliano ya mdomo bila maandishi( oraly contract or agreement) yakufanya kazi bila kupewa muda wa matazamio na mwajiri wako, halafu baada ya miezi mtatu tu mwajiri akakuandikia barua ya kukufukuza kazi bila hata kukupatia sitahili zako zozote, je unayo haki ya kumshitaki? Na kama utamshitaki ni kwa sheria gani utamshitaki?
wandugu, msihangaike kutafuta sheria. sheria zote za tz kuanzia mpya hadi za zamani, zipo kwenye website ya parliament of tz. nenda kule utaipata kwenye pdf. nashangaa wengine wanasema walikuwa wanatafuta sheria hizi, wakati ziko wazi sana, tena mno.
Mwajiri ana wajibu wa kumtibu mwajiriwa mpaka apone