Nimejitahidi kusoma yaliyowekwa na wachangiaji mbalimbali kwenye mada hii kujaribu kuelewa wengi wetu tunasimamia wapi katika jambo hili la utajiri.
Nimemsoma kidogo, 'technically' pale, na kufikiri kidogo aliyoweka hapo na kutaka kumuunga mkono ingawa hakufafanua zaidi.
Matajiri ni wale wale tu hakuna matajiri wapya. Tunataka middle class life kwa watanzania wote mamilione wanatuhusu nini watanzania wenye kipato cha chini?
Lakini baadhi yetu, kama.
Akina mkuu 'Gachuma' hapa wanajisikia raha kweli kweli kwa habari kama hiyo kana kwamba inawaongezea chochote mifukoni mwao!
'Anyways', bila shaka hawa matajiri wetu ni masalia ya Mzee Kikwete. Sioni kabisa jinsi gani hawa waliweza kupenya na kuwa matajiri katika hali iliyopo sasa hivi, sioni kamwe uwezekano wa hilo.
Sasa mtu asije hapa na kunilalamikia kwamba mimi sipendi matajiri, au sipendi watu wapate utajiri, napenda sana kuona tukiwa na matajiri wetu wengi tu, wakipigana vibega na sisi sote, "sio wanyonge" bali tulio na hali nzuri kimaisha hata kama hatuwezi kuwa kama hao matajiri wetu.
Napenda sana kuwaona matajiri wetu hawa, wakifanya kila juhudi za kuwekeza utajiri wao hapa, kuzalisha mali, kutoa ajira na kujenga uchumi wetu, na sio matajiri wa kupeleka faida inayozalishwa hapa kwenda kuwekezwa kwenye mahekalu ya ulaya.
Nawapenda sana matajiri wetu wenyewe wa hapa hapa, ambao utajiri wao umepatikana sio kwa wao kuwa kwenye Chama tawala, ambako kazi yao kubwa ilikuwa ni kulangua sukari ya magendo waliyoingiza nchini kwa kuhonga wabunge wenzao walegeze sheria za kulinda biashara zetu.
Matajiri hawa nawapenda sana, kama utajiri wao sio wa kuhujumu juhudi zetu katika kuimarisha Utalii wetu na mbuga zetu za wanyama.
Haya, ngoja mwisho niwaulize swali: Hawa matajiri 5,553 Tanzania ni akina nani?
Tunawajua MO, Bakhresa na wengine wachache, ambao kwa hakika wameweka jitihada kubwa kwenye biashara zao kwa sehemu kubwa.
Tunaowajua matajiri Kenya, (2,900) wengi wao utajiri wao ni kutokana na siasa, kama akina Kenyatta, Moi, Biwott, n.k.,
na baadhi yao wengi wakiwa wafanya biashara, hasa wa asili ya kihindi.
Hawa wa hapa kwetu ni akina nani?
Mwisho, kuna mambo mengi ya kutompenda Magufuli, hasa yale ya msingi kabisa ya haki za watu na kuheshimu sheria zetu.
Lakini yapo mengine ambayo kama angeyafanya kwa utulivu mzuri, yangemletea heshima kubwa sana, kama mambo yanayohusu kulinda utajiri wa nchi yetu na haki za wananchi wa nchi hii kuneemeka na raslimali alizowajaalia Mwenyezi Mungu.
Sasa sijui kwa nini aliamua kuyafanya hata haya mazuri kwa kuvurugavuruga!