Kampunyenye
Member
- Nov 14, 2023
- 37
- 106
sina kumbukumbu kama tulikuchagua kuwa msemaji wetu.Hakuna asiyemkumbuka hata aliyekuwa anamchukia nadhani sasa akili zimemkaa sawa
[emoji1]Yaani unaweza kusikia king'ora na pikipiki ukapisha kumbe ni Mwijaku!
Usiwajibu hao vichwani hakuna kitu na ni malimbukeni wa magari,au hawajasafiri nchi za watu na wanendekeza matakataka ya dunia,kifupi hao ni mbwaKwani ikikaa nyuma ya ist itageuka iwe ist na yenyewe? Kodi ya hizo ist ndio inanunua hayo mavi-8. Hakuna upekee wowote.
Ilikuwa swala la muda tu baada ya lile tamko la kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.'UNANIJUA MIMI NANI' imerudi kwa kasi
Wakati wa magufuli hakukuwa na magari kibao ya serikali yaliyokuwa yakikiuka speed limits, yakitanua, kupiga ving’ora, kuwasha vimulimuli na kupita taa nyekundu? Wala bila kuwa kwenye misafara inayoongozwa rasmi?Mwarobaini ulikuwa Magu, mkauponda acha watumie barabara nawe ikikuuma tumia hivohivo
Rejea mke wa Mahiga na DeD kule Tanga nini kiliwapata.Wakati wa magufuli hakukuwa na magari kibao ya serikali yaliyokuwa yakikiuka speed limits, yakitanua, kupiga ving’ora, kuwasha vimulimuli na kupita taa nyekundu? Wala bila kuwa kwenye misafara inayoongozwa rasmi?
ambao hawana magariUnawakilisha Watanzania wengi hasa vijana wa sasa.
Wapuuzi wapo awamu zote ila ukiona watu wanaandika thread hizi ujue wamezidi.Wakati wa magufuli hakukuwa na magari kibao ya serikali yaliyokuwa yakikiuka speed limits, yakitanua, kupiga ving’ora, kuwasha vimulimuli na kupita taa nyekundu? Wala bila kuwa kwenye misafara inayoongozwa rasmi?
Sawa, lakini kuna siku yao ya arubaini. Ngoja siku ninaendesha kijiko saa za jioni utasikia nilivyowabomonda. Na mazoea ndio yanazaa matukio kama hili hapa chiniWako makini wamefunzwa dangerous driving huku wakilinda uhai wao na wa wengine
Dangerous driving au VIP speed driving ni course askari madereva hupewa aweza katiza hata mataa Kwa spidi 200 kilo mia Kwa saa asisababishe ajali
Sio vizuri kuwa block waweza kukutandika risasi sababu waweza kuhisi vibaya kuwa unawazuia operation zao za kijeshi ukawekwa Kundi la wahalifu ukauawa Bure na kagari kako used
Ukisikia ving'ora au wanakuja park pembeni au acha njia wazi wapite .Hata iwe asubuhi waweza kuwa wanawahi mikutano ya kujadili Hali ya usalama wa mkoa,wilaya au Nchi na kuwahi kupekeka ripoti Kwa Raisi Kwa maamuzi au wakubwa wao asubuhi hiyo
Kifupi Wewe wapishe tu
Ujeuri haulipi na kigari chako used
Suala la marehemu mke wa marehemu Mahiga nalijua. Hata kemeakemea, fokeafokea, tumbuatumbua za viongozi wengine nazıjua.Rejea mke wa Mahiga na DeD kule Tanga nini kiliwapata.
Na huo ndio ukweli, impunity. Katika hizi zama za Raisi Samia kumekuwa na impunity ya kutisha toka kwa viongozi wa serikali, polisi na Usalama wa Taifa. Sijui ni kwa kuwa raisi ni mwanamke?Suala la marehemu mke wa marehemu Mahiga nalijua. Hata kemeakemea, fokeafokea, tumbuatumbua za viongozi wengine nazıjua.
Ninachouliza, simply, ni hali halisi iliyokuwa barabarani enzi hizo. Rejea mada na comment niliyoiquote. Wakati wa Magufuli, hakukuwa na magari ya serikali/taasisi za umma na wakuu wao nje ya misafara rasmi yaliyokuwa yakikiuka sheria za barabarani with impunity?
Wanafikiri ajali itaangalia cheo chaoSawa, lakini kuna siku yao ya arubaini. Ngoja siku ninaendesha kijiko saa za jioni utasikia nilivyowabomonda. Na mazoea ndio yanazaa matukio kama hili hapa chini
View attachment 2883640
Kipindi cha Magufuli askari polisi walishagundua jinsi ya kupata vyeo kirahisi toka kwa Magufuli. Na akawa anameza tu kirahisi na kusemampandishe cheo huyu. Jamaa hadi walikuwa wanaambiana jinsi ya kutafuta vyeo vya haraka kwa kitu ambacho raisi atajua, na wakawa hata visa vingine wanatunga. Kwa mfano huyu askari wala hakutukanwa. Alijua alipata fursa ya kupanda cheo na akaitumia barabara, ma Magufuli akaingizwa cha wanawake!Suala la marehemu mke wa marehemu Mahiga nalijua. Hata kemeakemea, fokeafokea, tumbuatumbua za viongozi wengine nazıjua.
Ninachouliza, simply, ni hali halisi iliyokuwa barabarani enzi hizo. Rejea mada na comment niliyoiquote. Wakati wa Magufuli, hakukuwa na magari ya serikali/taasisi za umma na wakuu wao nje ya misafara rasmi yaliyokuwa yakikiuka sheria za barabarani with impunity?
Tumefikia sasa kwamba hapa nchini tuna watumiaji wa barabara wa aina mbili - Watanzania wa kawaida, na Watanzania "wenye nchi" ambao sheria za barabarani haziwahusu.
Hili kundi la "wenye nchi" ni wale ambao hawataki kabisa wabugudhiwe katika kuendesha juu ya spidi inayoruhusiwa, au wakae kwenye foleni wakiwa kwenye magari yao. Kikundi hiki kinatia ndani waendeshaji wa gari za ST, polisi na Usalama wa Taifa. Baadhi yao wamekuwa wakitumia zile namba nyeusi kama sababu ya wao kutaka kutumia barabara kwa namna tofauti na wengine. Na pia utaona wamejipa hizi taa za blue na nyekundu ambazo wanazitumia kujihalalishia ukiukwaji wa sheria barabarani.
Kwa mfano najiuliza, hata kama wewe ni waziri, au kigogo wa serikali, au Usalama wa Taifa, na unaendesha gari kwenda nyumbani, kitu gani kinakufanya wewe uwe na umuhimu zaidi wa kwenda haraka kwa mkeo na watoto wako kuliko Watanzania wengine? Kwani mkeo au watoto wako wana tofauti gani na mke au watoto wangu? Asietaka kufika nyumbani mapema baada ya kazi ni nani?
Nimeona matukio mengi sana ya uendesheshaji wa hatari sana barabarani ambao unafanywa na watu hawa. Kuna wakati nimehusika katika ajali kwa sababu Landcruiser ya STL ilikuwa inaendeshwa kwa kasi usiku upande usio wake, na niliposhika breki baada ya kuiona, gari iliyokuwa nyuma yangu ilinigonga. Hiyo STL iliondoka bila hata kusimama.
Juzi usiku nikitoka kazini niliona watu wa Usalama wa Taifa wakiendesha gari kwa fujo na kuhatarisha watumiaje wengine wa barabara, na waliposimamishwa na trafiki wakaonyesha utambulisho wa kuwa wafanyakazi wa Usalama wa Taifa na kuaruhusiwa waendelee. Dereva aliyekuwa nyuma yao akichukulia advantage iliambiwa aweke gari pembeni. Nina amini kwamba hawa watu walikuwa wakirudi nyumbani na waliendesha kwa fujo hizi kwa sababu hawakuvumilia kuwa kwenye foleni.
Hasa hapa Dar es Salaam, hiki kikundi kinachojiona wao ni wa pekee katika utumiaji wa barabara na wana haki zaidi ya watumiaji wengine, kinazidi kukua kila siku. Kuna siku madhara makubwa yatatokea, na najua yameshatokea, kutokana na hasira za watumiaji wengine barabarani. Kuna siku tutasikia watu wamekufa kwa sababu ya ujinga huu ambao nchi hii inauendekeza. Tunaimba hakuna aliye juu ya sheria lakini ni wazi wale wanaoongoza kutuimbisha wimbo huu wao hili haliwahusu, wanajiona wako juu ya sheria. Tunakoelekea si kuzuri.