Tanzania limejitokeza tabaka la "wenye nchi" ambao wanaona hawastahili kuendesha gari kwenye foleni na wana haki ya kutofuata sheria za barabarani

Tanzania limejitokeza tabaka la "wenye nchi" ambao wanaona hawastahili kuendesha gari kwenye foleni na wana haki ya kutofuata sheria za barabarani

wana heri hao wanaokimbia masaa yote kama farasi,kuliko wale wanaotukoboresha mahindi saa zima ili wapite wakati wako makwao bado wanakata gogo.

kwanza hawa hawasababishi upotevu wa muda,ila usumbufu na mshtuko tu ambao kiasi unavumilika.

kuna nchi kama germany,foren ikifunga gari zinatanua kuacha nafasi katikati kwa ajiri ya gari za dharula,ila bongo kwa vibarabara vyetu mtihani kiasi.
 
Mwarobaini ulikuwa Magu, mkauponda acha watumie barabara nawe ikikuuma tumia hivohivo
Wakati wa magufuli hakukuwa na magari kibao ya serikali yaliyokuwa yakikiuka speed limits, yakitanua, kupiga ving’ora, kuwasha vimulimuli na kupita taa nyekundu? Wala bila kuwa kwenye misafara inayoongozwa rasmi?
 
Ukiwa na V8 unaweza paki gari kwenye zebra crossing ukaenda shopping na ukarudi usisumbuliwe. Ukipaki IST utakwenda kuikomboa jiji au halmashauri.

Kuna siku (mwaka jana) nilikuwa pale taa za Ohio kuingia Alihasan Mwinyi road. Ikaja landcruiser 76 series inanamba nyeusi hata hazieleweki.

Kwa kuwa kulikuwa na foleni(kutokea Ohio kuingia Alihasanimwinyi) jamaa alipita opposite road akaingia barabara kuu halafu naona katikati akabadili mawazo akaichekecha fasta akapiga uturn kama anarudi tena Ohio, napo nikaona kaingia Zebra crossing akaelekea barabara ya bibititi.

Kimoyomoyo nikajisemea ingekuwa babywalker imefanya ushubwada huo tena kwenye red angepata tabu sana.

IMG_20240126_103407.jpg
 
Wakati wa magufuli hakukuwa na magari kibao ya serikali yaliyokuwa yakikiuka speed limits, yakitanua, kupiga ving’ora, kuwasha vimulimuli na kupita taa nyekundu? Wala bila kuwa kwenye misafara inayoongozwa rasmi?
Rejea mke wa Mahiga na DeD kule Tanga nini kiliwapata.
 
Wapuuzi wapo awamu zote ila ukiona watu wanaandika thread hizi ujue wamezidi.
 
Wako makini wamefunzwa dangerous driving huku wakilinda uhai wao na wa wengine

Dangerous driving au VIP speed driving ni course askari madereva hupewa aweza katiza hata mataa Kwa spidi 200 kilo mia Kwa saa asisababishe ajali

Sio vizuri kuwa block waweza kukutandika risasi sababu waweza kuhisi vibaya kuwa unawazuia operation zao za kijeshi ukawekwa Kundi la wahalifu ukauawa Bure na kagari kako used

Ukisikia ving'ora au wanakuja park pembeni au acha njia wazi wapite .Hata iwe asubuhi waweza kuwa wanawahi mikutano ya kujadili Hali ya usalama wa mkoa,wilaya au Nchi na kuwahi kupekeka ripoti Kwa Raisi Kwa maamuzi au wakubwa wao asubuhi hiyo

Kifupi Wewe wapishe tu

Ujeuri haulipi na kigari chako used
Sawa, lakini kuna siku yao ya arubaini. Ngoja siku ninaendesha kijiko saa za jioni utasikia nilivyowabomonda. Na mazoea ndio yanazaa matukio kama hili hapa chini

1706287773440.png
 
Rejea mke wa Mahiga na DeD kule Tanga nini kiliwapata.
Suala la marehemu mke wa marehemu Mahiga nalijua. Hata kemeakemea, fokeafokea, tumbuatumbua za viongozi wengine nazıjua.

Ninachouliza, simply, ni hali halisi iliyokuwa barabarani enzi hizo. Rejea mada na comment niliyoiquote. Wakati wa Magufuli, hakukuwa na magari ya serikali/taasisi za umma na wakuu wao nje ya misafara rasmi yaliyokuwa yakikiuka sheria za barabarani with impunity?
 
Na huo ndio ukweli, impunity. Katika hizi zama za Raisi Samia kumekuwa na impunity ya kutisha toka kwa viongozi wa serikali, polisi na Usalama wa Taifa. Sijui ni kwa kuwa raisi ni mwanamke?
 
Suala la marehemu mke wa marehemu Mahiga nalijua. Hata kemeakemea, fokeafokea, tumbuatumbua za viongozi wengine nazıjua.

Ninachouliza, simply, ni hali halisi iliyokuwa barabarani enzi hizo. Rejea mada na comment niliyoiquote. Wakati wa Magufuli, hakukuwa na magari ya serikali/taasisi za umma na wakuu wao nje ya misafara rasmi yaliyokuwa yakikiuka sheria za barabarani with impunity?
Kipindi cha Magufuli askari polisi walishagundua jinsi ya kupata vyeo kirahisi toka kwa Magufuli. Na akawa anameza tu kirahisi na kusemampandishe cheo huyu. Jamaa hadi walikuwa wanaambiana jinsi ya kutafuta vyeo vya haraka kwa kitu ambacho raisi atajua, na wakawa hata visa vingine wanatunga. Kwa mfano huyu askari wala hakutukanwa. Alijua alipata fursa ya kupanda cheo na akaitumia barabara, ma Magufuli akaingizwa cha wanawake!
 
Tumefikia sasa kwamba hapa nchini tuna watumiaji wa barabara wa aina mbili - Watanzania wa kawaida, na Watanzania "wenye nchi" ambao sheria za barabarani haziwahusu.

Hili kundi la "wenye nchi" ni wale ambao hawataki kabisa wabugudhiwe katika kuendesha juu ya spidi inayoruhusiwa, au wakae kwenye foleni wakiwa kwenye magari yao. Kikundi hiki kinatia ndani waendeshaji wa gari za ST, polisi na Usalama wa Taifa. Baadhi yao wamekuwa wakitumia zile namba nyeusi kama sababu ya wao kutaka kutumia barabara kwa namna tofauti na wengine. Na pia utaona wamejipa hizi taa za blue na nyekundu ambazo wanazitumia kujihalalishia ukiukwaji wa sheria barabarani.

Kwa mfano najiuliza, hata kama wewe ni waziri, au kigogo wa serikali, au Usalama wa Taifa, na unaendesha gari kwenda nyumbani, kitu gani kinakufanya wewe uwe na umuhimu zaidi wa kwenda haraka kwa mkeo na watoto wako kuliko Watanzania wengine? Kwani mkeo au watoto wako wana tofauti gani na mke au watoto wangu? Asietaka kufika nyumbani mapema baada ya kazi ni nani?

Nimeona matukio mengi sana ya uendesheshaji wa hatari sana barabarani ambao unafanywa na watu hawa. Kuna wakati nimehusika katika ajali kwa sababu Landcruiser ya STL ilikuwa inaendeshwa kwa kasi usiku upande usio wake, na niliposhika breki baada ya kuiona, gari iliyokuwa nyuma yangu ilinigonga. Hiyo STL iliondoka bila hata kusimama.

Juzi usiku nikitoka kazini niliona watu wa Usalama wa Taifa wakiendesha gari kwa fujo na kuhatarisha watumiaje wengine wa barabara, na waliposimamishwa na trafiki wakaonyesha utambulisho wa kuwa wafanyakazi wa Usalama wa Taifa na kuaruhusiwa waendelee. Dereva aliyekuwa nyuma yao akichukulia advantage iliambiwa aweke gari pembeni. Nina amini kwamba hawa watu walikuwa wakirudi nyumbani na waliendesha kwa fujo hizi kwa sababu hawakuvumilia kuwa kwenye foleni.

Hasa hapa Dar es Salaam, hiki kikundi kinachojiona wao ni wa pekee katika utumiaji wa barabara na wana haki zaidi ya watumiaji wengine, kinazidi kukua kila siku. Kuna siku madhara makubwa yatatokea, na najua yameshatokea, kutokana na hasira za watumiaji wengine barabarani. Kuna siku tutasikia watu wamekufa kwa sababu ya ujinga huu ambao nchi hii inauendekeza. Tunaimba hakuna aliye juu ya sheria lakini ni wazi wale wanaoongoza kutuimbisha wimbo huu wao hili haliwahusu, wanajiona wako juu ya sheria. Tunakoelekea si kuzuri.

Nchi yoyote yenye utawala wa hovyo, hizi ndio ishara na dalili zake
 
Back
Top Bottom