Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wako makini wamefunzwa dangerous driving huku wakilinda uhai wao na wa wengine
Dangerous driving au VIP speed driving ni course askari madereva hupewa aweza katiza hata mataa Kwa spidi 200 kilo mia Kwa saa asisababishe ajali
Sio vizuri kuwa block waweza kukutandika risasi sababu waweza kuhisi vibaya kuwa unawazuia operation zao za kijeshi ukawekwa Kundi la wahalifu ukauawa Bure na kagari kako used
Ukisikia ving'ora au wanakuja park pembeni au acha njia wazi wapite .Hata iwe asubuhi waweza kuwa wanawahi mikutano ya kujadili Hali ya usalama wa mkoa,wilaya au Nchi na kuwahi kupekeka ripoti Kwa Raisi Kwa maamuzi au wakubwa wao asubuhi hiyo
Kifupi Wewe wapishe tu
Ujeuri haulipi na kigari chako used
Kwa nini isikae? Ujinga huu hata wa Japan waliotengeneza hayo magari hawana, washamba wa Tz ndio wananyanyasana kwa pesa za wizi!Mkuu japo sijasoma ulichoandika lakini hata kama ni ww unataka Vieite ikae nyuma ya IST kwenye foleni pale Nelson Mandela road?
Punguza hasira...Tz sio nchi ya kua serious sana utkufa kwa pressureKwa nini isikae? Ujinga huu hata wa Japan waliotengeneza hayo magari hawana, washamba wa Tz ndio wananyanyasana kwa pesa za wizi!
Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Mkuu japo sijasoma ulichoandika lakini hata kama ni ww unataka Vieite ikae nyuma ya IST kwenye foleni pale Nelson Mandela road?
Shida n kwamba kundi Hilo huwez kutambua n muda gn wa naelekea kazn au wa naelekea nyumban. Mfano n watu wa usalama wa taifa Kuna matukio muda wowote anaweza kuhitajka ofsn hata muda ambao ww unafkir n muda sahihi wa watu kwenda majumban kupumzka.Tumefikia sasa kwamba hapa nchini tuna watumiaji wa barabara wa aina mbili - Watanzania wa kawaida, na Watanzania "wenye nchi" ambao sheria za barabarani haziwahusu.
Hili kundi la "wenye nchi" ni wale ambao hawataki kabisa wabugudhiwe katika kuendesha juu ya spidi inayoruhusiwa, au wakae kwenye foleni wakiwa kwenye magari yao. Kikundi hiki kinatia ndani waendeshaji wa gari za ST, polisi na Usalama wa Taifa. Baadhi yao wamekuwa wakitumia zile namba nyeusi kama sababu ya wao kutaka kutumia barabara kwa namna tofauti na wengine. Na pia utaona wamejipa hizi taa za blue na nyekundu ambazo wanazitumia kujihalalishia ukiukwaji wa sheria barabarani.
Kwa mfano najiuliza, hata kama wewe ni waziri, au kigogo wa serikali, au Usalama wa Taifa, na unaendesha gari kwenda nyumbani, kitu gani kinakufanya wewe uwe na umuhimu zaidi wa kwenda haraka kwa mkeo na watoto wako kuliko Watanzania wengine? Kwani mkeo au watoto wako wana tofauti gani na mke au watoto wangu? Asietaka kufika nyumbani mapema baada ya kazi ni nani?
Nimeona matukio mengi sana ya uendesheshaji wa hatari sana barabarani ambao unafanywa na watu hawa. Kuna wakati nimehusika katika ajali kwa sababu Landcruiser ya STL ilikuwa inaendeshwa kwa kasi usiku upande usio wake, na niliposhika breki baada ya kuiona, gari iliyokuwa nyuma yangu ilinigonga. Hiyo STL iliondoka bila hata kusimama.
Juzi usiku nikitoka kazini niliona watu wa Usalama wa Taifa wakiendesha gari kwa fujo na kuhatarisha watumiaje wengine wa barabara, na waliposimamishwa na trafiki wakaonyesha utambulisho wa kuwa wafanyakazi wa Usalama wa Taifa na kuaruhusiwa waendelee. Dereva aliyekuwa nyuma yao akichukulia advantage iliambiwa aweke gari pembeni. Nina amini kwamba hawa watu walikuwa wakirudi nyumbani na waliendesha kwa fujo hizi kwa sababu hawakuvumilia kuwa kwenye foleni.
Hasa hapa Dar es Salaam, hiki kikundi kinachojiona wao ni wa pekee katika utumiaji wa barabara na wana haki zaidi ya watumiaji wengine, kinazidi kukua kila siku. Kuna siku madhara makubwa yatatokea, na najua yameshatokea, kutokana na hasira za watumiaji wengine barabarani. Kuna siku tutasikia watu wamekufa kwa sababu ya ujinga huu ambao nchi hii inauendekeza. Tunaimba hakuna aliye juu ya sheria lakini ni wazi wale wanaoongoza kutuimbisha wimbo huu wao hili haliwahusu, wanajiona wako juu ya sheria. Tunakoelekea si kuzuri.