Tusiwe wepesi kushabikia vita. Tuwe wepesi kupata suluhu ya kidiplomasia. Vita ni kitu kibaya sana sana. Ni lazima kwanza kutafuta njia zote za kumaliza tatizo bila shari kabla ya kuingia vitani. Je, tumefanya jitihada zote za kuelewa chanzo na kutafuta ufumbuzi usio wa shari? Je, mnafikiri Wamalawi waliamka tu na kuamua mpaka uwe hapo? Tusomeni historia. Kama jambo ni rahisi hivi kwa nini halijatatulika toka enzi za Mwalimu?

