Tanzania Mbioni Kununua Umeme Kutoka Ethiopia

Serikali ya CCM achieni nchi kwa wenye uwezo wa kuiongoza. Kwa miaka 60 ya uhuru na rasilimali tulizonazo Tanzania sio ya kununua umeme nje.
Wenye uwezo ni kina nani hao?
 
Kwanini tununue wakati vyanzo tunavyo? Wakati ethiopia wanajenga 10,000mw sie tunajenga 2000mw.

Uganda na Bukina faso wanajenga 15,000mw kila mmoja sie tunawaza kuagiza kutoka ethiopia, makubwa!
Inasikitisha na kufikirisha sana!🙁
 
Mkuu haingii akilini hata kidogo!
 
Huo ndiyo mchanganuo wa vyanzo vya umeme kwenye gridi ya taifa Ethiopia (2019) ambayo inauzia majirani zake!

Hapa kwetu kuna "wadau" walikuwa wanakandia mradi wa HEP at umeme wa maji umepitwa wakati.

Leo nimesikia mnajisifia REA kuunganisha 90% ya vijiji badala ya kututajia idadi ya kaya kwenye hivyo vijiji!

Si tuliambiwa lengo la sensa ni serikali kupata taarifa za watu na makazi kwa ajili ya kuwapatia maendeleo,mbona hamzitumii hizo takwimu sasa?
 
Mkuu ukiwa na chuki usikose kumbukumbu, makubaliano ya kununua umeme kutoka Ethiopia hayakufanywa na Rais Samia wala Ndugu Kikwete.

Mkuu yalifanywa na Ndugu Magufuli Tarehe 04.04.2017 wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia alpoitembelea Tanzania. Kama kuna mtu wa kulaumiwa kuhusu hii biashara ni Magufuli parse!
 
Jpm atatakasa kila dhambi
 
Nchi yetu, ni nchi ya punguani. Ukiwa punguani hata ukajengewa daraja, utapita kusiko na daraja, kwenye maji ya kina kirefu, na kuteketea kwa kuzama.

Ukinyimwa akili, umenyimwa kila kitu hata kama utakuwa umezungukwa na kila aina ya neema.
Hivi ni Kweli tumenyimwa akili au TUNAJITOA AKILI?na kuweka tamaa mbele?
 
Ni mambo ya ajabu na aibu sana,sio kutamka Bali hata kupata tu Hilo wazo la kwenda kununua Huo umeme Ethiopia
Tuna viongozi ambao upeo wao wa kufikiri umefika mwisho, Kama wanaweza kukopa bilioni 70 kwa ajili ya njia za umeme ni aibu kwa Taifa. Diplomasia yetu no ya uchumi, wakiongea na mrusi anaweza kutengeneza umeme wa nyuklia kwa Bei rahisi, Rwanda, Kenya wote wanakimbilia huko.
 
Kwanini tununue wakati vyanzo tunavyo? Wakati ethiopia wanajenga 10,000mw sie tunajenga 2000mw.

Uganda na Bukina faso wanajenga 15,000mw kila mmoja sie tunawaza kuagiza kutoka ethiopia, makubwa!
Mmmmh karudie data za ethiopia tena, wamejenga kubwa kuliko sisi.
 
Ethiopia wanatumia maji ya mto nile unaoanzian ziwa Victoria lisilokauka kutengeneza umeme. Sisi ziwa lipo kwetu tunasubiri mvua zinyeshe vijaze mito ya pwani kufuata umeme huku tukiogopa ziwa letu kwa mkataba wa misri na izrael eti tusitumie maji hayo bila kibali Chao , wao wanazalishia umeme, wanafanya kilimo Cha umwagiliaji ila sisi tunavua dagaa ,mumwi na degere tuu
 
Badala ya Kununua Umeme wafanye mbinu ya Kununua Akili na Maarifa ya hao watunga Sera au Tukodishe viongozi toka nje tuwape contract (waliopo hakuna value for money tunazowalipa)
 
Kwa hiyo mkuu unataka kusema Tanzania tunaweza kuzalisha umeme kupitia ziwa Victoria?

Haya nimaajabu...!!
 
Kwa hiyo mkuu unataka kusema Tanzania tunaweza kuzalisha umeme kupitia ziwa Victoria?

Haya nimaajabu...!!
Shida Iko wapi? Ni rahisi Sana na tunapata umeme wa milele. Yatolewa hapo yalipo yanatengenezewa slope na bwawa jingine artificial
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…