worms
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 978
- 911
Habari ya uzima ndugu Mla panya.Pm yangu haifunguki afadhali hata sasa kidogo napata kujua mtu akiquote kiujumla App haiko sawa niliupgrade
Niliota ndoto mimi , Dada yangu na mume wake ambaye aliambatana na wadogo zake wawili wa kiume Tupi kwenye boti baharini au ziwani sikujua tunaelekea wapi.
Ila kuna muda Dada yangu akawa uchi kabisa bila nguo yoyote anatembea ndani ya boti.
Na kuna muda niliona kama Dada na mume wake wanafanya mapenzi,
Na baada ya muda ilikuwa Tupo ufukweni na Dada yangu anaogelea uchi kabisa
Tena muda mwingine alikuwa kavaa nguo halafu anaogelea.
Ghafla Nilijikuta nipo nyumbani kwa mzazi wangu, ilikuwa usiku nimeshika kioo na sijavaa shati, najiangalia naona kidevuni, singoni na mwanzo wa kifua kuna mabaka ya duara yaan mapunje nikawa nasema kinyozi aliyeninyoa ndevu mashine yake ni chafu imenipa magonjwa ya ngozi.
Ghafla nikajiona nipo nnje maeneo ya nyumbani Karibu na nyumba ya jirani yetu., nikaona anatoka na amebeba amebeba kuku kama watatu hivi, alivyoniona akanambia ninunue kuku wale, mi nikaenda waangalia nikawa nimempenda kuku tetea mweupe na nikamuuliza Mdogo wangu kuwa yule kuku ana umbo kubwa kuliko waliopo nyumbani tumchukue ili tuweze pata mbegu ya kuku mwenye umbo kubwa.( kiuhalisia nyumbani kwa mzazi wangu kuna ufugaji wa kuku).
Mwingine kati ya wale kuku alikuwa
Mdogo na wa Rangi nyeusi hakuwa na manyoya mengi Bali alikuwa na mwonekano wa ngozi yenye manyoya kama ya mbwa. Hivyo nikawa namshangaa.
Tulikuwa tumesimama pembeni ya maji yaliyotwama na yule Jamaa anayeuza kuku akawa anatumia mkono kubonyeza ardhi yenye maji kwa kutumia mkono na vidole vilikuwa vinazama ardhini , akasema kumbe hapa kuna chemchem ya maji na sio maji yametwama tu. Na mimi nikawa nafanya kama kama yeye kuchomeka vidole ile sehemu ili kujua kama vitadumbukia ardhini nikawa hivyo.
Ndoto iliishia hivyo na hayo ndo matukio muhimu ninayo yakumbuka.
Naomba tafsiri tafadhari mkuu