Tanzania mkombozi wetu wa maendeleo na uchumi ni katiba itayofata Sharia za Kiislam

Tanzania mkombozi wetu wa maendeleo na uchumi ni katiba itayofata Sharia za Kiislam

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Wengi tunaongelea katiba mpya sasa hivi, lakini hatuongelei iweje.

Mimi nashauri tena nasisitiza, hakuna katiba yoyote bora iliyotungwa na itakayotungwa na binaadam. Muumba wetu anatuelewa ubora wetu na mapungufu yetu ndiyo maana akatuwekea Muongozo ulio bora kabisa. Sharia.

Sharia haijaacha kitu katika mfumo wa maisha ya mwanaadam ya kila siku, kama hatujaifuata sharia ya Mwenyezi Mungu basi tusitegemee mafanikio maisha.

Watanzania tusiopenda ufisadi, wizi na ubadhirifu tuungane na tuitake katiba yetu iwe kwa mfumo wa sharia.

Tujadiliane.
 
Wengi tunaongelea katiba mpya sasa hivi, lakini hatuongelei iweje.

Mimi nashauri tena nasisitiza, hakuna katiba yoyote bora iliyotungwa na itakayotungwa na binaadam. Muumba wetu anatuelewa ubora wetu na mapungufu yetu ndiyo maana akatuwekea Muongozo ulio bora kabisa. Sharia...
Sawa Mkuu nimekupata
 
Aisee kama hutaki kuishi Tanzania, nenda Sudan , Egypt, Iran au Saudi Arabia wanaoshika Sharia Law.
Unajua ndani ya Sharia Law , Mkristo haruhusiwi kumuomba Mungu wake na adhabu yake ni kifo. Kuna Faida Gani kuwa na sheria isiyompa mtu uhuru wa kuabudu au kuamini anachokiamini.
 
Attachments

Kwa hiyo katiba hii ya sasa ya Tanzania inayochota sheria nyingi za kanisa zilizofundishwa pia ktk vyuo vikuu vya elimu ya juu kutoa wanasheria, mahakimu, majaji, wana psycholojia n.k imefeli nchini Tanzania.

Je kufeli kwake ni kutokana sisi kuchukua imani, mafundisho na falsafa mageni yaliyokuja kwa merikebu hivyo ni bora sasa kujaribu yale yaliyofika kwa majahazi au tuamue kuenzi mila tamaduni na elimu za busara za kiAfrika ambazo tumezipuuza na kuzitupa kama siyo kuzizika kabisa ?

Wachambuzi wa sheria za kisekula wanasema katiba na sheria nyingi za nchi mbalimbali zimechota na kukopa sheria za kanisa na kuziweka ndani ya katiba zao.

Hili si jambo geni kwani kanisa kama taasisi kongwe na kubwa ililazimu kuwa na sheria, kanuni na taratibu ili liweze kujiongoza kama taasisi na pia waumini wake .

Ilipokuja mataifa kuundwa wafalme na washauri wao walibaini umuhimu wa taifa au nchi kuwa na utaratibu wa jinsi ya kujiendesha na hivyo watu makini waliokuwa washauri wa wafalme au marais waliamua na kugundua kanisa tayari kwa karne nyingi walikuwa mbele kwa kujiundia na utaratibu wa kujiendesha na kutoa hukumu n.k n.k kuhusu masuala mbalimbali ...

Pepa ya mtanziko baina ya sheria za kidini na zile za ki-secular umefanyiwa utafiti mkubwa na wanazuoni wa University of Chicago nchini Marekani

University of Chicago
https://chicagounbound.uchicago.edu › ...PDF
Conflicts between Religious and Secular Law

by RH Helmholz · Cited by 16 — The canon law claimed the right to decide all such disputes. So did the courts of the King. The common law claimed...
 
Wengi tunaongelea katiba mpya sasa hivi, lakini hatuongelei iweje.

Mimi nashauri tena nasisitiza, hakuna katiba yoyote bora iliyotungwa na itakayotungwa na binaadam. Muumba wetu anatuelewa ubora wetu na mapungufu yetu ndiyo maana akatuwekea Muongozo ulio bora kabisa. Sharia...
Ujinga mtupu, Kenya wamefika wapi na hiyo katiba mpya zaidi ya makelele tu
 
Wengi tunaongelea katiba mpya sasa hivi, lakini hatuongelei iweje.

Mimi nashauri tena nasisitiza, hakuna katiba yoyote bora iliyotungwa na itakayotungwa na binaadam. Muumba wetu anatuelewa ubora wetu na mapungufu yetu ndiyo maana akatuwekea Muongozo ulio bora kabisa. Sharia.

Sharia haijaacha kitu katika mfumo wa maisha ya mwanaadam ya kila siku, kama hatujaifuata sharia ya Mwenyezi Mungu basi tusitegemee mafanikio maisha.

Watanzania tysiopenda ufisadi, wizi na ubadhirifu tuungane na tuitake katiba yetu iwe kwa mfumo wa sharia.

Tujadiliane.
Ni kweli ni Katiba Mpya kuhusu Uislam sina hakika maana Somalia, Senegal na Sudani wanazo
 
Aisee kama hutaki kuishi Tanzania, nenda Sudan , Egypt, Iran au Saudi Arabia wanaoshika Sharia Law.
Unajua ndani ya Sharia Law , Mkristo haruhusiwi kumuomba Mungu wake na adhabu yake ni kifo. Kuna Faida Gani kuwa na sheria isiyompa mtu uhuru wa kuabudu au kuamini anachokiamini.
Hapana, siyo kweli, hakuna hilo kwenye "sharia law". Hizo ni sheria za kukataza kuabudu ni za kibinaadam, zinakiuka sharia. Sharia nasema hakuna kukirihishana katika dini.
 
Back
Top Bottom