Kuna wale jamaa zangu matoyo wa chuga walishindana kwenda Moshi na kurudi asee walikufa kadhaa ile kitu sio
Nilicho jifunza Ukiwa unaendesha pikipiki kwa safari ndefu:
1. Hakikisha umebeba maji ya kunywa ya kutosha na unywe sana maji
2. Hakikisha usibane sana mdomo muda wote muda mwingi jitahidi kuachama au kuongea ongea tu inasaidia misuli isikaze na meno yasipate ganzi.
3. Vaa koti zito ambalo litazuia upepo kuingia mwilini
4. Vaa Buti na hilo buti usifunge kamba kama unafunga kiatu maana ukifunga kama unafunga kiatu utafanya ukaze na mzunguko wa damu utakuwa mdogo sana miguuni kupelekea kuchoka miguu
5. Hakikisha ndani vaa Vesti tu au nguo nyepesi hii inasaidia wewe uwe huru na mwili kuwa huru.. maana ukivaa shati zito afu ukavaa na koti juu mwili utakosa kupumua na kujikuta unachoka haraka.
6. Vaa helment yenye kioo tena kioo kigumu sana.
7. Utakapo hisi njaa au kiu hakikisha unaupatia mwili hitaji lake usilazimishe safari kwenda mbele wakati unahisi mwili kupata joto.
8. Usile hovyo hovyo.. nunua biskuti au chocolate na maji au zile Energy Drinks
9. Zingatia sana tena sana Side Mirror uwiiiii madereva Side Mirror ni muhimu kuliko ata chochote
10. Ukihisi umechoka pumzika tena pumzika kwa kujilaza chini na sio kusimama au kukaa (hii itakusaidia sana uone utamu wa safari)
11. Hakikisha kiuno chako usifunge na kukazaa.. kama suruali ya mkanda basi funga kiuno chako kiwe relax kabisa kisibanwe na chochote
12. Hakikisha haumwi chochote ata mafua yaani upo na afya njema
MENGINE NITAONGEZA YALE NILIYOJIFUNZA