Tanzania Motorbike Road Trip - Tanga | Safari ya Tanga

Tanzania Motorbike Road Trip - Tanga | Safari ya Tanga

Tumepiga hesabu sawa kabisa. Kwa km 334 ilipaswa itumike 10 ltrs tena ijazwe mara 1 tu
Tank yangu mimi ni lita 4.8 tuseme 5... nampango wa kufanya trip to Kilwa or Arusha.

Hivyo naombeni elimu ya mafuta katika KM kwa pikipiki yangu 110cc
 
Safi sana mkuu .. Tafuta Boxer 150 utaEnjoy zaid

Mm safari yangu ya mbali zaidi kwa pikipiki ni Dar - Chalinze -Dar
Nitanunua boxer mkuu..

Chalinze pia nimeenda kama mara mbili hivi na hii pikipiki yangu..

Mafuta unaweka mara moja tu unaenda na kurudi nayo
 
Kwa huo umbali mbona umetumia mafuta mengi sana kufika?

Pikipiki ilikua na shida gani?
Ha ha mengi tena? Wakati mi naona machache, hivi pikipiki ikiwa standard kwa hizi zenye cc125 inatakiwa iende km kwa lita?
 
Kuna jamaa mmoja alitoka Dar kwenda Tanga akitumia pikipiki ya zamani aina ya honda (daz) alisafiri akawa anakalia tako moja anachoka anageuza na lingine anachoka hatimae wazo la kuhairisha safari likamjia. Umbali wa alipotoka na anakoenda ni kama nusu kwa nusu akaishiwa pozi ikabidi aendelee ivo hivyo.

Akafika sehemu akakutana na kibao ‘punguza mwendo upepo mkali’ akapunguza huku ameshusha kioo cha kofia yake (helmet) akahisi ‘mbona hakuna huo upepo’ akarudisha kioo chake na kukanyaga moto. Punde si punde akasikia kama kitu kisichoonekana kimemsukuma kiasi cha kuweza kumviringisha chini ya bara bara ndipo akaelewa maana ya kile kibao cha onyo la upepo.

Alipofika Tanga wazo la kurudi na pikiki Dar likafa kifo cha kawaida…………..,,,,,,,, nitaendelea siku nyingine kumalizia habari hii kulingana na muda utakavyo ruhusu.
 
Wakuu Habari zenu, poleni n majukumu.

Ile safari yangu ya Tanga kutumia pikipiki yangu cc110 nimefanikiwa kwenda salama na kurudi salama kabisa.. Mungu ni Mkubwa.

Niliondoka Ijumaa iliyopita, nikashinda jumamosi kwa kufanya Mizunguko ya Town na kulijua jiji pamoja na kwenda kule Amboni kwenye Mapango Ya Amboni.

Katika kuthibitisha hilo nilifunga camera kwenye Helment yangu so each and everything kipo recorded.

Video ya Safari ya kutoka Dar hadi Tanga ipo youtube nimeweka kipande cha kutoka Dar hadi Mkata then nitaedit tena kipande cha kutoka Mkata hadi Point nyingine.

Kwa upande wangu hakuna nilichopoteza, kwanza nimeenjoy road trip, nimeona vitu vingi sana barabarani pia na kunipa udhoefu mkubwa sana wa kuwapa kipaumbele mabasi au gari linalotaka kukupita.

Kiufupi, nimefanya kile moyo wangu unakipenda na hakuna mtu aliyenilazimisha kufanya.

Asante kwa wote walionishauri Service bora ya Pikipiki.

KAMA UNASWALI KARIBU UNIULIZE.

ASANTE.View attachment 2527409
Umefanya kitu ambacho ni ndoto yangu,bado natafuta pesa ya kuweza kupata Yamaha Super Tenere 700cc. Iko siku
 
Wale machalii ni kama walikuwa kwenye racing moto mwingi sana+plus pombe tena zile ngumu.

Arusha to Moshi walifika fresh, wakati wa kurudi wakakumbwa na dhahama.
Wapumzike kwa amani.. pikipiki ukiwa mstaarabu barabarani utaishi miaka mingi ila ukileta mazoefu barabarani haki uchukui round
 
Wapumzike kwa amani.. pikipiki ukiwa mstaarabu barabarani utaishi miaka mingi ila ukileta mazoefu barabarani haki uchukui round
Tena pikipiki ni risk, side mirror za muhimu sana, vijana wa toyo huwa wanang'oa wanasema hazina swaga [emoji23][emoji23]

Laiti wangejua umuhimu wake wangeziheshimu ila ndio hivyo tena wamechagua fungu baya.
 
Kuna jamaa mmoja alitoka Dar kwenda Tanga akitumia pikipiki ya zamani aina ya honda (daz) alisafiri akawa anakalia tako moja anachoka anageuza na lingine anachoka hatimae wazo la kuhairisha safari likamjia. Umbali wa alipotoka na anakoenda ni kama nusu kwa nusu akaishiwa pozi ikabidi aendelee ivo hivyo.

Akafika sehemu akakutana na kibao ‘punguza mwendo upepo mkali’ akapunguza huku ameshusha kioo cha kofia yake (helmet) akahisi ‘mbona hakuna huo upepo’ akarudisha kioo chake na kukanyaga moto. Punde si punde akasikia kama kitu kisichoonekana kimemsukuma kiasi cha kuweza kumviringisha chini ya bara bara ndipo akaelewa maana ya kile kibao cha onyo la upepo.

Alipofika Tanga wazo la kurudi na pikiki Dar likafa kifo cha kawaida…………..,,,,,,,, nitaendelea siku nyingine kumalizia habari hii kulingana na muda utakavyo ruhusu.
Hahaha eti tako moja Hahaha
Kwenye experience yangu mimi toka Dar to Tanga na Tanga to Dar ni usikaze mwili yaani mwili uwe flexible kuanzia buti hadi nguo za juu.

Pili, kunywa maji mengi, maji yanasaidia kuondoa uchovu.

Tatu, Usile ukavimbiwa ndo uendeshe pikipiki.

Nne, ukihisi umechoka tafuta sehemu pumzika.

Tano, Kama unaendesha pikipiki kusafiri kwa kutalii.. usishindane mbio na magari hao pikipiki wenzako endapo wakikupita utajikuta unakata tamaa.. so wewe tembea mdogo mdogo tu pikipiki ni Mali yako utafika uendako.

Sita, siku moja kabla ya safari jitahidi upumzishe mwili, usifanye kazi ngumu.. yaani mwili ukiamka uwe na nguvu mpya na sio unaamka na uchovu afu safari Hahaha utaomba msaada wa maloli
 
Back
Top Bottom