Statics
JF-Expert Member
- Dec 29, 2017
- 394
- 1,015
Piki piki ganihio full tank Lita nne labda Bata vuzi
Kibao cha mbuzi hicho 110cc
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Piki piki ganihio full tank Lita nne labda Bata vuzi
Safi sana. Umeelezea vizuri mno. Asante kwa ku share safari yako.Maswali Mazuri sana.
1. Kuhusu Mafuta.. Tank langu la Mafuta ni lita 4.8.. wakati nipo Dar niliweka mafuta ya elfu 12000 ambayo nilipata full Tank.. pia ilibeba kidumu cha lita 5 ambacho hicho niliweka mafuta ya elfu 14 ambayo lita kama 4 hivi.
Mafuta yaliyo kwenye tank la pikipiki nimetembea nayo mpaka Mkata (niliposimama chai) nikajaza tena yaliyo kwenye kidumu lita 4.. lita 4 hiyo ikanifikisha hadi muheza ambako kwenye dumu niliweka elfu 13000 na kwenye pikipiki niliweka elfu 9.
Mafuta hayo toka hapo muheza yalinifikisha mpaka kiwanda cha cement kile ndipo nikachukua ya kwenye dumu ambayo niliingiza kwenye pikipki kama lita 2 hivi hivyo mpaka nafika TANGA nilikuwa na Mafuta ya kutosha kwenye pikipiki na kwenye Dumu ambayo niliyatumia kesho yake kwenda Amboni Cave
NB. Sikupenda niishiwe mafuta njiani ndo nijaze.. hivyo nilikuwa nikitembea kilomita kadhaa nasimama najaza
(Kuna mtu aliniambia usisubili mafuta yaishe sababu utakuwa unahalibu kableta (sijui nimepatia jina) ile ya kuvuta mafuta wakati upo safari ndefu
PIKIPIKI YANGU KWENYE SWALA LA MAFUTA INANUSA TU ILA HOFU YANGU NDO ILIYOPELEKEA NITEMBEE NA KIDUMU BUT BILA KUDUMU NINGEFIKA BILA WASIWASI NA MAFUTA (NDO SAFARI YANGU YA KWANZA)
Sijui bei yake XR, ila xl 125 inakuwaga arround 6.9M kama saba tu.Kwa hapo Dar es Salaam unaweza jua Honda xr 125cc yaweza kua bei gani? Iwapo Kuna duka linauza new bike
Honda Crf250 inatumia fuel injection haina carburetaAisee mbona mafuta machache sana na engine ni kubwa? Hii inavutia sana kusikia hivyo
Hivi ile ajali ilitokeaga maeneo gani
EssentialsNilinunua kariakoo ilikuwa 95000.. yeah kazuri sana.. humo niliweka:
1. Mswaki
2. Sabuni
3. Nguo za kuvaa
4. Shuka la kimasai (ili nilibeba endapo ikitokea itilafu ya kunifanya nilale polini)
5. Koti la Mvua
6. Sendo/Ndala za kushindia
7. Baadhi ya Documents ya pikipiki
8. Maji na Biskuti
Vyote vilikaa humo.. sema uwe mzuri kwenye kuvipanga, ukipanga vibaya unaweza kuona Truck dogo kumbe ni kubwa sana
Sawa Mkuu najichanga hapa nitanunua hiyo Yamaha ybrKwa kukazia zaidi, chukua Honda Ace 125cc au Yamaha ybr 125. Hizi zote ni imara, mafuta zinatumia kidogo pia huchoki kuendesha na zina afya zaidi. Kama ni mpenzi wa 5 speed ni vema ukachukua hii Yamaha ybr 125 gearbox yake ni 5 speed.
Hahaha mkuu uoga huo.. Bagamoyo hapo karibu tembea ata ufanye utalii wa ndani tuMkuu hivi ndio wewe kuna uzi ulisema unaishi chalinze na kufanya kazi dar mkuu? Kwenda na pikipiki hadi chalinze kila siku ni risk na gharam za mafuta bora kupanga mjini.
Mi pia natumia pikipiki sana kwenye mizunguko yangu mjini ila sijawahi kutoka nayo hata bagamoyo tu
Hivi mkisema risk ni nini? Mimi kiukweli kusafiri kwangu na pikipiki sijaona risk yoyote sasa sijui nyie mnasema risk gani?Sio mm mkuu ...
Upo sahihi umbali mrefu huo kwa pikipiki ni risk sana...
Chalinze nilienda mwezi uliopita... ila bagamoyo nishaenda sana kama mara 5 ivi....
Mkuu risk zile njia zenye traffic kubwa wakati mwingine wenye magari hawaheshimu pikipiki. Unaweza kuwq upo upande wako kabisa lakin akakuletea hukohuko sasa kidogo unakuwa mwangalifu na ndio hapo inakuwa risk.Hivi mkisema risk ni nini? Mimi kiukweli kusafiri kwangu na pikipiki sijaona risk yoyote sasa sijui nyie mnasema risk gani?
Nachojua Risk ni wewe na uendeshaji wako only that.. nyie mnasema risk gani hiyo?
Uh pole sana Mkuu na Mungu Mwema kwa kuwa ulipona Salama..Mkuu risk zile njia zenye traffic kubwa wakati mwingine wenye magari hawaheshimu pikipiki. Unaweza kuwq upo upande wako kabisa lakin akakuletea hukohuko sasa kidogo unakuwa mwangalifu na ndio hapo inakuwa risk.
Mfano imewahi nitokea kwenye mapishano ya morogoro road pale jangwani ilipo yard ya mwendokasi. Mimi natoka fire naenda magomeni jamaa yupo na corolla anatoka magomeni akatishe kwenda jangwani kule ilipo jengo la Yanga. Sasa kikawaida ilipaswa asuburi nipite kabla yeye hajakunja kuja kuingia barabara yangu.
Licha ya kumpa warning kwa kuwasha taa na kupiga horn lakin nikastuka huyu hapa tayari kashaingia. Nikifunga brake kali lakin haikuzuiwa kuanguka japo sikuu hata kidogo naye hakuumia. Nilivunja indicator ya pembeni.
Mara nyingine ilikuwa barabara ya bandari mi natoka Kigamboni jamaa atoka bandari ndani aingie barabarani same mistake anaforce aingie kama nyoka tu.