Iyo story yote ilikua na faida gani?
kama hauna cha kuchangia kaa kimya.
Unatoa taarifa au unajigamba ili uonekane yaliyomo yamo?

Sometimes be humble hutapungukiwa na kitu.
Jamani, makasiriko yote haya ya nini ndugu zangu? Lols

Nilikutana na thread yenye heading “Kupotea kwa Internet, umepata changamoto gani?” Ndio nikaelezea changamoto yangu, shida iko wapi?

Naona Mods wamebadili heading, mmenishangaza sana as haikuwa katika namna mliyoichukulia nyinyi.

Anyways, poleni.
 
Mtaachana tu ipo siku

Utani tu mkuu
 
East Africa yote inapata mtandao from sub marine cables (mkongo wa bahari),Kenya,UG,TZ,Rwanda,Burundi,Somalia,Djibouti,Sudan zote 2.
Ukikatika huko baharini inaathiri kl mahali
 
Mimi swali langu ni:
Kwanini mitandao ya simu haijatuma sms kwa wateja wao kuwa kunashida ya kitaifa ya internet?
Matokeo yake kama mtu anamiliki line zaidi ya moja anajikuta anatumia hela kununua data kwenye lines zingine angali tatizo ni lile lile na mwisho wa siku kama ilinunua data ya muda mfupi itaisha bila yeye kuweza kutumia.

Naelewa kunanjia mbadala ya raia kujua kinachoendelea, ila mwisho wa siku mpaka huyu mtu anapata uelewa ameshatumia hela kununua kitu ambacho hatokitumia.
 
Halotel wako vizuri wakiboresha mtandao wao hawa jamaa watatisha.
 
Wanawaza pesa tu hawa na msg zao za usumbufu kila dakika. Mambo muhimu haya hawaangalii.
 
Leo naona Picha hazifunguki natumia Vodacom. Jana nilishindwa kununua Mtandaoni kwa Visa card.
 
Watu bwana kwahiyo mnataka kusema haya ndio maandalizi ya 2025 ili ikifika wakifanya yao muambiwe mbona mmezoea kila wakati samaki wanakula nyaya huko baharini? nchi ina mambo sana hiyo.
 
watu bwana kwahiyo mnataka kusema haya ndio maandalizi ya 2025 ili ikifika wakifanya yao muambiwe mbona mmezoea kila wakati samaki wanakula nyaya huko baharini? nchi ina mambo sana hiyo.
Huo ndio ukweli wa mambo hata tusifichane kwakweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…