Tanzania na China zasaini mkataba wa uendelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Mwanza - Isaka

Halafu atokee kichaa mmoja aje kutuambia reli inajengwa kwa pesa za ndani wakati ni mwendo wa kuongeza deni la taifa hadi basi.
 
Halafu atokee kichaa mmoja aje kutuambia reli inajengwa kwa pesa za ndani wakati ni mwendo wa kuongeza deni la taifa hadi basi.

Nikwambie kitu mkuu, uhuru wa kujieleza husizidi mipaka, you can agree to disagree without offending anyone - unapo mwita binadamu mwenzako mwenye dhamana ya kuongoza Taifa kwamba ni kichaa unamaanisha nini? husifikiri maneno yako ya kashfa hatujui yanamlenga nani - jitahidini kuheshimu binadamu wenzenu hata kama hukubaliani na sera zake, huna haja ya kutumia an abrasive language.
 
I dont fk your soft skin
 
Waturuki waliokuwa wanaimbwa kama Wimbo wa Taifa wameshidwa kazi? Wakati Waturuki wakipewa Dar-Moro kwa pesa zetu, viongozi wetu hawakuwaona Wachina? Miradi mingi ya Awamu hii ni substandard kwa sababu ya makandarasi dhaifu, je kugawa Mradi mmoja vipandevipande kila kipande na mkandarasi wake, haiwezi kuwa ndo sababu? TAZARA imejengwa na Wachina na ina umri karibu miaka 50, je imeleta faida gani kwa Taifa? Kipande cha Dar-Moro mbona hata hakiimbwi wala hakitajwi kimefika wapi na lini Walugulu wataanza kufaidi matunda ya Awamu ya Tano? Dar-Moro ni km 300 na ilikuwa ikamilike Novemba, 2019, Mwanza-Isaka ni km 340, ni lini Wasukuma wapiga kura wataachana na Musukuma Bus Service? Maswali mengi!
 

Mbona maswali yako ni totally incoherent! Kama kuna walio kuelewa wanisaidie.

Labda nizungumzie kuhusu TAZARA, ni kweli inaendeshwa ki hasara hasara bahati mbaya Serikali zetu mbili hazijawahi kulivalia njunga suala hili - TAZARA inaendeshwa kisiasa zaidi kuliko kibihashara - binafsi nilisha guduwa kwamba Serikali ya Zambia na Tanzania zinaoneana aibu, hakuna anae kubali kumfunga paka kengere!

Kuna mambo mengi ya kipuuzi yanatendeka bila ya Serikali zetu hasa ya Tanzania kuchukuwa hatuwa yoyote, mfano: kuna mantiki gani kwamba Managing Director wa Tazara lazima awe Mzambia hata kama hana sifa, kipengele hicho kimekuwa grossly misused, wanatumika kuuza mali zote za Tazara upande wa Tanzania siyo upande wa Zambia - waliuza Kurasini material base ikiwemo aridhi kubwa na majengo/Godowns yenye thamani kubwa waliwauzia Wahindi kwa hela zakutupwa, wakamega sehemu ya aridhi ya Tazara iliyojengwa nyumba za wafanyakazi huko Temeke Maganga karibu na Vetenary wakuwauzia Kampuni ya Oil Com, wakaenda TAZARA DSM Railway station sehemu ya Cargo base wakamkodisha Mhindi sijui kwa terms zipi, kinacho sikitisha zaidi ni uuzaji/ukodishaji wa chunk kubwa ya aridhi karibu na karakana ya TAZARA mnunuzi/mkodishaji kajenga depot kubwa ya kuhifadhi containers, kibaya zaidi alipora jengo lililo kuwa linatumika kitengeneza/service fuel injector pumps za locomotives na ku-calibrate injector nozzles - machines/equipment za gharama kubwa na umuhimu wa pekee zikang'olewa na kutupwa wapi sijui, hizi ni hujuma za wazi wazi - hivi sasa jengo hilo linatumiwa na Mhidi huyo kama ofisi ya kuratibu ma-containers yake, yaani yeye na-washirika wake wanaona Ofisi ni ya muhimu zaidi kuliko jengo na mali za TAZARA, ujasiri huu anaupata wapi??

Juzi juzi hapa nilipita sehemu hiyo tajwa nilishangaa kukuta sio kwamba Mhindi anahifadhi ma-containers tu bali amekwenda mbali zaidi na kujenga kituo kikubwa cha uuzaji mafuta, awezi kujenga kituo cha kuuza mafuta bila ya kumilikishwa aridhi kwanza! Swali ni,je, nani anampatia kibali cha kupora aridhi ya Tazara, jengo la Taraza, kujenga kituoa cha mafuta na kufanya apendalo as if Serikaki yetu imekwenda likizo?

Binafsi nashauri Dk. Magufuli,Wizara ya uchukuzi, PCCB, na vyombo vingine vya dola fatilieni suala hili kwa karibu zaidi ili kubaini undani wake na kuchukuwa hatua stahiki, hujuma za mali za TAZARA upande wa Tanzania ni kubwa mno - upande wa Zambia hawauzi chochote, kila kitu kipo intact kabisa.

Hapa nimezungumza mambo machache tu yanayo kwamisha utendaji mzuri wa Shirika, tatizo ni hujuma na kutojari ustawi wa TAZARA - Shirika likitaka kuendeshwa kiufanisi liondokane na kasumba ya kuendesha shirika kisiasa, hakuna mantiki yoyote ya kusema Mkurugenzi mkuu lazima atoke Zambia, kaimu wake Mtanzania, Mkurugenzi wa fedha Mzambia, Mkurugenzi wa Traffic Mzambia yaani mission critical posts zote wanapewa Wazambia hapo unategemea nini - tutavuna tunacho panda, lakini cha ajabu Board members wa Tazara upande wa Tanzania sio kwamba hilo hawalioni hawasemi chochote wapo kimya kabisa.

Kwa kumakizia risala yangu ndefu nataka kukufahamisha kwamba utendaji mbovu wa TAZARA wasilahumiwe Wachina, wachawi wa reli ya Tazara ni sisi wenyewe - maswali mengine kuhusu ujenzi wa SGR nimeshindwa kukujibu kwa sababu sijui unataka kujua nini!!
 
Dar Mbeya malori ya mizigo mengi mno. Yana haribu barabara.

Wenye magari ya malori wapewe hisa katika TAZARA mizigo yote isafirishwe kwa reli.

Wataalamu pigeni hesabu za kiuchumi mtuambie kama ni muafaka kuacha TAZARA iwe kama ilivyo.
 
Hii reli kwenda Mwanza Badala ya Kigoma ni uamuzi haramu, wa kifisadi na upendeleo mtupu.
Mizigo ya kwenda congo, burundi inauhakika, lakini ya uganda kupitia mwanza haina uhakika, kwanza huyu mpinzani WINI wa Uganda, akishinda basi uhusiano wa Tz na uganda kwisha
 
Naisoma google mwanza to isaka nimegundua isaka IPO Shinyanga. Sijajua na kujuzwa KIPANDE cha Dodoma-shiyanga isaka kama tayari kina mkandarasi au kinajengwa. Naomba kujuzwa taf
 
Sasa mshaija, leteni hii kupitia wabunge wenu serikali itaona cha kufanya...
 
Huyu kakazania kuwa China ni tajiri wakati serikali ya China officially ilikataa UN kuiingiza kwenye kundi la nchi tajiri Duniani baada ya US kutaka China iingizwe kwenye mataifa tajiri.

Maelezo ya China ni kuwa pato lake kubwa linatokana na uwingi wa watu lakini pato la mchina mmojammoja bado ni dogo na wachina wengi ni maskini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa nini hatuona umuhimu wa kuifikisha SGR kigoma kwenye business kubwa na DRC tukaamua kuipeleka mwanza kwanza?
huko ndiko hakuna biashara? ukiacha mengine idadi kubwa ya watanzania ipo mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mara,Mwanza,Kagera,Geitana Tabora umbari kutokamikoa hii hadi bandari ya salama ni kati km 700 hadi 1300,tofauti yabei za bidhaa kati ya Dar na mikoa hii ni kubwa mno kutokana na gharama za usafirishaji kwa kuwaona watanzania hawa na kuwahudumia ni sahihi zaidi kuliko kuangalia biashara na Kongo kwanza lakini korido hiyo iko kimkakati vizuri sana sio kidogo kwani kuna Rwanda,Burundi na Uganda. ukifikisha reli Mwanza tayari umefika uganda kwani tayari pale pana meri za kubeba mabehewa kwenda Uganda,lakini pia mzigo ukifika Isaka huo tayari umefika Rwanda,Burundi maana toka isaka hadi kwenye mpaka ni safari ya masaa tu.
 
Congo ni wa kwetu atake asitake that why tumemuweka kiporo pia kuna bandari ya kalema ipo ili tuteke soko la Congo

kuhusu bob kushinda akate uhusiano na Tz hicho kitu hakiwezekani Tz sera zake za mambo ya nje hazifungamani na upande wowote that peter mutharika alikuwa zinaunga na jiwe na alivyoshindwa Rais wa sasa wa malawi akawa pia ni rafiki wa jiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…