Tanzania National Football Team (Taifa Stars) | Special Thread

Tanzania National Football Team (Taifa Stars) | Special Thread

Msumbiji wachumba tu! Mimi hawa Zimbabwe ndo nilikua nawahofia zaidi

Haya umesahau walivyotukojolea kimoja tu taifa mwaka ulee! Wote vichwa chini? Msumbiji wana techniques nyingi za mchezo na wana profenals wengi kuliko zim. Hivyo linahitajika tizi la uhakika!
 
Hongera taifa stars, kazi ndo kwanza inaanza

Haya mahongera mnawapa hawa vijana katika hatua za awali kiasi hiki watabweteka waanze kujion abab kubwa. Inawezekana tumewaotea zim tu, mambo yao hayako vizuri. Ila kazi bado ni kubwa sana. Tuwatoe msumbiji halafu ndio twende makundi yale ya timu nne. Bado sana jamani, waambieni amejitahidi lakini bado!
 
Haya mahongera mnawapa hawa vijana katika hatua za awali kiasi hiki watabweteka waanze kujion abab kubwa. Inawezekana tumewaotea zim tu, mambo yao hayako vizuri. Ila kazi bado ni kubwa sana. Tuwatoe msumbiji halafu ndio twende makundi yale ya timu nne. Bado sana jamani, waambieni amejitahidi lakini bado!
subiri magazeti na tv za bongo mpaka watajaa viburi na mechi inayofuata wanajisahau nakufungw kama 10,taifa star sina imani nao kabisa
 
Mkuu Vin Diesel jamaa anajitahidi sana kutoa updates humu, rais yeye, yan kila kitu ajitahidi awape watu wengine kazi kama hii ya mitandaoni sana hapa JF si wana ofisa wa habari TFF sijui kazi yake nini..


nina imani Jamal Malinzi atasoma na kufanyia kazi hili, wenzake wanalalamika sana.
 
Last edited by a moderator:
Nikiwa mfuatiliaji na mkereketwa mkubwa wa soka la Bongo najitokeza kupongeza timu yetu Taifa Stars kwa kuweza kuitupa nje ya mashindano Zimbabwe. Ushindi huu unakuja wakati ambapo wapenzi wengi wa soka walishakata tamaa juu ya Taifa Stars hasa kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya iliyopata kuanzia mwishoni mwa 2013 na kipigo cha aibu kutoka timu ya Burundi cha 3-0 wakati wa sikukuu za Muungano.

Ushindi huu kwa kiasi kikubwa umeletwa na kocha mpya Mart Nooij kwa sababu baada ya matokeo yale mabaya dhidi ya Burundi alichukua uamuzi mgumu na wa ujasiri 'kupiga teke' mpango wa maboresho ya Taifa Stars kinyume na waajiri wake na akaamua kuchagua wachezaji wazoefu aliowataka mwenyewe. Huu ulikuwa ni uamuzi mkubwa na ambao kwa kocha asiyejiamini angelazimika kuendelea na maboresho angalau kuwaridhisha wakuu wake wa kazi na kwa hakika ingekula kwetu!

Pili ameonekana kuwa na mbinu tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mechi. Kitendo cha kumpanga Erasto Nyoni katika kiungo ktk mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi na hata wakati wa mechi yenyewe dhidi ya Zimbabwe kimeonesha ni jinsi gani kocha anavyozitumia vizuri mechi za kirafiki badala ya kukariri. Nyoni ni mzuri kwa kucheza mipira ya kichwa, ana nguvu ya kugombania mipira katikati ya uwanja, mtulivu na ana control nzuri japo tatizo lake kubwa ni kutokuwa na kasi, na mbaya zaidi sometimes anapoteza concentration. Jana alifanya kazi nzuri ya kuilinda defence na kupambana vilivyo na mabavu ya kiungo cha Zimbabwe. Hata hivyo alikuwa Nyoni hakufanya vzr sana kwenye kuiendesha timu hasa anapopokonya mipira na hii ni kutokana na kutokuwa kasi sana na pia tabia yake ya kuchelewa kutoa pasi. Anapaswa kulifanyia kazi hili

Niseme nini kuhusu Cannavaro? Kwa karibu misimu miwili iliyopita beki huyu kisiki amekuwa hana uhakika wa namba ktk Taifa Stars na wakati mwingine huwa hachaguliwi kabisa. Lkn kocha huyu mpya mara moja kamwita kwenye timu yake na ni nani hajaiona faida ya Cannavaro kwenye timu kuanzia ukabaji, uongozi, na hata kufunga magoli muhimu.

Hata ingizo la Said Morad kwenye mechi ya jana ilikuwa maalumu kwa ajili ya kucheza krosi zilizokuwa zinapigwa mara kwa mara kuelekea Stars lilionyesha kuwa na manufaa sana kwa sababu Morad alicheza karibu krosi zote mara tu baada ya kuingia. So mchezaji maalumu ktkt wakati maalumu na kwa sababu maalum.

Kwa kumalizia nasema tena huyu kocha anaonesha dalili nzuri kwa kucheza mpira wa matokeo badala ya mpira wa anao anao. Ktk mechi nne alizosimamia timu so far, hajaonyesha unyonge na anaonekana kuwaelewa vzr wachezaji wetu na kuwatumia kwa kadiri ya uwezo wao na mahitaji ya timu. Apewe ushirikiano wa kutosha anaweza kutufikisha mahali
 
Nawafiki, ingawa kwa tafsiri ya baadhi ya vigogo wa TFF, ushirikiano ni huo kupangiwa timu!
 
Mheshimiwa Rais naona sasa hivi unapatikana huku vizuri nakupongeza sana kwa hilo mimi swali langu ni lile lile ni vigezo gani vilitumika kuwapata makocha wasaidizi wa Taifa Stars yani SALUM MAYANGA na PATRICK MWANGATA?
Patrick na Salum waliteuliwa na kamati ya utendaji tokana na mapendekezo ya kamati ya ufundi,ndio utaratibu.Mwalimu Nooij hajalalamika kuhusu utendaji wao,hivyo naamini wako ok.
ulikwa na ushauri mbadala Malafyale?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa Africa hiyo kitu ni ngumu sana..mwaka 2012 washabiki wa timu ya taifa ya south waliandamana juu ya ishu kama hiyo.

Inabidi yawepo makubaliano ya pande zote mbili, na sio uamuzi wa nchi moja.
ManDla jr haki za kurusha matangazo ya TV Afcon sio za nchi zinazocheza,n
haki ni za shirikisho la mpira barani Afrika CAF,jana CAF waliwauzia Azam haki hizo.....and its not cheap.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana ManDla jr na hongera pia


Mechi ya Msumbiji itakuwa safi sana:
Kwa sababu Nooj aliwahi kuwafundisha hawa jamaa.

Unakumbuka hoja zangu mbili nilizouambia wiki chache zilizopita?
#1. timu inahitaji stability. Kikosi kisibadilishwe mara kwa mara.
#2. tunahitaji kusogea hadi top 100.

big up JAMAL🙂
 
Jamal Malinzi

Rais niwie radhi kama haya maswali yangu yameshaulizwa

Hiyo mechi inayofuata dhidi ya Msumbiji inachezwa lini? mechi ya kwanza na ya marudiano

Je mna mikakati gani kuhusu hizo mechi 2? kwani nina imani timu yetu ikiandaliwa vizuri ina weza kuitoa Msumbiji [ingawa hao the mambas ni wazuri}

Mwisho kuna hii kitu nakisikiaga sana kwenye media {Fitina za Mpira}, hiki kitu kama kinawezekana kitumike sana haswa kwa mechi yetu ya nyumbani ili kwa vyovyote vile tushinde mechi hiyo.
 
Msumbiji "the mambas"


waliwahi kututoa enzi zile za Maximo; tena hapa hapa taifa. Ilikuwa ndo mechi ya kwanza ya kimashindano kuchezwa kwenye Uwanja Mpya wa Taifa.. Walitufunga goli 1 kwa bila.

mechi kati ya Msumbiji na Tanzania huwa ina matokeo magumu; natumaini Nooj atalifanyia kazi hili. Kwa sababu anawajua vizuri majirani zetu hawa.
 
Pole sana ManDla jr na hongera pia

Nashukuru sana Rais wangu wa TFF, Lakini nakupongeza kwa kuwa na timu muda
wote Zimbwabwe. Na Mkuu Msumbiji naona kama ni wagumu kuliko Zimbabwe inabidi
tujipange mapema pia.

Mechi za majaribio zinajenga sana timu jitahidi kuongea na wadhani wa timu ya Taifa (Kilimanjaro)
tukacheze mechi nje ya Tanzania Mkuu. Waeleza umuhimu wa mechi ya Msumbiji watakuelewa tuu.

La mwisho, mechi ya Msumbiji sisi Tanzania tutaanzia mechi nyumbani na kumalizia Msumbiji au
tutaanzia Msumbiji na kumalizia hapa nyumbani??? Nimeuliza hivyo ili kama Shirikisho muweze kuchukua
tahadhari mapema, yasije tokea yale ya Zimbabwe kufungia nje ya Hoteli.

Mandla.
 
Back
Top Bottom