Nikiwa mfuatiliaji na mkereketwa mkubwa wa soka la Bongo najitokeza kupongeza timu yetu Taifa Stars kwa kuweza kuitupa nje ya mashindano Zimbabwe. Ushindi huu unakuja wakati ambapo wapenzi wengi wa soka walishakata tamaa juu ya Taifa Stars hasa kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya iliyopata kuanzia mwishoni mwa 2013 na kipigo cha aibu kutoka timu ya Burundi cha 3-0 wakati wa sikukuu za Muungano.
Ushindi huu kwa kiasi kikubwa umeletwa na kocha mpya Mart Nooij kwa sababu baada ya matokeo yale mabaya dhidi ya Burundi alichukua uamuzi mgumu na wa ujasiri 'kupiga teke' mpango wa maboresho ya Taifa Stars kinyume na waajiri wake na akaamua kuchagua wachezaji wazoefu aliowataka mwenyewe. Huu ulikuwa ni uamuzi mkubwa na ambao kwa kocha asiyejiamini angelazimika kuendelea na maboresho angalau kuwaridhisha wakuu wake wa kazi na kwa hakika ingekula kwetu!
Pili ameonekana kuwa na mbinu tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mechi. Kitendo cha kumpanga Erasto Nyoni katika kiungo ktk mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi na hata wakati wa mechi yenyewe dhidi ya Zimbabwe kimeonesha ni jinsi gani kocha anavyozitumia vizuri mechi za kirafiki badala ya kukariri. Nyoni ni mzuri kwa kucheza mipira ya kichwa, ana nguvu ya kugombania mipira katikati ya uwanja, mtulivu na ana control nzuri japo tatizo lake kubwa ni kutokuwa na kasi, na mbaya zaidi sometimes anapoteza concentration. Jana alifanya kazi nzuri ya kuilinda defence na kupambana vilivyo na mabavu ya kiungo cha Zimbabwe. Hata hivyo alikuwa Nyoni hakufanya vzr sana kwenye kuiendesha timu hasa anapopokonya mipira na hii ni kutokana na kutokuwa kasi sana na pia tabia yake ya kuchelewa kutoa pasi. Anapaswa kulifanyia kazi hili
Niseme nini kuhusu Cannavaro? Kwa karibu misimu miwili iliyopita beki huyu kisiki amekuwa hana uhakika wa namba ktk Taifa Stars na wakati mwingine huwa hachaguliwi kabisa. Lkn kocha huyu mpya mara moja kamwita kwenye timu yake na ni nani hajaiona faida ya Cannavaro kwenye timu kuanzia ukabaji, uongozi, na hata kufunga magoli muhimu.
Hata ingizo la Said Morad kwenye mechi ya jana ilikuwa maalumu kwa ajili ya kucheza krosi zilizokuwa zinapigwa mara kwa mara kuelekea Stars lilionyesha kuwa na manufaa sana kwa sababu Morad alicheza karibu krosi zote mara tu baada ya kuingia. So mchezaji maalumu ktkt wakati maalumu na kwa sababu maalum.
Kwa kumalizia nasema tena huyu kocha anaonesha dalili nzuri kwa kucheza mpira wa matokeo badala ya mpira wa anao anao. Ktk mechi nne alizosimamia timu so far, hajaonyesha unyonge na anaonekana kuwaelewa vzr wachezaji wetu na kuwatumia kwa kadiri ya uwezo wao na mahitaji ya timu. Apewe ushirikiano wa kutosha anaweza kutufikisha mahali