HOTUBA YA MHESHIMIWA JMK IMEPUNGUZA PRESHA ZA WATANZANIA NA KUREJESHA IMANI?
Jibu mpaka dakika hii ni bado, mmeshaona kitu bado, mmeshasikia kitu bado, mmesharejesha imani kwa CCM, Bado!
TANZANIA kila kitu kizuri. Jina zuri. Uchumi mzuri. Heshima ya kimataifa nzuri. Muungano mzuri. Muafaka mzuri. Na sisi wenyewe wazuri.Sasa tatizo letu ni nini?
Hotuba ya Mheshimiwa bado inaendelea lakini bado sijaona lolote lipya isipokuwa uigizaji na usanii mzuri wa kusafisha jina chama na wanasiasa wake ambao wananuka uoza mtupu.
Anatueleza nini? Eti mabilioni yote haya kukawa hamna ukaguzi na huku mnasema Benki Kuu na nchi ina viongozi. Mbona tunataniana jamani.
Hakika kutaka uongozi ni kitu kingine na kuweza uongozi ni habari mpya na ngeni kabisa pia.
Tunangoja sasa kusikia jinsi gani kina Marehemu watachukuliwa hatua na walio hai kuachiwa huru waendelee na mbwembwe zao!