Kwani hamjui kuwa kampuni lililojichotea bilioni 40 kati ya hizo linaitwa Kagoda Agricultural LTD?
Huenda sasa Kagoda itaanza kujihusisha na kilimo rasmi tutajuaje?
Ule mpango wa kuijadili hotuba ya Kikwete Bungeni umezimwa. taarifa kutoka huko, zilizothibitishwa na Spika Sitta, zinaeleza kuwa mjadala wa hotuba hiyo hautakuwepo hivi sasa, labda katika bunge la Novemba.
Taarifa ni kuwa mjadala huo umefutwa kwa sababu hotuba ya rais hadi hivi sasa bado haijakamilika. Alisema maneno mengi wakati wa hotuba ambayo yapo nje ya hotuba yake iliyokuwa imeandikwa. Imeshindikana kuingiza hayo maneno mengine kwenye hotuba na kuwahi kutengeneza vitabu vya hotuba ambavyo vingegawiwa kwa wabunge
Kazi ni kubwa sana tuliyo nayo. Kadri siku hizi zinavyoenda ubaya wa hotuba ya JK unabadilika kutoka ya ovyo kuwa mbaya, ya kawaida na hatimaye itafaika mahala itaonekana kuwa ilikuwa nzuri, hasa watakapomaliza kuijadili wabunge. Naambiwa wabunge wa CCM wamejipanga kuimwagia sifa hotuba hii kuanzia aya ya kwanza hadi ya mwisho. Na wameambiwa yeyote atakayejifanya kuikandia, 2010 ataula wachuya, na majamaa, kwa kuwa hayana ujasiri, yamenywea nywee!
Kuna makampuni mengi ya kisanii ambayo yamejivisha vazi la KILIMO na kupitia vazi hilo wamejichotea mabilioni na bado wanaendelea kuchota. Kipindi cha nyuma kulikuwa na watu kama CHAVDA na mashamba ya mkonge, METL mkonge na korosho, KAGODA Agricultural Ltd na mabilioni ya EPA, Sumbawanga Agricultural and Animal Food Industries Ltd (SAAFI ltd) inayomilikiwa na Mh. Mzindakaya ambayo nayo imepata bilioni kadhaa kutoka Serikalini. Kwa mtizamo wangu naona kuhamisha salio la EPA kwenda kwenye mfuko wa ruzuku ya mbolea na TIB kwa ajili ya mikopo kwa wakulima kuwa ni njia nyingine ya kutengeneza mazingira ya kumaliza hilo salio. Jaribu kufikiri awali hela zilikuwa NBC ikaonekana hakuna usimamizi mzuri wakahamishia BOT. BOT usimamizi umekuwa sio mzuri wanapeleka TIB/mfuko wa mbolea, lakini panya wanaotafuna hizo hela ndio hao hao wanaozibeba kwa ajili ya kuzitafutia hifadhi/matumizi mazuri. I am worried kwamba haya ni maandalizi/janja ya kupata hela za kutumia kwenye uchaguzi wa 2010!!!.
Kama Wabunge wako serious na wameshagundua janja ya Mh, wasihangaike kujadili bla bla zake alizotoa pale ukumbini. Spika kawaonyesha njia kwa kusimama na kumwambia wazi kwamba anafanya ndivyo sivyo. Kwa pamoja nao wangesimama na kutamka wazi kwamba MH IMETOSHA, NCHI YETU INAELEKEA KWENYE NJIA YA MBIGIRI, HATUNA IMANI NA UTENDAJI WAKO, TUNAOMBA UONDOKE ILI NCHI/TAIFA LETU LIONGOKE NA KUPATA NJIA ILIYO SAHIHI.
Taifa liko njia panda, kuna taarifa za kukatisha tamaa zaidi eti huenda EL akarudishwa kwenye cabinet soon.....
Viongozi wa CCM ni wapumbavu wa kwanza duniani!!! Ni mpaka lini wataendelea kufikiria kuwa njia ya kutatua tatizo ni kutolizungumzia/ku_assume halipo wakati lipo?? CCM isikwepe kutekeleza majukumu yake na badala yake ijaribu kuwaonyesha eti watu wanaozungumzia matatizo yaliyopo ni wakosaji wa adabu. Mtu kukiri kuwa una tatizo fulani ndio hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye uvumbuzi. Hii Kikwetemania au Rostamanian iliyoingia Tanzania ya sasa ya kufanya mambo kisanii itakuja tutokea puani Watanzania siku moja!!!!
Mtiririko wa hotuba yake umejaa mikanganyiko mitupu na ujanja ujanja wa kukwepa kuwajibika. kwa mfano alipojua watu watauliza hizo pesa zimewekwa kwenye akaunti ya benki ipi akasema kwamba fedha iliwekwa kwenye akaunti maalum hazinaAlisema pesa za EPA zipelekwe kwa wakulima kupitia TIB......tatizo litakuja kwenye accessibility ya wakulima hao kwenye hizo pesa (bond problems).....kitakachotokea.........ni mafisadi wale wale kwa kofia ya ukulima ndio watakao access kwa haraka zaidi......its good window of opportunity to the same mafisadi..............
Nadhani the best way ilikuwa ni kusaidia Vyama vya ushirika (kama bado vina-exist)direct
duh hiyo ni kuahirisha hukumu tu ila ngoma ipo palepale!
hivi haliwezi kutokea lijitu tuu lipindue hii nchi ilichukue na kuadabisha kila mshenzi alietesa wanchi kuanzia mjumbe wao wa nyumba 10 10 jamani... mimi nitamsapoti tuu