Kuna makampuni mengi ya kisanii ambayo yamejivisha vazi la KILIMO na kupitia vazi hilo wamejichotea mabilioni na bado wanaendelea kuchota. Kipindi cha nyuma kulikuwa na watu kama CHAVDA na mashamba ya mkonge, METL mkonge na korosho, KAGODA Agricultural Ltd na mabilioni ya EPA, Sumbawanga Agricultural and Animal Food Industries Ltd (SAAFI ltd) inayomilikiwa na Mh. Mzindakaya ambayo nayo imepata bilioni kadhaa kutoka Serikalini. Kwa mtizamo wangu naona kuhamisha salio la EPA kwenda kwenye mfuko wa ruzuku ya mbolea na TIB kwa ajili ya mikopo kwa wakulima kuwa ni njia nyingine ya kutengeneza mazingira ya kumaliza hilo salio. Jaribu kufikiri awali hela zilikuwa NBC ikaonekana hakuna usimamizi mzuri wakahamishia BOT. BOT usimamizi umekuwa sio mzuri wanapeleka TIB/mfuko wa mbolea, lakini panya wanaotafuna hizo hela ndio hao hao wanaozibeba kwa ajili ya kuzitafutia hifadhi/matumizi mazuri. I am worried kwamba haya ni maandalizi/janja ya kupata hela za kutumia kwenye uchaguzi wa 2010!!!.
Kama Wabunge wako serious na wameshagundua janja ya Mh, wasihangaike kujadili bla bla zake alizotoa pale ukumbini. Spika kawaonyesha njia kwa kusimama na kumwambia wazi kwamba anafanya ndivyo sivyo. Kwa pamoja nao wangesimama na kutamka wazi kwamba MH IMETOSHA, NCHI YETU INAELEKEA KWENYE NJIA YA MBIGIRI, HATUNA IMANI NA UTENDAJI WAKO, TUNAOMBA UONDOKE ILI NCHI/TAIFA LETU LIONGOKE NA KUPATA NJIA ILIYO SAHIHI.