Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Kwani hamjui kuwa kampuni lililojichotea bilioni 40 kati ya hizo linaitwa Kagoda Agricultural LTD?

Huenda sasa Kagoda itaanza kujihusisha na kilimo rasmi tutajuaje?

Sure, Mkuu Mk, hii inaleta maana duh! tunapigwa changa la macho kila kona, noma kweli!
 
Ukisikiliza hotuba yake utasikia wakati alipokuwa akionglea EPA alisema hivi .... hekla si za serikali na watu walikuwa wanazichota .... ila tu ni kwa bahati mbaya mmoja wao aliamua kutoa siri!.

Swali langu je Jk alipaswa kusema ni kwa bahati mbaya au nzuri???


mimi ninadhani alipaswa kusema ni kwa bahati nzuri kwa kuwa yeye anawakilisha serikali, je mnasemaje?
 
Ule mpango wa kuijadili hotuba ya Kikwete Bungeni umezimwa. taarifa kutoka huko, zilizothibitishwa na Spika Sitta, zinaeleza kuwa mjadala wa hotuba hiyo hautakuwepo hivi sasa, labda katika bunge la Novemba.
Taarifa ni kuwa mjadala huo umefutwa kwa sababu hotuba ya rais hadi hivi sasa bado haijakamilika. Alisema maneno mengi wakati wa hotuba ambayo yapo nje ya hotuba yake iliyokuwa imeandikwa. Imeshindikana kuingiza hayo maneno mengine kwenye hotuba na kuwahi kutengeneza vitabu vya hotuba ambavyo vingegawiwa kwa wabunge

Usanii wa serikali ya ya msanii JK na Bunge uchwara bado unaendelea!!!
 
Kazi ni kubwa sana tuliyo nayo. Kadri siku hizi zinavyoenda ubaya wa hotuba ya JK unabadilika kutoka ya ovyo kuwa mbaya, ya kawaida na hatimaye itafaika mahala itaonekana kuwa ilikuwa nzuri, hasa watakapomaliza kuijadili wabunge. Naambiwa wabunge wa CCM wamejipanga kuimwagia sifa hotuba hii kuanzia aya ya kwanza hadi ya mwisho. Na wameambiwa yeyote atakayejifanya kuikandia, 2010 ataula wachuya, na majamaa, kwa kuwa hayana ujasiri, yamenywea nywee!

Hilo ndilo tatizo kubwa tulilonalo Watanzania, kutegemea wengine wapigane vita yako na ya wote. Wacha Wabunge wafanye wanaloweza kufanya, wewe Je? Mimi je? Wao je? sisi je? Each one of us has a role to play kuonyesha kuwa hotuba hii haikufikia matarajio ya Watanzania!
 
Kwa style hii ya kuendesha mambo kwa kubania bado serikali yetu ina safari ndefu ya kuitimiliza sera ya uwazi na ukweli! Ni hodari kwa changa la macho!!!!!!
 
duh hiyo ni kuahirisha hukumu tu ila ngoma ipo palepale!
 
Yaani kikwete alivungavunga watu kwa mambo ambayo hayamo katika vitabu vy serikali kusudi apate waandamanji wa kumwunga mkono. duh!!!!!!!!!!!
 
Kuna makampuni mengi ya kisanii ambayo yamejivisha vazi la KILIMO na kupitia vazi hilo wamejichotea mabilioni na bado wanaendelea kuchota. Kipindi cha nyuma kulikuwa na watu kama CHAVDA na mashamba ya mkonge, METL mkonge na korosho, KAGODA Agricultural Ltd na mabilioni ya EPA, Sumbawanga Agricultural and Animal Food Industries Ltd (SAAFI ltd) inayomilikiwa na Mh. Mzindakaya ambayo nayo imepata bilioni kadhaa kutoka Serikalini.

Kwa mtizamo wangu naona kuhamisha salio la EPA kwenda kwenye mfuko wa ruzuku ya mbolea na TIB kwa ajili ya mikopo kwa wakulima kuwa ni njia nyingine ya kutengeneza mazingira ya kumaliza hilo salio. Jaribu kufikiri awali hela zilikuwa NBC ikaonekana hakuna usimamizi mzuri wakahamishia BOT.

BOT usimamizi umekuwa sio mzuri wanapeleka TIB/mfuko wa mbolea, lakini panya wanaotafuna hizo hela ndio hao hao wanaozibeba kwa ajili ya kuzitafutia hifadhi/matumizi mazuri. I am worried kwamba haya ni maandalizi/janja ya kupata hela za kutumia kwenye uchaguzi wa 2010!!!.

Kama Wabunge wako serious na wameshagundua janja ya Mh, wasihangaike kujadili bla bla zake alizotoa pale ukumbini. Spika kawaonyesha njia kwa kusimama na kumwambia wazi kwamba anafanya ndivyo sivyo.

Kwa pamoja nao wangesimama na kutamka wazi kwamba MH IMETOSHA, NCHI YETU INAELEKEA KWENYE NJIA YA MBIGIRI, HATUNA IMANI NA UTENDAJI WAKO, TUNAOMBA UONDOKE ILI NCHI/TAIFA LETU LIONGOKE NA KUPATA NJIA ILIYO SAHIHI.
 
Mjadala hotuba ya Kikwete bungeni 'wazimwa'



* Wabunge walipania kukataa mafisadi EPA kuongezewa muda
* Suala la Muungano, Serikali ya Tanganyika nalo lilikamiwa

Na Joseph Lugendo, Dodoma

SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw.
Samuel Sitta, amesema wabunge hawatapata muda kujadili
hotuba ya Rais Jakaka Kikwete aliyoitoa bungeni Alhamisi iliyopita kutokana na kutokuwepo uwezekano wa hotuba hiyo kuwa tayari wiki hii ambayo ni ya mwisho kwa Mkutano wa Bunge unaoendelea.

Bw. Sitta, alisema hayo bungeni jana muda mfupi baada ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kumaliza hotuba yake kushukuru ile iliyotolewa na Rais wa Visiwa vya Komoro, Bw. Ahmed Abdullah Mohamed Sambi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano jana.

Alifafanua kwamba kuchelewa kukamilika kwa hotuba hiyo
kwa ajili ya mjadala bungeni, kumetokana na usomaji wa Rais
Kikwete ambaye aliongeza baadhi ya mambo ambayo hayakuwepo kwenye hotuba ya maandishi aliyokusudia kuitoa.

Kutokana na nyongeza hiyo ya Rais katika hotuba yake, Bw.
Sitta alisema Ofisi ya Bunge imelazimika kupeleka hotuba
iliyokuwa imerekodiwa katika mitambo ya taarifa rasmi za
Bunge (Hansard) Ikulu ili ikapangiliwe katika mtiririko ambao
Rais Kikwete alikusudia.

Alifafanua kwamba kutokana na safari ya Rais Kikwete nje ya nchi,
imesababisha hotuba hiyo ambayo ilitakiwa kuchapishwa na
kugawiwa kwa wabunge kwa ajili ya rejea ya mjadala kuchelewa hivyo kutokuwahi kuwekwa kwenye ratiba za wiki hii ambayo ni ya mwisho kwa Mkutano huu wa Bunge la Bajeti.

Mjadala huo ulitarajiwa kuibua maswali mengi kuhusu uamuzi
wa Rais Kikwete kuwaongezea muda waliochota sh. bilioni 133
isivyo halali katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA)
katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa mujibu wa hotuba ya Rais Kikwete, baadhi ya
waliochota fedha hizo kwa kutumia nyaraka za kugushi,
pamoja na kunyang'anywa mali zao yakiwemo magari, nyumba
na kufungwa akaunti zao, waliomba muda ili waendelee kurejesha fedha hizo.

Vilevile, suala Zanzibar kuwa nchi lingeweza kuibua mjadala kwani ingawa Rais Kikwete alitoa ufafanuzi kuwa Zanzibar si nchi kimataifa na katika baadhi ya mambo ya Muungano na kwa upande mwingine ina mamlaka ya nchi katika baadhi ya mambo ya nje, mtazamo huo sio uliokuwepo ndani ya Bunge.

Kabla ya kutolewa kwa ufafanuzi wa Rais kuhusu hadhi ya Zanzibar kuwa nchi, wabunge wa upande wa Tanzania Bara walikuwa na mtazamo wa kutaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ivunjwe na ibaki serikali moja ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wa wabunge wa Zanzibar walipendekeza kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika na kuundwa kwa Mfumo wa Muungano wa Serikali tatu yaani Serikali ya Zanzibar, Tanganyika na ile ya Muungano.

Vilevile hoja ya wanasiasa kutakiwa kukabidhi biashara zao kwa mdhamini kabla ya kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nyadhifa za kisiasa majimboni mwaka 2010, ni moja ya hoja ambazo zilitarajiwa kuongeza chachu ya mjadala hasa ikizingatiwa baadhi ya wabunge maarufu ni wafanyabiashara.
 
Kuna makampuni mengi ya kisanii ambayo yamejivisha vazi la KILIMO na kupitia vazi hilo wamejichotea mabilioni na bado wanaendelea kuchota. Kipindi cha nyuma kulikuwa na watu kama CHAVDA na mashamba ya mkonge, METL mkonge na korosho, KAGODA Agricultural Ltd na mabilioni ya EPA, Sumbawanga Agricultural and Animal Food Industries Ltd (SAAFI ltd) inayomilikiwa na Mh. Mzindakaya ambayo nayo imepata bilioni kadhaa kutoka Serikalini. Kwa mtizamo wangu naona kuhamisha salio la EPA kwenda kwenye mfuko wa ruzuku ya mbolea na TIB kwa ajili ya mikopo kwa wakulima kuwa ni njia nyingine ya kutengeneza mazingira ya kumaliza hilo salio. Jaribu kufikiri awali hela zilikuwa NBC ikaonekana hakuna usimamizi mzuri wakahamishia BOT. BOT usimamizi umekuwa sio mzuri wanapeleka TIB/mfuko wa mbolea, lakini panya wanaotafuna hizo hela ndio hao hao wanaozibeba kwa ajili ya kuzitafutia hifadhi/matumizi mazuri. I am worried kwamba haya ni maandalizi/janja ya kupata hela za kutumia kwenye uchaguzi wa 2010!!!.

Kama Wabunge wako serious na wameshagundua janja ya Mh, wasihangaike kujadili bla bla zake alizotoa pale ukumbini. Spika kawaonyesha njia kwa kusimama na kumwambia wazi kwamba anafanya ndivyo sivyo. Kwa pamoja nao wangesimama na kutamka wazi kwamba MH IMETOSHA, NCHI YETU INAELEKEA KWENYE NJIA YA MBIGIRI, HATUNA IMANI NA UTENDAJI WAKO, TUNAOMBA UONDOKE ILI NCHI/TAIFA LETU LIONGOKE NA KUPATA NJIA ILIYO SAHIHI.

Ngoja nikupe siri kaka,

Hao jamaa waliozirudisha watapewa tena hizo pesa "zao" kupitia huo mfuko kwa kutumia makampuni hewa tena.

Ngoja na mimi nikaanzishe langu niliite Fairplayer Agricultural products. Ltd Nitakuwa nalima "hewani" na ku process agricultural products!. Dili hilo changamka wewe!

Ni usanii tu kaka.
 
Watanzania tuwapumbavu sio CCM. Mwakyembe alivyosema watanzania sio mabwege tena sasa tutasemanini sisi wasaniiiiiiiiiiiiii haswa. Watanzania wasanii wakumbwa wazazi wanaibia watoto wao bila kujua. sikilizeni nyimbo za Master ebbo. Mimi mmasai bwana.
 
Taifa liko njia panda, kuna taarifa za kukatisha tamaa zaidi eti huenda EL akarudishwa kwenye cabinet soon.....
 
huwezi kupoteza muda kujadili utumbo. ni bora wameacha kuijadili
 
Taifa liko njia panda, kuna taarifa za kukatisha tamaa zaidi eti huenda EL akarudishwa kwenye cabinet soon.....

Haiwezi kuwa ajabu kwa jinsi mambo yanavyoenda. Wanaamini kabisa hamna wa kupinga hilo. Lets wait and see
 
Ama kweli raisi tumempata!
Watu mpaka wanashindwa kupata exactly alichoongea!!!!!!!!!!!!!!!????????????
Thank God ata sikuisikiliza ile hotuba bse kwani it was far below my expectations.
 
Viongozi wa CCM ni wapumbavu wa kwanza duniani!!! Ni mpaka lini wataendelea kufikiria kuwa njia ya kutatua tatizo ni kutolizungumzia/ku_assume halipo wakati lipo?? CCM isikwepe kutekeleza majukumu yake na badala yake ijaribu kuwaonyesha eti watu wanaozungumzia matatizo yaliyopo ni wakosaji wa adabu. Mtu kukiri kuwa una tatizo fulani ndio hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye uvumbuzi. Hii Kikwetemania au Rostamanian iliyoingia Tanzania ya sasa ya kufanya mambo kisanii itakuja tutokea puani Watanzania siku moja!!!!

asante sana ndugu, yani hujui nikiasi gani nimepata hasira wakati nasoma ujumbe wako, maana ni kweli kabisa ulicho kisema yani tunakoelekea ni kubaya na wao wanajifanya kama hawaoni au wameshapanga kuwa awataikimbia nchi na sisi tubaki kuuana kama wanyama pori
 
Alisema pesa za EPA zipelekwe kwa wakulima kupitia TIB......tatizo litakuja kwenye accessibility ya wakulima hao kwenye hizo pesa (bond problems).....kitakachotokea.........ni mafisadi wale wale kwa kofia ya ukulima ndio watakao access kwa haraka zaidi......its good window of opportunity to the same mafisadi..............

Nadhani the best way ilikuwa ni kusaidia Vyama vya ushirika (kama bado vina-exist)direct
Mtiririko wa hotuba yake umejaa mikanganyiko mitupu na ujanja ujanja wa kukwepa kuwajibika. kwa mfano alipojua watu watauliza hizo pesa zimewekwa kwenye akaunti ya benki ipi akasema kwamba fedha iliwekwa kwenye akaunti maalum hazina

Swali: Hiyo akaunti ilifunguliwa lini na aliyeifungua na kwa maelekezo ya nani ,kwa madhumuni ya shughuli ipi na watia saini wake ni kina nani(Signatory)

Na hizo fedha zilipelekwa hazina zikiwa fedha taslimu au zilipelekwa kwa hundi na kama kwa hundi ni nani hao walisaini hizo hundi.

Pili kama fedha zipo kuna haja gani ya kuanzisha mfuko eti wakija wenyewe kuzidai wapewe,nadhani fedha hazipo na kinachofanyika ni kutafuta hela kutoka kwenye fedha za walipakodi, mwisho wa siku isemwe rais kasimamisha matumizi ya hela za EPA.wakati huo watakuwa wamesharudisha fedha walizojikopesha kwa mlango wa nyuma.

Mambo ya kudai kuna watu hali zao "ngumu sana" lakini hawasemi ni uzushi mwingine,kama wapo si angewasema ili wananchi wathibitishe kama kweli mali zao zimetaifishwa.Hapo ni kutengeneza jinamizi la fikra kwa watanzania.

kama hao watu wapo basi angetaja walikuwa wanamiliki nini na wapi na hivyo walivyokuwa wanavimiliki vina thamani ya shilingi ngapi. kwa kweli Tangu Omary Mahita aliposema yeye akiendelea kuwa IGP CUF haitashika madaraka ya nchi hii, nikakosa imani kabisa na Jeshi la polisi.

Na hivi sasa tunaambiwa kwamba naye Tibaigana kupitia CCM anataka kugombea kiti cha ubunge Muleba. hao ndiyo waliofanya utafiti kwa miezi kadhaa kuhusu swala la EPA
 
hivi haliwezi kutokea lijitu tuu lipindue hii nchi ilichukue na kuadabisha kila mshenzi alietesa wanchi kuanzia mjumbe wao wa nyumba 10 10 jamani... mimi nitamsapoti tuu
 
duh hiyo ni kuahirisha hukumu tu ila ngoma ipo palepale!


nakwambia hakuna kulala ngoja moto uwake atanywea mwenyewe, JK ni muoga sana we ngoja apigwe jambajamba kidogo tu na wabunge utaona mwenyewe ana badili kauli shenz*
 
hivi haliwezi kutokea lijitu tuu lipindue hii nchi ilichukue na kuadabisha kila mshenzi alietesa wanchi kuanzia mjumbe wao wa nyumba 10 10 jamani... mimi nitamsapoti tuu

Chondechonde ndugu yangu tusije tukafikia level ya Somalia!
 
Back
Top Bottom