Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Nadhani huu ni mjadala mzuri na nimeupenda sana. Katika suala hiili kuna mambo ambayo hatuna budi kuyaangalia moja moja ili kuweza kukielewa kitu kizima. Mara nyingi tunaposikia "Mradi wa Vitambulisho vya Taifa" tunachukulia kuwa ni kitu kimoja bila kuangalia vipande vyake.

a. Ni utambulisho wa nini?
Kuna mtu aliuliza swali hili huko nyuma kuwa hivi vitambulisho hasa vinachotaka kutambulisha ni kitu gani? Kama ni Taifa kama inavyotajwa sasa pasi za kusafiria tayari zipo hivyo ni duplication ya services kwani pasi inamtambulisha x,y kuwa ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, kitambulisho kingine ni cha nini basi? Tuzingatie kuwa hivi karibuni serikali ilifanya mabadiliko ya vitambulisho vyetu na kuvileta vya "kisasa" ambavyo navyo ni kama vinatumia teknolojia bora zaidi yenye kuzuia kughushi n.k. So, kama sivyo vya kutambulisha taifa vinatambulisha nini?

b. Vitambulisho vya Uraia?
Hili nalo ni kama (a) hapo juu. Kama vitambulisho hivi ni vya uraia na siyo vya kila mtu aliyemo ndani ya Taifa hilo basi bado mradi unaohitajika ni wa vitambulisho vya wageni! kwani Raia tayari wana vitambulisho vyao (pasi). Hivyo, basi kama ni kutaka kujua wageni hili nalo ni rahisi zaidi kutekeleza kwani tayari tuna vituo vya kuingilia nchini na tayari wageni wanapokuja wanakuja na pasi zao n.k Hivyo, kwetu sisi ni kutengeneza mfumo tu wa kawaida wa kuonesha mgeni ni nani na akiwa nchini lazima atembee na kitambulisho hicho. Utaona basi kuwa wageni ni wachache sana kuliko raia na hivyo mradi wa kuwatambulisha wageni nchini mwetu utakuwa wa gharama ndogo zaidi!

c. Mradi wa Kutambulisha Wakazi?

Yawezekana lengo la mradi huu ni kumtambulisha pia mkazi wa eneo fulani. Kwamba ndani ya hizo kadi kutakuwa na anuani ya mtu anaishi wapi. Hili hata hivyo litakuwa gumu sana kwani watu wanahamahama sana, na watu wengi wanaishi katika nyumba za kupanga ambazo si zote zina anuani tofauti ya chumba kwa chumba (apartments) ukiondoa anuani ya nyumba moja.

Kwa mfano, Mtaa wa Mkwepu kuna Nyumba ya Bw. Sadallah ambayo ndani yake kuna wapangaji wanne. Nyumba hiyo kwa nje imeandikwa namba 17xx. Hata hivyo wakazi wake wenye familia zao wakiandika kwenye kitambulisho wanasema kuwa wanaishi kwenye nyumba namba 17xx, lakini zaidi ya hapo hakuna taarifa zaidi. Hata hivyo, jirani ya nyumba hiyo kuna jamaa naye amejenga kibanda chake na hapo ni kwake lakini hakijapimwa na hivyo hana anuani. Kwa muda mrefu ndugu yetu huyo amekuwa akiwaelekeza watu kuwa anaishi "nyumba tatu toka kwa mzee Sadallah". Huyu tutamtambulisha vipi kwenye kadi yetu hii kwamba anaishi wapi?

Hapa basi utaona kuwa kutahitajika mradi mwingine mkubwa wa kupima na kutoa mfumo mpya wa namba za anuani kwa kila jengo na ofisi ambayo inatumiwa na watu au matumizi yoyote rasmi. Kwa kufanya hivyo, mradi mpya wa 'MFUMO MPYA WA ANUANI ZA MAKAZI NA OFISI" utaanzishwa.

lakini wakati huo huo tunatambua kuna halmashauri ambazo zinatoa vitambulisho vya aina mbalimbali kwa wafanyabiashara, wakazi n.k Hivyo utaona Halmashauri kwa kiasi kikubwa ndizo zenye nafasi kubwa na ya kwanza ya kukutana na watu wa kawaida na wageni kuliko serikali kuu. Hivyo, mpango au mfumo wa kutambulisha wakazi na makazi yao utaonekana kufanyika vizuri chini ya Halmashauri za Mitaa na Miji kuliko kwenye serikali kuu.

d. Kumtambulisha mtu?
Hata hivyo kwa kadiri inavyoonekana mradi huu una lengo la kumtambulisha mtu. Yaani huyo mtu ni nani, rangi yake, vinasaba vyake, hali yake ya afya, benki yake, anaishi wapi, ni wa jinsia gani? Hivyo utaona basi kuwa kwa kutambulisha vitu vingi vya mtu mmoja basi mradi huu unafaa sana kwani kwa kutumia teknolojia hiyo ya kompyuta tunaweza kabisa kuweka habari nyingi kwenye kitu kidogo sana.

Hata hivyo tutajiuliza tunafanya hivyo kwa faida ya nani? Je mtu wa kijijini mkulima au mhamaji akishakuwa na kitambulisho hicho kitamfaa vipi wakati kila mvua inyeshapo amehama au yuko sehemu nyingine? Je kila akihakama na ng'ombe wake itabidi aende kuupdate yuko mahali gani na mbuga gani au tutaweka na GPS humo humo ili kumjua mtu huyo yuko wapi kwa sababu hatujui kijiografia yuko wapi?

Kama lengo ni kuyatambulisha yote hayo manne kwenye kikadi kimoja, kwa watu milioni 40 na kutengeneza database, supporting staff, n.k gharama ya bilioni 200 ni kejeli ya akili za watu timamu, na wabunge wanaosapoti mradi huu akili zao tunaweza kuziweka kwenye kundi la "fyatu"!
 
Waafrika hatuwezi kujitawala! If you think otherwise, prove me wrong!

Tulipewa uhuru mapema. Hatukua tayari kujitawala.
 
Waanchane na huu mradi. Hauna maana. Nadhani the cost effective way ingekuwa ni kutunga sheria inayotambua uhalali wa aina mbalimbali za documents zilizopo kama vitabulisho halali, ikiwa ni pamoja na kadi za kupigia kura, passport, driving licence na zingine za aina hiyo.

Nchi nyingi tu kuna sheria kama hizi zinazotambua aina mbalimbali za ID (passport, a driving license, etc.).
 
Waanchane na huu mradi. Hauna maana. Nadhani the cost effective way ingekuwa ni kutunga sheria inayotambua uhalali wa aina mbalimbali za documents zilizopo kama vitabulisho halali, ikiwa ni pamoja na kadi za kupigia kura, passport, driving licence na zingine za aina hiyo. Nchi nyingi tu kuna sheria kama hizi zinazotambua aina mbalimbali za ID (passport, a driving license, etc.).

cynic, thank you for this proposal.. kwa sababu nadhani solution iliyowekwa mbele yetu ni ya kuunganisha vitambulisho hivi vyote into one badala ya kufikiria namna ya vitambulisho ambavyo tunaweza kuvitambua.

Kwa mfano, serikali ikisema watumishi wa serikali au sekta binafsi ambao wanatumia vitambulisho vyenye sifa hizi x,y, na z basi itavitambua vitambulisho hivyo. Na pia inaweza ikasema minimum requirements for ID rasmi na makampuni, taasisi n.k zikafanya mambo yao.

Hivyo ukafanya kama inavyofanya State Department hapa US kwenye masuala ya kazi. Unahitaji Documents tatu.

Ya kwanza ni any of Primary IDs: - Passport, Birth Certificate, Military Issued ID n.k (you must have one of them)

Secondary: Two of any of these (State ID, Government Issued ID, na nyingine zipo lundo).

Thanks again!
 
Tanzania tangu tupate uhuru tumekuwa na bahati mbaya ya kuwa na baraza la mawaziri vilaza, wasiokuwa na uwezo wa kufikiri beyond their political ambitions. Japo tuna baadhi ya maprofessor katika baraza lile ila ninaamini kuwa wengi wanaangalia maslahi binafsi na utashi wa kisiasa zaidi kuliko hali halisi ya Nchi katika kupitisha maazimio ya nchi.

Ni mwendawazimu pekee anayeweza kudhani kuwa kipaumbele cha Tanzania leo hii ni kuwa na vitambulisho vya kielectroniki. Nina uhakika wa 100% kuwa fikra zangu zipo sahihi kabisa kuuhusisha mradi huu na CCM's 2010 election funding strategy. Katika Nonprofit and Public finance kuna kitu kinaitwa "Nondistribution costraint" ambayo inazuia kugawanywa kwa ziada yoyote miongoni mwa wadau kama gawio "dividend", Strategy zinazotumika na mamanager na madirector katika sector hizi (pamoja na wanasiasa wenye dhamana ya nchi) ambao ni "accounting officers" ni kubuni miradi ambayo huipa gharama zaidi ya halisi (overstated price tags for projects) ambazo zitaonekana mbele ya wadau kuwa kitu kimefanyika. Miradi hii hupewa watu maalum waifanye ambao huwa kuna makubaliano ya nyuma ya pazia kuwa kinachozidi kirudishwe kwa manager kwa mlango wa nyuma.

Kama mnakumbuka 2000, kulikuwa na BOT twin towers, na 2005 walibuni EPA, 2010 ni "smart card" project kwa ajili ya kufund Campaign za waliopewa dhamana ya kuangalia mali za watanzania ambao wanazitumia kwa faida zao.

Leo hii Watanzania wengi, hawana kazi, hawana kipato, Hivi hizi Tshs 222 Billion zikiwekezwa kwenye kuanzisha ajira kwa kuwa na miradi ya mashamba ya kitaifa ya umwagiliaji katika kilimo, ufugaji na processing industries ya mazao yatokanayo na kilimo ni watanzania wangapi watapata ajira na hivyo kuwa na hela ya kuspend na kukuza uchumi na kuanzisha ajira nyingi zaidi? (stimulating the economy).

Nionacho hapa ni kwamba wanaotakiwa kutoa maamuzi ya vipaumbele Tanzania wamekosa utaalam wa ujasiriamali kwa Taifa ( enterpreneurial skills) wanachoangalia ni je nafasi walizo nazo (wao wanaita ulaji badala ya huduma) wataendelea kuzishika au watazikosa. Na ili wawe na uhakika wa kuendelea kushika wanachofanya ni kupitisha maamuzi yenye maslahi ya Chama (wao wenyewe) zaidi ya Taifa(wananchi masikini wa Tanzania), kwani wao tayari wanamaisha mazuri kupitia dhamana waliyopewa na wananchi, pia wameweza kujitajirisha wao na familia zao na kuona kuwa sasa ni wakati muafaka wa Vitambulisho.

Watanzania "TUUPINGE MRADI HUU MUFLISI" Hauna faida yoyote zaidi ya kuwa ni WIZI MTUPU unaopangwa na "Board of Directors" ya Nchi kwa jina la CCM ili kujiongezea bonus kwa kazi iliyowashinda ya KUENDELEZA NCHI.
 
Sasa ni mwaka wa 47 tangu tupate uhuru. Katika muda wote huo harukuwa na vitambulisho vya uraia lakini hatukuwa na matatizo yoyote ya kutishia usalama wa Watanzania au uhuru wetu.

Shilingi bilioni 222 ni pesa nyingi sana kama baadhi ya pesa hizo zikielekezwa kwenye Kilimo, Elimu, hospitali zetu, upatikanaji wa maji safi basi tunaweza kuinua maisha ya Watanzania walio wengi na kuyaboresha pia.

Kutumia mapesa mengi kiasi hicho hakuongezi tija wala maendeleo yoyote kwa nchi yetu, bali ni mradi uliotengezwa na wakubwa ili wajipatie mapesa ya kujiandaa kwa uchaguzi wa 2010. Zamani CCM ilikuwa inaendeshwa kwa ada toka kwa wanachama ambao siku hizi hawafanyi hivyo tena maana CCM si chama cha wakulima na wafanyakazi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma bali ni chama cha mafisadi. Na sasa hivi CCM hawana pesa hivyo lazima wauchangamkie mradi huo wa kifisadi na kuupitisha haraka haraka ili wajipatie mabilioni ya uchaguzi huo wa 2010.

Kigumu chama cha mafisadi....kigumu!!!!!

Mkuu mimi naunga mkono suala la vitambulisho, kwa sababu hasara ya kuwa na watanzania hewa au gharama ya kuwa na watanzania wasiokuwa documented ni kubwa kuliko hata hiyo bilioni 222.

Angalia jinsi kura zilivyovurugwa huko Zanzibar mara zote, angalia ni watanzania wangapi wenye uraia wa mashaka ambao wanafonza mabilioni ya pesa bila huruma?

Kuna baadhi ya mambo tukiwa tunasema hatuwezi kuyafanya eti kwa sababu ya gharama tutakuwa tunabehave kama wakomunisti.

Mfano mzuri ni jinsi watu wanavyopinga kujenga flyovers Tanzania, kisa eti gharama ni kubwa. Hizo bilioni 222 sio nyingi kama wakimanage vizuri, tatizo ni kuwa inawezekana imeletwa kwa sababu watu ulani wanataka kula, kama lengo ni kula kama ilivyokuwa wakati wa speed governors basi mradi huo upingwe tu.
 
Mkuu mimi naunga mkono suala la vitambulisho, kwa sababu hasara ya kuwa na watanzania hewa au gharama ya kuwa na watanzania wasiokuwa documented ni kubwa kuliko hata hiyo bilioni 222. Angalia jinsi kura zilivyovurugwa huko Zanzibar mara zote, angalia ni watanzania wangapi wenye uraia wa mashaka ambao wanafonza mabilioni ya pesa bila huruma? Kuna baadhi ya mambo tukiwa tunasema hatuwezi kuyafanya eti kwa sababu ya gharama tutakuwa tunabehave kama wakomunisti.
Mfano mzuri ni jinsi watu wanavyopinga kujenga flyovers Tanzania, kisa eti gharama ni kubwa. Hizo bilioni 222 sio nyingi kama wakimanage vizuri, tatizo ni kuwa inawezekana imeletwa kwa sababu watu ulani wanataka kula, kama lengo ni kula kama ilivyokuwa wakati wa speed governors basi mradi huo upingwe tu.

Kwa taarifa yako ni kwamba watoa maamuzi hata siku moja hawawezi kufanya kitu chenye negative outcome kwao.

Wewe kubali mradi kwa mtazamo wako huu ila wao wanaufanya kwa mtazamo tofauti na wako na kwa kuwa wao ndiyo watekelezaji basi mtazamo wako hauna nafasi hata kidogo kwenye hili
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu hapa kidogo unatoka nje.. passport ni kitambulisho cha kusafiria nje ya nchi yako.. Nchi zote duniani zinatumia passport kwa shughuli hiyo pia mara chache kama kitambulisho pindi mhusika anapokuwa hana kitambulisho kingine..i.e bank ktk kufungua account na kadhalika, niseme sawa na driver's licence ilivyokusudiwa..

Swali la msingi hapa ni kufahamu hivi vitambulisho vinatakiwa kwa ajili gani?.. ikiwa ni Uraia basi kitambulisho kama social security number tu kinatosha na sii lazima iwe ktk muundo wa smart card kwa sababu kazi kubwa ya kuhifadhi hivi vitambulisho ni ktk mitambo ya kuhifadhi sio kitambulisho chenyewe.

In fact hakuna kitambulisho ambacho watu wameshindwa kughushi isipokuwa watu wengi hushindwa kuingia ktk server ya kuhifadhi hizi data..
Binafsi naungana na Recta ktk hili kwamba tunahitaji vitambulisho vya Utaifa kwa sababu kila kitu kina mwanzo wake isipokuwa nachopinga ni gharama inayotakiwa kutumika tena wakati mbaya wa kiuchumi duniani kama huu.

Billioni 200 ktk hali hii ya kutatanisha kiuchumi duniani inatakiwa sana ktk kujenga miundombinu yetu, kuongeza uwezekano wa kuzalisha ktk kilimo na pengine zitumike ktk mfumo mpya wa ukopeshaji kwa wananchi ambao wanaweza kuinua hali ya uchumi wetu kuweza kuhimili matatizo ya usoni.

Vitambulisho ni kitu ambacho kinaweza kusubiri kabisa hali hii ipite kwanza kwa sababu vitambulisho hivi haviongezi ajira, kupunguza ama kuondoa Umaskini malengo ambayo yamekubalika kitaifa na kimatifa.

Misaada mingi inayomiminika nchini inalenga kupunguza au kuondoa Umaskini leo tuonekane tukitumia billioni 200 kutengeneza vitambulisho sii tutaonekana hamnazo.

Kifupi hii inanikumbusha sinema ya Tatanic, meli ambayo ilikuwa ikizama (uchumi wetu) unakuta kuna njemba mbili zinagombania mwanamke badala ya kutafuta njia za kujiokoa kwanza. Matokeo yake wote wanakufa na mwanamke pekee ndiye anapona naye kwa mapenzi ya hadithi za simulizi anaishi bila kuolewa hadi uzee wake.. conclusion ya matukio yote - All were loosers!

Inasikitisha sana kuona taifa letu likitumia billioni 200 kwa kitambulisho ambacho kinaweza kutengenezwa kwa billioni 95 na kikafanya kazi sawa...

Kenya wana vtambulisho wanavyoviita Kipande toka miaka ya 70 na vinafanya kazi vizuri sana kwa sababu ID hii inapatikana kutokana na vigezo vyao vya kiasili zaidi kama vile kabila nakadhalika.

Wapo watu wameghushi lakini askari anapokusimamisha ukamwonesha kipande kisha ukafgungua domo tu atajua kilichofanyika.
 
Last edited:
Mkuu mimi naunga mkono suala la vitambulisho, kwa sababu hasara ya kuwa na watanzania hewa au gharama ya kuwa na watanzania wasiokuwa documented ni kubwa kuliko hata hiyo bilioni 222. Angalia jinsi kura zilivyovurugwa huko Zanzibar mara zote, angalia ni watanzania wangapi wenye uraia wa mashaka ambao wanafonza mabilioni ya pesa bila huruma?
Kuna baadhi ya mambo tukiwa tunasema hatuwezi kuyafanya eti kwa sababu ya gharama tutakuwa tunabehave kama wakomunisti.
Mfano mzuri ni jinsi watu wanavyopinga kujenga flyovers Tanzania, kisa eti gharama ni kubwa. Hizo bilioni 222 sio nyingi kama wakimanage vizuri, tatizo ni kuwa inawezekana imeletwa kwa sababu watu ulani wanataka kula, kama lengo ni kula kama ilivyokuwa wakati wa speed governors basi mradi huo upingwe tu.

Vitambulisho hivi kama ilivyo fly-overs si panacea za matatizo yetu! Watu wanatembea toka Kimara au Mbagala kwa kushindwa nauli ya shilingi mia mbili halafu tutegemee kuwa watamudu vitambulisho kwa ajili yao, familia zao na wote wanaowategemea?

Kingine ni kuwa, kutokana na uzoefu, huu utakuwa mradi wa jamaa wanaovaa unifomu kuwanyanyasa na kuwabughudhi wananchi ili wawakamue!

Huu si wakati wa mradi kama huu.

Amandla.
 
...Hapa nchini, katika baadhi ya miradi ambayo inanichukiza kwa kiwango kikubwa kuliko yote - ni huu mradi wa vitambulisho. Sababu ni jinsi unavyoonesha jinsi tulivyoamua kuwa "malimbukeni" makusudi kabisa. Nakosa neno jingine la kutumia kuulezea mradi huu. Ni mradi nilioupinga tangu niusikie kwa mara ya kwanza January mwaka jana.

...Siupingi kama mradi unaofaa. Naupinga kwa sababu mazingira yetu (uchumi, elimu, n.k.) na sababu tunazotumia kuhalalisha mradi huu hazisimami. Niliandika HAPA yafuatayo:

Kwangu mimi, huu mpango wa vitambulisho usubiri rural electrification at least by 80%, usubiri postcode scheme (angalau kwa dar) kukamilika- sembuse nchi yote...!!, usubiri network ya trunkroads walau 5 za kuunganisha mikoa yote katika kiwango cha lami, usubiri upimaji miji/ardhi wa Tanzania yote, usubiri kukamilika kwa fibre optic network Tanzania au hizo wireless network at least by 60%, usubiri coverage ya TVT na Radio kwa nchi nzima at least by 85%..... ndipo tuangalie uwezekano wa kila mmoja wetu kuwa na kitambulisho hicho.

SteveD.
 
Last edited:
Mimi siupingi mradi wa Vitambulisho. Napinga gharama zake. Kwamba gharama ni kubwa mno.

Kitu cha muhimu kwanza ni record. Tunaweza kusema kuwa UK, USA hawana vitambulisho lakini wana records ambazo zinamtambulisha mtu iwe ni SSN au vitu vingine.

Mnamkumbuka yule mtoto DC sniper (Malvo). Yaani finger print zake tu zilifanya watu waelewe alisoma wapi?

Ukichukua kitambulisho cha mwanafunzi Marekani, unaweza kupata information zake zote.

Hivyo mwanafunzi au mfanyakazi wa serikali anaweza kutumia kitambulisho chake kama ID ya taifa.

Katika kipindi cha sasa. Watanzania ni lazima tuanze kujitambulisha. Kujitambulisha kuna faida nyingi.

Ukiwa mwaaminifu kama mimi, kujitambulisha kwako kunaweza kukupatia mikopo, kazi.

Nikiwa Tanzania nilishindwa kukopa pesa benki. Mkopo wa laki 3, ni lazima niandikishe nyumba.

Hapa Marekani, namba zenye tarakimu 9 (SSN) zimebadilisha maisha yangu.

Please don't get me wrong. Kujitambulisha hakutasaidia sana kuzuia wizi au ujambazi lakini kutawasaidia wenye nia ya kufanya mambo mazuri kufanya vizuri zaidi.

Vilevie kujitambulisha hakuna maana ya national ID. Kujitambulisha kuna maana ya mtu mmoja kuwa ni entity inayotofautiana entity nyingine na kuweza kujulikana kwa urahisi.
 
Mimi siupingi mradi wa Vitambulisho. Napinga gharama zake. Kwamba gharama ni kubwa mno.

Kitu cha muhimu kwanza ni record. Tunaweza kusema kuwa UK, USA hawana vitambulisho lakini wana records ambazo zinamtambulisha mtu iwe ni SSN au vitu vingine.

Mnamkumbuka yule mtoto DC sniper (Malvo). Yaani finger print zake tu zilifanya watu waelewe alisoma wapi?

Ukichukua kitambulisho cha mwanafunzi Marekani, unaweza kupata information zake zote.

Hivyo mwanafunzi au mfanyakazi wa serikali anaweza kutumia kitambulisho chake kama ID ya taifa.

Katika kipindi cha sasa. Watanzania ni lazima tuanze kujitambulisha. Kujitambulisha kuna faida nyingi.

Ukiwa mwaaminifu kama mimi, kujitambulisha kwako kunaweza kukupatia mikopo, kazi.

Nikiwa Tanzania nilishindwa kukopa pesa benki. Mkopo wa laki 3, ni lazima niandikishe nyumba.

Hapa Marekani, namba zenye tarakimu 9 (SSN) zimebadilisha maisha yangu.

Please don't get me wrong. Kujitambulisha hakutasaidia sana kuzuia wizi au ujambazi lakini kutawasaidia wenye nia ya kufanya mambo mazuri kufanya vizuri zaidi.

Vilevie kujitambulisha hakuna maana ya national ID. Kujitambulisha kuna maana ya mtu mmoja kuwa ni entity inayotofautiana entity nyingine na kuweza kujulikana kwa urahisi
.

Zakumi, again, you are retracting back to causes... and that is the poor planning we have at different levels in our society. How would you run and maintain database littered with a plethora of information through card leaders and authentication to servers that could be (centralized) localized in Dar or (decentralized) at makao makuu ya wilaya, whereas the means to run those servers is yet to be thought of. And in places where that seems to be a minor discouragement, migao ya umeme bado haiishi. (ooh, i know the alternative to this...readers zinazotumia battery na kurusha authentication packets kwa simu za mkononi mpaka makao makuu dar..!!!)

The acceptance of this project as one of many things beneficial to the nation is one thing. Rolling it out right away in our current social economic climate is another. We are rushing onto things. My compromising position on this matter is to halt it, let's postpone the project for another 15 - 20 odd years.

As I believe it would then be cheaper technologically and in general, feasible. some of the criteria necessary for effective implementation would've been dealt with by then (hopefully thru sera za CCM!). Urban/rural areas survey, electrification and road network are essential factors to a positive anticipated outcome of projects such like this.

We shouldn't dismiss them unless we are aiming for another Tanzanian giant white elephant!
 
Hivi kwani hivi vitambulisho ni lazima? Kipi cha muhimu hapa? Maji safi ya bomba kwa kila Mtanzania, umeme kila sehemu, au vitambulisho?


Nyani Ngabu,Tumeambiwa huo mradi utaanza kabla ya mwaka 2010.

Mwaka 2010 ndiyo kutakuwa na uchaguzi mkuu.

Gharama za awali ilikwua ni dola 152 million ila sasa ni dola 200 million.

200-152= dola 48 milion(hiii difference sasa)

Yaani bado tu unauliza maswali kuwa hivyo vitambulishao ni lazima.Kwa akili ndogo tu unaweza kujua lengo la huo mradi.Yaani na upara wote huo unashindwa kujua lengo ni nini?au ndiyo jinsi ulivyo?
 
Hivi tukiiachia Tume ya Uchaguzi ikaviboresha vile vikadi vinavyomtambulisha mpiga kura vikawa pia ndio vitambulisho vyetu kuna tatizo gani? Kwa maana hiyo, kila mtanzania atakapofikia umri wa miaka 18 atapewa kitambulisho hiki ambacho kitamsaidia pia kumtambulisha kama raia wa nchi hii.
 
Hivi tukiiachia Tume ya Uchaguzi ikaviboresha vile vikadi vinavyomtambulisha mpiga kura vikawa pia ndio vitambulisho vyetu kuna tatizo gani? Kwa maana hiyo, kila mtanzania atakapofikia umri wa miaka 18 atapewa kitambulisho hiki ambacho kitamsaidia pia kumtambulisha kama raia wa nchi hii.

Wilcard,

unataka uambiwe jibu gani?wanajua haya yote ila tatizo ni uchaguzi mkuu tu
 
Wilcard,

unataka uambiwe jibu gani?wanajua haya yote ila tatizo ni uchaguzi mkuu tu

Gembe,
Mbona mashirika ya UMMA yanayowasaidia kwenye uchaguzi bado yapo? Ipo NSSF, DAWASA, BOT, SIDO, PPF,.... Serikali ya CCM haiwezi kushindwa kupata mapesa haya!
 
Imani yangu ni kwamba, mradi huu hautaishia kutoa kadi tu, bali utaunda database ya waTanzania wote ambayo itawekewa kumbukumbu zote za mwenye kadi kadiri inavyowezekana. Kama ikifanyika hivyo, itakuwa na manufaa makubwa sana.

Mkuu huku unako waza huku bado sisi wabongo naviongozi wetu wavivu wa kutenda kazi hatujafikia.Maswala ya data base yanawenyewe.....angalia mifano kibao miradi inayo tumia computer kumekuwa na mizingua miiingi mfano zamani watu walikuwa wanatumia vitabu bank ukaja utaalamu wa computer na card lakini tatizo la kukaa kwenye foleni bado limekuwa halina ufumbuzi kwenye mabank ya makabwela tatizo hapa ni la ki management haswaa hatuna watu wenye kuchapa kazi miradi kibao inageuka dili kwa watu wachache na kujinufaisha.
 
Hizo pesa za vitambulisho kwa nini wasizipeleke vijijini tukainue kilimo ambacho ni uti wa mgongo?Kuliko kuhangaikia vitambulisho wakati takwimu za wahamiaji haramu kwa mwaka hazizidi hata 200000/= kwa hiyo kitambulisho na kilimo,elimu,maji safi,umeme na miundo mbinu kipi ni bora?Na hivi serikali imekuwa inasua sua kivipigia chapuo.
 
Back
Top Bottom