Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Kila kitu kitajulikana siku ya siku tenda mbofu mbofu na meneno ya kuozesha bongo za watanzania ndio bado yandumu karne hadi karne.
 
Zanzibar, Kenya, Israel and other developed countries,” Mr Ame told the 'Sunday News'. Mr Ame said that two dimensions barcode (2D-barcode) identity cards such as the ones used in Zanzibar were sufficient for Tanzanians. “What we need to store on the cards are specifically fingerprint and a photo of each adult.

[/COLOR][/SIZE][/FONT]

First Zanzibar has no National IDs, only a resident IDs

All the two countries they have quote (KENYA and Israel) are now moving to smart card system with much higher costs than Tanzania although they already have the Institution in place...

omarilyas
 
Siri ya vitambulisho vya taifa yafichuka

Shadrack Sagat
Daily News; Sunday,February 22, 2009

Kampuni mwelekezi wa mradi wa vitambulisho vya taifa Gotham Internation Ltd imesema kiasi cha Sh bilioni 200 ambazo zimepangwa kutumika katika mradi huo haziendi zote kwa mkandarasi atakayeshinda zabuni ya kutengeneza vitambulisho hivyo.

Badala yake, kampuni hiyo ya kitaalamu imesema kuna maeneo 14 ambayo fedha hizo zitatumika huku kampuni mkandarasi atakayepewa jukumu la kutengeneza vitambulisho hivyo atalipwa sio zaidi ya Sh bilioni 35.

Mkurugenzi Mtendaji wa Gotham International Dk. John Kyaruzi alitaja maeneo mengine ambayo alisema yatagharimu fedha nyingi kuwa ni majengo na wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho hivyo (NIDA), utambuzi wa Mtanzania, uboreshaji wa sheria pamoja na uelimishaji wananchi.

“Gharama kubwa iko kwenye kumtambua Mtanzania pamoja na kugharamia uhamasishaji kupitia vyombo vya habari na sio manunuzi," alisema Dk. Kyaruzi ambaye kampuni yake imeingia mkataba na serikali kutoa ushauri juu ya mradi huo.”

Kampuni sita za kigeni tayari zimepita katika hatua ya awali ya kuwania utengenezaji wa vitambulisho hivyo. Kampuni hizo ni Unisys ya Afrika Kusini, Giesecke & Devrient Fze ya Dubai, Iris Corpotaration Berhad ya Malaysia, Madras Security Printers ya India, Maruben Corporation ikishirikiana na Zetes na Nec ya Japan, Tata Consultancy Services ikishirikana na Ontrack Innovations Ltd ya India.

Mtaalamu huyo pia alitaja gharama nyingine kuwa ni baadhi ya kazi zilizotajwa katika mradi huo zitapata bajeti ya wizara nyingine husika na sio kweli kuwa zote ni za mradi huo. Alitoa mfano wa bajeti ya kuboresha mitandao iko katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia huku bajeti ya kuandikisha inaweza kuwa katika Serikali za Mitaa.

Kampuni hiyo imelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwapo malalamiko kuwa fedha nyingi zimetengwa katika mradi huo ambao unaonekana kuanza kuzua mtafaruku miongoni mwa wanasiasa.

Lakini alifafanua kuwa vitambulisho hivyo wao kama wataalamu wamependekeza kuwa vitolewe bure kwa Watanzania huku wageni wakiwamo wanadiplomasia na wakimbizi watalazimika kuchangia kidogo.

Dk. Kyaruzi alisema mradi huo ni wa muungano na ndiyo maana hakukabidhiwa Mpigachapa Mkuu wa Serikali au Wakala wa Vifo na Vizazi (Rita) kwa vile vyombo hivyo sio vya muungano.

"Ndiyo maana mradi huo uko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ni ya muungano, ndiyo maana imeundwa mamlaka na sio wakala," alisema Dk. Kyaruzi.

Alisema katika bajeti hiyo ya vitambulisho kuna fedha zitapitia kwenye wizara nyingine kama Uhamiaji, Rita na taasisi nyingine visiwani Zanzibar ambazo zinajishughulisha na usajili wa vizazi na vifo. "Hivyo sio kweli kwamba fedha zote ni za NIDA."

Mtaalamu huyo alitetea bajeti hiyo kwa kueleza kuwa mradi huo sio aghali kama nchini nyingine kwa sababu hakuna kitu kilichokwishafanyika bali taifa linaanza upya kwa kila eneo.

Naye Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Jack Gotham alisema kampuni yake imeajiriwa na serikali kufanya kazi hiyo chini ya sheria namba tatu ya mwaka 2001 na wanajitahidi kutoa ushauri kuhakikisha mradi huo unapata mafaniko makubwa.

Kuhusu teknolojia ya Smart Card, Gotham alisema walipendekeza hiyo kwa vile kitambulisho hicho kitakuwa na maelezo mengi hivyo kuwa faida kubwa kwa taifa katika masuala ya usalama na uhalifu.

Kuhusu habari ambazo zimekuwa zinaandikwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kampuni hiyo haina mkataba na serikali, Gotham alionyesha mkataba walioingia na serikali Novemba 10, 2004.

Alisema kampuni yake imekuwa inafanya kazi vizuri na taasisi zote za serikali ambazo zinajihusisha na vitambulisho hivyo akasisitiza kuwa ushauri ambao wameutoa kwa serikali wanaamini kuwa una lengo zuri la kuwafanya Watanzania waweze kutambuana.

Mradi wa vitambulisho vya taifa ulipitishwa na kikao cha Bazara la Mawaziri kilichoketi Februari 2, 2007 na kutangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa wakati huo Joseph Mungai. Mchakato wa maandalizi yake ulianza mwaka 1995 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2009.

Mradi huo wa vitambulisho hivi karibuni umekuwa unaandikwa zaidi kwenye vyombo vya habari hasa ikiwamo kuachwa kwa Kampuni ya Sagem ya Uswisi katika hatua ya pili ya kuwachuja wazabuni hao.

Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa Waziri Masha amelalamika kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda juu ya kuachwa kwa kampuni hiyo hadi akashauri Bodi ya Zabuni ipate ushauri PPRA kitendo kilichotafsiriwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa anataka kuibeba kampuni hiyo.

Lakini pia baadhi ya vyombo vya habari vimeibuka hivi karibuni vikiishambulia Kampuni ya Gotham kuajiriwa na serikali bila kuingia mkataba wowote. Hata hivyo kampuni hiyo jana iliwaonyesha wanahabari mkataba huo.
 
Last edited:
Jamani naombeni kuuliza hivi vile vitambulisho vya kupiga kura ni watanzania wangapi walivyo navyo kwa sasa?
 
Hii Kampuni ya Gotham iache kutufanya watanzania wote eti ni mbumbumbu, kwani wanaposema kuwa atakaye pata tenda atapewa bilioni 35 sio kweli kwani tenda ya kutengeneza vitambulisho ndio ilitangazwa na tenda hiyo ina thamani ya shilingi 222 bilioni .

Kusema kuna fedha zitaenda kwenye kuwatambua watanzania ni kupotosha ukweli halisi kwani hauko hivyo , na kilichotangazwa ni tenda ya kiutengeneza vitambulisho na sio vinginevyo.

Hoja kuwa Mpiga chapa Mkuu wa serikali hakupewa kwa sababu ni suala la Muungano ni upuuzi mtupu kwani anachapa mangapi yanayohusiana na Muungano?Mbona anacha sheria zinazohusu pande zote mbili?mbona anachapa machapisho mbalimbali ya pande zote mbili?

Mbona ikifika hapa wanatupotosha ? huu ni mradi wa kutafuta fedha za kampeni 2010 kwani huyu Gotham naye ni Mtandao tangia wakati huo .
 
Hii Kampuni ya Gotham iache kutufanya watanzania wote eti ni mbumbumbu, kwani wanaposema kuwa atakaye pata tenda atapewa bilioni 35 sio kweli kwani tenda ya kutengeneza vitambulisho ndio ilitangazwa na tenda hiyo ina thamani ya shilingi 222 bilioni .

Kusema kuna fedha zitaenda kwenye kuwatambua watanzania ni kupotosha ukweli halisi kwani hauko hivyo , na kilichotangazwa ni tenda ya kiutengeneza vitambulisho na sio vinginevyo.

Hoja kuwa Mpiga chapa Mkuu wa serikali hakupewa kwa sababu ni suala la Muungano ni upuuzi mtupu kwani anachapa mangapi yanayohusiana na Muungano?Mbona anacha sheria zinazohusu pande zote mbili?mbona anachapa machapisho mbalimbali ya pande zote mbili?

Mbona ikifika hapa wanatupotosha ? huu ni mradi wa kutafuta fedha za kampeni 2010 kwani huyu Gotham naye ni Mtandao tangia wakati huo .

Asante kwa uchambuzi huo kwa watanzania wote. Hivi utaratibu wa kumweka mtu kitimoto bongo kwanini haupo?, Nakumbuka ulishawahi fanyika mwaka mmoja huko nyuma.

Hawa wanatakiwa kuwekwa kitimoto na iwe broadcasted nchi nzima na ulimwenguni kwa ujumla tuwaone uongo wao wakiwa wanajikanyaga maana maswali ya hard talk hayana formula kama mtu anadanganya mtamuona tu.
 
...Mr Ame said that two dimensions barcode (2D-barcode) identity cards such as the ones used in Zanzibar were sufficient for Tanzanians. “What we need to store on the cards are specifically fingerprint and a photo of each adult.
Haya ndio mawazo ambayo tuliyategemea toka kwa kiongozi/mwananchi mwenye kujali maslahi ya nchi masikini kama Tanzania. "Smart-card technology" tunaikimbilia ilhali hatujafikia maendeleo yanayohitaji teknolojia hiyo. Bado tuna mambo mengine sana ya kuboresha kabla ya kufikia 'standard' ya maisha ya kuhitaji 'smart-card'. Inauma sana maana kuna mambo mengi hayafanyiki, ukiuliza kwanini utashangaa viongozi wanakwambia kwa sababu ya 'priority', sasa mbona hiyo 'priority' hajatumika hapa?
The 'Sunday News' learned that the University of Dar es Salaam (UDSM) in collaboration with Tanzania Bureau of Standards (TBS) conducted a feasibility study and advised the Home ministry to first work with local institutions and get advice on the process of IDs production.
...
Instead, it shifted the task to Gotham International Limited consultants who ‘probably advised them to float international tender’.
Hii yote ni sababu ya kujali maslahi binafsi, tunahacha kusikiliza taasisi ambazo tumezianzisha wenyewe tunakimbilia makampuni kusikiliza ushauri wa kampuni binafsi, tunategemea nini? Though smart but (Dr.?) Kyaruzi is typical entrepreneur and has never been loyal to public institutions of Tanzania, in this he want to play another fault. Ebu wamuulize kwanza huo udaktari au kama waandishi wa habari wanamuita hivyo basi akanushe.
 
Siri ya vitambulisho vya taifa yafichuka

SHADRACK SAGAT
Daily News; Sunday, February 22, 2009


Dk. Kyaruzi ( ambaye kampuni yake imeingia mkataba na serikali kutoa ushauri juu ya mradi huo)alisema mradi huo ni wa muungano na ndiyo maana hakukabidhiwa Mpigachapa Mkuu wa Serikali au Wakala wa Vifo na Vizazi (Rita) kwa vile vyombo hivyo sio vya muungano.

"Ndiyo maana mradi huo uko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ni ya muungano, ndiyo maana imeundwa mamlaka na sio wakala," alisema Dk. Kyaruzi.

Alisema katika bajeti hiyo ya vitambulisho kuna fedha zitapitia kwenye wizara nyingine kama Uhamiaji, Rita na taasisi nyingine visiwani Zanzibar ambazo zinajishughulisha na usajili wa vizazi na vifo. "Hivyo sio kweli kwamba fedha zote ni za NIDA."

Zanzibar rejects smart cards as identities


ISSA YUSSUF in Zanzibar,
Daily News, 21st February 2009


Authorities in Zanzibar are against the proposed technology of using smart cards as national identification cards. They also say the project is too expensive and that they were not involved fully in the project.

Both Minister for State- Office of the Zanzibar President Mr Suleiman Othman Nyanga and the Zanzibar Identity Card Registration Office Director Mr Mohammed Juma Ame, refuted reports that Zanzibar identity card office was among the dropped tender applicants for the project .“These are speculations. We did not apply for the union ID project, but we are against the smart card idea,” Minister Nyanga who is responsible for registration of Zanzibaris, told the 'Sunday News'.

He said that he had invited the Union Government (Home Affairs ministry) in 2006/2007 to come and study the ‘quality of Zanzibar IDs’ in order to get experience.Mr Ame said that his office was against the idea of using smart cards because the cards are ‘not durable especially when folded or in contact with water’. “We have attended at least two consultative meetings about the process of Union IDs.

We advised them to drop the idea of using smart cards because they are four-times the cost of other IDs such as IDs in Zanzibar, Kenya, Israel and other developed countries,” Mr Ame told the 'Sunday News'. Mr Ame said that two dimensions barcode (2D-barcode) identity cards such as the ones used in Zanzibar were sufficient for Tanzanians. “What we need to store on the cards are specifically fingerprint and a photo of each adult.
Nikisema Tanzania jamani hatuna press naonekana mtia chumvi mzushi. Sasa naomba mtu anifafanulie kuhusu hizi taarifa mbili zinazofuatana za gazeti hilo hilo, moja ya toleo la jana nyingine ya juzi yake. Mwandishi wa taarifa ya pili, akijua fika kwamba toleo lao la jana yake waliandika the polar opposite ya kile wanachoenda kuchapisha leo yake, ameshindwa kumuuliza huyo Mr. Kyaruzi, Mzee, mbona maofisa wa Zanzibar wanasema wao huu mradi wanaukataa, ina maana pande hizi mbili hazijakubaliana huko bungeni or someplace?

Mr. Kyaruzi anasema kuna hela zitapitia idara za Zanzibar, Wazanzibari wanasema wao huu mpango hawamo na hawataki kuwemo na wana wa kwao; fungu la hela ya vitambulisho vya Wazanzibar zitaishia mfukoni kwa nani?

Mwananchi ukilipia jasho lako kwa gazeti la Daily News siku hizi mfululizo utaelewa nini, Zanzibar wamo hawamo?
 
Last edited:
Kuhani thats very smart. Kila kitu kinakwenda kwenda tu. Hawa waandishi na mhariri hakuna uwajibikaji kabisa, sasa hapo tuamini lipi? au kuna chumvu za kuchokonoa tena huu muungano, manake inakuwaje Zanzibar wana vitambulisho vya 'utaifa' au niseme uzanzibari?
 
“Our data collection is limited to about a million population while the Union IDs project is for half the population of Tanzania said:
[/SIZE][/FONT]

they say the pen is mightier than a sword,hivi kweli gazeti la daily news wanaenda kuprint habari bila ku proof read au kufact check,kwa akili timamu kweli mnataka watu tuamini kwamba TBS walifanya feasibility study , na sio National Bureau of Statistics (NBS)? hivi ndio tulipofikia hapa,au tuandika kwa shinikizo la kina fulani fulani? najuwa cutting and pasting ndio njia mpya au inakuwezesha kupata pondezi kwakuwa na posts nyingi lakini hapa TBS na NBS ni vitu viwili tofauti kabisa,na kwa taarifa yako NBS ndiye walioshiri katika zoezi la feasibility study na UDSM

mungu ibariki Tanzania
 
ukisoma magazeti yote sasa hivi yameingiliwa,kila sehemu kumeingiliwa!mtazamo wa mtanzania wa sasa ni free enterprise, yani inakumbusha usemi wa zamani kwamba apendwi mtu linapendwa pochi tu!!!!

mungu ibariki Tanzania
 
Mzalendo, nimependa slogan yako hapo chini ya posti yako.

Huyo mtu aliyesema hivyo ningependa kumsoma zaidi! Duu, kali!
 
Nikisema Tanzania jamani hatuna press naonekana mtia chumvi mzushi. Sasa naomba mtu anifafanulie kuhusu hizi taarifa mbili zinazofuatana za gazeti hilo hilo, moja ya toleo la jana nyingine ya juzi yake. Mwandishi wa taarifa ya pili, akijua fika kwamba toleo lao la jana yake waliandika the polar opposite ya kile wanachoenda kuchapisha leo yake, ameshindwa kumuuliza huyo Mr. Kyaruzi, Mzee, mbona maofisa wa Zanzibar wanasema wao huu mradi wanaukataa, ina maana pande hizi mbili hazijakubaliana huko bungeni or someplace?

Mr. Kyaruzi anasema kuna hela zitapitia idara za Zanzibar, Wazanzibari wanasema wao huu mpango hawamo na hawataki kuwemo na wana wa kwao; fungu la hela ya vitambulisho vya Wazanzibar zitaishia kwa nani?

Mwananchi ukilipia jasho lako kwa gazeti la Daily News siku hizi mfululizo utaelewa nini, Zanzibar wamo hawamo?


Mimi naona tatizo unalo wewe mwenyewe! Chombo cha habari 'deals with what is NEWS and according to sources'. As long as there're different sources and different angles, the same story can be written as many times as it is practicable. Hiyo ndiyo 'journalism'.

Media outlets do not create/compose stories in the newsroom, they report what sources say and one story can be said many times and in different ways and all that is NEWS!
 
Mkuu KUhani, katika hili naomba kutofautiana. Angalia sopurces za story ni mbili tofauti, kwa hiyo contradiction iiyopo inatokana na statement za sources, si utungajiw a mwandishi au chombo cha habari.

Hapa wa kuwashangaa ni watawala ambao wanashindwa kueleza kinagaubaga iwapo Zanzibar inahusika katika mpango huu au la
 
Press tunayo na ndiyo hiyo. Hawa ndio waandishi wetu waliotokana na vyuo vyetu vya uandishi wa habari. Japo mnashangaa waandishi wa magazeti, watangazaji ndio kabisaa, ila tukubali tusikubali hiyo ndio media yetu tuliyonayo.

Kyaruzi ni boya tuu amewekwa hapo na Gotham. This Guy Gotham ni very clever na brilliant guy (not in class) up stares. Ana macho fulani ya kuona mbali. Baada tuu ya kumuona yupo kwenye mradi huu, nimeshapata picha kamili mradi ni wa nani.

Zanzibar kama sehemu inayojitegemea, wana haki ya kuwa na vitambulisho vyao ambavyo havitambuliwi na URT. Zanzibar kama sehemu ya muungano, haina jeuri ya kukataa issue yoyote chini ya wizara ya muungano. Kwa lugha nyingine, opinion ya Zanzibar is nothing. Mambo ya muungano, ni URT which dictate terms and ZnZ lazima iimplement and has no choice its a must.

Miongoni mwa mambo ya muungano ambayo opinion ya ZnZ haihitajiki, yaani ZnZ ni sawa na Shinyanga ama Singida ni pamoja na yale mambo yote 11 kwenye original Articles of Union,
ZnZ must take them as they are, na ndipo Uzanzibar wao ilipoishia. Mambo ya ndani ni miongoni mwake no mjadala.
Yale mambo mengine toka 11 mpaka 22/26/28 hayo ndiyo ZnZ inayapigia kelele kuwa kero za Muungano na ndiyo wanaruhusa ya kuyajadili.

Ni ukweli usiofichika URT inauendesha muungano kibabe, mojawapo ni mzizi wa muungano kati ya Karume na Nyerere ulifanywa kwa mdomo tuu kabla ya maandishi. Ni Karume baada ya mapinduzi, akamwambia Mwalimu, Waingereza wanaweza kuja kututia kibano, dawa ya haraka ni tuungane "WEWE RAIS MIMI MAKAMO". Huo ndio mzizi. Maandishi ndipo yakafuatia.

Bara kwa kuogofya na uwezekano wa upinzani kushinda ZnZ, itakuwaje Makamo mpinzani?. Tukaukata mzizi, infact tuliungoa toka kwenye shina kwa kufanya mabadiliko ya Katiba ya URT bila kuishirikisha ZnZ tukamvua Umakamo rais wa URT, hivyo kujikuta he is nothing kwenye URT, na akija huku ni kama Juma tuu na Ali. ZnZ wamelia wee, hatimaye sasa eti ndio kapewa angalau
uwaziri asiye na wizara na anahudhuria cabinet meeting.

Huo ni mfano mmoja tuu wa ubabe wa bara,mingine kibao ipo ambapo ZnZ inaburutwa itake isitake, ndio maana comment yoyote kuhusu ZnZ kwao its so bitter and they take it so emotional na kutaka kutunisha misuli.

Suala la vitambulisho vya Taifa, na waZanzibari lazima watapata sio kama raia wa huko,bali ni wa Tz kama watu wa Dodoma na Tabora tuu, huku kutunishiana misuli ni sawa na Sisimizi anamtunishia misuli Tembo.

Something is always better than nothing.
 
katika kipindi cha wiki moja au mmbili nimeona kwenye Magazeti, kwanza akitutafutia, mkopo Eu kwa ajili ya Vitambulisho ya Kitaifa, na Pia Akielezea Mradi mzima pamoja na Matumizi ya Hiyo Billioni 200, kana kwamba yeye ni serikali au anaujuzi zaidi ya watu wetu serikali. ikiwa ni hivyo kwanini wasimpe consutancy ya kuiongoza serikali, pale kivukoni badala Pinda kuwepo pale, basi Gotham International na Bendera Yao wakae pale. na Treasury pia etc etc. pale jumba Kubwa tunaweza kumuacha JK , kama symbol ya utaifa wetu.
 
Ni Karume baada ya mapinduzi, akamwambia Mwalimu, Waingereza wanaweza kuja kututia kibano, dawa ya haraka ni tuungane "WEWE RAIS MIMI MAKAMO". Huo ndio mzizi. Maandishi ndipo yakafuatia.


hahahaha So funny! wewe rais mimi makamo! hivi kuna watu waliwasikia
 
First Zanzibar has no National IDs, only a resident IDs

All the two countries they have quote (KENYA and Israel) are now moving to smart card system with much higher costs than Tanzania although they already have the Institution in place...

omarilyas

AS YOU WISH SIR godoro au tandiko ni kilaliotu
 
Back
Top Bottom