Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Sawa Pasco. Ndege mjanja siku zote hunasa katika tundu bovu. Ndiyo maana Wazanzibari wakakutangulieni kuwa na Vitambulisho vyao vya Mzanzibari. Ndivyo hivyo unavyoambiwa kuwa hata quality yake ni bora kuliko mnavyotaka kutengeneza nyinyi.

Sasa kwa Wazanzibari tutathamini vya U-zanzibari kwanza , ndio tuvitupie jicho vya Tanzania . Ni maana kwetu sisi tunasema ni Wazanzibari kwanza na Watanzania halafu.
 
Mkuu KUhani, katika hili naomba kutofautiana. Angalia sopurces za story ni mbili tofauti, kwa hiyo contradiction iiyopo inatokana na statement za sources, si utungajiw a mwandishi au chombo cha habari. Hapa wa kuwashangaa ni watawala ambao wanashindwa kueleza kinagaubaga iwapo Zanzibar inahusika katika mpango huu au la

Mkuu Mpita Njia, Kuhani hapa yuko sahihi. Gazeti la tarehe 21/02 limeripoti kuhusu Zanziba kukataa kuwemo katika mradi wa vitambulisho. Gazeti dada la kampuni hiyo hiyo kesho (22/02) yake linaripoti Dr. Kyaruzi wa kampuni ya kuishauri serikali anasema hata Zanziba wamo. Hapa alichosema Kuhani, ni vipi waandishi wasimhoji huyu Dr. Kyaruzi kuwa siku zilizopita Waziri Nyanga na Mkurugenzi Ame walishasema kuwa hawakubaliani na hilo la vitambulisho vya Taifa kupelekwa hadi Zanziba.

Waandishi wa habari wanatakiwa kuwa wapembuzi, hawatakiwi kuchukua habari tu kama ilivyo. Ndio maana mashirika kama BBC, wakisikia jambo na wakamoji mhusika, hujitahidi kumpata wa pande wa pili kumsikia naye atasemaje. Sasa hawa walikuwa na Dr. Kyaruzi wanashindwa hata kumuuliza jambo waliloandika siku moja kabla.

Hii inanikumbusha kauli wanazopenda toa kuwa tulipomtafuta simu yake ilikuwa haipatikani, japo hawakumtafuta mhusika.
 
Mkuu KUhani, katika hili naomba kutofautiana. Angalia sopurces za story ni mbili tofauti, kwa hiyo contradiction iiyopo inatokana na statement za sources, si utungajiw a mwandishi au chombo cha habari. Hapa wa kuwashangaa ni watawala ambao wanashindwa kueleza kinagaubaga iwapo Zanzibar inahusika katika mpango huu au la

Mpita Njia ndugu yangu, unakosea. Daily News wamevurunda big time.

Kazi moja kubwa ya chombo cha habari ni kutafuta na kuripoti facts. Kuripoti facts ili kuelimisha jamii.

Gazeti likiambiwa na source moja (viongozi wa Zanzibar ) kwamba Zanzibar wamekataa mradi wa vitambulisho, halafu kesho yake likaambiwa na source nyingine (ofisa wa kampuni yenye mkataba wa kuishauri Serikali ) kwamba vitambulisho ni suala la Muungano inabidi gazeti lifanye fact checking, na kwa hapa ilikuwa ni kiasi cha kumuuliza huyu source wa taarifa ya siku ya pili kwamba mbona Zanzibar wamesema kwamba hawamo, je makubaliano ya sheria ya Bunge hayawahusu Zanzibar? Kitu kama hicho.

Halafu kama toleo la siku ya pili lisingepata jibu, the very least they could have done ni kuandika sentensi moja tu "katika toleo la jana ofisa Fulani bin Fulani wa serikali ya Zanzibar alinukuliwa na gazeti hili akisema kwamba Zanzibar wamekataa mradi huu wa vitambulisho..." Simple as that. Faida yake nini hiyo sentensi? Umuhimu wa hiyo sentensi ni kwamba msomaji anajua, anhaa, kumbe hii stori niliyoisoma hapa sio conclusive, na kwamba bado kuna mabishano kati ya pande mbili za muungano. That's the point.

Hapana, Mpita Njia, gazeti haliwezi kuripoti habari mbili zinazojipinga siku mbili mfululizo halafu tukasema eti sources za habari ni tofauti kwa hiyo ni poa. No no no, kazi moja kubwa ya Newspapers ni kuelimisha jamii.
 
Mhhh!!! sasa unachotaka kusema ni kwamba Gotham hawana uhalali wa kufanya consultancy za serikali au serikali haina sababu ya kutoa consultancy kwa Gotham. Ninavyo elewa mimi si lazima kila kitu kifanywe na serikali yenyewe ndio maana shughuli nyingine hupewa consultant. Sasa hoja labda ni nani anapewa na kwa nini? hakuna serikali hata moja isiyo fanya hivyo. Na serikali kuipa kazi hizo Gotham haina maana imeshindwa kazi...aaaghrrrrr
 
Mpita Njia ndugu yangu, unakosea. Daily News wamevurunda big time.

...the very least they could have done ni kuandika sentensi moja tu "katika toleo la jana ofisa Fulani bin Fulani wa serikali ya Zanzibar alinukuliwa na gazeti hili akisema kwamba Zanzibar wamekataa mradi huu wa vitambulisho..." Simple as that. Faida yake nini hiyo sentensi? Umuhimu wa hiyo sentensi ni kwamba msomaji anajua, anhaa, kumbe hii stori niliyoisoma hapa sio conclusive, na kwamba bado kuna mabishano kati ya pande mbili za muungano. That's the point.

There you are. Nilichokuwa nimepinga awali ni kule kuonyesha kuwa gazeti limejipinga lenyewe. Lakini kwa maana ya kwua na background ya kuonyesha kuwa sources wamepingana, hapo wamechemka kweli
 
Kwani serikali ni nini? Ni wale wanaopanda ST..? au ni watu wa aina gani? Huyu Gotham ni sawa na mtumishi wa serikali ingawa ajira yake si kupitia utumishi. Na inaelekea an PR nzuri na watu wengi pia ni mbunifu wa biashara. Hapa serikali imetumia mbinu ya PPP ingawa ina mapungufu kwa jinsi ilivyotekelezwa.

Kwa ujumla ukisoma kwa makini ni kwamba biashara ya Gotham ilianza hata kabla Gotham Inernational haijaanzishwa. Hapo ndipo utata ulipo.
 
Mkuu Mpita Njia, Kuhani hapa yuko sahihi. Gazeti la tarehe 21/02 limeripoti kuhusu Zanziba kukataa kuwemo katika mradi wa vitambulisho. Gazeti dada la kampuni hiyo hiyo kesho (22/02) yake linaripoti Dr. Kyaruzi wa kampuni ya kuishauri serikali anasema hata Zanziba wamo. Hapa alichosema Kuhani, ni vipi waandishi wasimhoji huyu Dr. Kyaruzi kuwa siku zilizopita Waziri Nyanga na Mkurugenzi Ame walishasema kuwa hawakubaliani na hilo la vitambulisho vya Taifa kupelekwa hadi Zanziba.

Waandishi wa habari wanatakiwa kuwa wapembuzi, hawatakiwi kuchukua habari tu kama ilivyo. Ndio maana mashirika kama BBC, wakisikia jambo na wakamoji mhusika, hujitahidi kumpata wa pande wa pili kumsikia naye atasemaje. Sasa hawa walikuwa na Dr. Kyaruzi wanashindwa hata kumuuliza jambo waliloandika siku moja kabla. Hii inanikumbusha kauli wanazopenda toa kuwa tulipomtafuta simu yake ilikuwa haipatikani, japo hawakumtafuta mhusika.

Jamani, huyu Dr. John Kyaruzi alikuwa kule Tanzania Investiment Centre na sasa tunaambiwa ni Managing Director wa Gotham International, wizi mtupu!!

Nadhani sasa tuanze kumjadili huyu Dr. John Kyaruzi tangu alipokuwa kule UDSM, kisha akaenda TIC.
 
hahahaha So funny! wewe rais mimi makamo! hivi kuna watu waliwasikia
Haya aliyasema Mwalimu sikumbuki ni hotuba gani, ila alikuwa akizungumzia nia ya Karume kwenye Muungano.
Unajua Karume hakuwa msomi na alidhamiria muungano wa nchi moja sio mbili. Ni Mwalimu aliyempinga kutokana na udogo wa Zanzibar, kuungana na lijitu likubwa ka Tanganyika, ingemezwa. Hivyo hata hiyo nafasi ya Zanzibar ya leo, ni Mwalimu.

Kelele za ZnZ sio kwamba hawautaki Muungano, bali wamechoka kuburuzwa. Kama ingeachwa ifanye mambo yake, saa hizi tusingefuata magari Japan wala Dubai, mambo yote yangekuwa Zenj. Ni kwa kulitambua hilo ndio maana URT itajiunga na OIC kwa maslahi ya ZnZ.
 
Mcheki vizuri anafanana na nani, majina sio issue. Chief Burito alikuwa na wake 4 na watoto kibao. Mama Nyerere, Bibi Mgaya alikuwa ndio mke mdogo. Jee wajua wanaotumia jina la Nyerere ni wale watoto wa Bi. Mgaya tuu, Julius Kambarage, Joseph Kisurila na John Kiboko?

Inasemekana Chief alikuwa na watoto zaidi ya 20 ni kina nani hao? Watoto wa Mama Nyerere ndio waliosoma, kwa kusomeshwa na Kaka yake Bibi Mgaya, Chief Wanzagi Warioba. Jee wawajua ndugu wengine wa baba?

Wazee wa kiafrika si unawajua, na majina sio issue, hivi nduguze wa kuzaliwa na Mkulu mnawajua?.

Jamani sorry, inaweza kuwa ni just 'Amaizing Coincidence' and its just my insinuations. No facts!. No facts no right to speak, only to think aloud in black and white.

na John
 
Mcheki vizuri anafanana na nani, majina sio issue. Chief Burito alikuwa na wake 4 na watoto kibao. Mama Nyerere, Bibi Mgaya alikuwa ndio mke mdogo. Jee wajua wanaotumia jina la Nyerere ni wale watoto wa Bi. Mgaya tuu, Julius Kambarage, Joseph Kisurila na John Kiboko?.
Inasemekana Chief alikuwa na watoto zaidi ya 20 ni kina nani hao?.
Watoto wa Mama Nyerere ndio waliosoma, kwa kusomeshwa na Kaka yake Bibi Mgaya, Chief Wanzagi Warioba. Jee wawajua ndugu wengine wa baba?.
Wazee wa kiafrika si unawajua, na majina sio issue, hivi nduguze wa kuzaliwa na Mkulu mnawajua?.

Jamani sorry, inaweza kuwa ni just 'Amaizing Coincidence' and its just my insinuations. No facts!. No facts no right to speak, only to think aloud in black and white.







, na John

Akiwa ni ndugu wa mbali wa mkulu hastaili kupewa kazi hii, unaweza kusema kutakuwa na conflict of interest lakini katika hili yeye hatawajibika kwa mkulu atawajibika kwa watu wengine.

Pia hili la konflikti ofu interest kwa nchi zetu za kiafrika zenye uhaba wa wataalamu sio prayorite sana, cha msingi ni uwezo wa mtu anayekabidhiwa dhamana hiyo na si uhusiano wake na watu katika sirikali.
 
...... Huyu Gotham ................ Na inaelekea an PR nzuri na watu wengi pia ni mbunifu wa biashara.

Kwa ujumla ukisoma kwa makini ni kwamba biashara ya Gotham ilianza hata kabla Gotham Inernational haijaanzishwa. Hapo ndipo utata ulipo.

Jack Gotham ni mhuni tu wa mjini anayejifanya yuko kwenye system. Alipenda saana kukaa Meals Restaurant na Steers (ofisi yake). Ndoto za kuwa consultant wa mradi wa vitambulisho alikuwa nao miaka mingi (toka 1998 au mapema 2000).

My concern here is: what are Jack's professional qualifications that'd make him write a feasible feasibility study of such a big project??
KAMA ANASOMA HUMU AJITETEE

Huyu bwana ni mzanaki na yuko hapo Gotham International kama bouyer.
 
wakuu shikamooni.nimepata habari kwamba vitambulisho vya taifa ni kupata kwa kuchangia hela,je ni kweli.naomba maoni.
 
Mhhh!!! sasa unachotaka kusema ni kwamba Gotham hawana uhalali wa kufanya consultancy za serikali au serikali haina sababu ya kutoa consultancy kwa Gotham. Ninavyo elewa mimi si lazima kila kitu kifanywe na serikali yenyewe ndio maana shughuli nyingine hupewa consultant. Sasa hoja labda ni nani anapewa na kwa nini? hakuna serikali hata moja isiyo fanya hivyo. Na serikali kuipa kazi hizo Gotham haina maana imeshindwa kazi...aaaghrrrrr

u 've take it the wrong way, mimi nimemsifia na kumuona anaakili saana, ndio maana ameweza kutupa mchanganuo wa hizo nillioni 200 wakati waziri mkuu na mawaziri husika hawakuweza kuona hilo, pili ameweza kuongea na donors ili watusaidie wakati mkulo au waziri wa mambo ya ndani ameshindwa, conclusion apewe aidha consultancy ya kuiendesha serikali au to sub-contract uendeshaji wa serikali maana wahusika wameshindwa, kuanzia kwa Pinda kwenda chini, lakini kwa sababu ninaheshimu Watz na Mamlaka zake, then Raisi aendele kuwepo JK wetu.
 
ILI SAKATA LA VITAMBULISHO VYA URAI LIKOJE JAMANI !!!!NI KIINI MACHO AU NDO TUMELIWA ???

Ni vyema Waziri mwenye dhamana ya Urai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakatusaidia kupitia Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria wa Serikali (CPD) kwenye hili sakata la vitambulisho vya uraia.

Tafiti za sisi wachache "wafia nchi" zimebaini kuwa ipi sheria inaitwa "THE REGISTRATION AND IDENTIFICATION OF PERSONS ACT, ( No. 11 of 1986)Cap. 36 R.E.2002. Madhumuni makuu ya Sheria hii ni kuweka utartibu wa kusajiri watanzania na kutoa vitambulisho vyao na masuala maengine yanayohusiana " to provide for the registration of persons in the United Republic, the issue to them of identity cards and for connected purposes".

Kifungu cha 2 cha Sheria hii kinasomeka hivi kwa lugha ya kigeni:

" This Act shall come into operation on such date as the Minister may, by notice published in the Gazette, appoint"

(yaani kwa kibongo, inamaanisha " Sheria hii itaanza kufanya kazi baada ya Waziri husika kutangaza tarehe ya kuanza kazi kwenye Gazati la Serikali".)

Kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria hii, inatamkwa kuwa Sheria inapaswa kutumika kwa Tanzania Visiwan na Tanzania Bara.

Kifungu cha 5 cha Sheria hii kinampa Waziri mwenye dhamana ya Raia kuteu Msajili wa Urai (Ragistrar) Registration of persons.

Kifungu cha 7 cha Sheria hii kinamataka mtu yeyote anayeishi Tanzania baada ya kuanza kazi kwa sheria hii na amabye ametimiza miaka kumi na nane (1 kuomba kusajiliwa chini ya sheria hii.

Kwa kimombo kinasomeka " 7(1) Subject to subsection (2) and to other provisions of this Act, every person of or above the age of eighteen years who, on or after the commencement of this Act, is or resides in the United Republic and to whom this Act applies may make an application for registration in pursuance of this Act"

Kifungu cha 9 kinaweka utaratibu wa kuwasilisha maombi ya usajili. Sehemu ya Tatu (III) ya Sheria hii inaweka utartibu wa kutoa vitambulisho Kifungu na rejea ya kifungu cha 10 inaonyesha kuwepo kwa aina mbili ya vitambulisho (two types of identity cards) kwa kadiri ambavyo Waziri husika atakaovyoona inafaa ambavyo ni (a) citizens of the United Republic;
(b) aliens resident in the United Republic;

Kifungu cha 10(2) kinabainisha kuwa kitambulisho kitatolewa baada ya mwombaji kulipia gharama na kusajiliwa.

" (2) Upon the registration of a person in accordance with this Act and upon payment by him to the registration officer, of any fee payable in that behalf, the registration officer shall cause to be prepared and issued to that person an appropriate identity card"

KIINI MACHO NA CHA KUSIKITISHA NI KUWA:

  • Wakati utaratibu wa kutafuta wazabuni wa kutengeneza vitambulisho unaendelea, rejea kwenye vitabu vya sheria za Tanzania ambazo zimefanyiwa mapitio mwaka 2002 (Revised Edition) na kuchapishwa na kampuni ya Juta ya Afrika ya Kusini chini ya ufadhili wa Serikali ya Sweden, inaonyesha kuwa Sheria hii itakayosimamia usajili wa Wabongo na pia Vitambulisho vyao hajawahi kutangazwa kutumika hapa nchini tokea kutungwa kwake mwaka 1986 (Not yet in force????).
  • Aidha, hata kama sheria ingekuwa inatumika, bado ingepaswa kwa utartibu uliowekwa na sheria, kwa mtu kupata kitambulisho ni lasima kwanza asajiliwe na ndipo kitambulsho kitolewe.
  • Kama sheria haijatangazwa kufanya kazi ni wazi hakuna ofisi za watendaji akiwemo Msajili, Je ni nani anayeratibu mchakato wa sasa wa vitambulisho vya raia??? Je Waziri mwenye dhamana ya Uraia anapata wapi nguvu hii ya kusimamia sheria isiyofanya kazi???.
EBU MTUSAIDIE JAMANI, ILI ZOEZI LA KUPATA WAZABUNI ILI WATENGENEZE VITAMBULSHO SASA VITASIMAMIWA NA SHERIA GANI???
 
sisi wazanzibar tushachoka.

kwani hapa kuna wakenya, waganda, wacongo, warwanda , warundi na wazanzibara.

wala hajulikani mzanzibar karume kasema hawa ndio wazanzibar.

usistaajabu ukiambiwa mtu kazaliwa na mdoriani mwera?
 
Shukrani kwa kutufumbua macho kuhusu suala la vitambulisho kisheria. Cha kufanya ni kulikabidhi kwa watu kama Dr. Slaa wa Chadema alifanyie kazi bungeni. Kama kinachofanyika ni kinyume cha sheria mchakato wa vitambulisho unapaswa kusimama mpaka hapo matakwa ya kisheria yatapokuwa yametimizwa.
 
Ndugu watanzania wenzangu kutokana na hali ya kwamba ktk nchi yetu sasa tunakaribia kuanza kutoa vitambulisho kitu ambacho mimi binafsi naona nicha muhimu sana kwetu kama nchi, nemekuwa na pendekezo moja ambalo nnaona ni lazima tulifwate ktk zoezi hili la utoaji wa vitambulisho nalo ni kwamba ni lazima tutoe vitambulisho tofauti kwa watu tofauti nikimaanisha kwa mfano watu ambao hawana asili ya Tanzania (waarabu, wahidi, wazungu, wasomali, n.k) tuwape vitambulisho tofauti na sisi wenye asili ya hapa nchini kwetu lengo ni kwamba kuweza mwishowe kutoa tofauti kati yetu sisi na wazaliwa wageni.

Je sijui ninyi mna mawazo gani juu ya hilo...
 
najua kuna tofauti kati ya uraia wa kuzaliwa na uraia wa kuomba, ukifika nchi kama botswana, hivyo vitambulisho vinakuwa na herufi C kwa mzaliwa wa pale na F kwa wale wenye uraia wa kupewa

kwa hiyo kuna mambo ambayo ni sensitive ambayo yanawahusu wenye C tu, ingawa utakuwa raia lakini kwa sababu una F basi unakuwa na limitation ya vitu
 
Kijakazi ktk Mawazo ya Kibaguzi haya no.1....

Haya mawazo yako yalikuwepo wakati wa Tanganyika under MKOLONI...na yalifutwa chini ya Tanganyika Huru. Wakati hao ulio wataja walikuwa 1st Class citizen. na walikuwa na shule zao....

Kijakazi baada ya mawazo yako kufanyiwa kazi unataka nini next...?wawe na shule zao? maduka yao?...Masoko yao?....mitaa yao?

Tukimaliza hayo itabidi tuje 2nd Phase "Wakuja wote warudi kwao Mikoani" kila mmoja arudi Mkoani kwake...kwani mmekuja kuwanyonya wenyeji..."wazawa wa Dar es Salaam"...

Baada ya hapo itabidi tuvunje Muungano, maana wenzetu wa Zenj wao Mixing yao na rangi yao sijui utasemaje..."baada ya hapo tutarudi like Rwanda/Burundi tukiona wakuja hamuwezi kuondoka mijini kwetu...."...wataka twende Huku...?

Hivi ni nini hasa kinachokukera kuwaona watu wa sampuli uliotaja?
 
By the way Huu MRADI tumechangia kule kuwa HAUFAI...na hao wananchi ambao wanakaa kusubiri mlo wa siku moja....wala hawana mpango nao....Wenye Kuhitaji vitambulisho ni nyie mnaosafiiri kwenda nje au mliopo DSM mnakwamishwa ktk bank....Wakulim kule Karatu wala hawatonufaika na huu mradi ulioanza kufunikwa na UFISADi....

Kijakazi waambie hao wanaoona Wakubwa zako au Viongozi wako etc... wa Vitambulisho kuwa pesa za mradi huu Wanunue Matreka kila Kijiji kiwe na Trekta lake....sehemu za ukame wapeleke pipes za maji kumwagilia...
 
Back
Top Bottom