GAME THEORY,
Mkuu hapa naungana sana na DUA ktk hili,
Hivyo vitambulisho ulivyovitaja, kama Driver's licence, Cheti cha ndoa na kadhalika ni vitambulisho ambavyo hutolewa kwa mtu yeyote sio lazima uwe Mtanzania. Nchi nyingi duniani zinatumia vitambulisho hivi kwa maswala maalum yanayohusiana na vitu hivyo tofauti na ID ya Uraia ambayo lengo lake ni uhtibitisho wa Uraia wa mtu na huwa ni moja ya utaratibu wa LAZIMA kutolewa kwa kila raia tofauti na vitambulisho vingine.
Leo hii Bongo huwezi kutenganisha kati ya raia na mhamiaji ambaye yupo nchini kisheria ama bila sheria na wote hawa wanaweza changia sana ktk mapungufu ya huduma nyingi kwa wananchi wake. Mbali na yote haya ni muhimu kuyatazama mambo ambayo yametuweka hapa tulipo, waswahili husema kama hujui ulikotoka ni vigumu sana kuelewa unakokwenda nikiwa na maana kukwaza kwetu kiuchumi kuna mengi sana ambayo tumerudi nyuma kuyatazama na taratibu tunayatafutiana dawa. Iwe maswala ya Maazimio, Ufisadi, Mikataba na kadhalika.
Bila kadi za Uraia serikali inaweza kushindwa kutoa huduma kwa wananchi ambazo wako entitled to na pia kuweza recognize una deal na wananchi wako wangapi ktk kila sehemu.
Kama nilivyokwisha sema Paasport haitolewi kwa kila mtu kama kitambulisho cha kutumia ktk shughuli za kila siku, passport ina malengo yake pamoja na kwamba ni moja ya kitambulisho..Huwezi kuwalazimisha wananchi kubeba passport kila wanapokwenda wala sio lazima kisheria kila raia kuwa na passport ingawaje kila raia yuko entitled to have one.
Kisha umemzungumzia mtu kama Mkapa ktk issue hii kwamba isingeweza kuikubali nadhani mkuu hapa unatuonyesha wazi Mkapa ni mtu wa aina gani..Unajua kuna wale wanaoiba kukithiri bila matunda bila ujenzi wa kitu kwa raia zake... huyu ndiye Mkapa. Macho yake yote yalihusiana na FEDHA tu.. Kila penye fedha ndipo aliweka attention yake aidha kuboresha production lakini fedha haziendi ktk mfuko wa serikali..Mkapa ni sawa na mfanyabiashara tajiri anayefikiria Utajiri lakini fedha zake zinakwenda kwa Malaya akiacha familia yake ikichemka kila siku.. Ni mtu ambaye hajui hata ana watoto wangapi wala hawezi kuona haja ya kufahamu ana watoto wangapi kwa sababu kutoa huduma kwa wanawe sio moja ya kazi zake, ndio maana alituita sisi wote (raia) wapumbavu kutegemea yeye kuwa mlezi wa Taifa...