Omuhabhe,
REMEMBER: A GOOD MANAGER DOES NO WORK; SIMILARLY A GOOD LEADER DOES NO WORK!
NADHANI Tutafikwa zaidi maana safari hatujaanza, papa hapa tumeanza kugombea daladala hii ya Tanzania huku wengine wakipitia mlango wa dereva kwa ruksa ya dereva; wengine wakitumia mitulinga kuingilia madirishani; na wanafunzi wakijipanga kupiga au kuzipiga na waheshimiwa watongozaji dada zao na shangazi zao na magelifiend wao -sio girlfriend!
Kwa hiyo hilo la TUTAFIKA sahau. Nishawahi kusema na nitarudia kusema hakuna atakayeweza kuiongoza Tanzania vyema kama anashindwa tu kuhakikisha kuwa kuna utawala wa kisheria barabarani na sehemu mbali za kutolea huduma. Wewe kwa fikra zako kweli unaona tuna uongozi hapa? Uongozi ulioshindwa hata kuwatia adabu daladala kufuata sheria, kuvaa mavazi waliyoamriwa na watu kusafiri kwa heshima na adabu-wakati huu ambapo hata nyie mliokuwa na magari sasa mnalazimika kupanda daladala!
Huruma paka bwana, lakini ukimvuta mkia lazima akuache na alama.
Na Rais safi, ndugu yangu sio suala la sura au ucheshi au kuwaonea unaowapenda huruma. Mkumbuke bada wa Taifa hakuwa na mswalie nani wala nani hata kwa mwanawe wa kumzaa!
Ninachosema ni kuwa ipo miundo-mbinu ya kitabia, kitawala, kisheria, taratibu na maingiliano katika jamii ambayo bila kuwepo utawala bora utatoka midomoni kwa wale wanaojisifia kwa maneno lakini sio unaonekana, sio kwa vitendo ng'oo!
Na haya yote pia yanategemea unazungukwa na watu wa namna gani; unashibishwa ukweli na hoja za kimsingi kiasi gani; unayaona na kuyasikia kwa macho kwa kiasi gani? Kama umezungukwa na wapaka mafuta na marashi ndugu yangu umeliwa!
HALAFU Bwanae kuna hili la delegation na decentralization. Unakumbuka mwalimu nani alivyotufundisha kwenye menejimenti au umesahau. Nikukumbushe. Ticha wetu maarufu enzi zile mlimani na huku kwenye kutafuta maisha, yaani, hapa mjini ambaye nilionana naye jana tu akitembea kwa mguu nikamuuliza vipi gari umeuza akasema la. Lipo nyumbani. Sikutaka kumuuliza zaidi. Mtu mwenye fikira za kina na za kindanindani zinazoweza kuibadili nchi hii eti kasahaulika kwa sababu tu haandiki tena magazetini lakini wallahi vile yote aliyoyaandika yakifanyiwa kazi nusu ya matatizo yetu-nej, NJE!
Yeye alituambia: ' A GOOD MANAGER DOES NOT WORK!' Ambayo sasa itafsiri hivi: " A GOOD LEADER DOES NOT WORK!"
Unakumbuka sote tulibaki na sura ya KUULIZA? Kisha akatungua macho na masikio: ' Kiongozi mzuri bwana hufanya kazi kupitia kwa watu walio chini yake na sio vinginevyo!'
Kwa hiyo ndugu ukishamuona mtu NI FAILURE kwenye DELEGATION and DECENTRALIZATION- tambua hakuna teamwork hapo na tena ni ndoto za Alinacha kabsaaa kabsaaa kudhani eti A LONE PLAYER can equal a team, not to mention a dream team like USA Basketball teams kama vile CHIGACO, Uttah Jazz and so on.
Benki Kuu yeye, Richmond yeye, mikoa yeye, Muafaka yeye, Madini yeye, Mchuchuma na mchuchumaaa yeye, umeme na WALAJI WA TANESCO yeye, na MICHEZO YEYE. Hao mawaziri wake wanafanya nini yarabi? Hao wakuu wake wa mikoa wanafanya nini yarabi, Bodi husika zinakula na kunanihii tu.... laini performance management na contracts ziko wapi.... Management by Objectives iko wapi?
Tuzungumzeni, lakini, nawaambia wallahi sio mimi wala sio wewe....mtu mmoja hawezi kuinusuru achilia mbali kuifanya nchi hiyo iwe kweli inayoelekea kwenye njia ambayo tutaanza kuona unafuu tena kwangu, kwako na kwa yule.....