Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Du hii survey ya hotuba inafungwa 2036?,. Haya wale mtakaokuwepo kila la kheri siku ya ufungaji.

mpaka mwakwa huo hata kwenye historia hii hotuma itakuwa haipo na vitukuu vyetu vitakuwa havijui kikwete ni nani
 
Safi sana mkuu. Uki forge document na kujipatia fedha hata kama hizo fedha ni za nani ni KOSA LA JINAI.

Sasa mkuu anaposamehe kosa la jinai kweli nakuwa sielewi!
 
Kenge mla Mamba ndo umepost hii thread? Hapa jamnvini tunaweka vitu venye busara maana watu walio humu ndani na wale wasomaji wasio members wana hadhi zao. Usitake kuuliza maswali ya kupotezea watu muda.

Tatizo la watanzania wengi hatujui maana ya muda wala kutunza na kuheshimu muda. Jaribu kuukomboa wakati. Ndiyo maana hata JK jana alisema hatuba ni saa tano, yeye akaanza saa sita na dakika 20 na kumaliza saa tisa na dakika 37 badala ya saa saba na robo kama ilivyokuwa tangu awali.

Yaani hata viongozi muda wanauchezea ndiyo maana hata wajanza wanapata muda wa kukaa kupanga mipango ya kukwapua mihela kiulaini. Wakishtuka wanakurupuka utafikiri panya kakamatwa na mtego. Jamani tuwe serious. Moderator ondoa hii maana tangu jana tumechangia sana kuhusu hotuba. Mwanzishaji anashauriwa aende kupitia thread zote zinazohusu hotuba na majibu atapata.

Kama ni rearcher mzuri then observe comments, collect results then atapata kila kitu, mean, median, upper and lower limits, coefficients, etc. then from there utafanya analysis then reporting. and concluding. Thanks.
 
NIMESHINDWA kufanya tathmini halisi lakini pengine tunaweza kujadili maswali niliyobakia nayo baada ya Rais kumaliza hotuba yake na shukrani za Spika kwa Rais:

. Washauri wa rais hawamwandai rais kiasi cha kutosha?

. Hivi kuna vitu asivyovifahamu kwamba ana uwezo wa kuvibadili kwa kufuata katiba na sheria za nchi?

. Tulianza kwa kuwapa watu matumaini makubwa sasa haionekanai kama visingizio vimeanza?

. Watu wana uwezo wa kujiwezesha wenyewe kweli. Au kuna miundombinu aina mbalimbali ambayo serikali inatakiwa kuiweka na kuwepo na ufuatiliaji wa karibu wa utendaji wa watumishi wa umma?

. Baada ya kulazwa chali na ahadi za Muafaka Zanzibar hivi Wazanzibar wana hamu na pendekezo jipya?

. Kama Zanzibar ingelikuwa na serikali ya mseto madai ya Zanzibar kuwa nchi yangejitokeza kwa mtindo huu huu tuliouona?

. Je, matatizo yetu mengi na vilio vya wananchi vinatokana na ukweli kuwa bado hatujaweza kuwa na chachu ya kuchochea

uanzishwaji na uendelezaji wa ujasiliamali na uzalishaji mali kwa kiwango cha kuridhisha ambapo faida itaanza kuwafikia hata wanyonge na masikini katika jamii?

. Tumeona mbunge wa Upinzani Moshi anavyojitahidi kuleta maendeleo, je, CCM na vyombo vya dola na taasisi za serikali vinahusika kwa kiasi gani katika kuzuia upinzani kuchangia maendeleo ya wananchi?

. Bwamkubwa hajajua yeye ni rais-maana sehemu fulani za hotuba zinakufanya umuonee huruma maana anaonesha kuonewa au kuzidiwa au kukata tamaa hivi ?

. Bwankubwa hajajua utaratibu wa kutumia vyombo kama bunge na mahakama ili kuzifanya sheria na taratibu za nchi kuchangia maendeleo na sio kuirudisha nchi nyuma?

. Je, kauli kama kuna uwezekano wa Rais aliyepo na ajaye kukurupuka na kusema fulani atiwe ndani na Inspekta Jenerali wa Polisi asiulize lolote lile husuan mtu anashtakiwa kwanini haioneshi kuwa Rais wa nchi hapa Tanzania ana mamlaka au uwezo kupindukia na kuwa uwezo huo ungestahili kuangaliwa upya ili mkuu wa nchi na timu zake asionee watu na watu nao wasiwaonee wao kwa upande mwingine?

Maana nadhani ni muhimu kuangalia vitu vifuatavyo:
-ili kuongoza vizuri lazima ujenge mazingira ya kuwepo kwa aina za sheria zinazochangia ufumbuzi wa matatizo na uchangamkiaji fursa
-bunge linaweza kuketi wakati wowote na kupitisha sheria zinazolinda kwa mfano ufisadi au viongozi wazembe
-ili mradi tu katiba na sheria zinalinda walio wengi

. Suala la Mahakama ya Kadhi linafuata mkondo gani? Hivi hili jambo likionekana kama vile Waislamu wanaonewa na kunyimwa

haki zao za Msingi wakati Wakatoliki wakiwa na ubalozi wa Vatican na kupata upendeleo wa kila aina pamoja na kupewa majengo ya Chuo cha Benki Iringa kwa bei sawa na bure itakuwaje hapo baadaye?

. Hivi hata Waziri anayehusika na michezo hana uwezo wala ubunifu wa kufufua michezo na hasa ile inayoshindaniwa katika olimpiki mpaka rais aseme....au sera ya madaraka kwa wizara na mikoa imekufa na kuzikwa kabisa?

. Hivi kweli tuna uhakika wa kule tulikotoka [umaskini] , hapo tulipo [umasikini] na kule CCM inakotaka kutupeleka [neema kwa wote] ?
 
Kuna kigugumizi cha aina fulani Ikulu kutoa hotuba ya Rais jinsi ilivyotolewa jana katika soft copy ili vyombo vya habari na wananchi waweza kuisoma taratibu na kuichambua. Ka "Nzi" kanasema kuwa hilo ni makusudi ili kwa muda kuzuia uchambuzi mkali wa hotuba hiyo na hivyo wanasubiri mambo yapoe kwanza.....

Kwanini vyombo vya habari visipewe hotuba ya Rais kama ilivyo sehemu nyingine? Huwa ninapata hotuba za Balozi wa Uingereza au wa Marekani hapo Tanzania kabla hawajazisoma kwenye matukio mbalimbali na huwa wanaweka "as prepared"...

Salva anafanya nini Ikulu? Mbona huwa anaharakisha kuitisha waandishi kujibu hoja mbalimbali lakini kubonyeza "Attach" and hit "send" a file ya Doc au PDF ya hotuba ya Rais inakuwa mbinde? Tatizo la Ikulu na mawasiliano yao na wananchi ni nini? GRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRR
 
THis is pure comical!I guess either hotuba rais aliyosoma siyo yenyewe ameibadilisha tuu pale alipokuwa anaisoma ama wao kama Ikulu na huyu hoodwink we have for a President mwenyewe anajua whatever he presented to the people was pure gibberish!

JK alichosoma ama kupresent kwa wananchi kilikuwa a waste of time therefore he is shit scared with the denigration.

Jana was the only time for him to attest to the people that they made the right choice but he botched and now he knows that his days are numbered maana kila kitu kina mwanzo na mwisho!
 
Ndo Tanzania hiyo mzee ...vumi vumi vumilia kidogooo hohooo vumilia kidogo!
 
Hotuba imeeleza mambo ya msingi kijuujuu tu. nadhani mtanzania wa kawaida alipaswa kujua hatma ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za epa, hatma ya mapendekezo ya kamati ya richmond, hatma ya muafaka wa zanzibar, hatma ya wizi unaofanywa na wageni kwenye rasilimali zetu kama dhahabu, hatma ya muungano na mijadala iliyojitokeza, hatma ya mahakama ya kadhi, hatma ya radar.

Sijaona hitimisho kwa yote hapo juu. kwangu mimi sisemi mbaya au nzuri, ninachosema ni hotuba inayoendelea kuleta speculation juu ya maswali yote hapo juu ambayo bado majibu yake hatuna.
 
Yaani tangu jana nimefuatilia na leo masaa zaidi ya 24 baadaye hawataki kutoa; hata Bunge hawakupewa nakala ya soft copy kwa hiyo inabidi watranscribe kutoka kwenye rekodi zao za Bunge ili kutengeneza hansard.
 
Wengi tulisha anza kupotezwa na wa roho wa madalaka...
Jk mlizidi kumuona mjinga nyie ndio mna akili..haya sasa hebu tuambieni...
hii hotuba ya pili ya raisi pale BUNGENI Dodoma....umejisikiaje na unasemaje!?

Ni Nzuri
au ni Mbaya

Duh! Maswali Mengine Bwana! Sasa huku kama sio kutusanifu ni nini......wacha nijinyamazie mie maana jibu ninaloweza kutoa sichelewi nikafungiwa humu..!
 
Omuhabhe,


REMEMBER: A GOOD MANAGER DOES NO WORK; SIMILARLY A GOOD LEADER DOES NO WORK!

NADHANI Tutafikwa zaidi maana safari hatujaanza, papa hapa tumeanza kugombea daladala hii ya Tanzania huku wengine wakipitia mlango wa dereva kwa ruksa ya dereva; wengine wakitumia mitulinga kuingilia madirishani; na wanafunzi wakijipanga kupiga au kuzipiga na waheshimiwa watongozaji dada zao na shangazi zao na magelifiend wao -sio girlfriend!

Kwa hiyo hilo la TUTAFIKA sahau. Nishawahi kusema na nitarudia kusema hakuna atakayeweza kuiongoza Tanzania vyema kama anashindwa tu kuhakikisha kuwa kuna utawala wa kisheria barabarani na sehemu mbali za kutolea huduma. Wewe kwa fikra zako kweli unaona tuna uongozi hapa? Uongozi ulioshindwa hata kuwatia adabu daladala kufuata sheria, kuvaa mavazi waliyoamriwa na watu kusafiri kwa heshima na adabu-wakati huu ambapo hata nyie mliokuwa na magari sasa mnalazimika kupanda daladala!

Huruma paka bwana, lakini ukimvuta mkia lazima akuache na alama.

Na Rais safi, ndugu yangu sio suala la sura au ucheshi au kuwaonea unaowapenda huruma. Mkumbuke bada wa Taifa hakuwa na mswalie nani wala nani hata kwa mwanawe wa kumzaa!

Ninachosema ni kuwa ipo miundo-mbinu ya kitabia, kitawala, kisheria, taratibu na maingiliano katika jamii ambayo bila kuwepo utawala bora utatoka midomoni kwa wale wanaojisifia kwa maneno lakini sio unaonekana, sio kwa vitendo ng'oo!

Na haya yote pia yanategemea unazungukwa na watu wa namna gani; unashibishwa ukweli na hoja za kimsingi kiasi gani; unayaona na kuyasikia kwa macho kwa kiasi gani? Kama umezungukwa na wapaka mafuta na marashi ndugu yangu umeliwa!

HALAFU Bwanae kuna hili la delegation na decentralization. Unakumbuka mwalimu nani alivyotufundisha kwenye menejimenti au umesahau. Nikukumbushe. Ticha wetu maarufu enzi zile mlimani na huku kwenye kutafuta maisha, yaani, hapa mjini ambaye nilionana naye jana tu akitembea kwa mguu nikamuuliza vipi gari umeuza akasema la. Lipo nyumbani. Sikutaka kumuuliza zaidi. Mtu mwenye fikira za kina na za kindanindani zinazoweza kuibadili nchi hii eti kasahaulika kwa sababu tu haandiki tena magazetini lakini wallahi vile yote aliyoyaandika yakifanyiwa kazi nusu ya matatizo yetu-nej, NJE!

Yeye alituambia: ' A GOOD MANAGER DOES NOT WORK!' Ambayo sasa itafsiri hivi: " A GOOD LEADER DOES NOT WORK!"

Unakumbuka sote tulibaki na sura ya KUULIZA? Kisha akatungua macho na masikio: ' Kiongozi mzuri bwana hufanya kazi kupitia kwa watu walio chini yake na sio vinginevyo!'

Kwa hiyo ndugu ukishamuona mtu NI FAILURE kwenye DELEGATION and DECENTRALIZATION- tambua hakuna teamwork hapo na tena ni ndoto za Alinacha kabsaaa kabsaaa kudhani eti A LONE PLAYER can equal a team, not to mention a dream team like USA Basketball teams kama vile CHIGACO, Uttah Jazz and so on.

Benki Kuu yeye, Richmond yeye, mikoa yeye, Muafaka yeye, Madini yeye, Mchuchuma na mchuchumaaa yeye, umeme na WALAJI WA TANESCO yeye, na MICHEZO YEYE. Hao mawaziri wake wanafanya nini yarabi? Hao wakuu wake wa mikoa wanafanya nini yarabi, Bodi husika zinakula na kunanihii tu.... laini performance management na contracts ziko wapi.... Management by Objectives iko wapi?

Tuzungumzeni, lakini, nawaambia wallahi sio mimi wala sio wewe....mtu mmoja hawezi kuinusuru achilia mbali kuifanya nchi hiyo iwe kweli inayoelekea kwenye njia ambayo tutaanza kuona unafuu tena kwangu, kwako na kwa yule.....
 
It is a fact that even Samuel Sitta was disappointed by the damn speech.
 
Yaani tangu jana nimefuatilia na leo masaa zaidi ya 24 baadaye hawataki kutoa; hata Bunge hawakupewa nakala ya soft copy kwa hiyo inabidi watranscribe kutoka kwenye rekodi zao za Bunge ili kutengeneza hansard.
Nashukuru bado upo, hata humu unaweza kutema cheche siyo lazima kwenye jarida la cheche. Vumilia mzee hata Roma haikujengwa kwa siku moja!
 
Yaani tangu jana nimefuatilia na leo masaa zaidi ya 24 baadaye hawataki kutoa; hata Bunge hawakupewa nakala ya soft copy kwa hiyo inabidi watranscribe kutoka kwenye rekodi zao za Bunge ili kutengeneza hansard.
Mwanakijiji,

Nani kakwambia alikuwa anasoma Hotuba? Kwa ninavyofikiria ni kuwa JK aliandaa notice mwenyewe ambazo alikuwa anazisoma via Teleprompter na zilikuwa kwenye mtiririko anaoutaka yeye na sasa jamaa wapo wanahangaika kusikiliza Audio na kuandika kazi ambayo ni ngumu kwa wengi!

Got me?
 
TUNAWALETEA MKULIMA WA KISASA
Mkulima wa kisasa Mfugaji wa kisasa..... Ukisikia hapa kwetu Tanzaniaaaa wananchi X 2
.......Ohooooo mkulima wa kisasa Tanzania
.......Ohooooo mfugaji wa kisasa Tanzania
 
TUNAWALETEA KIPINDI CHA MKULIMA​
Mkulima wa kisasa Mfugaji wa kisasa..... Ukisikia hapa kwetu Tanzaniaaaa wananchi X 2
.......Ohooooo mkulima wa kisasa Tanzania
.......Ohooooo mfugaji wa kisasa Tanzania

umekusudia nini sheikh..... au una maanisha mambo ni yale yale?
 
Wanajua imejaa ahadi hewa na michemsho kibao ndo maana wanaogopa kuitoa hadharani.
 
Kenge mla Mamba ndo umepost hii thread? Hapa jamnvini tunaweka vitu venye busara maana watu walio humu ndani na wale wasomaji wasio members wana hadhi zao. Usitake kuuliza maswali ya kupotezea watu muda. Tarizo la watanzania wengi hatujui maana ya muda wala kutunza na kuheshimu muda. Jaribu kuukomboa wakati. Ndiyo maana hata JK jana alisema hatuba ni saa tano, yeye akaanza saa sita na dakika 20 na kumaliza saa tisa na dakika 37 badala ya saa saba na robo kama ilivyokuwa tangu awali. Yaani hata viongozi muda wanauchezea ndiyo maana hata wajanza wanapata muda wa kukaa kupanga mipango ya kukwapua mihela kiulaini. Wakishtuka wanakurupuka utafikiri panya kakamatwa na mtego. Jamani tuwe serious. Moderator ondoa hii maana tangu jana tumechangia sana kuhusu hotuba. Mwanzishaji anashauriwa aende kupitia thread zote zinazohusu hotuba na majibu atapata. Kama ni rearcher mzuri then observe comments, collect results then atapata kila kitu, mean, median, upper and lower limits, coefficients, etc. then from there utafanya analysis then reporting. and concluding. Thanks.


Ama kweli mswahili ame-frustrate kila mtu.



.
 
Back
Top Bottom