Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Ngoja nikupe siri kaka,

Hao jamaa waliozirudisha watapewa tena hizo pesa "zao" kupitia huo mfuko kwa kutumia makampuni hewa tena.

Ngoja na mimi nikaanzishe langu niliite Fairplayer Agricultural products. Ltd Nitakuwa nalima "hewani" na ku process agricultural products!. Dili hilo changamka wewe!

Ni usanii tu kaka.

Fairplayer, surelly you are not a positive thinker nor Fairplayer from yo comments above, hebu jipange tena tunataka inchi ikombolewe sasa na kila mtu ashiriki kwa dhati (though najua ulikuwa unatani, lkn hamasisha inchi ikombolewe.. imetekwa...)
 
BAVICHA, Chuo Kikuu Dom, wampinga JK




na Edward Kinabo na Esther Mbussi



BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), kimelaani maandamano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yenye lengo la kuunga mkono, hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa bungeni wiki iliyopita.

Mkurugenzi wa Vijana Taifa, John Mnyika, alisema Rais Kikwete ameshindwa kuboresha maisha ya vijana katika kipindi cha miaka miwili na nusu ya utawala wake na badala yake amechochea zaidi ugumu wa maisha kwa vijana kuliko wakati mwingine wowote.

"Rais Kikwete amedhihirisha kwamba mabadiliko ya kweli, hayawezi kuletwa na watu walewale, wa chama kilekile, chenye ubovu ule ule, wakiendeleza yale yale, eti kwa ari, nguvu na kasi mpya. Hotuba ya Kikwete imeshindwa kutoa mwelekeo makini wa taifa katika kipindi kilichopita na kilichobaki," alisema Mnyika.

Alisema serikali imeshindwa kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira na hakuna tofauti kubwa kati ya serikali ya Kikwete na ile ya Mkapa katika kukuza ajira kwa vijana.

Alisema wakati Rais Kikwete anajisifu kuwa serikali yake imetengeneza ajira 600,000 ndani ya kipindi cha miaka miwili na nusu, kila mwaka zaidi ya vijana 700,000, wanaingia kwenye soko la ajira.

Akizungumzia suala la wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Mnyika alisema, BAVICHA imefadhaishwa na hatua zilizochukuliwa na Rais Kikwete katika kuwashughulikia wezi hao.

"Wakati rais anatoa msamaha huo kwa mafisadi, vijana wezi wa kuku na vitu vingine vidogo vidogo wamejaa magerezani. Tunataka rais aagize vyombo vya dola ikiwemo mahakama kwa kutumia mapazia ya hizo kampuni yafunuliwe, wahusika watajwe, mali zote zikamatwe mara moja na wahusika wapelekwe mahakamani," alisema.

Katika hatua nyingine, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, wamesema hawajaridhika na uamuzi wa Rais Kikwete kuwaongezea muda wezi wa EPA.

Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Ryoba Mrema alisema, hatua ya kuwanyang'anya hati za kusafiria na kuwafilisi pekee, haitoshi kwani ni sawa na kubariki wizi wa aina hiyo, uendelee.

"Yaani wezi wanabembelezwa kana kwamba hizo fedha walikopa huku wananchi wakiendelea kubaki maskini, sh bilioni 133 ni nyingi sana, zingeelekezwa kwenye mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, zingesaidia kupunguza hata migomo ya wanafunzi kuhusu mikopo inayotolewa kwa matabaka, mara huyu asilimia 40, huyu asilimia 60," alisema Ryoba.
 
Spika ameshaminywa hapo maana ingekuwa aibu kwa JK. Tumeibiwa wadanganyika kwa mara ingine. kazi ipo.
 
Hivi kwa nini Ikulu hawataki kutoa copy ya hotuba hii, hata original copy ambayo wanasema mkuu aliongeza mambo mengine?
 
Hivi kwa nini Ikulu hawataki kutoa copy ya hotuba hii, hata original copy ambayo wanasema mkuu aliongeza mambo mengine?
Muwape Muda,

Walikuwa wako Busy wakiandaa hotuba za RAis akiwa Huko Marekani,si unajua mkulu anapenda hotuba ndefu hivyo akirudi watatengeneza.

Ila unadhani kipindi wakifungua Mziki kwenye Harusi ya Riz waliongea nini??Enyi watanzania msiwa kama wale wasiojua jinsi tunavyotawaliwa
 
MP's wapigwa stop kumjadili Kikwete.

Shauku ya wabunge kuichambua hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa bungeni wiki iliyopita imekwama, baada ya uamuzi wa kuijadili kuzuiwa kwa sasa.

Hatua ya kuzuiwa kwa mjadala huo ambao ulitangazwa kwa mbwembwe na Spika Samuel Sitta wiki iliyopita, tayari kumeibuka mgawanyiko wa mawazo miongoni mwa wabunge ambao baadhi yao wanaielezea hali hiyo kuwa inayotokana na shinikizo au maelekezo ya serikali.

Tamko la kusitishwa kwa mjadala huo lilitangazwa jana na Sitta mwenyewe, ambaye alisema uamuzi huo umeahirishwa kutokana na kile alichokieleza kuwa ni kutokukamilika kwa kitabu cha hotuba kilichokuwa kikiandaliwa kwa ajili ya wabunge.

Katika maelezo yake Sitta, alisema hali hiyo inatokana na baadhi ya mambo aliyozungumza Rais Kikwete kutokuwa katika mpangilio wa hotuba yake, hali iliyosababisha haja ya kufanyika kwa marekebisho.

Alisema wamelazimika kuipeleka hotuba hiyo Ikulu, ili ikafanyiwe marekebisho hayo, hivyo haitaweza kupatikana mapema kwa sababu Kikwete mwenyewe anatarajia kuanza ziara nchini Marekani kuanzia kesho.

Alisema badala yake hotuba hiyo sasa ambayo ilikuwa ijadiliwe Alhamisi hii itapangiwa wakati mwingine kwenye mkutano wa 13 wa Bunge, unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Akizungumzia hatua hiyo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohammed, aliielezea kuwa ni ya kushangaza na itakayosababisha kushuka kwa morali wa wabunge.

"Kusema ukweli, kuchelewesha kujadili hotuba hii si jambo jema kwa wabunge, kwani wangependa waijadili sasa kuliko kungoja hadi Novemba ambapo itakuwa imepoa," alisema Hamad.

Alisema wabunge walikuwa bado wana fursa ya kuijadili hotuba hiyo kwa kutumia kumbukumbu rasmi za Bunge (Hansard) badala ya kusubiri kuchapishwa kwa vitabu hivyo.

'‘Kwa hatua hii na kwa jinsi hali ilivyo, kuna mambo yanatengenezwa pamoja na kusogeza muda ili yale yaliyosemwa kuhusu wezi wa EPA, hasa wale waliopewa muda wa kurejesha fedha hizo ambao inawezekana wakazirejesha kabla ya muda waliopewa, hivyo wabunge hawatakuwa na
jipya kuhusu EPA," alieleza kiongozi huyo wa upinzani bungeni.

Kwa upande wake, Mbunge wa Karatu, Dk.Willibrod Slaa, alisema kuahirishwa kwa mjadala huo kuna athari kubwa kwa taifa, kwani kuna baadhi ya watu wamejitokeza na kuanza kufanya maandamano ya kupongeza hotuba hiyo kwa lengo la kuficha ukweli kuwa ilikuwa na upungufu.

Alisema hotuba hiyo ilipaswa ijadiliwe ingali moto bila kutoa nafasi kwa serikali kujipanga na kufanya mambo yao kisiasa zaidi na hivyo kuipa fursa CCM iendelee kuwa kichaka cha mafisadi ambao kila kukicha huwaza namna ya kutafuna rasilimali za taifa.

"Kuna watu wanaolichukulia jambo hili kijuu juu na wanafikiri kupindua mambo ndiyo ujanja. Hii ni hatari kwa taifa, kwani tuna nyaraka za kutosha kuhusu EPA na mengineyo, hivyo ni vyema wakakaa chonjo," alionya Dk. Slaa.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), aliungana na Hamad na kusema amepigwa butwaa kusikia sababu zilizotolewa na spika ambazo alidai kuwa si za msingi, kwani hotuba hiyo ipo kwenye kumbukumbu za Bunge ‘hansard' na lingekuwa jambo rahisi kutumia kumbukumbu hizo kuijadili.

Alisema kama Bunge litaendelea kushindwa kufanya kazi kwa kutegemea maagizo ya serikali ambayo kimsingi inapaswa kuwajibika kwa Bunge, litakuwa jambo la ajabu na aibu, na huo ndio utakuwa mwanzo wa kudidimia kwa demokrasia na kufifia kwa makali ya Bunge yaliyoanza kushika kasi katika siku za hivi karibuni.

Alisema mpaka sasa, kuna viporo vingi vya taarifa ambazo zinapaswa kutolewa kwa wabunge, lakini hazijatolewa.

Alitaja baadhi ya ripoti hizo kuwa ni ripoti ya kwanza na ya pili ya EPA, ripoti ya kamati ya madini na sasa ni hii ya hotuba ya Rais Kikwete,ambayo alisisitiza haoni sababu yakutojadiliwa sasa.

"Ni lazima tufike mahala, Bunge liache kupokea maagizo ya serikali, kwani sababu zilizotolewa haziridhishi, Bunge lina kumbukumbu zake, zilipaswa zitumike hizo kujadili hotuba ya rais," alisema Zitto.

Naye Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher ole Sendeka, alisema kuahirishwa huko kwa hotuba hiyo kutatoa nafasi kwa wabunge kuipitia kwa makini ili watakapoijadili, waweze kugusa maeneo yote.

Alisema kwa jinsi hali ilivyo, macho na masikio ya wabunge wengi yalijielekeza katika EPA wakati kama wakipata nafasi zaidi, wataweza kuichambua kwa umakini na kutoa mawazo yatakayoweza kujenga nchi.

Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM), alisema uharaka wa Watanzania katika mambo mbalimbali, ndiyo sababu ya kutopatikana kwa suluhu nzuri, na wamekuwa wakitaka watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani bila kujua kwamba kuna taratibu za kisheria ili mtuhumiwa apate fursa ya kusikilizwa.

Alisema tabia ya Watanzania kuhukumu watu kwa hisia, si jambo jema na Rais Kikwete katika hotuba yake kaligusia suala hilo kuwa si vema kumhukumu mtu kwa lengo la kumdhalilisha, kumfedhehesha na kumchafulia jina.

"Rais Kikwete katueleza wazi kuwa nia yake ni kuona watu hawabambikizwi kesi, sasa ni vema tukaacha tabia ya kuhukumu kwa hisia," alisema Shibuda.

Wiki iliyopita Spika Sitta, alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima alisema hotuba hiyo itajadiliwa wiki hii, tena ingali moto, kwani kama ikisubiri kipindi kijacho, itakuwa imepoa na wabunge wanaweza wasichangie vema.

"Bwana mdogo, hotuba ya rais itajadiliwa katika mkutano huu, kwani mchuzi unywewe ungali moto, na nimemuagiza katibu wangu aingize jambo hilo katika ratiba, kabla ya kuliahirisha Bunge," alisema spika wakati huo.

Aidha, katika hatua nyingine, akizungumza jana, Sitta alisema siku ya Alhamisi ya wiki hii (Agosti 28), Waziri Mkuu Mizengo Pinda, atawasilisha utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge, kuhusu kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond.
 
Siamini kama kuna hotuba ya kujadili.

Huyu Rais wetu yabidi ajifunze jinsi ya kuandika kitu kinachoitwa Hotuba. Kama anategemea wengine basi pia inabidi awe na wenye akili ya kuandika hotuba.

Yeye anadhani ni kila kinachochekesha, basi ni hotuba nzuri. Yawe matusi, sawa tu!
Tuendelee kusikiliza lakini mpaka mwisho wa miaka 5, hatutakuwa na lolote la ku-quote toka ktk hotuba zake.
 
Ni kweli hata mimi nilimsikia Spika akisema kuwa vitabu vimepelekwa Ikulu kwa ajili ya kufanyiwa uhariri sasa uhariri wanini kama Hansard walirekodi?si hata TV walitoa live na wengine kuirudia usiku?hapa maji yamezidi unga sasa ugali utaiva? na uji haunyweki kwani watu walilala njaa......

Tatizo usanii ulizidi kwenye ile hotuba wakaogopa kwani wabunge wenye akili zao wange point out usanii ule!
Mfano tofauti katika pesa za EPA zilizorejeshwa tume ilisema ni bil 60 CC ya CCM iliambiwa ni 64 Bil na JK bungeni amesema ni 53 Bil.

JK amesema watuhumiwa wa EPA wamenyang'anywa Pasi za kusafiria wabunge makini watashinikiza Serikali itutajie majina ya hao waliozuiliwa Pasi maana wakiwaona Airport wanasafiri waulize wamesafiri kwa kutumia pasi gani? Na hapa wabunge makini hawata kubali blah blah kwani Serikali inawajua kwa majina hawa watu ndio maana wamechukua pasi zao na pesa 53 Bil "wamezirudisha"

Kuna utata wa kama kweli pesa zimerudishwa au la maana Dr Slaa amesema kuna usanii umefanywa. Pesa za EPA zimekuwa allocated kwenye viombo ambavyo haviwajibiki kwa bunge kwahiyo wabunge kupitia bunge letu tukufu hawatakuwa na access kuona kama kweli pesa hizo zimerudi au changa la macho!

Hapo ndipo Anne Kilango aliposema kabla wabunge hawatakubaki ripoti ya karatasi watataka waoene pesa zikirudi ili zisaidie wananchi! na kama hazitaruri pale bungeni hapatatosha patachimbika.

Wabunge waliomakinika watakumbuka kufichwa kwa majina ya watuhumiwa wa EPA kunatokana na kauli ya mjumbe wa kamati aliyoitoa mwezi march kuwa watuhumiwa wa EPA ni hatari kama magaidi! Hapa wabunge makini wataomba itumike sheria ya ugaidi iliyopitishwa na bunge mwaka 2002 ili kuwabana watuhumiwa ikiwezekana wapelekwe guantanamo bay!

Sipati picha kama wangekosea kuruhusu mjadala wa hotuba ya bwana mkubwa bungeni hakika pasingetosha na pangechimbika kiswawa sawa!

Au mwaonaje wakubwa?
 
Wabunge wang'ang'ania kumjadili Kikwete


*Zambi :Kama Balali alifukuzwa, waliochota EPA wawajibishwe
* Rwilomba: Tunabembeleza wahalifu kurejesha fedha za wizi?
*Zitto : Rais amekosea kupangia matumizi pesa zinazorudishwa

Na Joseph Lugendo, Dodoma

WABUNGE wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, juzi na jana walilazimisha kujadili hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa bungeni Alhamisi iliyopita,mbali ya Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta juzi kutoa kauli ya kusogeza mbele mjadala huo mpaka mkutano ujao wa Bunge Novemba mwaka huu.

Wabunge hao walitumia nafasi ndogo waliyopata kuchangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi tangu juzi na jana iliyotarajiwa kuhitimishwa jana jioni na Waziri wa Wizara hiyo,Bw. Mustafa Mkulo, 'kuchomeka'kujadili hotuba hiyo ya Rais Kikwete na baadae kujadili bajeti ya wizara hiyo.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Kabwe Zitto, alisema Rais Jakaya Kikwete amekosea kupanga jinsi ya kutumia sh. bilioni 133 zilizochotwa isivyo halali katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu (BoT), kwakuwa jukumu hilo si lake kisheria bali ni la Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Zitto pia alisema licha ya kukosea kupanga fedha hizo, hata kuzipeleka katika mfuko wa pembejeo na kukuza mtaji wa Benki ya Rasilimali Nchini (TIB), ni kosa kwakuwa fedha zisizokuwa na mwenyewe, kisheria zinapaswa kupelekwa kwa Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali ambaye kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, atazifikisha bungeni kwaajili ya kupangiwa matumizi.

Mbunge wa Mbozi Mashariki, Bw. Godfrey Zambi (CCM), alisema kwa mtazamo wake, wote waliojihusisha na kuchota sh. bilioni 133 za EPA ni wezi na kuongeza kuwa tukio hilo ndilo lililosababisha aliyekuwa Gavana wa BoT, marehemu Daud Balali kufukuzwa kazi.

"BoT nayo inajiandaa kufukuza watumishi waliohusika, sasa na hawa waliohusika kughushi nyaraka wawajibishwe," alisema Bw. Zambi wakati alipopewa nafasi ya kuchangia hotuba hiyo ya Wizara ya Fedha na Uchumi.

Mbunge wa Busanda, Bw. Kabuzi Rwilomba (CCM) kwa upande, alianza kwa kumpongeza Rais Kikwete kwa hotuba nzuri na kuongeza kuwa serikali inakusanya fedha kwa kubembeleza watu.

Huku akionekana kumjibu, Bw. Zitto, Mbunge wa Iramba Mashariki Bw. Mgana Msindai (CCM) alipongeza uamuzi wa Rais Kikwete kupeleka fedha zilizopatikana kwa wakulima na kuongeza kwamba hata wanaosema kuwa Rais kakosea, wakulima wa majimboni kwao wanashida ya mikopo.

Kwa upande wa Mbunge wa Kongwa, Bw. Job Ndugai (CCM) aliitaka TIB kuweka utaratibu maalumu wa kutoa fedha hizo kwa wakulima kwakuwa kwa taratibu za kawaida za mifuko na benki nyingine, wakulima hukosa mikopo.

Kutokana na msururu wa wabunge hao kujadili hotuba hiyo juzi jioni ambayo ilikwisha tolewa ufafanuzi na Spika Sitta, Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge, Mbunge wa Peramiho, Bi. Jenista Muhagama (CCM) alitumia nafasi yake kama Mwenyekiti kuwazuia wabunge kuendelea kujadili hoja hiyo.

Bi. Muhagama alisema kuendelea kujadili hoja ambayo imekwishapangiwa muda wake kabla ya muda huo ni kinyume na kanuni ya 53 ya Bunge inayokataza kufanya hivyo.

Hata hivyo jana baada ya kipindi cha maswali na majibu, Spika Sitta aliporuhusu mjadala wa kuchangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi uendelee, wabunge walijikuta wakisahau tamko la juzi na kuendelea kujadili hotuba ya Rais Kikwete.

Katika mjadala wa jana, Mbunge wa Viti Maalumu, Bi. Halima Mdee (CHADEMA), alianza kwa kumpongeza Spika wa Bunge, Bw. Sitta kwa kutoa hotuba fupi ya kushukuru baada ya Rais Kikwete kutoa hotuba yake, na kuongeza kuwa japo hotuba hiyo ilikuwa fupi, lakini ilibeba hisia za Watanzania.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu Bi. Susan Lyimo (CHADEMA) alirudia pongezi kwa Spika na kwa hotuba hiyo na kuongeza kuwa ingekuwa mtu mwingine asingesema hivyo na hiyo imedhihirisha jinsi alivyo Spika wa kasi na viwango.

Bi. Lyimo ambaye alikiri uvunja kanuni ya 53 alirudia kauli iliyotolewa na Bw. Zitto kuwa Rais Kikwete alikosea kugawa fedha hizo kwa kuwa jukumu hilo ni la Bunge.

Kutokana na kauli hiyo, Spika Sitta alisimama na kutoa ufafanuzi kuwa Rais Kikwete hakukosea kitu kwakuwa fedha nyingi hutokea wakati Bunge limemaliza muda na hupelekwa kwenye matumizi na taarifa ya matumizi huletwa bungeni.

"Kazi ya Bunge ni kuidhinisha siyo kupanga, zinapotokea fedha nyingine ambazo hazijaidhinishwa wakati Bunge limemalizika hupelekwa sehemu husika kisha taarifa huletwa bungeni," alisema Bw. Sitta.
 
Wamjadili ama wasimjadili nothing is gonna happen!He delivered the insignificant speech and walked out of the parliamentary building all smiles na saa hivi yupo Marekani ana kula raha kwa kwenda mbele so nothing is gonna change!

hawa wabunge hawaoni kama wameshachonga sana its time for actions? Wabunge wengine hawaelewi even what the law says regarding their powers hilo la Zito kwamba Wabunge ndiye wapitishe hayo matumizi ya fedha ni la sahihi ila hao wengine ni ma saddists tuu kama kawaida yao!

Very hopeless to have such people for Leaders!
 
Hawa wamekula hela za EPA:
1. CCM- wakati wa uchaguzi
2. Mkapa-
3. RA
4.Mboma (Meremeta)
Sasa kamata mmojawapo uyaone
 
pesa za EPA zilikuwa zinaliwa kila mwaka. Lakini waswahili walikuwa hawapewi kwa sababu ni limbukeni bana. Maskini akipata expletive hulia mbwata.

Please forgive me my fellow swahili. Watu walipata vichaa pesa nakuwa mingi sana sasa fanya nini anza tamba ovyo. nani gundua kama mtu analala hapana amsha wewe. quote ya gabachori mmoja.
 
Wana JF,

Nilijaribu kufuatilia hotuba ya JK Bungeni na sikusikia sehemu akizungumzia Ufisadi wa Kiwira Coal Mine. Au alizungumzia lakini sikumpata? Kipi kinamfanya awe kimya kwenye wizi wa mchana katika ununuzi wa KCM? Au naye ni Mbia?
 
..ni kwasababu na yeye ana uchafu wake mkubwa kuliko hiyo kiwira.
 
Siku dakika 10 za Spika Sitta zilipofunika dakika 180 za Rais Kikwete!

Chesi Mpilipili Agosti 27, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

NAUNGA mkono (kwa asilimia mia) hoja ya kumpongeza Spika wa Bunge letu tukufu, Mheshimiwa Samuel Sitta kwa 'hotuba' yake isiyozidi dakika kumi aliyoitoa bungeni baada ya ile ya saa tatu na ushee ya Rais wetu, Jakaya Kikwete.

Naamini kuwa Mheshimiwa Sitta anastahili pongezi zetu kwa kuzungumza kile ambacho kilikuwa mioyoni mwa wengi wetu, na kwa maana hiyo kuwakilisha kile ambacho Watanzania wengi wangekizungumzia iwapo wangepata nafasi ya kuzungumza bungeni.

Mheshimiwa Sitta ametumia nafasi yake katika jamii na busara zake kumuambia Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete kile ambacho Watanzania tulio wengi tulitegemea ndio kingekuwa ajenda kuu ya hotuba yake iliyochukua saa tatu na nusu kuhusiana na suala muhimu kabisa la wizi wa fedha za EPA. Tulitarajia angetangaza kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa timu aliyoiunda.

Bila shaka shauku kubwa ya wananchi ya kutaka kujua majina ya watuhumiwa wa sakata la EPA na hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yao ilichochewa zaidi na habari 'zilizovujishwa' na baadhi ya magazeti kwamba kulikuwa na mpango wa kuandaliwa kwa vyumba maalumu kwenye magereza yetu kwa ajili ya wahalifu wa ufisadi!

Kwa hakika, shauku ya wananchi ya kutaka kufahamu majina ya watuhumiwa wa ufisadi ilizidi hata ile muhimu zaidi ya kupaswa kuhoji mtuhumiwa wa wizi anakuwa na hadhi ipi aliyobaki nayo kiasi cha kustahili kuandaliwa chumba maalumu kama yuko hotelini!

Kwa sononeko la wananchi walio wengi, hotuba ya Rais haikuweza kutoa majibu yanayokidhi shauku yao; hususan kwenye suala la kutaja majina ya wanaohusika na ukwapuaji wa fedha za EPA.

Ni kweli kwamba Rais Kikwete alifafanua kwa mapana na marefu kuhusu fedha za EPA. Kwamba hizi hazikuwa fedha zetu bali za makampuni makubwa ya biashara ya nje. Kwamba iwapo wenyewe wangejitokeza na kuzidai, tungelazimika kuwalipa ingawaje kwa sasa hawafahamiki!

Hapa akawa amethibitisha maneno yaliyokuwa yamesemwa wiki kadhaa nyuma na Waziri wa Fedha Mheshimiwa Mustafa Mkullo kwamba pesa za EPA hazikuwa za Watanzania; bali za wafanyabiashara, maneno ambayo yalipingwa vikali na baadhi ya wana jamii.

Nikienda likizo na kumuachia nyumba rafiki yangu na ninaporudi nikakuta ameiba pasi ya kunyooshea nguo, uzito wa kosa la kuiba hauwezi kupunguzwa kwa ndugu kuniambia kuwa kwanza pasi yenyewe sio yangu ni ya jirani! Suala ni kwamba ameiba ndani ya nyumba yangu na anastahili kushitakiwa hivyo.

Rais Kikwete alisema pia kwamba baada ya uchunguzi huo ameamua kuchukua hatua ya kuhamisha akaunti ya fedha hizo kutoka BoT na kuipeleka Hazina ambako zitapelekwa kusaidia shughuli nyingine za maendeleo, zikiwemo zile za kilimo na mifugo kama vile kuongeza ruzuku ya mbolea na dawa za mifugo.

Kwamba pia fedha nyingine zitapelekwa kwenye Benki ya Rasilimali (TIB) kwa ajili ya kutoa mikopo ya muda mrefu na yenye masharti nafuu, lengo likiwa ni mchakato wa kuanzisha Benki ya Wakulima ambayo itachukua muda mrefu kuanzishwa.

Kwamba hata kama fedha hizo hazikuwa zetu, tusingeweza kuziweka Hazina halafu tukawa tunaziangalia tu; bali zingetusaidia kwenye masuala muhimu kama kilimo na pale mwenyewe angejitokeza kuzidai, basi, tungeangalia namna ya kumlipa.

Nina wasiwasi kuhusu mpango huu wa pesa hizi kupitishwa 'juu kwa juu' kutoka kwenye akaunti yenye matatizo ya EPA tunayoaminishwa kuwa zimerudishwa humo na waliozikwapua na kupelekwa moja kwa moja hazina kisha kwenye kuongeza ruzuku ya pembejeo za kilimo na kusaidia mchakato wa kuanzisha Benki Maalumu ya Wakulima.

Nani atahakikisha kwamba zilirudishwa kwenye hiyo akaunti ya EPA in the first place, chambilecho wenye lugha yao?

Nikiangalia mlolongo huu, naanza kuwa na wasiwasi na utekelezaji, na hatimaye, matokeo ya zoezi hili. Hapa kuna kila dalili ya kuzuka matatizo kama yaliyotokea kwenye ugawaji wa 'Mamilioni ya Kikwete' ya kujiingiza waliomo na wasiokuwemo, kama sio kuzusha EPA nyingine tena!

Ninaamini kwamba ni kwa faida yetu kutafakari na kuifanyia kazi kauli ya mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mheshimiwa Wilbroad Slaa ya kutaka pesa hizo kupitia bungeni ambalo ndilo tumelipa mamlaka kisheria ya kugawa pesa za wananchi

Rais pia amesema kuwa baadhi ya watuhumiwa wa ukwapuaji wa fedha za EPA wameshafilisiwa mali zao mbali na kunyang'anywa pasipoti zao ili wasiweze kuingia mitini.

Hakutaja majina ya waliofilisiwa mali zao na kunyang'anywa pasipoti zao. Hii ingetia uzito zaidi hotuba yake. Kwa hakika, huu sio wakati wa kusema juu juu tu kwamba kuna fedha ambazo zimeisharudishwa bila kutaja ni nani aliyezirudisha; achilia mbali mkanganyiko uliopo juu ya tarakimu zinazotofautiana za fedha zinazodaiwa kuwa zimesharudishwa.

Ni vigumu kuelewa Serikali ambayo watendaji wake kadhaa wa ngazi za juu kabisa huko nyuma walishatuambia, mara kadhaa, kuwa mafisadi hawawezekaniki, ghafla leo, ijiamini kiasi cha kutamba kuwa kwa kuwanyang'anya watuhumiwa pasipoti zao na kufilisi mali zao, imewadhibiti!

Toleo Namba 042 la Agosti 13 la gazeti hili kuna taarifa kwamba sehemu kubwa ya fedha zinazodaiwa kurudishwa na watuhumiwa hazijaingia serikalini kutokana na watuhumiwa kutoa hundi za muda mrefu (post dated cheques) ambazo zimehifadhiwa kwenye majalada. Hili halijatolewa maelezo.

Zaidi ya maelezo haya, mategemeo ya Watanzania wengi yalikuwa ni kwa Rais Kikwete kuacha sheria ichukue mkondo wake baada ya timu aliyoipa kazi ya kuchunguza ukwapuaji wa fedha za EPA kumaliza kazi yake nusu na kumkabidhi ripoti nusu pamoja na kwamba hili halikuwa moja ya hadidu za rejea ilizopewa timu hiyo wakati inaanza kazi.

Nasema makusudi 'kumaliza kazi nusu na kutoa ripoti nusu' kutokana na maelezo ya Rais kuwa timu ilikuwa bado ikiwasiliana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) ili kupata taarifa za nje za makampuni tisa ambayo hayakuwa na nyaraka zilizokamilika.

Kutokana na hili, timu imeomba kuongezewa tena muda ili kukamilisha kazi yao. Imekubaliwa. Sina hakika hili linasomeka vipi katika masuala ya gharama, lakini ninapokumbuka kuwa timu iliyoundwa kuchunguza ugomvi kati ya Mheshimiwa Malima na Mzee Mengi ilitumia karibu milioni mia moja kwa miezi mitatu tu, napata kiwewe ninapofikiria hii ya miezi sita, ambayo pia imeshaongezewa muda, itatugharimu walipa kodi Shilingi ngapi!

Kuna jambo lingine ambalo pia naona halikufafanuliwa vizuri. Rais Kikwete alisema amekubali maombi ya timu hiyo ya kuongezewa muda wa kufanya kazi. Haikusemwa ameyakubali kwa muda gani. Papo hapo tumeambiwa kuwa watuhumiwa wa ukwapuzi wa EPA wamepewa hadi Oktoba 31 wawe wamerudisha chenji yetu la sivyo watajikuta Kisutu mahakamani.

Najiuliza iwapo itafika hiyo Oktoba 31 mafisadi wawe wamerejesha pesa zetu au la lakini timu hiyo ikawa bado haijaletewa taarifa inazotaka kutoka kwa Polisi wa Kimataifa, itakuwaje? Wataomba tena kuongezwa muda? Mafisadi ambao watakuwa hawajarudisha fedha zetu hadi wakati huo nao wataambiwa waendelee kupumzika kwanza hadi tume itakapopokea ripoti inazohitaji kutoka nje ili kukamilisha uchunguzi?

Nirudi kwa Mheshimiwa Sitta. Nataka kuungana na wenzangu wengi ambao wametangulia kumpongeza Spika Sitta kwa kuwakilisha kile ambacho wengi tuliokuwa tukisikiliza hotuba ya Rais Kikwete ndio tulitegemea kingezungumzwa.

Kwamba kwenye vita ya rushwa na ufisadi haya mambo ya haki za binadamu yanawekwa kapuni kwanza, na ndio maana wenzetu wa nchi za Mashariki ya Mbali wameweza kupunguza kwa kiasi tatizo la rushwa kwenye nchi zao.

Hapa labda tuhoji kwa nini tuwe wepesi wa kuwapa watuhumiwa wa ufisadi haki zao za kibinadamu wakati wao ndio wameanza kuzivunja za kwetu kwa kukwapua fedha ambazo zingesaidia mno katika kuinua hali za maisha ya mwananchi wa kawaida?

Kwamba Rais Kikwete anatakiwa kuongeza ukali kidogo kwenye masuala ya rushwa na ufisadi na kwamba pia Bunge lipo tayari kurekebisha sheria zilizopo ili ziendane na hali halisi pale inapoonekana kuwa sheria hizo zinalegalega katika kushughulikia mafisadi na wala rushwa.

Spika Sitta aligusia jambo muhimu pale alipotamka pia kwamba mwananchi wa kawaida anayetafuta ugali wake kwa tabu hataelewa anapoona mafisadi wakibembelezwa bembelezwa kurudisha walichoiba badala ya kupelekwa wanapostahili wezi wa aina yoyote.

Napenda kuamini kuwa maneno machache, lakini mazito mno aliyotamka Mheshimiwa Sitta baada ya hotuba ya Rais ni kielelezo tosha cha jinsi ambavyo hakufurahishwa sana na jinsi ambavyo suala la EPA linashughulikiwa.

Ni matumaini yangu, na bila shaka ya wananchi walio wengi, kuwa Mheshimiwa Sitta atatumia 'hasira zake kusimamia vyema mjadala wa taarifa ya Serikali kuhusu Richmond na 'kumkoma nyani giladi' itakapolazimu kufanya hivyo.
 
Nilimpata Sitta, Six Stars. He was straight to the point. Sio JK anachosha na pumba tupu. Hata data za kiasi cha mabilioni kilichorudishwa alizozitoa zina utata.
 
Back
Top Bottom