Tanzania nchi yenye ardhi nzuri kwa kilimo na makazi lakini wananchi wake ni masikini

Tanzania nchi yenye ardhi nzuri kwa kilimo na makazi lakini wananchi wake ni masikini

Tanzania nchi yenye kila aina ya raslimali nchi yenye nguvu kazi ya kutosha watu mil.60

Nchi yenye ardhi nzuri kwa kilimo na makazi lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa wamerundikiwa furushi la tozo kila mwananchi kalibeba furushi

Ili tuyaepuke hayo maisha ni muhimu katiba mpya ikapatikana ili tuwe na siasa safi na viongozi watakao wajibishwa na wananchi sio wananchi wawajibishwe na viongozi kama sasa Serikali ni ya wananchi sio ya viongozi

Sent from my sm-j600f using jamiiforums mobile app
Lima wewe
 
Si uchumi wa kati hiyo hizo tozo za nini
Uchumi ukipanda na tozo zinapanda zaidi, kwani wafadhili wanapunguza misaada, na watu wanahitaji huduma za kisasa zaidi.

Katika uchumi huu wa kati jaribu mnunulie mpenzi wako simu ya kitochi ya Techno, usikie utavyofukuzwa na zawadi yako. Huu ndio uchumi wa kati, maana yake lipa zaidi.

Enzi zetu sisi wapenzi walifurahia kwa kitechno- tochi mpaka jino la mwisho.
 
Nchi yenye ardhi nzuri kwa kilimo na makazi lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa wamerundikiwa furushi la tozo kila mwananchi kalibeba furushi
Baada ya kuigundua hiyo fursa, anza haraka kilimo ujijengee utajiri kama akina Bakhresa au Mohammed Dawji (Mo). Haitakaa itokee wananchi wote milioni 60 wagombanie fursa moja. Fursa zipo kwa ajili ya wachache wenye kung'amua mapema.

Kila la Kheri.
 
Tunatuma tozo inapobidi, tumerudia zile njia za kuweka pesa dukani kwa Wapemba Kinondoni na ndugu yako anachukua kwa mdogowake Dodoma
Wasomali, Indians, Arabs na Chinese kokote waliko duniani, wanatumia sana mfumo huu kuweka/kuchukua fedha kwa tozo ndogo sana.
Serikali imepoteza mapato makubwa kwa kutunga sheria na kanuni ambazo hazikushirikisha walipaji. Kwa taarifa kama wamekuwasanya 48bn/mwezi ambayo ni chini ya theluthi (33%) matarajio yao; wakati huo kuna indirect taxes ambazo ingevuna kwa watoa huduma kwa fedha ambazo wangepata na ku-spend kwa manunuzi ya bidhaa na huduma.

Uwazi na ushirikishwaji wa wananchi ungetengeneza compliance na wangeweza kutoza kidogo-kidoko na wangepata kwa wingi; mtu ameweka hela yake kwa sim anatoa 1,000 unamkata 300, yaani 30% makato kutoa elfu moja tu (yaani upate 1000 mkononi, 310 inakatwa).

Mtu anaetoa 10,000 unamkata zaidi ya 1800 (yaani ili upate 10,000 yako unalazimika kulipa 1800 zaidi) kwa waheshimiwa wakiwa mjengoni wanaweza kuchukulia poa, ila kwa common ciziten, hii hela ni nyingi sana. Bado ya kutuma nayo inakatwaa!!!

Well, ngoja tuone kwa uharaka kiasi gani wataitikia mwito wa wananchi (kwenye tozo)
 
Tumechoka kunyang'anywa hata kidogo tunachokipata
 
Ni ujinga kuwakata wananchi tozo wakati unaweza kuanzisha kilimo cha mazao ya biasharq
A na chakula kila wilaya ( Halmashauri) nchini. Ardhi mapori matupu..vijana wanauza soksi na masufulia mijini

Dhambi sana hii.
 
Back
Top Bottom