Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kupambana na kuenea kwa Corona

Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kupambana na kuenea kwa Corona

Status
Not open for further replies.
Kwa siku tunapima 300, nyie hadi juzi waziri wenu alisema mumepima 300, sisi tuna maabara tano za kupima Corona ambazo zimezagaa nchi yote kuanzia Mombasa kupitia Nairobi hadi Eldoret kule magharibi, nyie mna moja inayotegemewa Tanzania yote kuanzia visiwani, kuja bara, kwenda mikoani Tanzania kaskazini, kanda ya ziwa mpaka Kigoma, sasa hapo sijaelewa mna nini cha kuigwa.

Kwetu hadi juzi tulikua tumepima 1,400 na kugundua kesi 110
Nyie hadi juzi mlikua mumepima 300 na kugundua kesi 20
Sasa hapo kwa mahesabu ya haraka hamuwezi mkakaa na kubweteka kwamba mna mfano wa kuigwa, ni kama mtu ambaye hajapima UKIMWI aanze kuwachekelea wale ambao wamepima.
Ifahamike hiki kirusi kinasambaa kwa watu kiasi kwamba unaweza ukaambukizwa na kuanza kuambukiza bila ya wewe kuhisi dalili zozote, yaani mpaka uje kuhisi dalili, umekitembeza tayari na ndio kinachowamaliza Ulaya.

Huu sio muda muafaka kwa Watanzania kujiona wababe kisa kesi zao chache ilhali hawana uwezo wa kupima watu wengi, maabara moja ya Dar ina msongamano wa sampuli zinazosubiri kupimwa. Hao wachache mliowagundua ifahamike huko walikotoka kuna uwezekano kila mmoja aliambukiza kadhaa na hao kadhaa wakaambukiza, mtandao mkubwa wa kutisha, muhimu mkachukua tahadhari, acheni misifa.
Tehteh..usimpe mkenya uwanja wa kujitetea.

Umeeleweka mkuu...nimeona kwenye takwimu za Dunia nyie idadi ya walipimwa ipo ila kwa Tanzania sijaona.
 
Tehteh..usimpe mkenya uwanja wa kujitetea.

Umeeleweka mkuu. Nimeona kwenye takwimu za Dunia nyie idadi ya walipimwa ipo ila kwa Tanzania sijaona.

Wala sijajitetea, naiweka kama ilivyo, kwamba hii issue ni hatari watu waache kubweteka na kujisifu kisa kwao namba ni chache ilhali uwezo wa kupima bado mdogo. Hata sisi hao 300 kwa siku bado wachache sana, UK anapima 100,000 kwa siku na bado anapokea mapigo ya kufa mtu, sasa Tanzania unapima 300 kwa wiki mbili halafu unajisifia.

Hiki kitu ni ile tu Afrika kwa miujiza fulani basi kimetukosa kosa lakini hakuna yeyote kwetu anafanya lolote kubwa la kuzuia. Kwa umaskini wetu huu, kikitua kwa mtu mmoja hapo Tandale itakua kiama maana hata uwezo wa kuwalisha watu kwenye lockdown haipo, leo bado kuna watu hawana hata access ya maji na huduma za msingi kama vile afya, uwapige Licorona utakua unawafuta duniani.

Kwetu hapa tunajua uwezo wa kama Ulaya hatuna, lakini hatukai hovyoo, tunajichimbia, tayari shule za bweni 900 zimeanza kuandaliwa kama vituo vya karantini, huku tukiongeza maabara za kupima, na kujiwekea curfew maana usiku ndio watu wanafanya vya hovyoo, hawachukui tahadhari kisa hawaonekani, pia daladala hairusiwi msongamano, mtu mmoja viti viwili, na kila abiria lazima anawe mikono, ni mifano tu ya jinsi gani tunajichimbia.

Tunafahamu haitoshi kuthibiti kiama kinachokuja, ila kama wanajeshi kwenye nchi yoyoe inayovamiwa, huwa wanajichimbia na kujiandaa kupokea mashambulizi hadi afe wa mwisho. Nyie hapo mliambiwa muombe inatosha, mnasongamana kwenye vilabu vya pombe na kulewa huku mkisema mnaomba, Mungu awasklize.
 
Jibu zuri, angalia idadi ya wagonjwa Tanzania na Japan, Vs Kenya na USA

Sent using Jamii Forums mobile app
Japan is a bad choice for comparison .You should be comparing to countries where they have managed to flatten the curve such as South Korea.
1102777-blank-355.png
 
Tehteh..usimpe mkenya uwanja wa kujitetea.

Umeeleweka mkuu...nimeona kwenye takwimu za Dunia nyie idadi ya walipimwa ipo ila kwa Tanzania sijaona.
Tatizo la wakenya hawana malengo, sina uhakika kama lengo lao ni kupunguza maambukizi, wao wanadhani wakishapima watu na kujua idadi ya wslioambukizwa, huo ni ushindi kwao. Lengo la kupima ni ili ujue kama mbinu zako za kuzuia maambukizi zinafanya Nazi au unapswa kuzibadili. Kenya ni wazi kwamba mbinu wanazotumia hazisaidii sana, jambo la kushangaza, hawazibadili wanaendelea na mbinu zilezile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wala sijajitetea, naiweka kama ilivyo, kwamba hii issue ni hatari watu waache kubweteka na kujisifu kisa kwao namba ni chache ilhali uwezo wa kupima bado mdogo. Hata sisi hao 300 kwa siku bado wachache sana, UK anapima 100,000 kwa siku na bado anapokea mapigo ya kufa mtu, sasa Tanzania unapima 300 kwa wiki mbili halafu unajisifia.

Hiki kitu ni ile tu Afrika kwa miujiza fulani basi kimetukosa kosa lakini hakuna yeyote kwetu anafanya lolote kubwa la kuzuia. Kwa umaskini wetu huu, kikitua kwa mtu mmoja hapo Tandale itakua kiama maana hata uwezo wa kuwalisha watu kwenye lockdown haipo, leo bado kuna watu hawana hata access ya maji na huduma za msingi kama vile afya, uwapige Licorona utakua unawafuta duniani.

Kwetu hapa tunajua uwezo wa kama Ulaya hatuna, lakini hatukai hovyoo, tunajichimbia, tayari shule za bweni 900 zimeanza kuandaliwa kama vituo vya karantini, huku tukiongeza maabara za kupima, na kujiwekea curfew maana usiku ndio watu wanafanya vya hovyoo, hawachukui tahadhari kisa hawaonekani, pia daladala hairusiwi msongamano, mtu mmoja viti viwili, na kila abiria lazima anawe mikono, ni mifano tu ya jinsi gani tunajichimbia.

Tunafahamu haitoshi kuthibiti kiama kinachokuja, ila kama wanajeshi kwenye nchi yoyoe inayovamiwa, huwa wanajichimbia na kujiandaa kupokea mashambulizi hadi afe wa mwisho.

Nyie hapo mliambiwa muombe inatosha, mnasongamana kwenye vilabu vya pombe na kulewa huku mkisema mnaomba, Mungu awasklize......
Umesema tushukuru Mungu kwasababu huku kwetu bado kirusi hakijatuvamia sana, mwishoni unadharau kwamba huku tumeambiwa tuombe Mungu hatuna tunalofanya, mwanzo unasema Mungu ndio amesaidi, mwisho unadharau wazo la kumuomba Mungu, huko ni kuchanganyikiwa.

Uzi huu unaonyesha mambo yanayofanyika Tanzania katika kukabiliana na kusambaa kwa Corona, tunaomba wakenya mtuonyeshe "activities which have direct effects in controlling the spread of the Virus". Kupima hakuna direct effects ya kupunguza kuenea kwa Virus.

Katika ukanda huu, Tanzania ni mfano bora kabisa wa kuigwa katika hii vita, pamoja na mapungufu tuliyonayo, bado ni nchi ambayo imejipanga vizuri zaidi kuliko nchi zote zinazotuzunguka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie apeleke jeshi mipakani akianza Kenya-Tanzania, Uganda-Tanzania na Rwanda-Tanzania. Kwa mfano mpaka wa Tanzania na Kenya kuna panya roads zaidi ya 1000!

=====

AUTHORITIES at the Namanga border post in Arusha Region have raised alarm over motorcycle taxi operators who ferry people from the Kenyan side into Tanzania through ‘panya routes’ to avoid screening for Covid-19 and undergoing mandatory quarantine for 14 days.

NAMANgA%20ed.jpg

Dr Gabriel Mdachi, the officer in charge of health at the Namanga One Stop Border Post (OSBP) said here yesterday that those who procure services of bodaboda to flaunt rules are foreigners as well as Tanzanians returning home from Kenya.
He said they hire services of motorcycle taxi riders to evade scanners mounted at OSBP and enforcement of mandatory quarantine.

Dr Mdachi said they came to learn of the dangerous practice the hard way after it emerged that people who came through the official border had normal temperatures but when told about the quarantine, opted to go back to Kenya only to be spotted in Tanzania much later.

“We later found out that they hire bodaboda riders who ferry them through the bush into the Tanzanian side, ride them to the main road where they board public transport and continue with their destinations,” he said.

After learning of the practice, authorities became more alert and recently caught one Tanzanian and two Rwandans who refused to be quarantined at their own cost and instead chose to go back to Kenya which they were allowed to do.

However, the trio did not go beyond no-man’s land into Kenya but disappeared into the bush and called a motorcycle taxi rider who took them inside Namanga where they landed in the hands of law enforcers.

“They were arrested while boarding a mini bus heading to Arusha. Their passports have been taken away and they are being quarantined under supervision of the defence and security committee of Longido District,” he said.

Dr Mdachi appealed to bodaboda riders in the area to stop ferrying people through illegal routes as the practice jeopardises lives of millions of Tanzanians.

He also called on public transport operators plying Namanga-Arusha route as well as passengers on such vehicles not to accept passengers emerging from the bush.

Nevely Mungaya, the Namanga town executive director acknowledged the challenge, saying that the focus is now to sensitize bodaboda riders in the area so that they understand the threat posed by their greed for a few extra coins.

Motor taxi operators were taking part in other illegal activities and strategies were being laid down to stop them, he asserted.

“They are believed to be behind the transportation of illegal immigrants from the Horn of Africa into Tanzania as well as narcotics. Now they are helping people enter Tanzania illegally,” he stated.

Samweli Chala, the secretary of the association of minibus drivers in the area said they held a meeting and resolved not to take passengers brought by bodaboda riders from the bushes.

“We agreed that operational licences will be revoked for a driver caught taking passengers brought by bodaboda from unauthorized spots. The vehicle will be brought back to Namanga, impounded and the driver involved prosecuted,” he added.

Kuna Wanajushi wa kumwaga Tarakea na maeneo mengi mpakani Kenya
 
Mkuu kwa sasa ni mapema sana kujua kama maambukizi ni machache ama lah!Bado hatujajua mbinu zetu zimepiga hatua kwa kiasi gani.Ila mkuu ugonjwa upo ni kujiadhari kabisa.Nadhani tuache muda useme lakini naamin nchi yangu kuna kitu hakiko sawa.Niishie hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila Italy na Spain ndio kuko sawa au sio?
 
ujinga gani hii, without robust testing you can't say how many cases you have...
and the Magufuli govt is capable of shutting down anyone who announces any infection numbers against the govt sources..
Kwahiyo tuambie wewe basi Tz kuna wagonjwa wangapi?
 
For a whole month US had only 15 cases.That means there were so many undetected persons who were still roaming around and spreading the virus without their knowledge.
The numbers only increased exponentially when they started rigorous testing
Alafu jamaa anaisifu serekali yake kwa kuwaweka watu 84 kwenye mandatory quarantine ati ndiko kuwadhibiti wageni.
While more than 2000 people are in different government facilities here in Kenya.
Kwahiyo hao 84 kuna shida gani kuwekwa karantini sasa, wewe ulitakaje maana hao ndio wasafiri waliokuja, sasa tulazimishe wageni waje ili tuongeze idadi ya watu waliokarantini ili wafike 2000 kama nyinyi? Ulitakaje?
 
Hao 20 tumewajuaje kama hatupimi?
Hakuna waziri yeyote yule wa Afya aliyejibu hivyo, hao wameshiwa na hoja wanaanza kuokoteza maneno ya kujiliwaza, kama walivyoshindwa kuwasambaratisha Ashabaab wakaanza kutoa visingizio, ndio kinachotokea ktk Corona. Hawa hawawezi lolote zaidi ya rushwa na ukabila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kweli kwa mpango na mbinu hizi bado kuna mwenye kujiuliza kwanini Tanzania maambukizi ya virusi vya Corona ni machache ukilinganisha na nchi za Jirani?.
Too early to conclude, tuendelee tu kuomba Mungu huku tukifuata masharti ya kinga na tiba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom