Tanzania ni nchi moja, kwanini Prof. Mbarawa aseme aliyosema kuhusu mkataba wa bandari

Tanzania ni nchi moja, kwanini Prof. Mbarawa aseme aliyosema kuhusu mkataba wa bandari

Magufuli ndio nani, Mungu wako? Sisi siyo wafu km vipi mfuate. Magufuli mwenyewe alikuwa failure
Nimekuchoma, polee!.

Magufuli licha ya madhaifu yake mengine lakini kamwe, kamwe asingeweza kutugeuza watanganyika watumwa ndani ya nchi yetu.

Ikikuuma tena katafute kidonge cha maumivu umeze.
 
Miaka miwili ya waziri prof Mbarawa inatia shaka na kusikitisha sana, hakuna flyover hata Moja iliyokamilika, hakuna barabara mpya hata Moja iliyokamilika,treni ya SGR haijaanza kufanya kazi! Kwa kweli ni masikitiko makubwa Kwa waziri huyu wa ujenzi.

Kwenye ilani ya ccm 2020 - 2025 Kuna ma flyover kibao yameahidiwa kujengwa ,je tutafanikiwa Kwa mwendo wa konokono huu wa waziri prof Mbarawa?

..msimlaumu Mbarawa.

..upigaji mkubwa kiasi hiki hauwezi kufanyika bila ya ridhaa au kumhusisha kiongozi mkuu.

..na kama makosa yangekuwa ni ya Mbarawa basi angekuwa ameshatimuliwa.
 
Miaka miwili ya waziri prof Mbarawa inatia shaka na kusikitisha sana, hakuna flyover hata Moja iliyokamilika, hakuna barabara mpya hata Moja iliyokamilika,treni ya SGR haijaanza kufanya kazi! Kwa kweli ni masikitiko makubwa Kwa waziri huyu wa ujenzi.

Kwenye ilani ya ccm 2020 - 2025 Kuna ma flyover kibao yameahidiwa kujengwa ,je tutafanikiwa Kwa mwendo wa konokono huu wa waziri prof Mbarawa?
Hawa wana roho ya hapa siyo kwetu, tuwauze
 
Wazanzibari ni wezi duniani hakuna mfano. Mnakumbuka Fimbo ya Polisi Africa nzima ya dhahabu ilifanya Tour Zanzibar, ikawa mwisho wake.
 
Katika mkutano wake hivi karibuni na viongozi wa bandari, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alitoa taarifa kwamba Zanzibar haikuwemo katika mkataba uliosainiwa kati ya serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji katika bandari. Sababu ya kutolewa taarifa hii ni kwamba sheria inayounda Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inatoa jukumu la kusimamia na kuendesha bandari za Tanzania Bara pekee.

Ni kweli kwamba mkataba huu umesababisha maswali mengi kutoka kwa wananchi, wakihoji kwa nini Zanzibar haikuhusishwa katika mkataba huo. Waziri Mbarawa amefafanua kuwa Sheria Na. 17 ya mwaka 2004, inayounda TPA, inalenga kusimamia na kuendesha bandari za Tanzania Bara tu, na sio Zanzibar.

Hata hivyo, tunapozingatia sheria na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaweza kuona umuhimu wa kuzingatia Zanzibar katika mchakato huu. Sheria Na. 15 ya mwaka 1984 inathibitisha kuwa Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. Sheria Na. 4 ya mwaka 1992 inaendelea kueleza kuwa eneo la Jamhuri ya Muungano linajumuisha Tanzania Bara na Zanzibar, pamoja na sehemu yake ya bahari.
View attachment 2659610
Ni muhimu kukumbuka kwamba Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, na inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, kama inavyotajwa katika Sheria Na. 4 ya mwaka 1992. Hii inamaanisha kuwa masuala ya kitaifa yanapaswa kushughulikiwa kwa kuzingatia usawa na ushirikiano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Hivyo basi, tunapendekeza kuwa serikali ichukue hatua za ziada kuhakikisha kuwa Zanzibar inahusishwa kikamilifu katika mchakato wa uwekezaji wa bandari. Hii inaweza kufanyika kwa kushirikisha viongozi wa Zanzibar na kuweka mazingira mazuri ya kisheria yanayowezesha ushiriki wao. Aidha, mashauriano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar yanapaswa kufanyika kabla ya kufanya maamuzi muhimu yanayohusu Zanzibar.

Tunasisitiza umuhimu wa kuendeleza umoja, usawa, na ushirikiano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni kupitia ushirikiano huu tunaweza kufanikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa pande zote za muungano. Tunatarajia kuona hatua zinazochukuliwa ili kuhakikisha kuwa maslahi ya Zanzibar yanazingatiwa na kuwa pande zote zinafaidika na uwekezaji huu katika sekta muhimu ya bandari.

Tunakaribisha serikali kutenda kwa uwazi na kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha kuwa maamuzi ya kitaifa yanafanywa kwa njia ya haki na kuzingatia maslahi ya pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatua hii itasaidia kuimarisha umoja wetu na kuleta maendeleo thabiti na endelevu kwa nchi yetu.
View attachment 2659611
Mnakuja na uzi mnaojua utasababisha Mbarawa atukanwe na baadhi ya watu humu ndani. Haswa wale bendera hufuata upepo.

DPW hakuwa na sababu ya kutaka kuitumia bandari yoyote ya Zanzibar kwani huko hakuna mzigo anaoutaka.

Zanzibar hakuna madini anayoyataka hivyo hana anachokitafuta huko visiwani.

Pili kuna bandari zinazoendelezwa na serikali ya Mwinyi muda huu, kuna bandari ya mpigaduru inaendelezwa hivyo hakuna sababu hata ya kuumiza kichwa kuwazia suala hilo.

Ni majungu tu ya wale wale waliokuwa nyuma ya Mbarawa katika awamu ya RIP Magufuli leo hawampendi Samia basi na Mbarawa nae ni adui yao!.
 
Back
Top Bottom