Tanzania ni ngumu kutoboa kibiashara kwasababu ya mrundikano wa kodi

Tanzania ni ngumu kutoboa kibiashara kwasababu ya mrundikano wa kodi

FURY BORN

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2020
Posts
638
Reaction score
1,150
Baada ya kupambana saana na Maisha ya ajira, nikafikiria nitafute namna ya kuingiza kipato kingine. Akili ikanutuma shambani kweli nimeingia shambani na Hali siyo mbaya. Wazo likaja tena niachane na wakati wa Kati mazao yangu niyaongezee thamani.

Lengo likiwa kuanzisha mashine ya kukoboa mahindi, kusaga na kupaki. Hapo ndo kwenye mziki Kodi zilizoko hapo utajuta kuzaliwa Tz, kama ifuatavyo service Levy 324,000, mapato laki 8 mpaka milioni 3, Kodi ya vipimo elfu70, Kodi ya uzani laki 120, leseni laki3, Stop laki 3, haijalishi kama unastoo yako, TFDA laki 7 bado sijaenda TBS na tayari naona kama nimeshashindwa ngoja nibaki huko huko porini atakayenunua ndo akapambane huko
 
Duh! hizi Kodi zote unalipa kila mwezi au?!
Zinalipwa Kwa mwaka, swali utakuwa umefanya biashara ya faida shilingi ngapi Kwa mwaka kulipa serikalini milioni 2,544,000. Hizi Kodi ndo wanazolipa hao wazalishaji wakubwa wa unga kama Azania and the likes, wewe unayeanza utachomoka kweli ?

Kilichobaki nikuchukuwa Kadi ya CCM Tu na kufanya kinyemela ukiomba usifunguliwe kesi ya uhujumu chumi na kukwepa kodi
 
Na hayo makadirio unatakiwa ulipe kabla hujaanza hata huo uzalishaji wenyewe! Na wakati huo huo ukiwa hujui utauza wapi bidhaa zako! Yaani unafanyiwa makadirio kwenye ofisi zao, na siyo ulipojenga huo mradi, ili hayo makadirio yawe sahihi na yenye uhalisia.

Kiukweli dawa ni kuwa tu wakwepa kodi! Maana kodi zenyewe siyo rafiki hata kidogo. Mtaji wa kwako, kila kitu cha kwako! Lakini unatakiwa kugawana sawa, au uwazidishie kabisa watu ambao muda wote wako kivulini, wakila tu viyoyozi!

Mbaya kuliko zote, hizo kodi zaidi ya nusu ya makusanyo hutumika kulipa mishahara na posho! Inahuzunisha sana.
 
Na hayo makadirio unatakiwa ulipe kabla hujaanza hata huo uzalishaji wenyewe! Na wakati huo huo ukiwa hujui utauza wapi bidhaa zako! Yaani unafanyiwa makadirio kwenye ofisi zao, na siyo ulipojenga huo mradi, ili hayo makadirio yawe sahihi na yenye uhalisia.
Ukweli nimechoka baada ya kufanyiwa haya makadirio nikasema hee? Fikiria Mimi nzalisha unga lakini Katika unga huo huo Kwa vile tu nitafunga Kwa ujazo tofauti basi kila ujazo Una Kodi yake, Kwa maana ya kg 5, kg10, kg25 na kg 50.

Sioni sababu hiyo nitarajia makadilio yawe kulingana na uzalishaji na si ufungaji. Haya bado unanambia Kwa sababu ni unga nilipie leseni ya kuhufadhi na siyo kwamba unanihifadhia wewe.

Yaani nijenge stoo au nikodishe, nilipie Kodi ya jengo lakini pia nilipie kibali cha kuhifadhi unga ambao tayari nimepewa kibali cha kuzalisha. Unajiuliza hivi watunga Sera akili zao ni Sisi tubaki maskini au tukwepe Kodi ili tuwape rushwa
 
Baada ya kupambana saana na Maisha ya ajira, nikafikiria nitafute namna ya kuingiza kipato kingine. Akili ikanutuma shambani kweli nimeingia shambani na Hali siyo mbaya. Wazo likaja tena niachane na wakati wa Kati
Jisajili SIDO kama ni mjasiriamali ukipitia mgongo wa sido au ukahudhuria mafunzo yao ukapewa cheti hakuna atakayekusumbua
 
Kwa kupitia uchochoro wa kodi, Serekali ya CCM wamekua wakipata njia ya kunyang'nya watu pesa, Kinachouma kuliko yote hiyo pesa wanayokusanya inaishia kwenye matumbo yao.
 
Pole sana mkuu, sasa utakuwa ukiwaona wafanya biashara waliofanikiwa unaelewa manaake nini! Ni kote duniani mafanikio yamewekwa nyuma ya struggle, ukitaka makubwa zaidi basi ujue kupanda milima mikubwa zaidi. cha muhumu ni kukaa na walioweza, ukichanganya mbinu zao na masomo uliyoojifunza, utafika tuu
 
Zinalipwa Kwa mwaka, swali utakuwa umefanya biashara ya faida shilingi ngapi Kwa mwaka kulipa serikalini milioni 2,544,000. Hizi Kodi ndo wanazolipa hao wazalishaji wakubwa wa unga kama Azania and the likes, wewe unayeanza utachomoka kweli ? Kilichobaki nikuchukuwa Kadi ya CCM Tu na kufanya kinyemela ukiomba usifunguliwe kesi ya uhujumu chumi na kukwepa kodi
Mkuu, ni unga wa mahindi huu huu au ni tofauti? Kuna kitu umeruka ama?
 
Back
Top Bottom