Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokua kwa kasi sana barani Afrika. Ili kufikia malengo kati ya miaka 5 hadi 25 ijayo, inatakiwa kuboresha sekta mbalimbali.
Elimu ni nyanja muhimu sana katika taifa letu. Ili kufikia lengo, inatakiwa mitaala yetu ya elimu iboreshwe ili kumuandaa kijana wa kesho kujitegemea na si kutegemea kuajiriwa. Wengi wetu tunasoma ili tuje tuajiriwe, jambo ambalo linakuwa janga kwa taifa na familia zetu.
Afya ni nyanja muhimu sana. Ili mtu aweze kuzalisha mali, lazima awe na afya bora. Serikali inatakiwa kuboresha mfumo wa bima kwa kila Mtanzania kwa gharama nafuu ili kila mtu awe na bima ya matibabu. Hii itasaidia kutokupoteza nguvu kazi na kuweka kituo cha afya kwa kila kijiji, jambo litakalosaidia wazee ambao hawawezi kutembea umbali mrefu.
Kilimo ni sekta mama katika taifa letu. Ili mtu afanye kazi, anatakiwa ale vizuri. Serikali inatakiwa kuhamasisha kilimo cha kisasa kwa kila kaya ili kuinua uchumi wetu. Wanaohusika na kilimo wafanye tafiti za kina kujua kilimo gani kipo katika soko la dunia na kukiboresha ili kufikia malengo. Hii itasaidia kupiga hatua katika sekta ya kilimo.
Madini ni sekta ambayo Tanzania imebarikiwa nayo. Takribani robo tatu ya nchi imezungukwa na madini. Serikali inapaswa kuweka watafiti wa serikali kwa kila mkoa. Hii ingesaidia kuongeza wigo katika sekta ya madini na kuongeza pato la taifa.
Miundombinu bora ni sekta kubwa kwa mataifa mbalimbali. Serikali yetu inapaswa kuongeza juhudi katika upanuzi wa barabara kuu zote nchini ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kupanua wigo wa kiuchumi katika taifa.
Nishati ni sekta muhimu sana kwa sababu takribani 99% ya wananchi wanategemea nishati katika shughuli za kiuchumi. Serikali inatakiwa kuongeza juhudi katika kutengeneza mabwawa makubwa ya kuzalisha nishati kwa kiwango kikubwa ili kuwavutia wawekezaji wengi kuja nchini. Hii itainua uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja kupitia uwekezaji na utoaji wa ajira, na pia itapunguza umasikini.

Upvote
2