Tanzania Premier League: Kuna ulazima wa klabu moja wapo (Simba au Yanga) iondoke Dar na kuhamia Arusha au Mwanza ili kuongeza ladha ya mchezo wa soka

Tanzania Premier League: Kuna ulazima wa klabu moja wapo (Simba au Yanga) iondoke Dar na kuhamia Arusha au Mwanza ili kuongeza ladha ya mchezo wa soka

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania mimi binafsi ninadhani;

Kuna umuhimu wa klabu moja wapo kubwa (Simba au Yanga) kuondoka Dar na kuhamia majiji mengine makubwa kama Arusha au Mwanza ili kuongeza ladha ya mchezo wa soka katika Tanzania Premier League.

images (18).jpg

Kama serikali imeweza kutoka Dar na kuhamia Dodoma ili kuiacha Dar ipumue kutoka katika msongamano wa magari, kelele, watu kwanini hivi vilabu vishindwe? Mbona vilabu vya Barcelona na Real Madrid vipo majiji tofauti huko nchini Spain lakini wakiwa wanacheza uwanjani siku hiyo dunia nzima inasisimuka?

Kuna ulazima gani wa vilabu hivi vyote kuwa jiji moja kubwa, maarufu na la kibiashara mpaka sasa ilhali mashabiki wao wapo nchi nzima? Kwanini kusiwe tu na ofisi ndogo ya timu moja wapo kati ya simba au yanga kisha ofisi kuu pamoja na wachezaji wote wakahamia Mwanza au Arusha?

Kuna siku moja mwaka jana wa 2019 niliwahi kuwaza kwamba, kwanini kila mkoa usiwe na mashindano yake ya mchujo wa ndani kisha ukatoa timu moja tu itakayoshiriki ligi kuu ya Tanzania ili kuleta picha ya utaifa?

Lakini kabla sijawasilisha wazo hilo hapa kuna jambo likaniambia moyoni, itakuwaje kwa mkoa wa Dar ambao ndio kitovu cha soccer la hapa bongo kwa maana ndio mkoa unaobeba vilabu viwili vikubwa vinavyofahamika Afrika na duniani (Simba na Yanga)?

We need to counterbalance na kuongeza ladha ya mchezo wa soccer. Kwanini mechi ya Simba na Yanga iwe "big match" na "derby" kwa wakati mmoja?

Mbona Inter na Juventus zikicheza inakuwa ni big match lakini sio Derby?

Mbona kuna baadhi ya mechi za La Liga zinachezwa nje ya Spain lengo likiwa kuwapa ladha watu wengine nje ya nchi yao kwa maana ligi yao sasa ni super brand.

Kwani lazima mechi zote za nyumbani za Simba na Yanga zichezwe Dar? Kwanini mechi zingine za nyumbani za miamba hiyo miwili zisichezwe katika mikoa iliyoshindwa kuingiza timu katika ligi kuu ya soka ya Tanzania bara ili kuwapa ladha mashabiki ya mikoa hiyo?

images (17).jpg

SWALI: Bado kuna ulazima gani wa vilabu hivi vikubwa viwili kuendelea kuweka makazi yao makuu katika jiji moja la Dar ilhali wana mashabiki nchi nzima?

SOMA PIA>>> Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Tenga? Tunakwama wapi kama taifa?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau;
=====
Unajuwa sio dhambi kupenda Simba na Yanga tatizo kubwa nchi hii ni washabiki wa miji mingine kidogo kuna miaka ya nyuma kulikuwa kama mfano Mwanza ukisikia Pamba, Coastal, Reli ya Moro au Tukuyu hata CDA hizi team zilikuwa zinapata support kubwa katika mikoa yao na hii ilileta upinzani. Ukisikia mechi Pamba na Yanga au Simba hii ni big game Tanzania au hata team za Zanzibar ulikuwa ukisikia Small Simba, Miembeni, Malindi au Kikwajuni ni hatari. Tatizo limeanzia hapa hizi team hazipati support kutoka kwa wenyeji chukulia mfano kwa wenzetu mfano Spain, Real na Barca na uhakika hata Spain watu wote wana unazi na team hizi ila mapenzi yao kwa team zao wanaonesha kwa wazi haiwezi kwenda Real Sevilla halafu ukute wakazi wa pale wanashangilia Real hakuna au EPL huwezi kukuta mtu Stoke city anacheza na Man halafu mji wa Stoke wavae jezi za Man hakuna hata kama moyoni wana support Man lakini ikicheza na team ya mji wake full support mji wao.
Washabiki wamiji mingine sio dhambi pendeni Simba na Yanga sana tu lakini inapokuja kucheza na vijana wenu simameni na vijana wenu team zenu mbaya zaidi hata viongozi wa kiserikali utasikia mimi Simba au Yanga sawa sio mbaya wote tumezaliwa tunapenda hizi team kwa ukubwa wao hakuna wa kukataa ila simama sema kama mbunge wa Kagera sema mimi Kagera Sugar kama Tanga support Coastal au African union tulete ushindani. Kuna mtu kawahi kuona Dortmund wanavaa jezi ya Bayern.
=====
 
Shida sio kuhama Dar
We need to counterbalance na kuongeza ladha ya mchezo wa soccer mkuu. Kwanini mechi ya Simba na Yanga iwe "big match" na "derby" kwa wakati mmoja?

Mbona Inter na Juventus zikicheza na big match lakini sio Derby?...
 
Kwani kuhimili kwa uwanja ndio kukoje maana vipimo ni vile vile au vinatofauti?
 
Uwanja gani wenye uwezo wa kuhimili mechi ya simba na yanga nje ya Dar ipelekwe huko?
Kwani lazima mechi ya Yanga (ikiwa nyumbani) na Mwadui FC ichezwe Dar? Kwani haiwezi kuchezwa katika mkoa ambao haujafanikiwa kupeleka timu ligi kuu?
 
Nikiwaona mashabiki wa hizi team mbili wanavyokuwa na mood hasa siku yenyewe tu ya timu hizi mbili hasimu kukutana hakika huwa najutia sana hivi vilabu kuwepo...natamani siku moja itokee club moja kubwa iwe bora kuliko team hizi ili kutokomeza huu usimba na uyanga uliopo nchi hii kwa miaka sasa uligeuka na kuwa ushamba!!!!!!
 
Yanga ina uwezekano wa kuwa na makazi hata Ulaya, ila simba itaamia kwenye compound ya Mo Dewji au singida kabisa alikozaliwa.
 
Back
Top Bottom