Tanzania Premier League 'TPL' Singida United Vs Simba SC Uwanja wa Namfua Singida

Tanzania Premier League 'TPL' Singida United Vs Simba SC Uwanja wa Namfua Singida

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kuelekea kumalizika msimu wa Ligi Kuu Tanzania TPL, Patashika hiyo kushika kasi kwa viwanja tofauti kupigwa ambapo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mbao FC wanamenyana na KMC, huku Uwanja wa Namfua mkoani Singida wanyeji Singida United wanapapatuana na Mabingwa watetezi Simba SC.

Mchezo wa Singida United dhidi ya Simba SC, unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika tisini

Msimu uliopita Simba SC walitangaza ubingwa rasmi kwenye uwanja huo huo wa Namfua Stadium, wakati walipopepeta na Singida United na wenyeji hao kukubali kipigo cha 1-0

Na leo tena Mei 21, 2019 Mabingwa hao wanahitaji ushindi muhimu ili kuweza kutangaza rasmi ubingwa msimu 2018/2019. Je historia itajirudia au Singida United wanaweza kumsimamisha Simba SC kwa muda?

Usikose ukaambiwa..Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 jioni na utakuwa mubashara kupitia Azam Sports 2.
FB_IMG_1558439696843.jpeg
IMG_20190521_145204_814.jpeg


Naaaaaaam mpira umeanza uwanja wa Namfua mkoani Singida TPL..

Singida United 0-0 Simba SC

02' Mchezo umeanza kwa kasi kwa Simba kuliandama lango la wenyeji na kupata kona mbili ambazo hazikuzaa matunda.

05' Singida United, wanajaribu kujibu mashambulizi ambapo shuti la Maganga limetoka nje sentimita chache lango la Simba.

09' Goooooooooooooooooooaaal gooooooooaaal.. Maddie Kagere anaipatia Simba SC bao la kwanza baada beki wa Singida United kushindwa kuondosha mpira wa hatari ulipigwa na Mohammed Hussein

Singida United 0- 1 Simba SC

14' Singida wanaokoa mpira wa hatari ambao ungeweza kuipatia Simba bao la pili.

Mchezo umechangamka kwa pande zote mbili, Singida wakijihakikishia kusalia TPL, huku Simba wakihitaji ushindi.

15' Singida United 0-1 Simba SC

Kinyombo anakwenda lango la Simba lakini mwamuzi anasema umejiangusha na mpira wanachukua Simba

20' mpira umetawaliwa na Simba, japo Singida ni wenyeji

Free kick kuelekea Simba.Inapigwaaaaa lakini Munishi anadaka bila wasiwasi.

24' mpira umesimama baada ya mwamuzi mpira kumpiga kichwani, madaktari wanaitwa kumpatia matibabu..

Haya mpira unaendelea, TPL uwanja wa Namfua baada ya mwamuzi kupata rabsha na kutibiwa

26' Okwi anapata nafasi safi anapiga lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick

30' Inapigwa free kick kuelekea Simba, sio mbali, inapigwaaa lakini mpira unakuwa hafifu na kudakwa na Munish

35' Singida wapiga pasi za hapa na pale kujaribu kulifikia lango la Simba, anatokea mchezaji wa Singida anapiga nje na kuwa goal kick

Bocco anaambaa na mpira, na anapiga kwake Kagere..Lakini mwamuzi anasema mpira ulitoka nje kabla ya kupiga

40' Singida United 0-1 Simba SC

Simba wanasogea langoni mwa Singida anachukua Okwi mpira anapiga lakini mpira unapaa na kutoka nje na kuwa goal kick

45+2' kuelekea kuwa mapumziko

Naaaaaaam Mpira ni mapumziko uwanja wa Namfua, ambapo Simba wanatoka mbele kwa bao moja bila kwa yai, likiwekwa kambani na Maddie Kagere

Singida United 0-1 Simba SC


Kipindi cha lala kwa buriani kimeanza

46' Singida United ameanza kwa kasi kwa mashambulizi mawili makali ambayo yangeweza kupata bao, lakini mashuti yao yote yametoka nje ya lango.


50' John Bocco shuti lake linashindwa kulenga lango la Singida

Kona inapigwa kuelekea Simba, inapigwa lakini Simba wanaondosha

Mwashuya yuko chini baada ya kupata rabsha, ameinuka anaendelea

Singida United 0-1 Simba SC

Mabadiliko Singida, anatoka Mwashuya na anaingia Juma

61' Goooooooooooooooooooaaal gooooooooooaaaal..John Bocco anaipatia Simba bao la pili kwa kichwa safi baada golikipa kutoka na kuacha lango.

Mpira unaandelea...wakati huo huo golikipa wa Singida anatibiwa baada kupata rabsha.

70' Singida United 0-2 Simba SC

Inapigwa shuti kali lango la Simba SC, golikipa Munish anapangua wakati huo huo Mlipili anaondosha hatari hiyo

75' Anatoka Okwi na anaingia Mkude upande wa Simba SC

Hakuna matumaini kupata bao kama hawatabadilika Singida

Anatoka Maganga na anaingia Michael, upande wa Singida Utd

Na Simba wanafanya mabadiliko..Anatoka Niyonzima na anaingia Dilunga

80' zikiwa zimesalia dakika 10, kumalizika mpira huu, matokeo yakiwa hivi ni Dhahir Simba watakuwa mabingwa wapya

Anachukua Wilson, anapiga mpira unanaswa na Simba na wanapiga pasi fupi

85' Anatoka Maddie Kagere anaingia Triple C Chama upande wa Simba SC

Singida wanapiga mbele. Lakini wanapoteza na kuwahiwa na mabeki wa Simba

90+8' Kuelekea kumalizika kwa mchezo huu wa TPL

Naaaaaaaaaaaaaaam..Mpira umemalizika Uwanja wa Namfua ambapo Simba SC wamekuwa Mabingwa Wapya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili bila majibu.

Mabao yamewekwa kimiani na Maddie Kagere 09' Na John Bocco 61'

Singida United 0-2 Simba SC

Kwa niaba ya Simba SC na team JF niiiiiii Ghazwat
 
Ushindi wowote unaipa Simba ubingwa kwa msimu huu wa 2018/19.

Ingekuwa Singida Utd ya msimu uliopita walau ningefikiria ugumu wa mechi hii. Kwa Singida Utd ya msimu huu Simba atashinda na kujinyakulia ubingwa bila ukakasi wote.

All the best, ABIJO.
 
Ushindi wowote unaipa Simba ubingwa kwa msimu huu wa 2018/19.

Ingekuwa Singida Utd ya msimu uliopita walau ningefikiria ugumu wa mechi hii. Kwa Singida Utd ya msimu huu Simba atashinda na kujinyakulia ubingwa bila ukakasi wote.

All the best, ABIJO.
Hata drwa tu mkuu. Maana simba ana magoli 1000 wakati yanga ana magoli 10. Sasa simba na yanga watafungana point kama simba ata draw leo na kufungwa mechi zilizobakia huku yanga akitakiwa ashinde mechi zake zote.
 
Back
Top Bottom