#COVID19 Tanzania: Serikali yaagiza uvaaji barakoa kwenye mikusanyiko

Mimi binafsi, hata kabla Magufuli hajazi-dongo-a barakoa, nilishaweka msimamo wa kutovaa. Wavae wanaoona kinga zao za mwili ni za mashaka.
... hivi ukivaa barakoa kumkinga jirani yako mwenye kinga ya mashaka kama unavyodai itakupunguzia nini? S hata maandiko yanasema mpende jirani yako? Kwa kuwa kinga yako ni imara hata humjali aliye dhaifu? Kwamba bora afe tu yanihusu nini? Hebu fikiria mara mbili rafiki; kila mwanadamu anahitaji kuishi!
 
No problem...leo asubuhi nilikuwa naliangalia box langu la barakoa nililolinunua 20000/ na sanitizer ya 5000 miezi 4 iliyopita nikajua nimeshapata hasara ya

Maswala ya serikali na mikopo ya IMF wala siyaingilii,nchi yangu kushindana na wazungu BADO SANA watoe tu takwimu mambo yaende[emoji40]

Nitavaa barakoa kwa sababu niliwahi shuhudia vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ndo maana nilinunua barakoa na sanitizer kwa tahadhari ama dharura kama hizi
 

Kama kawaida ile mijinga jinga miumini ya upigaji nyungu, isiyotaka kusikia kuhusu chanjo, isiyotaka kuamini hii ni awamu ya sita nk, itajitokeza kupinga.

Madhara ya moja kwa moja ya nadharia mfu za mwendazake.
 
Kwani lazima? Kila mtu asimamie anachokiamini,wewe na uelewa wako simamia msimamo wako,wasiojielewa waache na wao wasimamie misimamo yao.
Hoa wasiojielewa ndio wanaosambaza vijidudu vya korona kwa kupuuza kwao na kuwambukiza watu innocent ....Utakuta jitu linapiga chafya hadharani bila hata kujifunika na kitambaa hadi unajiuliza huyu mtu ana brain kweli?
 
Ngoja awasikie Magufuli awashukie kama mwewe
 
Mimi binafsi, hata kabla Magufuli hajazi-dongo-a barakoa, nilishaweka msimamo wa kutovaa. Wavae wanaoona kinga zao za mwili ni za mashaka.
Wakuu wa mikoa wakishaambiwa watapimwa kwa utendaji wao utapimwa kwa hiyo, hiyari haipo tena. Jiandae virungu vya polisi na mafaini na mambo kama hayo. Unfortunate reality!
 
cha kuazima hakistili matako!
 
Watanzania wengi wanadharau uvaaji wa barakoa ,mwendazake alibrainwash watu sana ,wanaovaa barakoa kwasasa ni watu ambao wanaojielewa lakini hawa wavuja jasho hawezi kukuelewa kuvaa barakoa.
WEWE ACHA MAMBO YAKO. MTU ASUBUHI AMEAMKIA KUBEBA MIZIGO KUPAKIA NA KUSHUSHA PALE KARIAKOO UNA MWAMBIA VAA BARAKORAAA ataweza kufanya kazi yake kwa ufanisi kweli?? hewa safi ya oksijeni ataipata wapi na hayo madude yenyuuu, pelekeni huko kwa amsterdam mukayausudu naye. Sisi bado tuna amin mungu wa Yakobo, Isaka bado yupo katikati ya ardhi yetu. Nyie mnao usudu hiyo hela haya abuduni kama zitawaokoa
 
Hivi ni daktari gani hapa Tanzania anayeweza kuwaambia watanzania kwa ujasiri kuwa barakoa kwa uhakika inamkinga mtu dhidi ya kirusi cha corona. Hata barakoa za N95 hazina uwezo wa kuchuja virusi kwa asilimia 100! Surgical masks hazikutengenezwa kwa ajili ya kumlinda mvaaji dhidi ya virusi!! Kwa nini tunadanganyana mchana kweupe?
Huko ulaya na marekani na India karibuni wote wanaokutwa na maambukizi mapya kila siku ni wavaaji wa barakoa, na theluthi moja ya wanaokutwa na maambukizi mapya wamechanjwa chanjo ya kuwakinga na corona !!
Hakuna aliyethubutu hadi sasa kuweza kusema kuwa chanjo ya corona inamkinga mtu asiambukizwe virusi vya corona. Wenyewe wanasema "vaccine breakthrough infection" yaani maambukizi yanayopenya kwenye kinga ya chanjo. Wamelazimika kusema eti chanjo inapunguza watu WALIOAMBUKIZWA kulazwa hospitali kwa kuzidiwa na corona!
Huo ni uongo maana hata bila chanjo ni asilimia ndogo sana ndio wanaolemewa na corona kiasi cha kulazwa. Wengi wanapata corona bila hata kuonesha dalili zozote za ugonjwa, na wao wenyewe huwasema kama "Asymptomatic cases"!! na wengine huishia kupata mafua na kikohozi tu ambacho hujiishia chenyewe au huisha kwa kujifukizia au kwa kutumia limao na tangawizi! To most people, corona virus is just part of the NORMAL FLORA!!
 
Ndo maana nimesema kila mtu asimamie anachokiamini na si vinginevyo!
Tatizo kwa maelezo hayo hapo, liberty of conscience haipo. Utalazimishwa kuvaa. Kumbuka hao DCs na RCs ni wenyeviti wa NSC kwenye wilaya na mikoa. Maagizo yao polisi hufuata bila swali. Unaweza kusimamia unachokiamini, but naamini gharama yake itakuwa kubwa sana.

Unfortunate reality!
 
Hao wanaopiga kelele wimbi ka tatu hizo nchi si zimeishachanja? Kwa nini mtu ahangaike na wasiochanja wakati yeye yuko salama tayari?

Kama mtu amevaa barakoa tayari kwa nini ana wasiwasi wa kuambukizwa na asiyevaa?

Tusilazimishane kila mtu achague mwenyewe kuvaa au kutokuvaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…