Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Ashukuriwe Mwenyezi Mungu...mwakani kuna mwanangu wa darasa ilimpasa nae akae boarding! Halafu ni lazima...lilikuwa linanifikirisha sana.
 
Serikali ya ccm imeamua kufanyia tangazo la jiran zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kua ni mkubwa mno...
Naunga mkono kwa hili
 
Wazazi wanatakiwa wapeleke wanafunzi shule za karibu na nyumbani.
Hata hizo za karibu shule zinalazimisha mtoto akiwa std 4 na 7 akae kwa ulazima boarding. Mimi niliwagomea wakanambia uwe una uwezo wa kumpeleka mtoto saa 12 asubuhi au nimuhamishe nikawaambia fresh tu kwakuwa siko mbali na shule akawa anawahi. Wanafosi kutaka ada za boarding kiulazima.
 
No wonder kuna mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa sana. Tunazaa ila kulea hatutaki, hivi mtu baki aweza kuwa na uchungu na mwanao kuliko wewe?

Hizo pesa tunawatafutia akina nani ikiwa tunaowatafutia tumewatelekeza!!
 
% kubwa ya mashoga na wasagaji wamejifunza boarding school.

Nyumbani wazazi wanakuwa makini sana kuwaangalia mienendo ya wanawe.
Swala hapa sio shule za boarding ndizo zinazopelekea mmomonyoko wa maadili. Hili swala ni Pana sana... Swala la maadili ni Pana sana.

Je, tabia ya uchokoraa watoto wanajifunzia bording school?

Je, tabia ulevi na kutumia madawa ya kulevya wanajifunzia boarding?

Je tabia ya kutukana matusi yote ya nguon wanajifunzia boarding?

Je, tabia ya udokozi na wizi wanajifunzia boarding?

Je tabia ya ulawiti na ushoga wanajifunzia boarding?

Hizo tabia zote hapo juu 98% watoto wanajifunzia mitaan na majumban huo ndo ukweli
 
Swala hapa sio shule za boarding ndizo zinazopelekea mmomonyoko wa maadili. Hili swala ni Pana sana... Swala la maadili ni Pana sana...
Ushoga/Usagaji ndiyo janga kuu ,hayo mengine siyo issue sana! Ukweli ulio wazi hao mashoga/wasagaji % kubwa wamejifunzia boarding.

Imagine unampeleka boarding mtoto mdogo hata kujitambua hajitambua halfu huko anakutana na watoto wenzake above 13 yeye minne au mi3 unategemea nini?

Michezo ya kibaba na kimama ipo mitaani lakini wazazi wanakuwa makini ila kwa boarding watoto wanakuwa free kwenye madom yao.
 
Swala hapa sio shule za boarding ndizo zinazopelekea mmomonyoko wa maadili. Hili swala ni Pana sana... Swala la maadili ni Pana sana...
Bording ndio kitovu cha kufilana. Hayo mengine tuyaache yapo toka zamani.

99% ya wafilwaji na wafilaji mwalimu wao ni bording
 
Wazazi wengine makatili sana.....yaani mtoto wa miaka mitatu/ mi nne unamtelekezea Walimu?????????????
Kisa pesa tu!!!!!!!!
 
Ashukuriwe Mwenyezi Mungu...mwakani Kuna mwanangu wa darasa ilimpasa nae akae boarding! Alafu ni lazima...lilikuwa linanifikirisha sana.
Hiyo lazima ya shule sio lazima kama mzazi ukiwa na msimamo kuhusu kutokutaka mwanao asikae boarding.

Mie mwaka jana nilikataa wakwangu (Grade 4) kukaa boarding akaendelea kuwa day-schooler mpaka alivyofanya mtihani wa taifa.

Tatizo siku hizi wazazi wengi hawataki kabisa kujishughulisha na swala la malezi kwahiyo wanatumia boarding school kukwepa majukumu yao kwa visingizio vya kuwa busy. 😕
 
Hata hizo za karibu shule zinalazimisha mtoto akiwa std 4 na 7 akae kwa ulazima boarding. Mimi niliwagomea wakanambia uwe una uwezo wa kumpeleka mtoto saa 12 asubuhi au nimuhamishe nikawaambia fresh tu kwakuwa siko mbali na shule akawa anawahi. Wanafosi kutaka ada za boarding kiulazima.
Na wanavyong'ang'ania mtoto akae boarding hamna hata la maana zaidi yakuwa-exhaust watoto masaa na masaa bila kuwapa muda wa kupumua.

Mie hata hiyo saa 12 sikuwa nampeleka, alikuwa anachukuliwa na bus muda wa kawaida na kurudishwa saa kumi. Mtoto wa miaka 9 anakaaje shule tangu saa 12 asubuhi mpaka saa 2 usiku kama sio ujinga??
 
Serikali ya ccm imeamua kufanyia tangazo la jiran zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kua ni mkubwa mno.

Mimi ni mdau wa elimu hii sababu sio kweli hata siku moja.. SEMA kwa sababu serikali yetu haifanyi tafiti za kujua tatizo wao huja maamuzi yao bila kufanya utafiti wa kina.
Kukaa bwenini kunamnyima mtoto mdogo haki zake za msingi.
 
Back
Top Bottom