Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekumbusha kuwa hairuhusiwi huduma ya bweni kutolewa kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne, isipokuwa kwa kibali maalum kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mdau husika.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa imeeleza kuwa shule zote ambazo zinatoa huduma ya bweni kwa madarasa yasiyoruhusiwa zinatakiwa kusitisha huduma hiyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza mwaka 2023.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo ni utekelezaji wa mwongozo wa uanzishaji na usajili wa shule uliotolewa na wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwezi Novemba mwaka 2020.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika baadhi ya shule zimekuwa zikipokea watoto wenye umri mdogo kuanzia darasa la awali hadi la nne, huku huduma zinazotolewa kwa wanafunzi hao zikiwanyima fursa ya kushikamana na familia na jamii zao, kujenga maadili na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya familia zao.

Kulingana na tafiti zilizopo, madhara ya muda mrefu yatokanayo na tabia ya kulaza watoto bweni katika umri mdogo ni watoto kukosa mapenzi kwa wazazi ama walezi na jamii zao na hivyo kushindwa kuwa sehemu ya familia na jamii husika.

Taarifa hiyo ya Kamishna wa Elimu pia imesema kuwa hairuhusiwi kwa shule yeyote kuwa na makambi ya kitaaluma na kuzielekeza shule kuweka mikakati thabiti ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kuzingatia kalenda za mihula zinazotolewa mara kwa mara na Kamishna wa Elimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa malezi na makuzi ya mtoto yanategemea sana mchango mkubwa unaotolewa na familia kupitia wazazi ama walezi wa watoto.

Credit TBC
 
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekumbusha kuwa hairuhusiwi huduma ya bweni kutolewa kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne, isipokuwa kwa kibali maalum kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mdau husika...
Kibalu gani maalumu Tena au mrungula!
 
Safi sana. Mtoto analelewa katika ngazi ya familia na siyo boarding school
Mzazi hawezi kuona athari zake kwa sasa hadi hapo baadaye.
Futa kabisa haya masuala ya bweni kwani hayana tija yeyote zaidi ya usumbufu kwa mzazi. Muhimu walimu waajiriwe wa kutosha kufundisha watoto/wanafunzi.
 
Hayo ni majanga msingi kumpeleka bweni ni ndio unapata kizazi kisichojua mema na mabaya.

Mtoto inatakiwa awe chini ya mzazi wake hadi akivuka kipindi cha upumbavu.

Angalau kuanzia miaka 14, hata chini ya miaka 18 inatakiwa uwepo ukaribu wa mzazi
 
Futa kabisa haya masuala ya bweni kwani hayana tija yeyote zaidi ya usumbufu kwa mzazi. Muhimu walimu waajiriwe wa kutosha kufundisha watoto/wanafunzi.
Zipo fact zinazomsukuma mzazi kumpeleka mtoto bweni,

Wengine sababu ya majukumu ya kikazi au biashara ulazimika kutokukaa na watoto nyumbani.

Wengine ni single parents.
 
kama ni kweli, WAKO SAHIHI, na ikiwezekana iwe marufuku shule bweni shule ya msingi mpaka sekondari.. bweni ianzie form six na hivi vyuo vya kati.. Vyuo vyote ambavyo wanasoma vijana baada tu ya kumaliza shule ya msingi navyo bweni iwe marufuku.
Mimi nina uhitaji wa kupeleka mtoto wangu St.Francis, Cannosa, Maria Golet kidato cha kwanza,kwa hiyo unataka mtoto wangu akose hiyo nafasi sababu unataka Sekondari O-level pia ziwe day scholars?

At least kwa Primary inaeleweka lakini siyo Sekondari.Tutapeleka tu watoto wetu Boarding kidato cha kwanza,hakuna namna.
 
Futa kabisa haya masuala ya bweni kwani hayana tija yeyote zaidi ya usumbufu kwa mzazi. Muhimu walimu waajiriwe wa kutosha kufundisha watoto/wanafunzi.
Kwa Primary mpaka grade 4 walau inaeleweka,lakini baada ya hapo,kila mzazi achague njia anayoona ni sahihi kwake,ndiyo maana Serikali imeweka zuio mpaka grade 4 peke yake.
 
Zipo fact zinazomsukuma mzazi kumpeleka mtoto bweni,
Wengine sababu ya majukumu ya kikazi au biashara ulazimika kutokukaa na watoto nyumbani.
Wengine ni single parents.
Wanadhani kila mtu anapeleka mtoto boarding kwa kupenda,hawawezi kukuelewa point yako.
 
Habari wakuu. Nilikuwa nasikiliza muhtasari wa habari TBC leo saa sita mchana nikasikia wizara ya elimu imepiga marufuku huduma ya bweni kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la Tano.

Kwa sababu nilikuwa busy na kazi nikasema labda sikusikia vizuri. Mwenye taarifa kamili anijuze tafadhali.
 
Hapo ndio huwa wanaharibu
Amri inatoka na vipengele kibao
Immunity ama
Wanafeli sana.

Wakishaanza kuweka uwezekano tu kwa kuomba lazima shule zote zitaomba.

Hapo itachochea rushwa na mwisho lengo husika linaweza lisitimie.
 
Mimi nina uhitaji wa kupeleka mtoto wangu St.Francis,Cannosa,Maria Golet kidato cha kwanza,kwa hiyo unataka mtoto wangu akose hiyo nafasi sababu unataka Sekondari O-level pia ziwe day scholars?

At least kwa Primary inaeleweka lakini siyo Sekondari.Tutapeleka tu watoto wetu Boarding kidato cha kwanza,hakuna namna.
Hao watoto wanaosoma sekondari nao wanakuwa wadogo sana kiasi chakuwa rahisi kuharibiwa...

Inawezekana zipo shule zenye umakini lakini zilizonyingi umakini ni mdogo sana kwenye malezi ya hawa watoto.
 
Ni jambo la kupongera sana, hata ingepaswa kwa bweni ni kuanzia Secondary tu pekee.
 
Hili swala ilitakiwa pasiwe na kibali kama shule za serikali hazina boarding kwa primary iweje waruhusu kwa wengine.

Wafute boarding kwa wanafunzi wote chini ya sekondary.

Wasiyumbishwe na mtu

Ufatiliaji uwe mkubwa
 
Shule zitaanzisha hostel na watoto kuanza kutokea huko kwenda shuleni.

Hili swala latakiwa liwe la mzazi zaidi, mzazi anatakiwa aangalie hata wazungu hawana boarding
 
Back
Top Bottom