Walianza Kenya mwaka jana kufuta shule za bweni kwa primary schools...nikajisemea mwakani ama miaka saba ijayo itakuja Tanzania..safari hii naona tumekuwa fast kuact sijui labda kuna mkubwa kaumizwa na jambo ama hali imekuwa tete sana.
Ila Tanzania bado km kawaida tunalainisha mambo wamesema mwisho grade 4 au uwe na kibali maalum, ambapo kiuhalisia sababu maalumu zipo ndio maana wazazi wakawapeleka...kwahio zitaendelea kuwepo
Kiukweli nyakati zimebadilika...mzazi anatakiwa kuwa karibu sana na watoto below 18yrs bila hivyo tutalia sana baadae...maana changamoto ni nyingi, akili ni changa kuhimili hata addiction zingine zimeletwa wazazi tunachemka kuzihimili sembuse mtoto lakini sasa tunafanyaje na shule zenye walimu wazuri ni private na nyingi ni boarding schools..
Nikiangalia upande wa pili ndugu zetu wa rangi za mtume wanaacha wife home anatunza watoto, wao wanachakarika...sisi tunachakarika wote ili kuweza kukeep status fulani ya maisha.
Kwa single parents maana wengine ni kwa kudra za mwenyezi Mungu wengine ni changamoto za nyakati...wanatakiwa kufanya nini maana mahangaiko ya kutafuta pesa nyumbani uangalizi wa watoto ni finyu...na je sasa hv akirudishiwa mtoto nyumbani atajiadjust vipi.
Ama tunajiendekeza, kutafuta pesa sikuhizi hakuna limit ya muda...zamani mzazi akitoka kazini saa kumi yupo home.
Mtoto kashatoka tuition anakutana na mzazi home, sikuhizi mpaka analala hajamuona mzazi sijui ni foleni, ama order zimezidi emails za kutuma ni nyingi, ama utandawazi umekua demand ni kubwa inapelekea mzazi kuwork overtime...
Anyway ni jambo la kufikirisha...mizani sijui tutaubalance vp