Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Childcare ni changamoto Dunia nzima. Kuna mtu mwingine analeta boarding kwa sababu mazingira aliyopo hakuna shule. Wengine ni wafanyakazi was TANAPa au mashirika mengine ambayo vituo vyao by kazi ni porini n hakuna huduma ya shule. Pia wapo ambayo wanawaachia mahouse girl wakija jioni watoto wameigwa ,hawajalishwa n ni wachafu. Sera inabidi inanglie hayo yote. Wengi tunapigs makelele ila hata hao watoto walimu was shule wanawajua kuliko mzazi maana muda mwingi hatupo. Hata jumamosi na jumapilli pia hatupo. Wanaosaini hayo makratasi wengi watoto wao wao Feza au international school. Tukae tuangalie suala la malezi vizuri. Suala sio boarding ni malezi. Pia serikali Ina shule za boarding wilaya nzima ya Monduli. Je itazifunga? Arusha school itafungwa? Tusishabikie tu bila kutafakari.
Sheria ni msumeno,ngoja tuone mwisho wa muhula huu sio mbali.

Au labda watatumia upenyo wa kibali maalum. Watu wanatengeneza mbadala mapema
 
Wazazi tuache ukatili kwa watoto wetu, hata Kama ni single mom, au single daddy, tujitahidi kadri ya uwezo wetu. Mungu wa mbinguni ametupa zawadi hii ni kubwa sana lakini pia ni faraja. Tangazo hili tulipokee kwa moyo mkunjufu.
 
Kwa asilimia kubwa kuna ukweli mtoto unampeleka boarding Yuko darasa la Kwanza Cha Kwanza kwa umri alionao angetakiwa karibu na wazazi na apate upendo Cha pili kwa umri huo mtoto ajitambui serikali imefanya vizuri Kwanza ingetakiwa mtoto angalau aanze darasa la Saba angalau ameshaanza kujitambua

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Juzi arusha baba kamuua mwanae kisa fungu la mchicha
 
Sheria ni msumeno,ngoja tuone mwisho wa muhula huu sio mbali.

Au labda watatumia upenyo wa kibali maalum. Watu wanatengeneza mbadala mapema
Swali je watazifungia? Maana Monduli bila boarding huendeshi aisee
 
Msichana wa kazi??[emoji848]


Hawa watu siku hizi mmh
Msichana wa kazi ambaye kidg unaweza kumwamini ni yule mwenye undugu na mzazi mmojawapo aidha Baba au Mama kwasababu atakuwa na uchungu na mtoto au Uoga
 
Mdau gani wa elimu unaepinga hatua nzuri ambazo zimechukuliwa na serikali ,hivi kuna ulazima gani mtoto asiyejua kufua wala kujiogesha aende akaishi bweni??
 
Wazazi wanatakiwa wapeleke wanafunzi shule za karibu na nyumbani.
Kuna wazazi kazi zao zinawafanya kua busy na kazi kuliko kukaa nyumbani na familia. Vipi waache hizo kazi?
 
Serikali ya CCM imeamua kufanyia tangazo la jirani zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kuwa ni mkubwa mno.

Mimi ni mdau wa elimu, hii sababu sio kweli hata siku moja.. SEMA kwa sababu Serikali yetu haifanyi tafiti za kujua tatizo wao huja maamuzi yao bila kufanya utafiti wa kina.
===

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekumbusha kuwa hairuhusiwi huduma ya bweni kutolewa kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne, isipokuwa kwa kibali maalum kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mdau husika.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa imeeleza kuwa shule zote ambazo zinatoa huduma ya bweni kwa madarasa yasiyoruhusiwa zinatakiwa kusitisha huduma hiyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza mwaka 2023.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo ni utekelezaji wa mwongozo wa uanzishaji na usajili wa shule uliotolewa na wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwezi Novemba mwaka 2020.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika baadhi ya shule zimekuwa zikipokea watoto wenye umri mdogo kuanzia darasa la awali hadi la nne, huku huduma zinazotolewa kwa wanafunzi hao zikiwanyima fursa ya kushikamana na familia na jamii zao, kujenga maadili na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya familia zao.

Kulingana na tafiti zilizopo, madhara ya muda mrefu yatokanayo na tabia ya kulaza watoto bweni katika umri mdogo ni watoto kukosa mapenzi kwa wazazi ama walezi na jamii zao na hivyo kushindwa kuwa sehemu ya familia na jamii husika.

Taarifa hiyo ya Kamishna wa Elimu pia imesema kuwa hairuhusiwi kwa shule yeyote kuwa na makambi ya kitaaluma na kuzielekeza shule kuweka mikakati thabiti ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kuzingatia kalenda za mihula zinazotolewa mara kwa mara na Kamishna wa Elimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa malezi na makuzi ya mtoto yanategemea sana mchango mkubwa unaotolewa na familia kupitia wazazi ama walezi wa watoto.

waraka-wa-elimu-na-2-mwaka-2023-kuhusu-utoaji-huduma-ya-kulaza-wanafunzi-bweni-kwa-ngazi-ya-el-jpg.2539134

waraka-wa-elimu-na-2-mwaka-2023-kuhusu-utoaji-huduma-ya-kulaza-wanafunzi-bweni-kwa-ngazi-ya-el-jpg.2539135

waraka-wa-elimu-na-2-mwaka-2023-kuhusu-utoaji-huduma-ya-kulaza-wanafunzi-bweni-kwa-ngazi-ya-el-jpg.2539136
Wizara ya Elimu itaendelea kuboronga mpaka siku tukipata watu sahihi wa kusimamia Elimu ya Taifa letu. Maamuzi yasiyo na tija kabisa
 
Swala hapa sio shule za boarding ndizo zinazopelekea mmomonyoko wa maadili. Hili swala ni Pana sana... Swala la maadili ni Pana sana.

Je, tabia ya uchokoraa watoto wanajifunzia bording school?

Je, tabia ulevi na kutumia madawa ya kulevya wanajifunzia boarding?

Je tabia ya kutukana matusi yote ya nguon wanajifunzia boarding?

Je, tabia ya udokozi na wizi wanajifunzia boarding?

Je tabia ya ulawiti na ushoga wanajifunzia boarding?

Hizo tabia zote hapo juu 98% watoto wanajifunzia mitaan na majumban huo ndo ukweli
Tatizo letu tunafanya maamuzi bila kutumia watu sahihi....
 
Msichana wa kazi??[emoji848]


Hawa watu siku hizi mmh
Sasa baba ana kazi..mama ana kazi unataka wafanyaje?? kwani zamani walikuwa hawaajiri wadada wa kazi... Mimi naona mtoto anakuwa salama zaidi akiishi shule za bweni kuliko huku mtaani aiseee mtaaa umechafukaa mnoooo. So serikali iliangalie hili upya na kwa umakini
 
kama unadhani mtaani ni salama kuliko shule za bweni bhasi hujaishi shule za bweni na huna mtoto ila MTAANI HALI NI MBAYA SANA KIMAADILI MBAYA MNOO.. Matusii...watoto kuiga kufanya vitendo vibaya wanavyoona kwenye mavideo hasa kwenye mabanda kama sio nyumbani..kucheza kamarii.. mambo mengi kibao na ukiona mtoto bweni ana tabia mbovu jua KATOKA NAYO KWAO kwa asilimia 90.
 
Hatari sana, kitanda kimoja wanalala watoto wawili unategemea nini? Ni kaumri ambapo kale karungu kanasimama usiku halafu anamgusisha mwenzake na ukute ni mnyonge wake.Lets us shout, "no boarding for our kids below 14 years."
 
Back
Top Bottom