Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Hata hizo za karibu shule zinalazimisha mtoto akiwa std 4 na 7 akae kwa ulazima boarding. Mimi niliwagomea wakanambia uwe una uwezo wa kumpeleka mtoto saa 12 asubuhi au nimuhamishe nikawaambia fresh tu kwakuwa siko mbali na shule akawa anawahi. Wanafosi kutaka ada za boarding kiulazima.
Me pia lilinikumba hilo wazazi wenzangu kwenye kikao wakawa wananisengenya chinichini nadekeza mtoto duh nilipata wakati mgumu sana nilisimamia msimamo hakai boarding nkawa napeleka 12asubuh,na mtoto akafaulu vizur sana zaid ya walio bweni wakawa wananipongeza kinafisi huku roho zinawauma.
 
Boarding haifai kabisa kwa watoto shule zimejaa maeneo mengi. Mzazi mpeleke mtoto shule ya karibu kwako, hii itamsaidia mtoto kutosumbuka
 
mshatengeneza vichoko kibaaaaao ndio mwashtukia eeh, haya pumbaf zenu wakati wanaanzisha hizo boarding za vitoto mlikuwa wapi? maana wengine hawana hata chembe ya sababu za kupeleka watoto huko ni uvivu tu uliopitiliza na kujitia uzungu.
Bora wameshtuka wewe ulitaka wasishtuke
 
Hapo Ndiyo Utakumbuka Chorus Ya Wagosi Wa Kaya
Kucheka Mtacheka Lakini Mkoa Unadoda



Biashara Za Shule Zinadoda, Na Kuzorota Kabisa
 
Yote haya tumesababisha wazazi vitoto vidogo tumedhani simu nikibembelezeo Cha mtoto ,daddy ,mamu ,omba tuni (katuni) ,mtoto kajua mapaka password .KAZI tunayo
 
Mashoga wote wanatokea huko bording hata hicho kibali maalumu kifutiliwe mbali

Kuna ndugu yangu mmoja ana wake wawili basi ana wazalisha chap chap wake zake sasa ana watoto wengi kama wadogo wadogo alafu wote wanapelekwa bord!!

Yaan katoto kakifikisha miaka miwili tu kanapelekwa bord chalinze huko alafu wao wanaishi mkoa mwingine!! Cha wake zake ni mama wa nyumbani tu !!

Huyu mzee anaandaa mashoga wa mbeleni huko shauri yake.
 
Childcare ni changamoto Dunia nzima. Kuna mtu mwingine analeta boarding kwa sababu mazingira aliyopo hakuna shule. Wengine ni wafanyakazi was TANAPa au mashirika mengine ambayo vituo vyao by kazi ni porini n hakuna huduma ya shule. Pia wapo ambayo wanawaachia mahouse girl wakija jioni watoto wameigwa ,hawajalishwa n ni wachafu. Sera inabidi inanglie hayo yote. Wengi tunapigs makelele ila hata hao watoto walimu was shule wanawajua kuliko mzazi maana muda mwingi hatupo. Hata jumamosi na jumapilli pia hatupo. Wanaosaini hayo makratasi wengi watoto wao wao Feza au international school. Tukae tuangalie suala la malezi vizuri. Suala sio boarding ni malezi. Pia serikali Ina shule za boarding wilaya nzima ya Monduli. Je itazifunga? Arusha school itafungwa? Tusishabikie tu bila kutafakari.
 
Ashukuriwe Mwenyezi Mungu...mwakani kuna mwanangu wa darasa ilimpasa nae akae boarding! Halafu ni lazima...lilikuwa linanifikirisha sana.
Ombea lifanyiwe kazi mkuu..

Nchi hii matamko hutoka tu bure.. utekelezaji sifurii..
 
Shida iko pale pale, dada wakazi hachelewi kumrambisha mtoto cunt🙆‍♀️,ukiwa job
Huko boarding wanalishwa kabisa hizo takataka.

Naipongeza sana Serikali kwa maamuzi haya.
 
Serikali ya CCM imeamua kufanyia tangazo la jirani zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kuwa ni mkubwa mno.

Mimi ni mdau wa elimu, hii sababu sio kweli hata siku moja.. SEMA kwa sababu Serikali yetu haifanyi tafiti za kujua tatizo wao huja maamuzi yao bila kufanya utafiti wa kina.
===

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekumbusha kuwa hairuhusiwi huduma ya bweni kutolewa kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne, isipokuwa kwa kibali maalum kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mdau husika.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa imeeleza kuwa shule zote ambazo zinatoa huduma ya bweni kwa madarasa yasiyoruhusiwa zinatakiwa kusitisha huduma hiyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza mwaka 2023.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo ni utekelezaji wa mwongozo wa uanzishaji na usajili wa shule uliotolewa na wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwezi Novemba mwaka 2020.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika baadhi ya shule zimekuwa zikipokea watoto wenye umri mdogo kuanzia darasa la awali hadi la nne, huku huduma zinazotolewa kwa wanafunzi hao zikiwanyima fursa ya kushikamana na familia na jamii zao, kujenga maadili na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya familia zao.

Kulingana na tafiti zilizopo, madhara ya muda mrefu yatokanayo na tabia ya kulaza watoto bweni katika umri mdogo ni watoto kukosa mapenzi kwa wazazi ama walezi na jamii zao na hivyo kushindwa kuwa sehemu ya familia na jamii husika.

Taarifa hiyo ya Kamishna wa Elimu pia imesema kuwa hairuhusiwi kwa shule yeyote kuwa na makambi ya kitaaluma na kuzielekeza shule kuweka mikakati thabiti ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kuzingatia kalenda za mihula zinazotolewa mara kwa mara na Kamishna wa Elimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa malezi na makuzi ya mtoto yanategemea sana mchango mkubwa unaotolewa na familia kupitia wazazi ama walezi wa watoto.

waraka-wa-elimu-na-2-mwaka-2023-kuhusu-utoaji-huduma-ya-kulaza-wanafunzi-bweni-kwa-ngazi-ya-el-jpg.2539134

waraka-wa-elimu-na-2-mwaka-2023-kuhusu-utoaji-huduma-ya-kulaza-wanafunzi-bweni-kwa-ngazi-ya-el-jpg.2539135

waraka-wa-elimu-na-2-mwaka-2023-kuhusu-utoaji-huduma-ya-kulaza-wanafunzi-bweni-kwa-ngazi-ya-el-jpg.2539136
Ni jambo la msingi sana, hii itasaidia wazazi kuwajibika katika malezi na makuzi ya watoto, nadhani serikali ingeenda mbali zaidi kupiga marufuku ya boarding kwa shule za msingi yaani kuanzia awali mpaka darasa la saba
 
Hivi hawa panya road ambao wengine wameishia tu darasa la pili ni Boarding Schools ndiyo zimewaharibu?
Naona mmiliki wa shule unanyang'anywa tonge mdomoni sio..!!?

Acheni janjajanja nyinyi.
 
Shida kubwa ya mmomonyoko wa maadili ya watoto ni umasikini sehemu kubwa. Wazazi wako busy sana kuhangaika na kutafuta hela.

Kama ni swala la watoto kulawitiana nitaani ndo kunaongoza kwa sababu watoto wako huru mno.

Kwenye familia zenye uwezo, ulawiti wa watoto hufanyikia majumbani mwao walio wengi eidha kwa kufundishwa na wasichana wa kazi au house boy. Kujifunza kuangalia move za mapenzi muda mwingi wawapo majumbani.
Nakubaliana na hoja zako zote, ni kweli lazima tuangalie kwanza maadili lakini tukumbuke kwamba nafasi ya mzazi katika maadili ya mtoto ni kubwa kuliko nafasi ya mtu mwingine yeyote

Kama huyu mtoto atakua boarding that means mzazi hatimizi wajibu wake katika makuzi na malezi ya huyo mtoto ndio maana nasema hii ni hatua moja wapo kubwa katika kuhakikisha mzazi anatimiza wajibu wa malezi kwa mtoto

Lakini hatua nyingine inabidi serikali kwa kushirikiana na jamii nzima iangalie suala zima la maadili kwenye jamii pamoja na kuweka sheria kali zinazowawajibisha wale wote wanaotekeleza ukatili dhidi ya watoto na kuwawajibisha wazazi ambao wanashindwa kutekeleza wajibu wao katika kuwalinda watoto wao dhidi ya ukatili
 
Swala hapa sio shule za boarding ndizo zinazopelekea mmomonyoko wa maadili. Hili swala ni Pana sana... Swala la maadili ni Pana sana.

Je, tabia ya uchokoraa watoto wanajifunzia bording school?

Je, tabia ulevi na kutumia madawa ya kulevya wanajifunzia boarding?

Je tabia ya kutukana matusi yote ya nguon wanajifunzia boarding?

Je, tabia ya udokozi na wizi wanajifunzia boarding?

Je tabia ya ulawiti na ushoga wanajifunzia boarding?

Hizo tabia zote hapo juu 98% watoto wanajifunzia mitaan na majumban huo ndo ukweli
Kila kitu kina upande wa pili. Kuna wakati mama anakukimbia na kukuachia zigo la watoto. Watu wengi katika hali hii kimbilio lao lilikuwa boarding school. Ili mtu uweze kuendelea na shughuli zako na hasa zile zinazohitaji kusafiri mara kwa mara kwa single fathers au single mothers boarding school ilikuwa kimbilio lao. Ukipiga marufuku hili baba au mama wa hawa watoto atafanyaje? Aache kazi awe anawapeleka watoto shule.

Nafikiri kitu cha muhimu ni namna ya kuboresha hizo shule ili ziweze kukithi changamoto zilizopo. Huwezi kutatua tatizo kwa kukataza au kupiga marufuku. Labda serkali ije na mkakati wa kuziboresha hizi shule. Je, serkali itafuta vituo vyote vya kulelea watoto yatima? Je, serkali itavifuta vituo vyote vya kulelea watoto watukutu? Serkali, iache kumtafuta mchawi baada ya kuwa na mitala mibovu, walimu wachovu, madarasa yaliyojaa wanafunzi na wengi wanasomea chini ya miti.

Mimi nakumbuka wakati wangu darasa lilikuwa na wanafunzi 45 ( 1-8), 35 (9-12), na 25 (high school). Siku hizi kuna wanafunzi had 90 kwa darasa moja, alafu tunategemea mwalimu awe effective. Shule nyingi za msingi kinatawala kiboko kuliko kufundisha. Nidhamu mbovu iko zaidi kwenye shule za serkali kuliko binafsi. Shule binafsi wakitaka kuongeza muda wa kufundisha na kuwatayarisha watoto kimasomo wanaambiwa hairuhusiwi. Hivi kweli wasomi wa wizara wa elimu wanadiriki jkuwakataza wadau wa elimu kutoa muda wa ziada wa kujifunza, kwa sababu shule zao zinafanya vibaya na walimu wao hawawezi kujitolea kuwasaidia watoto wafanye vizuri kwenye mitihani!

Dhumuni kubwa la serkali kuweka sheria za mgandamizo kwenye elimu ni kufuatana na aibu wanayoipata kwenye matokeo ya mitihani shule za serkali. Kila kukicha serkali inamtafuta mchawi anayeroga shule za serkali. Wanadhani mchawi ni shule za binafsi, Ndiyo maana utaona wana sheria za ajabuajabu. Mimi mtoto (yatima) wa marehemu dada alinyimwa ufadhili eti kwa sababu alisoma shule ya kulipia. Ushahidi ulikuwepo kuwa ni yatima. Lakini utakuta watoto wa wakubwa na wenye pesa wanapewa mikopo kusoma nje na ndani ya nchi! Kuna maelfu ya wabarikiwa wanaosoma nje ya nchi kwa mikopo ya elimu ya juu, lakini mtoto wa maskini huo mkopo wa kusoma Chuo Kikuu cha St. Rwegalurira au St. Mwakaleli chenye gharama nafuu ananyimwa.
 
Kujishusha na kujidharau namna hiyo dhidi ya jirani ni upuuzi. Wakenya ndiyo wameiga kwetu. Sisi tulipiga marufuku mambo hayo kitambo tu.
nyiyi mlikuwa na maandishi tu wakenye wamenyayuka na vitendo
 
Back
Top Bottom