Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Ashukuriwe Mwenyezi Mungu...mwakani kuna mwanangu wa darasa ilimpasa nae akae boarding! Halafu ni lazima...lilikuwa linanifikirisha sana.
Kwanini shule za mitaala yetu ndo zinakimbilia kukaririsha wanafunzi?

Mbona Cambridge, IB hawakaririshi?
 
Hata hizo za karibu shule zinalazimisha mtoto akiwa std 4 na 7 akae kwa ulazima boarding. Mimi niliwagomea wakanambia uwe una uwezo wa kumpeleka mtoto saa 12 asubuhi au nimuhamishe nikawaambia fresh tu kwakuwa siko mbali na shule akawa anawahi. Wanafosi kutaka ada za boarding kiulazima.
Wanaenda karirisha watoto kujibu
 
S
Serikali ya CCM imeamua kufanyia tangazo la jirani zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kuwa ni mkubwa mno.

Mimi ni mdau wa elimu, hii sababu sio kweli hata siku moja.. SEMA kwa sababu Serikali yetu haifanyi tafiti za kujua tatizo wao huja maamuzi yao bila kufanya utafiti wa kina.
Sahh
 
Wazazi wengine makatili sana.....yaani mtoto wa miaka mitatu/ mi nne unamtelekezea Walimu?????????????
Kisa pesa tu!!!!!!!!
Wanshindwa waiga wazungu mazuri. Wazungu hawapeleki wanafunzi boarding.
 
Tatizo serikali imeruhusu biashara ya shule, mitihani, ufaulu
 
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekumbusha kuwa hairuhusiwi huduma ya bweni kutolewa kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne, isipokuwa kwa kibali maalum kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mdau husika.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa imeeleza kuwa shule zote ambazo zinatoa huduma ya bweni kwa madarasa yasiyoruhusiwa zinatakiwa kusitisha huduma hiyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza mwaka 2023.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo ni utekelezaji wa mwongozo wa uanzishaji na usajili wa shule uliotolewa na wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwezi Novemba mwaka 2020.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika baadhi ya shule zimekuwa zikipokea watoto wenye umri mdogo kuanzia darasa la awali hadi la nne, huku huduma zinazotolewa kwa wanafunzi hao zikiwanyima fursa ya kushikamana na familia na jamii zao, kujenga maadili na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya familia zao.

Kulingana na tafiti zilizopo, madhara ya muda mrefu yatokanayo na tabia ya kulaza watoto bweni katika umri mdogo ni watoto kukosa mapenzi kwa wazazi ama walezi na jamii zao na hivyo kushindwa kuwa sehemu ya familia na jamii husika.

Taarifa hiyo ya Kamishna wa Elimu pia imesema kuwa hairuhusiwi kwa shule yeyote kuwa na makambi ya kitaaluma na kuzielekeza shule kuweka mikakati thabiti ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kuzingatia kalenda za mihula zinazotolewa mara kwa mara na Kamishna wa Elimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa malezi na makuzi ya mtoto yanategemea sana mchango mkubwa unaotolewa na familia kupitia wazazi ama walezi wa watoto.

Waraka wa Elimu Na 2 mwaka 2023 kuhusu Utoaji huduma ya kulaza wanafunzi Bweni kwa Ngazi ya El...jpg

Waraka wa Elimu Na 2 mwaka 2023 kuhusu Utoaji huduma ya kulaza wanafunzi Bweni kwa Ngazi ya El...jpg


Waraka wa Elimu Na 2 mwaka 2023 kuhusu Utoaji huduma ya kulaza wanafunzi Bweni kwa Ngazi ya El...jpg

Waraka wa Elimu Na 2 mwaka 2023 kuhusu Utoaji huduma ya kulaza wanafunzi Bweni kwa Ngazi ya El...jpg
 
kama ni kweli, WAKO SAHIHI, na ikiwezekana iwe marufuku shule bweni shule ya msingi mpaka sekondari.. bweni ianzie form six na hivi vyuo vya kati.. Vyuo vyote ambavyo wanasoma vijana baada tu ya kumaliza shule ya msingi navyo bweni iwe marufuku.
 
Ni jambo jema lakini huwa najiuliza kama Taifa, hivi wasomi wanasiasa wetu tumewakosea nini? Maamuzi haya yalipaswa kufanywa mapema sana lakini kwa maslahi wanayoyajua wao wanavumilia utumbo hadi mambo yaharibike.

Anyway, maamuzi haya yafanyiwe kazi na itoshe kusema sasa basi kwa watoto wadogo kuishi bweni.
 
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekumbusha kuwa hairuhusiwi huduma ya bweni kutolewa kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne...
Elimu yetu imechakachuliwa sana na huu ubabaishaji wa kila mwanafunzi lazima afaulu beyond measures.
Tunasahau bila kuelimika, elimu haina msaada wowote
 
kama ni kweli, WAKO SAHIHI, na ikiwezekana iwe marufuku shule bweni shule ya msingi mpaka sekondari.. bweni ianzie form six na hivi vyuo vya kati.. Vyuo vyote ambavyo wanasoma vijana baada tu ya kumaliza shule ya msingi navyo bweni iwe marufuku.
Na mimi nakazia hapo kabisa. Boarding ingeanzia kidato cha kwanza.
 
Ninachoelewa sheria zipo tatizo wanaozisimamia ndiyo hawapo na kama wakiwepo wanakuwa wamelala, siku jua linachomoza kama hivi sasa (kwa sababu ya haya mambo ya kulawitiana nk) ndipo wana amka na msisitizo.

📌Naendelea kujifunza tabia ya mwanadamu.
 
Back
Top Bottom