Kila kitu kina upande wa pili. Kuna wakati mama anakukimbia na kukuachia zigo la watoto. Watu wengi katika hali hii kimbilio lao lilikuwa boarding school. Ili mtu uweze kuendelea na shughuli zako na hasa zile zinazohitaji kusafiri mara kwa mara kwa single fathers au single mothers boarding school ilikuwa kimbilio lao. Ukipiga marufuku hili baba au mama wa hawa watoto atafanyaje? Aache kazi awe anawapeleka watoto shule.
Nafikiri kitu cha muhimu ni namna ya kuboresha hizo shule ili ziweze kukithi changamoto zilizopo. Huwezi kutatua tatizo kwa kukataza au kupiga marufuku. Labda serkali ije na mkakati wa kuziboresha hizi shule. Je, serkali itafuta vituo vyote vya kulelea watoto yatima? Je, serkali itavifuta vituo vyote vya kulelea watoto watukutu? Serkali, iache kumtafuta mchawi baada ya kuwa na mitala mibovu, walimu wachovu, madarasa yaliyojaa wanafunzi na wengi wanasomea chini ya miti.
Mimi nakumbuka wakati wangu darasa lilikuwa na wanafunzi 45 ( 1-8), 35 (9-12), na 25 (high school). Siku hizi kuna wanafunzi had 90 kwa darasa moja, alafu tunategemea mwalimu awe effective. Shule nyingi za msingi kinatawala kiboko kuliko kufundisha. Nidhamu mbovu iko zaidi kwenye shule za serkali kuliko binafsi. Shule binafsi wakitaka kuongeza muda wa kufundisha na kuwatayarisha watoto kimasomo wanaambiwa hairuhusiwi. Hivi kweli wasomi wa wizara wa elimu wanadiriki jkuwakataza wadau wa elimu kutoa muda wa ziada wa kujifunza, kwa sababu shule zao zinafanya vibaya na walimu wao hawawezi kujitolea kuwasaidia watoto wafanye vizuri kwenye mitihani!
Dhumuni kubwa la serkali kuweka sheria za mgandamizo kwenye elimu ni kufuatana na aibu wanayoipata kwenye matokeo ya mitihani shule za serkali. Kila kukicha serkali inamtafuta mchawi anayeroga shule za serkali. Wanadhani mchawi ni shule za binafsi, Ndiyo maana utaona wana sheria za ajabuajabu. Mimi mtoto (yatima) wa marehemu dada alinyimwa ufadhili eti kwa sababu alisoma shule ya kulipia. Ushahidi ulikuwepo kuwa ni yatima. Lakini utakuta watoto wa wakubwa na wenye pesa wanapewa mikopo kusoma nje na ndani ya nchi! Kuna maelfu ya wabarikiwa wanaosoma nje ya nchi kwa mikopo ya elimu ya juu, lakini mtoto wa maskini huo mkopo wa kusoma Chuo Kikuu cha St. Rwegalurira au St. Mwakaleli chenye gharama nafuu ananyimwa.