Tanzania sihami, Matokeo ya Sensa yakioneshwa kwa Helkopita

Inasikitisha sana, Jana kulikuwa na Mkesha wa Sensa....... Yaani watu wanaandaa Bajeti kwaajili ya kusoma matokeo ya Sensa


Viongozi wamekusanyika Dodoma na kulipana Posho kwaajili ya kupokea Report ya Sensa..... Lengo ni kuzitumbua tu tozo
 
 
Magufuli pamoja na kumsema alikuwa mbaya alijitahidi kubana matumizi Ili Hela ionekane. .
Aliposema tutamkumbuka ndiyo kama ulivyofanya wewe sasa!
Wenye kumtukana na wamtukane tu, lakini mwamba asingekubali upuuzi kama huu.
Mama asipokuwa mwangalifu Tanzania inarudi kule kule kwa enzi za Kikwete, watu wanajitengenezea marukio ili wapige mkwanja. Maskini Tanzania!
 
Wametia shs ngapi? Si afadhali hiyo hela ya sherehe za kutangaza sensa na hata za mchakato mzima wangewekeza kwenye dawasa? Maji hamna...
Watu wa pwani ni wapenda shuhuli yaan wao hawana shuhuli ndogo na haya ndio madhara yake
 
Shida ya kuongozwa na Waswahili. Kila kitu shughuli. Kila mtu analaumu,jiulize waliopanga hii kitu wanafikiria nini. Wana akili kama hizi zetu au?
 
Tunashule za sekondari elfu tano nchi nzima badala tujitafakari, umeme/maji/chakula shida badala tutafakari tunaalikwa tukashangilie helkopta.

Mimi nilimjibu niletee maji nioge ndio nije maana hamna maji huku kwetu! sijui aliisoma?
Mimi siyo mtaalam sana kwenye hilo eneo lakini sms kama hizo huwa hazitoki kwenye simu personal ya mtu husika hata kama imeandikwa jina lake. Hivyo hata majibu huwa hayafiki. Wenye utaalam zaidi wataongea.
 
Yeye kila safari zake helkopta ilikuwa angani inamlinda, sasa sijui ni matumizi gani alibana. Yeye alifanikiwa kubana wanaohoji lakini sio kubana matumizi.
Bora zilikuwa zinamlinda akienda kukagua miradi ya maendeleo kuliko hizi takataka
 
Shida ya kuongozwa na Waswahili. Kila kitu shughuli. Kila mtu analaumu,jiulize waliopanga hii kitu wanafikiria nini. Wana akili kama hizi zetu au?
Walitaka walifanye ni tukio moja kubwa sana ili watusahaulishe ishu za mma na umeme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…