Tanzania sio pango la wanyanganyi period Rais chukua hili kwa uzito mkubwa

Tanzania sio pango la wanyanganyi period Rais chukua hili kwa uzito mkubwa

Genge la uhujumu uchumi la hatarisha ustawi wa nchi kwa maslahi yao binafsi kwa kuuza kila raslimali ya nchibila kuweka mbele uzalendo ,hatari kubwa sana
 
Watu wanadhani dunia itatusubiri miaka 40 mbele au 50 mbele ndio tuuze,
Mafuta yauzwe leo leo asubuhi,
Zipatikane hela, vijengwe vyuo vikuu vikubwa, veta ziboreshwe, barabara zipigwe lami nyingi, hospital zijengwe za grade A,
Vizazi vijavyo tutawachia elimu bora, viwanda, na makampuni makubwa yatayozalishwa kwa sababu ya shughuli za uchumi zitazoletwa na mafuta
Usisahau na VETA mkuu
 
Viuzwe tu kiasi kipelekwe kwenye michezo, kila team ya Kariakoo ipewe fungu nono la usajili, kuwe na Samia Cup kila kitongoji, wananchi tupewe tickets za bure tuujuze uwanja wa Mkapa, matamasha kibao, Konda apewe mgao wake kwa ajili ya stunts zake na pia ziongezwe tunzo tusishie kwa wachekeshaji na waimbaji tu, kwenye hizo hela liwekwe donge nono kwa ajili ya tunzo za wachezaji zilizoboreshwa zaidi.
 
Gentleman,
kwa dhamana nzito na muhimu niliobeba kwaniaba ya wananchi jimboni, wadau wa JF na waTanzania wote, ukiniangalia mimi ni mtu wa kubabaishwa na dhana amabzo hazina athari zozote kisiasa?

yaani kweli mimi nitishike na mihemko na makasiriko yako ya kindezi namna hiyo? :pedroP:

neema na baraka za Mungu ziambatane na kuandamana nawe katika mapumziko yako ya leo.
Mungu akubariki sana, na nitaendelea kukuombea pia ili hatimae uwe mtu mwema na mstaarabu.
Hukutakiwa kuwa ccm ,jitahidi kutubu ,acha uchwa utabarikiwa,ila ukiendelea na uchawa laana Mungu haitakuacha salama.
 
Hukutakiwa kuwa ccm ,jitahidi kutubu ,acha uchwa utabarikiwa,ila ukiendelea na uchawa laana Mungu haitakuacha salama.
ni Baraka na Neema za Mungu alizonijalia, ndizo ambazo zinanipa ujasiri na nguvu ya kueleza ukweli kwa ujasiri bila kubabaika na mbambamba za wenye chuki binafsi dhidi ya dhamira na nia njema ya mbeba mono ya waTanzania Dr.Samia Suluhu Hassan.

huna haja ya kunitisha na ushirikina na ramli zako gentleman :pedroP:
 
Watu wanadhani dunia itatusubiri miaka 40 mbele au 50 mbele ndio tuuze,
Mafuta yauzwe leo leo asubuhi,
Zipatikane hela, vijengwe vyuo vikuu vikubwa, veta ziboreshwe, barabara zipigwe lami nyingi, hospital zijengwe za grade A,
Vizazi vijavyo tutawachia elimu bora, viwanda, na makampuni makubwa yatayozalishwa kwa sababu ya shughuli za uchumi zitazoletwa na mafuta
Mkuu acha utapeli wa kisiasa, haya mambo yanawezekana ila sio kizazi cha sasa ambacho kimejaa ubinafsi badala ya kujali Taifa , kuna kizazi kinakuja kitaweza kutekeleza aya yote .

Yani nchi ya watu mil 60 akili zetu zote tumeweka katika kuuza na kubinafisisha kweli.

Haiwekani lazima kama Taifa kuwatumia first class thinkers , sio wale wamejazana vitambi ila kufikili kesho ya taifa hili hamna,kama taifa kuna sehemu tunakosea kwa kuamini ili tusonge mbele suruhu ni kuuza na kubinafishisha kila kitu
 
Viuzwe tu kiasi kipelekwe kwenye michezo, kila team ya Kariakoo ipewe fungu nono la usajili, kuwe na Samia Cup kila kitongoji, wananchi tupewe tickets za bure tuujuze uwanja wa Mkapa, matamasha kibao, Konda apewe mgao wake kwa ajili ya stunts zake na pia ziongezwe tunzo tusishie kwa wachekeshaji na waimbaji tu, kwenye hizo hela liwekwe donge nono kwa ajili ya tunzo za wachezaji zilizoboreshwa zaidi.
Ndo maana nasema kizazi cha kutekeleza miradi mikubwa kama hii sio cha sasa ila kinakuja asema Bwana
 
Watumishi wa Mungu wa dini zote mpo na jambo la kufanya.

1. Ombea viongozi wawe na maono ya Taifa hili kwa miaka 200+ ijayo hasa kwenye rasilimali za Taifa bila kupepesa macho
2. Achana na biashara ya kupoteza nguvu nyingi ati kuombea uchaguzi ambao no reforms no election.

3.zidisheni maombi kwa taifa badala mtu binafsi na neema ya Bwana itakua juu yenu.
4. Fungeni na waumini wenu juu ya Taifa hili, achana na chunvi, mafuta ya upako na rejea msabani kwa wakristu.

Note
Mimi sio mwalim,mchungaji, askofu na sina kanisa na wala sio wito wangu katika huduma hizi, ila mlio katika wito huu tekeleza na neema ya Mungu itakua juu yenu , huu ndo ujumbe wenu ,
 
Leo nipo na hasira sana , nimeona maneno ya mwajiriwa wetu ndugu Rais kwamba nchi hii ipo na mafuta mengine mengi , ila taarifa inasema tutauza kama nchi .

Ndugu Rais nikuombe na watakiwa kujua kwamba umevikuta kwa maana watangulizi wako waliviacha , na sio kwamba hu Rais basi unawazidi wenzako waliokutangulia namanisha ,Mwalim, Mwinyi, Mkapa Jk , Magufuli , hii acha mara moja asema Bwana.

Leo tupo kesho hatupo , vitukuu vyako unataka kuwachia nini ndani ya Taifa lao ????

Nikuombe hachana na hii by mzalendo a. k.a mbatizaji 47
🚮🚮
 
Ndo maana nasema kizazi cha kutekeleza miradi mikubwa kama hii sio cha sasa ila kinakuja asema Bwana
Kama sikusikia vibaya hata hizi mbuga nyingi za wanyama kuna madini so usishangae ukiona magari ya mchanga Selous. Vitu vingi vitawekwa lehani tu hasa has hiki kipindi pesa inahitajika sana.

Naomba tu mwisho wa siku hivi vitu vimnufaishe mTanzania.
 
Jikite kwenye mada, na zingatia neo kuuza sio kubuni miradi, Taifa linakufa kifo kibaya kwa kuwa na watu vilaza kama wewe,
Nimejikita katika mada yako na kukupa mifano tofauti lakini unatung'ang'aniza twende inavyotaka mentality yako.....sasa kama si ukilaza ni nini kuikataa awamu ya rais Samia isianze uwekezaji huo na ziwe awamu nyingine....

Hapa ndipo penye mzizi wa hoja yako....

Haya nijibu ,ni kwanini isiwe awamu ya rais wetu Samia Suluhu Hassan?
 
ni muhimu sana kua na heshima na nidhamu walau ya kibinadamu tu kwa viongozi wakuu wa Taifa letu,

mihemko, ghadhabu na chuki binafsi dhidi ya mipango mahususi ya serikali sikivu ya CCM kwa maslahi mapana ya waTanzania wote, sio turufu ya kukufanya umdhihaki kiongozi mkuu wa nchi.
Kumbuka,
kila zama na kitabu chenye hadithi yake, vitisho vyako tishianeni kwenye chama chenu gentleman 🐒
Mtoa maada hajakosea chochote, yeye katoa hoja. Hivyo yapasa hoja ikitolewa ijadiliwe na ukiona haikufai kutokana na mtazamo wako, si lazima uchangie
 
Nimejikita katika mada yako na kukupa mifano tofauti lakini unatung'ang'aniza twende inavyotaka mentality yako.....sasa kama si ukilaza ni nini kuikataa awamu ya rais Samia isianze uwekezaji huo na ziwe awamu nyingine....

Hapa ndipo penye mzizi wa hoja yako....

Haya nijibu ,ni kwanini isiwe awamu ya rais wetu Samia Suluhu Hassan?
Nilijua tu utajaa kwenye mfumo,
Jibu Rais anaweza kuwa na nia nzuri ila watu wake mfano wewe wapo na ubinafsi wa kujaza matumbo yao , nchi imejaa ufisadi wa kutisha, leo kama nchi hata mabasi ya mwendo kasi , shirika la ndege , SGR mnashindwa kuonesha ufanisi itakua miradi mikubwa kama ya mafuta.

Mpaka sasa mradi wa Gesi umelinufaisha vipi Taifa? Kwa nini hamsemi ukweli mpaka mnakimbilia kuwekeza pesa nyingi kwenye bwawa la Mwalim ili hali umeme bado ni changamoto.
Tumebinafisisha Bandari n.k tija iko wapi ili hali tunaendelea kukopa daily deni la taifa linapaa.

Hakuna kuuza hapa mafuta ,kipo kizazi chenye uchungu na taifa hili kitakuja na ndipo watz wataona matunda ya rasilimali zao,
 
Wamesha Saini mikatba ya mafuta tayari kwa hiyo wananchi hatuna chetu tena ktk nchi hii viongozi ni madalali wote wa kuuza nchi na raslimali yetu chura kiziwi dalali mkuu
 
Mtoa maada hajakosea chochote, yeye katoa hoja. Hivyo yapasa hoja ikitolewa ijadiliwe na ukiona haikufai kutokana na mtazamo wako, si lazima uchangie
Gentleman,
hata mihemko na makasiriko dhidi ya mawazo na maoni mbadala dhidi ya kitu ambacho hujapenda kielezwe hadharini kwa usahihi ni miongoni mwa ubabaifu katika mjadala 🐒
 
Wamesha Saini mikatba ya mafuta tayari kwa hiyo wananchi hatuna chetu tena ktk nchi hii viongozi ni madalali wote wa kuuza nchi na raslimali yetu chura kiziwi dalali mkuu
Kama ndivyo , ni hatari sana
 
Back
Top Bottom