SoC04 Tanzania tuitakayo ambayo wananchi wake hawapotezi muda barabarani hasa katika majiji makubwa kutokana na foleni

SoC04 Tanzania tuitakayo ambayo wananchi wake hawapotezi muda barabarani hasa katika majiji makubwa kutokana na foleni

Tanzania Tuitakayo competition threads

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
346
Reaction score
522
UTANGULIZI.
images.jpg

NB: picha kwa hisani ya mtandao

Tatizo la foleni ni changamoto kubwa katika maeneo mengi ya mijini hasa Dar Es Salaam hapa Tanzania.Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha ongezeko la foleni hasa kwa jiji letu pendwa la Dar Es Salaam .Watu wanapokwama kwenye foleni, wanachelewa kufika kazini na kwenye mikutano muhimu hivyo kusababisha kutokuwepo kwa wakati na kuharibu mahusiano ya kitaalamu na hata kusababisha adhabu au kupoteza fursa za kazi ,pia foleni zinasababisha mazingira hatari kwa ajali za barabarani kutokana na msongamano wa magari.
Naweza kuzitaja kwa uchache sababu za kwanini kuna foleni hasa kwenye majiji ;
  1. Ongezeko la idadi ya magari barabarani linasababisha msongamano wa trafiki jam, kutokana na ukuaji wa idadi ya watu, uchumi unaoendelea, au ongezeko la umiliki wa magari.​
  2. Barabara zilizopitwa na wakati na zenye miundombinu duni zinasababisha foleni kwa kuwa hazitoshelezi mahitaji ya trafiki iliyopo.​
  3. Kazi za ujenzi wa barabarani na miundombinu mingine zinasababisha vikwazo kwenye barabara ambazo zinaweza kusababisha foleni.​
  4. Matatizo katika mfumo wa usafiri wa umma uchache wa mabusi,kujazana na kushonana kwenye magari pomoni, uchelewaji wa mabasi unasababisha watu kutumia magari binafsi zaidi na hivyo kuongeza msongamano wa trafiki (trafic jam).​
  5. Tabia mbaya za madereva kama vile kutokuwa na nidhamu barabarani, kupita kwa nguvu, na kusimamisha magari kiholela hasa daladala na kusababisha msongamano wa trafiki jam.​
  6. Mvua kubwa na hali mbaya ya hewa inasababisha foleni kwa kuzuia mwendo wa kawaida wa tmagari.​
  7. Nyakati nyingine misafara ya viongozi.​

TUFANYE NINI KUPUNGUZA FOLENI HIZI ZA MAGARI BARABARANI.
Uwekezaji katika miundombinu bora ya barabara na mifumo ya usafiri wa umma ni muhimu sana katika kupunguza foleni.

UJENZI WA MIUNDOMBINU.
download.jpg

NB; picha kwa hisani ya mtandao.

  1. Kuongeza idadi ya njia za kusafiria kwa magari kunaweza kupunguza msongamano wa trafiki kwa kuruhusu magari kupita kwa urahisi zaidi.,Angalau tuwe na barabara 4 ways pamoja na njia za waenda kwa miguu.
  2. Kujenga barabara za kasi au njia za mabasi yaendayo kasi kunaweza kusaidia kutoa chaguo mbadala kwa madereva na kusafirisha abiria kwa haraka, hivyo kupunguza foleni kwenye barabara za kawaida.
  3. Kuwekeza katika mifumo ya usafiri wa umma kama vile mabasi yamwendo kasi, treni za mwendo kasi,na mfumo wa treni za mitaani kunaweza kuhamasisha watu kutumia usafiri wa umma badala ya kutumia magari binafsi.
  4. Kujenga njia za kupita kwa watembea kwa miguu na baiskeli kunaweza kusaidia kupunguza trafiki jam kwa kuhimiza watu kutembea na kupanda baiskeli badala ya kutumia magariambayo pia ni salama kiafya.
  5. Kuwekeza katika teknolojia za usafiri kama vile mifumo ya kutabiri foleni, programu za kusaidia kuepuka foleni, na mifumo ya usimamizi wa trafiki inaweza kusaidia kuboresha usimamizi wa trafiki na hivyo kupunguza foleni.
KUWEKEZA KATIKA TEKINOLOJIA.
  1. Ujenzi wa madaraja ya juu (flyovers) ni njia mojawapo ya kukabiliana na foleni kwa kuzingatia mazingira na mahitaji ya kila jiji. Mfano kwa Dar maeneo kama MWENGE, Goba madukani,Morocco, airport ,buguruni,Magomeni,Karume,na maeneo mengineo ya makutano ya barabara panahitajika hizi barabara za madaraja ya juu katika kupunguza foleni.
  2. Kuwepo kwa taa za kuongozea magari za kisasa ni njia muhimu ya kukabiliana na foleni na kusimamia trafiki kwa ufanisi zaidi. Trafiki light za kisasa zinaweza kusaidia kuzuia ajali kwa kutoa maelekezo sahihi na wazi kwa madereva na kusimamia kwa njia inayofaa.
  3. kuweka kamera za usalama barabarani kote, serikali na mamlaka husika zinaweza kuboresha usalama wa barabarani na kuchangia katika kupunguza ajali na foleni kwenye barabara. Ni muhimu kuzingatia pia masuala ya faragha na kutumia teknolojia hii kwa njia inayofuata kanuni na taratibu za kuheshimu haki za watu.
  4. Vitendo vya kutoa upendeleo kwa magari ya upande mmoja tu kuvushwa kwenye foleni za makutano ya barabara wakati wengine wanahangaika kwenye foleni ni suala linalosababisha mafadhaiko kwa madereva na linaweza kuchangia hisia za kutokuwa na haki katika jamii mfano eneo la Mwenge DAR nyakati za jioni hasa kwa magari yanayotoka posta mjini.

KUWEKEZA KATIKA USAFIRI WA UMMA.
images (2).jpg

NB; picha kwa hisani ya mtandao.

  1. Kuwekeza katika upanuzi wa mtandao wa usafiri wa umma na kuboresha ubora wa huduma kunaweza kuwavutia watu kutumia usafiri wa umma badala ya kutumia magari binafsi. Hii inaweza kujumuisha kuongeza idadi ya mabasi au treni, kuimarisha mifumo ya tiketi, na kuboresha vituo vya usafiri.
  2. Serikali na mamlaka husika zinapaswa kuwekeza katika kununua na kuleta magari ya mwendo kasi ya kisasa ambayo ni ya hali ya juu na yanatoa huduma bora kwa abiria. Magari haya yanapaswa kuwa na vigezo vya juu vya usalama na kukidhi haja za watumiaji.
  3. Mamlaka za usafiri zinapaswa kushirikiana na makampuni ya usafiri ili kuhakikisha kuwa mahitaji ya abiria yanazingatiwa na kujumuisha maoni yao katika kuboresha huduma. Pia, mawasiliano mazuri kati ya watoa huduma na watumiaji ni muhimu katika kujenga imani na uaminifu.

KUSIMAMIA SERA BORA ZA MIPANGO MIJI.
Kusimamia sera bora za mipango miji ni muhimu sana katika kupunguza msongamano wa magari barabarani na kuboresha maisha ya watu katika miji.
  1. Kusimamia sera bora za mipango miji kunaweza kuhusisha kuweka mipango mipya ya makazi ambayo inaweka kipaumbele kwa njia za usafiri wa umma na miundombinu inayohamasisha watu kutembea au kutumia baiskeli.

MAGARI MAKUBWA YA MIZIGO YATUMIE BARABARA NYAKATI ZA USIKU NA JIONI ,YASIINGIE MJINI MCHANA.
Kuweka sera ambazo zinahimiza magari makubwa ya mizigo kutumia barabara nyakati za usiku na jioni na kuzuia kuingia mjini mchana ni njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafirishaji mijini.

USHAURI JUU YA MISAFARA YA VIONGOZI KATIKA KUKABILIANA NA FOLENI HASA KWENYE MAJIJI KAMA DAR ES SALAAM.
  1. Misafara ya viongozi inaweza kupangwa kufanyika nyakati ambazo zina athari ndogo kwa usafiri wa kawaida, kama vile nyakati za mapumziko ya jioni au asubuhi mapema. Kupanga misafara kufanyika wakati ambapo kuna idadi ndogo ya magari barabarani kunaweza kusaidia kupunguza msongamano na foleni.
  2. Maafisa wa usimamizi wa trafiki watoe mwongozo maalum kwa misafara ya viongozi ili kuhakikisha inapita kwa urahisi na kwa haraka bila kusababisha msongamano mkubwa.(hili ndio hufanyika).
  3. Teknolojia inaweza kutumika kutoa taarifa za wakati halisi kuhusu harakati za misafara ya viongozi kwa umma ili watu waweze kuepuka maeneo ambayo misafara hiyo inapita.
  4. Kutoa taarifa kwa umma juu ya misafara ya viongozi itakayofanyika na njia itakayopitia kunaweza kuwasaidia watu kupanga mipango yao ya safari na kuepuka maeneo ambayo yana uwezekano wa kusababisha msongamano.
  5. Kama kuna uwezekana matumizi ya ndege (helkopta) kwa misafara ya ghafla inaweza kupunguza foleni.

MWISHO.
Foleni inasababisha kupoteza muda mwingi, msongamano wa magari, uchafuzi wa mazingira, na hata athari za kiuchumi. hatuna budi kujitahid kupunguza ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza.
 
Upvote 6
Nyakati nyingine misafara ya viongozi.
Halafu hii kitu hiii, sijui tuweke utaratibu wa kiongozi naye atembee na foleni kama kawaida ili suluhisho lije harakaharaka zaidi kila mmoja apate uzoefu wa kukwamishiwa shughuli zake kwa ajili ya foleni.

Kusimamia sera bora za mipango miji kunaweza kuhusisha kuweka mipango mipya ya makazi ambayo inaweka kipaumbele kwa njia za usafiri wa umma na miundombinu inayohamasisha
Nakubali, hatujajua tu nchini kwetu. Lakini walioendelea tayari kama Scandinavia yaani baiskeli ni kitu cha lazima na fahari.

Kuweka sera ambazo zinahimiza magari makubwa ya mizigo kutumia barabara nyakati za usiku na jioni na kuzuia kuingia mjini mchana ni njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafirishaji mijini
Huu hautakuwa upendeleo kwa wwngine na kuwanyang'anya wengine nafasi ya kujenga uchumi usiku na mchana?
 
Halafu hii kitu hiii, sijui tuweke utaratibu wa kiongozi naye atembee na foleni kama kawaida ili suluhisho lije harakaharaka zaidi kila mmoja apate uzoefu wa kukwamishiwa shughuli zake kwa ajili ya foleni.
Kuna wakati fulani foleni zinakwaza ,zinatugombanisha na waajiri wetu ,na Wengine wanachelewa kwenye shughuli zao za kiuchumi .
 
Nakubali, hatujajua tu nchini kwetu. Lakini walioendelea tayari kama Scandinavia yaani baiskeli ni kitu cha lazima na fahari.
Sasa Huku Dar Es Salaam, service road NI sehemu ya kufanyia biashara ndogondogo hasa jioni ,yaani 😁 wafanyabiashara wadogo kila ikifika jioni wanapanga vitu vyao wanaendelea na biashara ,yamkini hawalipi kodi wala nini ,mfano maeneo ya Mwenge ,Buguruni, Ubungo interchange -njia panda ya chuo ,karume nk..,Mamlaka zinapaswa kulitizama hilo.
 
Huu hautakuwa upendeleo kwa wwngine na kuwanyang'anya wengine nafasi ya kujenga uchumi usiku na mchana?
NI kweli lakini katika Hali ya kawaida tunaweza tukalitazama Kwa busara ya kawaida ili kila mmoja aone yeye ni muhimu na ahakikishiwe kupata nafasi sawa ya kujenga uchumi bila upendeleo.
 
NI kweli lakini katika Hali ya kawaida tunaweza tukalitazama Kwa busara ya kawaida ili kila mmoja aone yeye ni muhimu na ahakikishiwe kupata nafasi sawa ya kujenga uchumi bila upendeleo.
Hakika, ni kutunga sera tu ambazo wote wanafaidi. Mfano ile iliyoruhusu magari kisafiri masaa 24 imesaidia sana.
 
Back
Top Bottom