SoC04 Tanzania tuitakayo: Elimu ya Fedha kwa Raia ni Muhimu kwa Maendeleo ya Taifa. Tuanze na watoto sasa

SoC04 Tanzania tuitakayo: Elimu ya Fedha kwa Raia ni Muhimu kwa Maendeleo ya Taifa. Tuanze na watoto sasa

Tanzania Tuitakayo competition threads

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
TUANZE NA WATOTO ELIMU YA KIFEDHA
Moja ya elimu muhimu sana tulio ikwepa ni elimu ya fedha, ambayo huenda ingetusaidia sana kwenye mipango yetu ya maisha ya kila siku na hivyo kusaidia taifa hili.

Watanzania wengi hatuna elimu ya kifedha nikiwemo mimi ninaye andika hii story. tusichanganye elimu ya kifedha na Degree zetu na Masters zetu.

Miradi mingi huko vijijini inayo anzishwa na Serikali na hata taasisi binafisi huwa mwisho wa siku haionekani kwa sababu walengwa wenyewe elimu ya kifedha hawana, Unaweza peleka mradi kwenye jamii (TASAFU) wana jamii wakipata pesa kikubwa ni kuoa au kuanza mashindano ya kununua nguo na vitu kama simu na kufanya sherehe. Unashangaa kuna maeneo kuna kilimo unakuta cha Korosho, Machungw, Pamba na kadhalika ila raia unakuta umasikini uko pale pale na wanavuna na wanauza na wanapata pesa kabisa.

Wenzetu hii elimu ilitolewa kuanzia wakiwa watoto wadogo sana na ndio leo tunaona inavyo wasaidia sana na sisi kubakia kuona kwamba wana pesa sana kumbe sio.

Nini maana ya elimu ya kifedha? Elimu ya kifedha inajumuisha ujuzi, tabia na majukumu ya kukuwezesha kufanya maamuzi sahihi ya pesa yako ili kufikia kuwa na uwezo binafisi wa kifedha au uhuru wa kifedha. Elimu ya kifedha inaleta uwezekano wa mtu kuwa na uelewa wa juu kabisa wa kifedha. Watu wengi tunafananisha Financia education na masoma ya Finance au Business education, hivi ni vitu viwili tofauti kbisa. Elimu ya kifedha pia wala haifanani na elimu ya ujasiriamali.

Elimu ya Kifedha ndio inayo wafanya wenzetu waonekane wana pesa sana kumbe sio ila tu wanajua matumizi ya pesa, wapi watumie pesa na wapi wasitumie pesa, Elimu hii ndio inafanya watu kule Arusha wawaone watalii kama watu wenye pesa kumbe ni wamejichanga miaka 10 ili tu wasafiri waje kuna Tembo au Simba.

Madhara ya kuto kuwa na rai wenye elimu ya kifedha;

Matumizi ya hovyo ya fedha; Ukweli ni kwamba tuna matumzi ya hovyo sana ya fedha, unaweza kuta mtu asubuhi anaenda kazini ila jioni anarudi na viatu, hakuwa ameplani kununua viatu ila tu kakutana na Machinga anauza kiatu basi kaona anunue. Ni mara ngapi umenunua vitu ambayo hukuwa navyo na plan kabisa ila tu umekutana nacho kikakuvutia basi ukanunua, Hii ni ukosefu wa elimu ya kifedha na hakuna kingine.

Kutumia pesa katika mambo yasio kuwa na muhimu; ,michango isio isha ya harusi, sendoff, mara kuwatoa offer mashikaji, party zisizo kuwa na maana, masindano ya kuvaa vizuri, kula vizuri, haya yote yanasababishwa na watu kuto kuwa na elimu ya kifedha.

Kukosa akiba muhimu ya fedha; Watu wengi hasa wafanya kazi, huwa hawana akiba ya maana ya pesa kwa sababu mara nyingi pesa inatumika ndivyo sivyo,vyakula vinapikwa vingi ndani na baadae vina mwagwa, kununua nguo nyigi ambazo hata hatuzivai. Kukosekana kwa elimu ya kifedha kunatufanya hata kuto kuwa na akiba ya fedha, na tukitetereka kidogo tu hali huwa ni mbaya sana.

Watoto kujifunza tabia mbaya kwenye matumizi ya pesa; Wenzetu wakienda na watoto wao Super Market au hata mjini, huwezi ona mtoto analilia kila kitu kinacho katiza mbele yake mara mdori, mara juice mara hiki, watoto walisha jifunza kutoka kwa wazazi wao au wanafundishwa shuleni, na ndio maana ni ngumu sana kukuta wanadanganyika kwa pesa. Familia huridhika na kile ilicho nacho kwa sababu wanaishi kwenye bajeti yao.

Rushwa, Ufisdi, kwa sababu ya kukosa elimu sahihi ya kifedha, imepelekea mashindano makubwa ambayo sasa ili uweze kupata pesa ya kukidhi mashindano ni inabidi uchukue rushwa au ufanye ufisadi, rushwa nyingi ni kwa sababu ya kutaka kukidhi mashindano mtaani, nyumba kari sana, gari kari sana, Bata sana na kadhalika.

Kuwa na mtazamo kwamba watu weupe ni watu wenye pea nyingi sana; Sisis mara nyingi na iko hivi hadi sasa tunaamini watu weupe wana pesa nyingi sana, kumbe sio kwamba wana pesa sana ila wana mpangilio sahihi wa pesa zao, hawana mashindano kabisa ya aina yoyote kwenye maisha, hawaishi kuwafurahisha watu kama ilivyo sisi. Famili nyingi sisi tunaishui kufurahishana, kujaza vyombo kabatini, wageni wakija washangae shange, Sofa kubwa kuwafanya wageni wapigwe butwaa, wenzetu hawana haya mambo kabisa.

Uhusiana wa elimu ya kifedha na Uchumi wan chi?

Raia wanapo kuwa na uelewa sahihi wa elimu ya kifedha inawasaidia sana kwenye kupangilia mmambo ambayo yanakuja kusaidia hata nchi, ikiwemo ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali, Fikiria unadaiwa kodi na hapo hapo unaamua kwenda kuchangia harusi kwa sababu usipo changia harusi utaonekana mbaya, utaoneakana huna pesa, utadharuliwa, utachekwa.

Nini sasa tufanye kwenye elimu ya kifedha?

Il nchi kuwa moja ya nchi zenye uchumi mkubwa sana, hatuwezi acha nyuma elimu kama hii ya kifedha ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ya nchi.

Ni kwati sasa wa Serikali kuanzisha mitala ya elimu ya kifedha mashuleni, hii inaweza anzia chini kabisa ambako watoto wataanza kujengewe msingi imara kabisa wa pesa. Serikali inawez punguza baadhi ya masomo ya shule za awali na masingi ili kuingi hili somo muhimu sana la kifedha. Hii inawezekana kabisa na ina umuhimu mkubwa sana kwa nchi.

Watoto wakiwa bado wadogo sana watajifunza Kubajeti, kukopa, kuwekeza, uwekaji wa kabisa na jinsi ya kutumia pesa kwa unagalifu mkubwa sana, Spend wisely, hii ikifanyika kwa watoto wadogo itakuwa na matokeo hasi sana kwenye jamii na sijui kwa nini Serikali haijawahi kuliona hili.

Elimu ya kifedh ikianzishwa mashuleni itauwa ni njia pekee ya kuwiangizia uelewa wa kifedha kwenye masiha yao. Mapema hii elimu inavyo tolewa ndivyo mapema inaenda kuwa namatokea chanya.

Bila kuwa na kizazi kinacho jua tangia utotoni elimu ya kifedha ni vigumu sana hata kuja kusimamia miradi ya Serikali,au ni vigumu sana kuondoa umasikini kwenye jamii.

Kuna njia nyimgi ambazo zinaweza tumika kuanzisha somo la elimu ya kifedha kwa watoto wadogo mashuleni kama vile kuwapatia mifano halisi, visa mbali mbali vya matumizi ya pesa,michezo kama Game, na shughuri mbalimbali ambazo zinaweza jumuisha mambo ya kifedha, Watoto wanaweza wakawa wanapewa kazi za kutengeneza hata bajeti za safari zao, Bajeti za matumizi nyumbani kwao na kadhalika.

1716714672088.png
Kitabu cha elimu ya kifedha kwa shule za Zambia. Zambia Wameanziha hili somo. Picha mtandaoni.

TUANZE NA WATOTO ELIMU YA FEDHA
 
Upvote 2
Matumizi ya hovyo ya fedha; Ukweli ni kwamba tuna matumzi ya hovyo sana ya fedha, unaweza kuta mtu asubuhi anaenda kazini ila jioni anarudi na viatu, hakuwa ameplani kununua viatu ila tu kakutana na Machinga anauza kiatu basi kaona anunue.
Fedha nayo ni tata sana, mfano hapo tukiangalia kwamba hapo uchumi umejongea biashara zimefanyika inakuwaje hapo bro?

Kuwa na mtazamo kwamba watu weupe ni watu wenye pea nyingi sana; Sisis mara nyingi na iko hivi hadi sasa tunaamini watu weupe wana pesa nyingi sana,
Hahahahaah 😆🏃

Kuna njia nyimgi ambazo zinaweza tumika kuanzisha somo la elimu ya kifedha kwa watoto wadogo mashuleni kama vile kuwapatia mifano halisi, visa mbali mbali vya matumizi ya pesa,michezo kama Game, na shughuri mbalimbali ambazo zinaweza jumuisha mambo ya kifedha, Watoto wanaweza wakawa wanapewa kazi za kutengeneza hata bajeti za safari zao, Bajeti za matumizi nyumbani kwao na kadhalika.
Wazo zuri bro. Elimu ndiyo inafanya mtu atawale kitu. Kuwa na elimu ndogo ua kitu hufanya hicho kitu kimtawale mtu.

Katika hiyo elimu ya fedha naomba waanze na difinisheni ya fedha halisi
Fedha: Ni cheti anachotunikiwa mtu aliyetenda kitu chochote cha kuinufaisha jamii inayomzunguka. Naye yeye hukitumia cheti hicho kuwatunuku watu watakaomnufaisha katika jamii yake. Hivyo kwa mzunguko unaojirudia.

Ili tangu mwanzo kabisa wajue na waelewe kwamba fedha ni mali ya jamii kimsingi.
 
Back
Top Bottom