SoC04 Tanzania Tuitakayo: Kuwepo na utofauti kati ya vyama vya siasa vya uraiani na vile vinavyotumika vyuo vikuu na kati

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kong xin cai

Member
Joined
Dec 12, 2020
Posts
76
Reaction score
87
UTANGULIZI
Nchi yetu ni ya kidemokrasia, na mifumo yote ya kiutawala inazingia misingi ya kidemokrasia.
Hivyo Kila Raia anayo Hali ya kuchagua chama Cha siasa anachokiona Bora.
Zipo tawala mbali mbali nchini zinazotumia mifumo ya vyama vingi kupata watawala au viongozi.
Tawala Moja wapo ambazo hasa tunategemea ziwe mfano Kwa jamii ni hizi za ngazi za elimu yaani vyuo vikuu na kati.
Ombi langu ni kwamba vyama vitakavyotumika vyuo visiwe vile vinavyotumika kupata viongozi ngazi ya kata, wilaya mpaka taifa hapa nazungumzia Chama tawala (CCM) na vyama vya upinzani

FAIDA KUTENGANISHA UHUSIANO WA KIUTAWALA KATI YA VYAMA VIKUU NA VITAKAVYOTUMIKA VYUONI

1. Ili kuleta mabadiliko. Mabadiliko haya ni Yale ambayo yamekuwa changamoto Kwa vyama VIKUU au chama tawala. Sote tunafahamu mabadiliko mengi yanatoka Kwa wanazuoni, hivyo hii itasaidia kuleta mitazamo mipya ambayo inaweza kuigwa na vyama VIKUU. Kuendelea kutumia vyama VIKUU vyuoni ni kuendelea kurithirishana haya haya yanayoendelea kwenye siasa za sasa.

2. Kuleta viongozi wenye mitazamo tofauti. Vyama VIKUU vimekuwepo Toka uhuru, ni wazi kwamba baadhi ya sera na itikadi zake zimepitwa na wakati, ni wakati sasa serikali kutoa uhuru Kwa wanazuoni kuja na itikadi tofauti na kuzalisha viongozi wenye mitazamo tofauti.

3. Kuleta changamoto chanya kwenye vyama VIKUU. Kwa sasa vyuo vimekuwa vingi sana vyuoni, hivyo kukiwa na utawala wenye itikadi chanya itakuwa chachu Kwa vyama VIKUU kuanzA kufanya mabadiliko ya kisera kulingana na nyakati. Hii itasaidia sio tu utawala Bora Bali hata kuijenga jamii inayojitambua. Kuendelea MFUMO huu WA sasa unatengeneza hofu, na demokrasia dhaifu Kwa kizazi kijacho.

4. Itaendoa dhana ya utegemezi. Viongozi wengi Kwa ngazi za vyuo wanategemea nguvu kutoka vyama VIKUU hivyo wao wanakuja hawana Cha ziada wanachofanya zaidi ya kupokea amri fanyeni hivi fanyeni hivi. Hii unatengeneza Hali ya kutegemea hasa Kwa wale tunaotegemea wakawe viongozi huko uraiani. Vile vile wanafunzi wengi wanashindwa kupaza sauti zao Kwa kuhofia kuikosea serikali kuu. Hivyo MFUMO huu utatenganisha sera, itikadi zote kati ya vyama vya vyuoni na vile VIKUU.

Mfano ni jambo na aibu kiongozi ngazi ya chuo anapiga kampeni nae tukimchagua atajenga daraja sijui darasa au Barbara, hizi sera za ujenzi WA madaraja sio za miakaa hii, tunataka mikakati madhubuti ya kuimarisha elimu vyuoni sio kuja kuijenga madaraja au barabara
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…