Tanzania Tulikuwa salama zaidi Mikononi mwa Ujamaa kuliko Tulivyo sasa Mikononi mwa Ubepari/Ubeberu

Kabisa kabisa ! Sisi wengine tulikuwepo wakati ule na sasa pia bado tupo we knew and we know the whole truth !!
Hatujalishwa matango pori sisi !!
 
Mkuu Burkinabe, kwanza asante kwa mjadala huu, japo umejiita mzee, kwa posts zako wewe ni kijana wa 80s, wazee humu JF tupo ila tumebaki wachache wale wangumu wenye uwezo wa kuvumilia ujinga ujinga wa vijana humu.

Nimefurahi kuona bado kuna vijana wa Nyerere type, wanaoamini kwenye Ujamaa. Nakuunga mkono, Tanzania ingekuwa njema zaidi na salama zaidi kwenye Tanzania ya Ujamaa kuliko Tanzania hii ya ubepari.

Ukilisoma Azimio la Arusha lililotangaza Tanzania kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ni zuri kabisa, tatizo lilikuja kwenye utekelezaji, tulifanya mistakes ya kwanza ni kwenye mzizi wa mfumo wenyewe wa Ujamaa wa Mwalimu, ulikuwa na kosa moja kubwa la msingi ambalo ndilo chanzo cha kufeli kwa Ujamaa. Kosa hilo nililitaja kwenye uzi wangu huu Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza? Hivyo the 1st mistake ya Ujamaa wa Nyerere ni kwenye root cause ya kuamini ili tuendelee tulihitaji vitu 4, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, vitu vyote hivi tulikuwa navyo, kwanini tulishindwa kuendelea?. Kosa la kwanza ni kuaminishwa na Mwalimu kuwa fedha, sio msingi, fedha ni matokeo!.

That was wrong, ili tuendelee tulihitaji mitaji, bila mitaji hatuwezi ku exploit potentials zozote tulizo nazo, hivyo licha ya kuwa na watu wa kutosha na ardhi yenye rutuba, kilimo cha jembe la mkono hakiwezi kulikomboa taifa, bila mitaji ya kufanya Mapinduzi ya kilimo, kilimo hakiwezi kuwa productive hivyo hapa Nyerere alifeli.

Tulipofanya Operesheni Vijiji, that was another mistake, Kilimanjaro, Bukoba na Mbeya walimgomea ndio makabila yenye afadhali kiuchumi.

Ilipojuja vita ya Kagera ndio ikafunga kazi, uchumi wetu ukadidimia kabisa, IMF na WB wakatuletea masharti ya kutukopesha na kutulazimisha kuukumbatia ubepari, hivyo Mwalimu Nyerere akaamua kuliko kugeuka nyuma ageuke jiwe, bora anyooshe mikono juu na kuachia ngazi, ndipo akang'atuka na kumpisha Mwinyi aliyekubali kila kitu.

Mkapa, na JK nao played their part lakini the biggest impact came with JPM. Huyu alikuwa kama Nyerere, kupitia Magufulification, alikuwa anairudisha Tanzania kuwa nchi ya Kijamaa na chama kimoja. Akaanzisha elimu bure, alikuwa anakuja na afya bure!, Mungu ndio akamchukua.

Mimi ni mtu wa Nyerere type, na nimefurahi kuona watu wa Nyerere type bado wapo wengine ni hawa Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere! na hawa Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa na huyu Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa? na huyu Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...

Jumapili Njema
P
 
Unapenda ujamaa ?
 
China wamefanya hivyo na wamepiga hatua.

Mambo mengi hutegemea political will ili yaende.

Sisi hatuna viongozi wa aina ya China na Russia.

Yaani viongozi mabeberu lakini wazalendo, hao hatuna.
 
Wewe ndio huna akili na ikiwezekana una matope kabisa,badlands ya kusema athali za ujamaa katika kipindi chake wewe unaleta athali za ujamaa baada ya mabeberu kuwapiga pini juu ya kuendesha Nchi kwa sera ya Ujamaa.
 
Mto hoja wewe ni Mwamba sana,tumerudi nyuma mara 1000 na sababu kuu ni moja veranda vyote vilivyojengwa na kufanya kazi katika kuishi sera ya ubepari vilibinafisihwa na wajanja wachache wakanufaika na badaye vilikufa-na matatizo ya kiuchumi kama kukosekana kwa ajili yakaanzia hapo.
 
Kwa sasa watanzania wengi hawana matumaini na hawaijui kesho yao, nchi imekuwa ya ovyo maradufu.
 
Alifanyiwa figisu na mabeberu ili kukwepa aibu ndio akaamua kung'atuka.
Miradi yake ya kijamaa ilifeli, kuficha aibu na hasara aliyoingia akamwachia kijiti Mwinyi ila akamsihi aje na sera ya capitalism ili apate misaada hali ilikuwa mbaya
 
Mkuu ulizoandika hapa ni propaganda,ukweli ni kuwa kuanzia miaka ya 1970's USA alianzisha mgogoro wa kiuchumi kupitia uhaba wa mafuta wenye lengo la kuua Sera ya ujamaa Duniani ili kuendeleza ukiranja wake wa Dunia ili apate uungaji mkono na kudidimiza Russia na China.
 
Ni kweli unachosema Mkuu, kuna baadhi ya mambo yaliyopelekea hiyo hali ngumu;
1. Athari ya njaa iliyotokana na ukame miaka ya mwanzoni mwa 70 (1973/1974)
2. Vita ya Kagera dhidi ya Nduli Idi Amin
Hali ngumu ya kimaisha ilitengenezwa na USA,jamani someni haya mambo.
 
Miradi yake ya kijamaa ilifeli, kuficha aibu na hasara aliyoingia akamwachia kijiti Mwinyi ila akamsihi aje na sera ya capitalism ili apate misaada hali ilikuwa mbaya
Miradi ya ujamaa ilibinafisishwa,emu tuleteee maendeleo ya hiyo miradi baada ya kubinafisishwa.
 
Miradi yake ya kijamaa ilifeli, kuficha aibu na hasara aliyoingia akamwachia kijiti Mwinyi ila akamsihi aje na sera ya capitalism ili apate misaada hali ilikuwa mbaya
IMF walimfinya na kwakua hakutaka kukubaliana na masharti yao akasepa.
 
Watu wengi wanamlaumu Nyerere na kuponda ujamaa wakidhani USA anauchukia ujamaa.
Ujamaa ni usoshalist ambao upo Israel ambao wana kibbutzim na Moshav.
Sweden ni wajamaa. Ujerumani ni wajamaa na ndio maana wana mpaka chama cha kijamaa (SDU cha akina Gerhard Shroder)
Japan ni wajamaa.

Na fuatilia mataifa yenye ujamaa, hakuna umasikini wala hakuna tajiri sana kama Elon Musk ila unashangaa taifa lenye uchumi mkubwa Ulaya ni wajamaa.
Hata timu kubwa ya kandanda kama Beyern Minchen inaendeshwa kijamaa.

Nyerere alikosa watu ambao walikuwa falsafa ya kujenga uchumi as kijamaa. Bahati mbaya alimpa Kawawa kuongoza jahazi wakati akiwa hajui model ya ujamaa inafanya vip kazi.
 
Mkuu tunashukuru sana kwa bandiko hili lililosheheni "madini" tupu. Binafsi huwa navutiwa sana na nyuzi zako pamoja na michango yako kwa ujumla ukiachilia michache ambayo kwa kweli binafsi huwa nafikiria kuna watu huwa wanatumia account yako! Huyu aliyetoa "madini" haya ndo Pascal Mayala original.
😁😁😁😁
Ubarikiwe sana Mkuu.
 
Nathubutu kusema wewe Pascal Mayalla ni "genius ". Una uwezo mkubwa sana wa kuchambua na kupembua mambo.
Nina imani siku moja utatufaa sana sehemu mojawapo serikalini endapo tukipata viongozi wazalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…